ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

Saturday, May 18, 2013

YANGA YASHEREHEKEA UBINGWA KWA KUMNYOA MTANI WAKE

Nahodha wa Yanga, Nidir Haroub  'Canavaro' akiwa amenyanyua kombe la Ubingwa
wa 
Ligi Kuu ya Soka Tanzania Bara pamoja na wachezaji wenzake.

Beki wa Simba, Musa Mudde (kushoto) akichuana na mshambuliaji wa Yanga, Didier Kavumbagu katika mchezo wa Ligi Kuu ya Soka Tanzania Bara uliofanyika kwenye
Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam, leo.


Kikosi cha Simba.

Makocha wa yanga wakipanga mikakati ya Ushindi.
Timu zikiingia uwanjani.

Beki wa Simba, Shomari Kapombe akimtoka mshambuliji wa Yanga, Simon Msuva

Msanii Juma Nature akitumbuiza wakati wa mchezo huo.
Mashabiki wa Yanga
.
Raha ya ushindi.
Kocha wa Yanga, Ernst Brandts akiwa amebebwa na wachezaji wake.
Mashabiki wa Yanga.
Kipa wa Simba, Juma Kaseja akijaribu bila mafanikio kuokoa mpira wa kichwa 
uliopigwa na mshambuliaji wa Yanga, Didier Kavumbagu katika mchezo wa kufunga 
pazia la Ligi Kuu ya Soka Tanzania Bara uliofanyika kwenye Uwanja wa Taifa 
jijini Dar es Salaam leo.


Mashabiki wa Yanga wakiwa wamembeba mshambuliaji wa Simba, Mrisho Ngasa 
mara baada ya mpira kumalizika, ikiwa ni ishara ya kumkaribisha katika klabu yao.


Refa wa mechi ya Simba na Yanga, Nartin Saanya akiwa chini baada ya kugongwa 
kwa bahati mbaya na mchezaji wa Yanga, Didier Kavumbagu.
PICHA ZOTE KWA HISANI YA HABARI MSETO

JONAS SEGU AILETEA TANZANIA HESHIMA MPYA KWENYE NGUMI ZA KULIPWA . AMHENYESHA MTHAILAND VILIVYO. AUMIZWA MKONO KWENYE RAUNDI YA 6



International Boxing Federation Africa (IBF/AFICA) – SATURDAY 18 MAY, 2013, DAR ES SALAAM, TANZANIA –  Tanzania imetengeneza historia mpya kwenye ngumi za kulipwa nchini Thailand baada ya mabondia wake kuwa wanapigwa kila mara wanapokwenda kuiwakilisha nchi na bara la Afrika. Safari hii JEMBE, kijana mtanashati anayeinukia kwenye masumbwi Jonas Segu kutoka katika ukumbi wa mazoezi wa Respect Gym Boxing Club ya Mabibo Loyola chini ya kocha Christopher Mzazi ameonyesha kipaji kikubwa cha kusukuma msumbwi alipoushangaza umati wa maelfu ya wananchi wa Thailand pamoja na nchi za ukanda wa Indo-China.

Segu alikuwa anachuana na bingwa wa IBF katika mara la Asia Pacific Patomsuk Pathompothong kutoka Thailand katika uzito wa Light Welter ambaye ni bondia namba 7 duniani katika viwango vya IBF. Mpambano wao ulifanyika katika jiji lenye mahekalu ya dhahabu la Bangkok na kurushwa na television katika nchi zote za ukanda wa Indo-China za Laos, Myanmar, Cambodia, Vietnam na Thailand yenyewe.

Mpambamo wa Segu na Pathompothong ulianza kwa bondia wa kitanzania kuchomoka kama upinde kwenye kona yake na kumshambulia Pathompothong kwa makonde mazito ya kumshikisha adabu. Segu alitupa makonde ya mchanganyiko na kumzidi Pathompothong kutokana na uzito na umakini wa ngumi zake. Kwa kipindi chote cha raundi ya kwanza ilimbidi Pathompothong ajilinde na kukimbia akizunguka ndani ya ulingo ili kudhoofisha masumbwi ya Segu aliyekuwa anayachanganya kama mashine ya kukomboa mpunga ambao unalimwa kwa wingi nchini Thailand!

Jonas Segu alikuwa chini ya uangalizi makini wa bondia maarufu mstaafu George “Lister” Sabuni ambaye aliweza kumpa maelekezo ya nini cha kufanya kwenye mpambano huo wa mwaka. Katika raundi ya 2, 3 na 4 Segu aliuonyesha umati wa mashabiki wa Thailand kuwa yeye kweli ni bingwa mtarajiwa na hakwenda Thailand kula wali wao ila kuiwakilisha nchi yake ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Segu alimhenyesha Pathompothong vilivyo kwa kumchakaza kwa makondde mfululizo hususan akiutumia mkono wake hatari wa kulia ambao ulionekana dhahiri kuwa unaleta madhara makubwa kwa Pathompothong.

