DIWANI wa Kata ya Kitangili Manispaa ya Ilemela Mkoani Mwanza
Henry Matata na Diwani wa Kata ya Igoma
Halmashauri ya Jiji la Mwanza (Nyamagana) Adam Chagulani wote kutoka Chama cha
CHADEMA wametoa tamko lao kwa vyombo vya habari leo kupinga maamuzi ya Kamati
kuu ya Chama hicho ya kuwavua uanachama hivi karibuni kwa madai ya kukisaliti
chama na kula njama kukushinikiza kumung’oa aliyekuwa Meya wa Jiji la Mwanza Josephat
Manyerere (Nyakato).
Diwani wa kata ya Kitangili Henry Matata. |
Diwani
Matata (Kitangili) alisema kwamba kikao cha kamati kuu kilichoketi mwishoni mwa
juma lililopita na kutoa uamuzi huo Jijini Dar es salaam kiligubikwa na
ushabiki na pia ukiukwaji wa Katiba ya Chama hicho na ile ya Jamhuri ya
Muungano wa Tanzania hivyo wameamua kwenda mahakamani kufungua kesi ya kuzuia
uamuzi huo wa Kamati kuu ya CHADEMA wa kuwavua uanachama ili kukosa madaraka
(Udiwani) ikiwa wao walichaguliwa na
wananchi zaidi ya elfu nne.
Akifafanua
Matata amedai kuwa moja ya sababu kubwa zilizowafanya kukimbilia mahakamani yeye
na diwani mwenzake Chagulani ni kutaka haki itendeke kwa vile madai na tuhuma
zilizotolewa dhidi yake ni za uongo ambazo hazina ukweli bali kwa shinikizo la
wabunge wa chama hicho wa majimbo ya Ilemela, Nyamagana na Ukerewe kutokana na
kuwepo kutokuelewana baina yao na madiwani hao wanaodaiwa kuwahofia kisiasa.
Diwani wa Igoma Adam Chagulani. |
Chagulani
alisema kwamba umefika wakati wa viongozi wa chama hicho kuacha kutumia ubabe
wa kuamua kuwafukuza wawakirishi wa wananchi waliochaguliwa kwa kisingizio cha
kukisaliti chama hicho bali watambue kuwa wao ni kiungo cha kuwatumikia
wananchi na kuwawakilisha kwenye mabaraza ili kuzitafutia kero zao ufumbuzi na
CHADEMA lazima itumie vikao vya chini na kuifuata vyema Katiba yake na hatua za
wenye makosa kujadiliwa kuanzia ngazi ya kata, wilaya, mkoa na Taifa badala ya
kuanzia juu kisha kutoa uamuzi hiyo si demokrasia hata kidogo bali ni udikiteta
wa demokrasia ndani ya vyama vya siasa.
BARUA ALIYOANDILIWA MH. DIWANI CHAGULANI KUVULIWA UANACHAMA CHADEMA
Tupe maoni yako
0 comments:
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.