Mtuhumiwa Simon Jumbe anayetajwa kujifanya afisa wa Takukuru. |
Akitoa taarifa kwa
waandishi wa Habari ofisini kwake Kamanda wa TAKUKURU Mkoa wa Mwanza Ayubu
Akida alisema kwamba kukamatwa kwa mtuhumiwa huyo aliyefahamika kwa jina la
Simon Jumbe (32) lakini amekuwa akitumia majina mengie kwa kujiita Mapunda na
SP ni kutokana na mtego uliowekwa na maafisa wake.
Kamanda wa TAKUKURU mkoa wa Mwanza Ayoub Akida, akizungumza na waandishi wa habari ofisini kwake leo. |
“Tuliweka mtego huo
kutokana na kuwepo taarifa za siri kutoka kwa raia wema ambapo walitueleza
kwamba kuna wimbi la baadhi ya watu ambao wamekuwa wakiwadanganya watu kuwa wao ni
maafisa na watumishi wa TAKUKURU baada ya kuweka mtego Mei 13 mwaka huu tumefanikiwa
kumnasa huyu maeneo ya Kata ya Mkuyuni Wilayani Nyamagana” alisema Akida.
Kamanda Akida alieleza kwamba tangu mwezi
April na Mei tumekuwa katika hekaheka za kuwatafuta watu hao baada ya taarifa
za kuwepo watu hao wanaojitambulisha kuwa watumishi na wamekuwa akiwadanganya
watu na kufanya kazi ambazo si za ofisi ya Takukuru ikiwa ni zile za Taasisi
zingine za serikali.
Kamanda wa TAKUKURU mkoa wa Mwanza Ayoub Akida |
Naye mmoja wa watu
walioathirika na kutapeliwa aliyejitambulisha kwa jina la James Belindo mkazi
wa Nyakato Buzuruga Wilayani Ilemela alisema kwamba alimfahamu mtuhumiwa kwasababu alikuwa jirani yake naye mtuhumiwa alitumia mwanya huo wa ujirani akimweleza kuwa kuna
magari 12 yameletwa ofisini kwao yaani TAKUKURU hivyo kuna nafasi za kazi ambazo anaweza kumuunganishia.
James Belindo mmoja kati ya waliotapeliwa Bofya play msikilize kwa kina hapa chini. |
Kamanda Akida
amewatahadharisha wananchi kuwa makini na kundi la matapeli hao wanaojifanya
watumishi wa Takukuru ambao wamekuwa wakiidhalilisha na kuipaka matope ofisi
yake na kuharibu taswira iliyopo kwa jamii na kuwataka kufika ofisi za Takukuru
na kutotoa fedha bila utaratibu wa taasisi hiyo.
Hirizi iliyotumiwa na mtuhumiwa Simon Jumbe |
Baada ya kuhojiana naye kwamaana alikuwa anaficha ila baada ya 'kumsalimia sana' mtuhumiwa alisema kuwa hirizi hii huwa anailamba asubuhi, akishailamba asubuhi yule mtu aliyepanga kwenda kuonananaye, akishaonana naye hawezi kupingana naye kwa kila atakachomwamuru afanye.
Mtuhumiwa Simon Jumbe akiri tuhuma dhidi yake huyu ndiye anayetajwa kujifanya afisa wa Takukuru Bofya play hapa chini kumsikiliza. |
Iliwachukuwa muda maafisa hao kuipata hirizi hiyo iliyokuwa ikitumiwa na mtuhumiwa huyo, kwani alikuwa ameifunga ndani kwenye kaptula ya jeans, juu akiwa amevaa mashati matatu, yaani T-shirt mbili za mikono mirefu moja ikiwa nyeupe na shati moja juu yake.
Hivyo aliweza kubadilika badilika kutokana na mazingira, kwamba anaweza kufanya tukio la utapeli mahali fulani ndani ya dakika chache anahamia upande wa pili wa
barabara akavua shati la juu na kuwa na T-shirt rangi nyingine akijiunga na watazamaji wa tukio.
Hii ni kwa mujibu wa mmoja kati ya maafisa wa Uchunguzi TAKUKURU waliofanikisha kumnasa tapeli huyo.
Katika hatua nyingine Jumbe amekiri kwa kauli yake kwenye mahojiano kushiriki kingono na wanafunzi 24 wa Chuo cha SAUT, na wengine 16 wa Chuo cha Ualimu Butimba kwa gia hiyo hiyo ya kuwalaghai kuwa atawapatia nafasi ya ajira Takukuru.
Tupe maoni yako
0 comments:
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.