Ilididi timu ya wataalam wa Pathompothong kutafakari namna ya kumdhibiti kijana huyo wa Kitanzania ambaye kweli alionekana kuwa alienda Thailand kuuchukua mkanda wa IBF Pan Pacific na sio kufuata ulaji!

Raudi ta 5 Pathompothong aliingia ulingoni akiwa mtu tofauti kabisa akirusha msumbwi mfululizo na kutembea ulingoni kama siafu huku akimvuta Segu kenye kamba ili amkandamizie masumbwi yake. Kijana huyo nadhifu wa kitanzania (mwenye sura nzuri ya kuvutia na ambaye wasichana wengi wa Thailand walishinda karibu na hoteli aliyoshukia ili kuweza kuongea naye) alitumia wakati huo kumwonyesha Pathompothong kuwa yeye hababaishwi na masumbwi yake kwani amefanya mazoezi ya kutosha. Segu alibadilishana masumbi na Pathompothong vilivyo na kuufanya umati wa mashabiki waliojazana kwenye ukumbi huo kumshangilia kama vile yeye ndiye bondia wao wakiimba Tanzania, Tanzania, Tanzania!

Katika raundi ya 6 mabondia wote waliingia ulingoni kama vifaru na kubadilishana masumbwi ya mchanganyiko (combinations) wakitafuta kudhibiti harakati za mpinzani mwenza. Ni katika kubadilishana huku kwa masumbwi ambako Segu aliumizwa mkono na Mthailand Pathompothong. Inawezekana kuwa ni katika juhudi za kumzuia ili asiendelee kurusha masubwi ya nguvu na kudhoofisha nguvu zake.

Kuumia mkono kwa Segu ilikuwa dhahiri kwani mwanzoni mwa raundi ya saba wakati Pathompothong alipokuwa anamiliki ulingo dhidi ya kijana huyo mtanashati wa kitanzania. Katikati ya raundi ya saba Segu aliona kuwa hawezi kuutumia mkono wake vizuri na kumwashiria refarii wa mpambano kuwa anaacha!

Segu aliacha pambano hilo katika raundi ya saba wakati mashabiki wengi katika ukumbi huo wakiwa wanaimba Tanzania, Tanzania, Tanzania kwa jinsi alivyokuwa anapeperusha vyema bendera ya “Jamhuri ya Muungano wa Tanzania”

"NKABAaaa....HII HAPA ZE UTAMU YA ROCK CITY...!!!"

'Kinachotia nakshi Bismakini'


Mjumuisho...


Ze area Bismack Rock.


Mawe yaliyoota majini ni viwanja vya starehe kwa ndege.


Zoom ...


Jicho toka bustanini... 


Adimu...


The stone is kumea from inside water?


Machweo...


Hii ndiyo ze utamu ya Rock City na G.sengo Blog
!....uMeChUkiA...?

Friday, May 17, 2013

MICHUANO YA SAFARI LAGER HIGHER LEANING NATIONAL POOL CHAMPIONSHIP KUANZA RASMI KESHO JIJINI MWANZA

Meneja wa Matukio wa bia ya Safari mkoa wa Mwanza Bernad Nahum (kushoto) akizungumza na waandishi wa habari ambapo pia alitumia fursa hiyo kukabidhi jezi kwa washiriki, kulia ni captein wa timu ya SAUT Jimmy Nikitas,  inayotetea taji la ubingwa wa pool kwa vyuo nchini.


Mashindano ya Safari Lager Higher Leaning Pool kwa mkoa wa Mwanza yanataraji kuanza kutimua vumbi kuanzia kesho katika ukumbi wa Villa Park jijini Humo.

Kwa mujibu wa Meneja wa Matukio wa bia ya Safari mkoa wa Mwanza Bernad Nahum amesema kuwa Mashindano ya Higher Leaning Pool kwa mkoa wa mwanza yatashirikisha vyuo vinne ambavyo ni CBE Mwanza, Chuo cha Bugando, SAUT na TIA ambapo vyuo hivyo vitashindana kupata mwakilishi  mmoja atakaye shiriki mashindano ya Pool Taifa kwa mikoa mingine hapa nchini kama Mbeya, Dar es salaam, Morogoro, Dodoma, Kilimanjaro na Arusha  
Kushoto aliyesimama ni Afisa habari wa michuano ya Safari Lager Higher Leaning Pool Machel akitoa ufafanuzi juu ya mafanikio yaliyopatikana hadi sasa kwa vyuo shiriki kupitia michuano hiyo.

