ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

Saturday, October 8, 2011

KUELEKEA NYERERE'S DAY BW. JUMA MAKONGORO AKABIDHI MADAWATI KWA SHULE YA MSINGI IKIZU A.

Mgeni rasmi mwakilishi wa Familia ya Hayati Baba wa Taifa, Bw. Madaraka Nyerere akikata utepe kuzindua mradi wa kuchangia madawati na elimu Shule za mitaa na vijiji vya kata ya Nyamswa na Ikizu ambapo jumla ya madawati 50 yalitolewa jana.

Ndugu Juma Makongoro akikabidhi Madawati 30 kwa Bw. Madaraka Nyerere ambaye aliyawasilisha kwa uongozi wa shule.

Wanafunzi wa Shule ya Ikizu A wakikabidhiwa madawati 20 toka mwakilishi wa Mradi wa Zinduka mkoani Mara.

"Mimi binafsi nilisoma katika shule hii kongwe, lakini kama mtamkumbuka Mwalimu aliyenifundisha darasa la kwanza, marehemu Karemela Diaz kwenye mazishi yake nilipata nafasi ya kutoa ushuhuda wa namna ninavyomfahamu na nikaahidi na kutoa wito kwa Waikizu wote kutafuta njia bora ya kumuenzi. Sasa njia moja wapo tumeianzisha leo..."Says Juma Makongoro.

Naye Mgeni rasmi mwakilishi wa Familia ya Baba wa Taifa Bw. Madaraka Nyerere amesema kuwa kuna haja ya vijana wote waliopita katika shule hiyo kuungana kwa pamoja na kuona ni jinsi gani wanaweza kuifanikisha na kuiwezesha shule hiyo katika hatua zake za maendeleo ya elimu .

Kifimbo ni zawadi kwa madaraka Nyerere toka kwa uongozi wa shule ya Ikizu A.

Mama wa Juma Makongoro akitoa yake.

Wanafunzi wa shule ya Ikizu A na madawati yao 50 waliyokabidhiwa.

Wakiimba wimbo wa shukurani hawa ni wanafunzi wa shule ya ikizu A wilayani Bunda mkoani Mara.

Ngoma ya jadi ya kabila la Waikizu.

Picha ya Pamoja part one.

Makongoro amesema kuwa lengo la msaada huo ni kutaka utumike kama wito kwa jamii yote ya Waikizu kujenga tabia ya kujiletea maendeleo wenyewe badala ya kutegemea nguvu za serikali kwani serikali nayo bado ina mzigo wa majukumu na changamoto nyingi zinazoikabili.

Thursday, October 6, 2011

MTAALAM Apple, iPad, iPod, iPhone AFARIKI DUNIA

Steve Jobs, the mastermind behind Apple's iPhone, iPad, iPod, iMac and iTunes, has died, Apple said. Jobs was 56.

Taarifa zaidi yanasema Jobs amefariki dunia kwa amani akiwa amezungukwa na watu wa familia yake.

Si familia ya Jobs' wala Apple hakuna aliyethubutu kutaja mahali Jobs alipofia wala sababu za kifo chake au nini kilichomuua,
though in recent years he had fought a form of pancreatic cancer and had a liver transplant.

"We are deeply saddened to announce that Steve Jobs passed away today," read a statement by Apple's board of directors. "Steve's brilliance, passion and energy were the source of countless innovations that enrich and improve all of our lives. The world is immeasurably better because of Steve. His greatest love was for his wife, Laurene, and his family. Our hearts go out to them and to all who were touched by his extraordinary gifts."

Kurasa za mtandao wa Apple zimefanya chapisho la ukurasa mzima wenye picha ya Jobs inayoambatana na neno, "Steve Jobs 1955-2011." (Steve Jobs Tangu 1955 hadi 2011)

"Apple has lost a visionary and creative genius, and the world has lost an amazing human being," the text read. "Those of us who have been fortunate enough to know and work with Steve have lost a dear friend and an inspiring mentor. Steve leaves behind a company that only he could have built, and his spirit will forever be the foundation of Apple."

Kifo cha Jobs' chaigusa ikulu ya Marekani.
"Michelle and I are saddened to learn of the passing of Steve Jobs," President Obama said in a written statement. "Steve was among the greatest of American innovators - brave enough to think differently, bold enough to believe he could change the world, and talented enough to do it."

