Kwenye uwanja wa wa CCM kirumba jijini mwanza Toto Africans inaikaribisha JKT Oljoro kutoka Arusha |
Toto Africans ndani ya dimba la CCM Kirumba muda huu. |
JKT Oljoro kutoka Arusha ndani ya dimba la CCM Kirumba muda huu. |
Ligi kuu soka Tanzania Bara inaanza leo jumamosi ambapo timu zote 14 zinazoshiriki michuano hiyo zitajitupa kwenye viwanja saba tofauti nchini.
Kwenye uwanja wa wa CCM kirumba jijini mwanza Toto Africans inaikaribisha JKT Oljoro kutoka Arusha huku Kagera Sugar wakiwa wenyeji wa Azam Fc ya Dar es salaam kwenye uwanja wa Kaitaba mjini Bukoba.
Mabingwa wa kombe la Kagame Young Africans wataianza ligi hii ugenini dhidi ya Tanzania prisons kwenye Uwanja wa Sokoine mjini Mbeya.
Mabingwa watetezi wa ligi hii Simba Sc wao wako uwanja wa Taifa jijini Dar es salaam wakiumana na African Lyon.
Timu mbili za Morogoro Polisi Morogoro na Mtibwa Sugar zitapambana kwenye Uwanja wa Jamhuri mjini humo, wakati MaMagombo JKT ikichuana na Costal Union mjini Tanga.
Pia Timu mbili za mkoani Pwani JKT Ruvu na Ruvu Shooting Stars nazo zinaanza ligi hii kwa kucheza kwenye uwanja wa Chamanzi.