Zawadi kwa washindi Timu za Pool 
Mshindi wa kwanza mkoa ni shilingi laki 5
Mshindi wa pili shilingi laki 3
Mshindi wa tatu shilingi laki 2
Na mshindi wa nne shilingi laki 1

Washindi Single wanaume 
Mshindi wa kwanza shilingi laki 1.5
Mshindi wa pili shilingi laki 1

Washindi Single wanaume
Mshindi wa kwanza shilingi laki 1
Mshindi wa pili shilingi elfu 50. 



Timu captein wa timu bingwa Chuo cha SAUT Jimmy Nikitas (kulia) akizungumza na waandishi wa habari kuelezea jinsi timu yake ilivyojiandaa kwa michuano ya Safari Lager Higher Leaning Pool 2013.


Meneja wa Matukio wa bia ya Safari mkoa wa Mwanza Bernad Nahum (kushoto) akimkabidhi jezi timu captein wa Chuo cha SAUT Jimmy Nikitas kwaajili ya michuano hiyo inayotaraji kuanza rasmi kesho Villa Park Resort Mwanza.


Meneja wa Matukio wa bia ya Safari mkoa wa Mwanza Bernad Nahum (kushoto) akimkabidhi jezi timu captein wa Chuo cha Bugando Bernad Okamo, kwaajili ya michuano hiyo inayotaraji kuanza kutimua vumbi rasmi kesho katika Viunga vya burudani vya Villa Park Resort Mwanza.


Meneja wa Matukio wa bia ya Safari mkoa wa Mwanza Bernad Nahum (kushoto) akimkabidhi jezi timu captein wa Chuo cha CBE Mwanza George Izengo, kwaajili ya michuano ya Safari Lager Higher Leaning Pool inayotaraji kuanza rasmi kesho Villa Park Resort Mwanza.


Meneja wa Matukio wa bia ya Safari mkoa wa Mwanza Bernad Nahum (kushoto) akimkabidhi jezi timu captein wa Chuo cha TIA Beatrice Benignus, kwaajili ya michuano ya Safari Lager Higher Leaning Pool inayotaraji kuanza rasmi kesho viunga vya burudani Villa Park Resort Mwanza.

BABA JONII AITAMBULISHA MIXTAPE YAKE YA KWANZA SIKU YA BIRTHDAY YAKE JANA MAY 16 2013

Adam Mchomvu a.k.a baba jonii Radio presenter clouds fm mwenye crown ya best presenter, jana alifanikisha zoezi la kuitambulisha na kutoa mixtape yake yenye  ngoma kumi na nane alioshirikiana na wasanii mbali mbali kama Jose Mtambo, Banana Zorro, Illimatix, Cliff mitindo, G.nako, Nikk war 2, Babuu war kitaa, TID, na wasanii wengine wengi kama zawadi kwa mashabiki wake ibaki kama kumbukumbu kwa kile anachokifanya hewani (on...Read More

Thursday, May 16, 2013

MKUU WA GENGE LA MATAPELI WANAOJIFANYA MAAFISA WA TAKUKURU ANASWA JIJINI MWANZA, ALIKUWA AKITUMIA HIRIZI KUFANIKISHA WIZI

Mtuhumiwa Simon Jumbe anayetajwa kujifanya afisa wa Takukuru.
 TAASISI ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (Takukuru) Mkoa wa Mwanza imefanikiwa kumnasa mtu mmoja ambaye anasadikika kuwa mkuu wa genge la watu wanaojifanya Maafisa wa Ofisi ya TAKUKURU Mkoani hapa.


Akitoa taarifa kwa waandishi wa Habari ofisini kwake Kamanda wa TAKUKURU Mkoa wa Mwanza Ayubu Akida alisema kwamba kukamatwa kwa mtuhumiwa huyo aliyefahamika kwa jina la Simon Jumbe (32) lakini amekuwa akitumia majina mengie kwa kujiita Mapunda na SP ni kutokana na mtego uliowekwa na maafisa wake.
Kamanda wa TAKUKURU mkoa wa Mwanza Ayoub Akida, akizungumza na waandishi wa habari ofisini kwake leo.
“Tuliweka mtego huo kutokana na kuwepo taarifa za siri kutoka kwa raia wema ambapo walitueleza kwamba kuna wimbi la baadhi ya watu ambao wamekuwa wakiwadanganya watu kuwa wao ni maafisa na watumishi wa TAKUKURU baada ya kuweka mtego Mei 13 mwaka huu tumefanikiwa kumnasa huyu maeneo ya Kata ya Mkuyuni Wilayani Nyamagana” alisema Akida.

 Kamanda Akida alieleza kwamba tangu mwezi April na Mei tumekuwa katika hekaheka za kuwatafuta watu hao baada ya taarifa za kuwepo watu hao wanaojitambulisha kuwa watumishi na wamekuwa akiwadanganya watu na kufanya kazi ambazo si za ofisi ya Takukuru ikiwa ni zile za Taasisi zingine za serikali.

Kamanda wa TAKUKURU mkoa wa Mwanza Ayoub Akida
“Katika kipindi hicho tuliweza kupokea taarifa za matukio kumi ya kutoka kwa watu waliotapeliwa katika Wilaya za Misungwi na Jiji la Mwanza ambapo baada ya kumnasa mtuhumiwa huyu na kumhoji alidai kuwa yeye peke kwa kutumia utapeli huo ameweza kujipatia kiasi cha shilingi milioni 4,637,000/= kutoka kwa watu kumi na mbili”alisema Kamanda.

Naye mmoja wa watu walioathirika na kutapeliwa aliyejitambulisha kwa jina la James Belindo mkazi wa Nyakato Buzuruga Wilayani Ilemela alisema kwamba  alimfahamu mtuhumiwa kwasababu alikuwa jirani yake naye mtuhumiwa alitumia mwanya huo wa ujirani akimweleza kuwa kuna magari 12 yameletwa ofisini kwao yaani TAKUKURU hivyo kuna nafasi za kazi ambazo anaweza kumuunganishia.

James Belindo mmoja kati ya waliotapeliwa
Bofya play msikilize kwa kina hapa chini.
“Alidai kama nina ujuzi wa kuendesha gari yaani udereva basi nimwambie,  nilimweleza sina lakini kuna jamaa yangu, naye akasema hamna tabu nimpeleke atakuwepo ofisi ya Takukuru Mkoa, akaomba vyeti na leseni kisha akamweleza kuwa inatakiwa kufunguliwa majarada matano na kuomba kiasi cha 475,000/- lakini hakupata kazi hiyo”alieleza kwa masikitiko.

Kamanda Akida amewatahadharisha wananchi kuwa makini na kundi la matapeli hao wanaojifanya watumishi wa Takukuru ambao wamekuwa wakiidhalilisha na kuipaka matope ofisi yake na kuharibu taswira iliyopo kwa jamii na kuwataka kufika ofisi za Takukuru na kutotoa fedha bila utaratibu wa taasisi hiyo.

Aidha alisema kwamba kutokana na kuwepo kundi hilo ofisi yake imewataka wananchi kuendelea kutoa taarifa za siri zitakazofanikisha kunaswa kwa watu hao ambao wamekuwa wakiwadanganya kuwatafutia kazi,kuwatisha ili wawapatie fedha kunyume na huduma zinazotolewa na ofisi za Takukuru Wilayani na Mkoa.


Hirizi iliyotumiwa na mtuhumiwa Simon Jumbe

Baada ya kuhojiana naye kwamaana alikuwa anaficha ila baada ya 'kumsalimia sana' mtuhumiwa alisema kuwa hirizi hii huwa anailamba asubuhi, akishailamba asubuhi yule mtu aliyepanga kwenda kuonananaye, akishaonana naye hawezi kupingana naye kwa kila atakachomwamuru afanye.


Mtuhumiwa Simon Jumbe akiri tuhuma dhidi yake
huyu ndiye anayetajwa kujifanya afisa wa 

Takukuru
Bofya play hapa chini kumsikiliza.
Akitaka kupatiwa fedha atapewa, hata vingine vya kufikirika kwa kutumia akili kuwa haviwezekani mtapeliwa atakubali kama vile kutoa fedha akafunguliwe akaunti nakadhalika.

Iliwachukuwa muda maafisa hao kuipata hirizi hiyo iliyokuwa ikitumiwa na mtuhumiwa huyo, kwani alikuwa ameifunga ndani kwenye kaptula ya jeans, juu akiwa amevaa mashati matatu, yaani T-shirt mbili za mikono mirefu moja ikiwa nyeupe na shati moja juu yake. 

Hivyo aliweza kubadilika badilika kutokana na mazingira, kwamba anaweza kufanya tukio la utapeli mahali fulani ndani ya dakika chache anahamia upande wa pili wa 
barabara akavua shati la juu na kuwa na T-shirt rangi nyingine akijiunga na watazamaji wa tukio. 

Hii ni kwa mujibu wa mmoja kati ya maafisa wa Uchunguzi TAKUKURU waliofanikisha kumnasa tapeli huyo.

Katika hatua nyingine  Jumbe amekiri kwa kauli yake kwenye mahojiano kushiriki kingono na wanafunzi 24 wa Chuo cha SAUT,   na wengine 16 wa Chuo cha Ualimu Butimba kwa gia hiyo hiyo ya kuwalaghai kuwa atawapatia nafasi ya ajira Takukuru.