Jobs co-founded Apple Computer in 1976 and, with his childhood friend Steve Wozniak, marketed what was considered the world's first personal computer, the Apple II.

Shortly after learning of Jobs' death, Wozniak told ABC News, "I'm shocked and disturbed."

Industry watchers called Jobs a master innovator -- perhaps on a par with Thomas Edison -- changing the worlds of computing, recorded music and communications.

Wednesday, October 5, 2011

BOMOA BOMOA ENEO LA GHANA ZAIDI YA FAMILIA 80 ZAKOSA MAKAZI

Zaidi ya kaya 80 katika Mtaa wa Ghana jijini Mwanza hazina mahali pa kuishi kutokana na Uongozi wa Halmashauri ya Jiji la Mwanza jana majira ya saa 3 asubuhi kubomoa nyumba walizokuwa wanaishi ili kupisha ujenzi wa mradi wa Jengo la Machinga Complex.

Kwa siku ya leo imekuwa ni kama mwendelezo watu waliokuwa wakiishi katika nyumba hizo wameonekana wakihangaika huku na kule kuhamisha vifaa vyao kutoka katika nyumba hizo.

Wengine wakifanya mikakati ya hamahama.

Kutokana na bomoa bomoa inayoendelea Eneo la Ghana kwa sasa limekatiwa umeme hali inayosababisha ulinzi wa mali kuwa mgumu, usiku mzima wananchi hao wamekesha kulinda mali zao kwani vibaka walikuwa wakilandalanda kuiba mali zilizonje ya magofu ya nyumba zilizobomolewa sambamba na kung’oa flemu za milango na madirisha.

Wananchi hao wameiomba serikali kuwapatia maturubai kwa ajili ya kujisitiri wakati wakiwa katika harakati ya kutafuta sehemu nyingine ya kupanga.

Hii ndiyo hali.

Huduma za maji tayari zimekwisha sitishwa.

Hapa alikuwa akiishi balozi.

Vibaka nao wamekuwa wakipitia mabati na mengineyo..

Kwaheri mjengo...

Akizungumzia tukio hilo, Mkurugenzi wa Jiji la Mwanza, Bw. Wilson Kabwe amesema kuwa tayari notisi ya kuhama wakazi hao aliowaita kuwa ni wavamizi ilikwishatolewa kwa zaidi ya miaka miwili iliyopita na kwamba kilichokuwa kinasubiriwa ni wao kuhama bila ya kubughudhiwa lakini wakakaidi agizo mpaka bomoabomoa ilipowakuta.

Kabwe, ameongeza kuwa tayari usanifu wa mchoro kwa ajili ya ujenzi wa Jengo la Machinga ulikwishafanyika na soko hilo linajengwa katika eneo hilo la Mtaa wa Ghana, Wilaya ya Ilemela.

Tuesday, October 4, 2011

MTIHANI WA KIDATO CHA PILI WAREJESHWA.

WAKATI jana wanafunzi wa kidato cha nne wakianza mitihani yao ya kuhitimu elimu ya sekondari, hatimaye serikali imerejesha tena mtihani wa kidato cha pili.

Naibu Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Ufundi, Philip Mullugo, alitangaza urejeshaji huo mbele ya wananchi wa jimbo lake la Songwe lililoko wilayani Chunya, mkoani Mbeya.

Mullugo alisema kuwa ili kupunguza kushuka viwango vya ufaulu hapa nchini hasa kwa kidato cha nne, serikali imeamua kurejesha mtihani huo wa kidato cha pili na wanafunzi wote watatakiwa kufikisha wastani wa alama 25 ili kuendelea na masomo ya kidato cha tatu.

“Kuanzia mwaka huu hakuna mwanafunzi atakayeruhusiwa kuendelea na kidadto cha tatu bila kufanya mtihani wa kidato cha pili na kufikisha wastani wa 25,” alisema Mullugo.

Wakati huohuo, Naibu Waziri huyo wa Elimu na Mafunzo ya Ufundi alitoa msaada wa zaidi ya shilingi mil. 277 kwa ajili ya kusaidia elimu jimboni humo.

LONDON MODERN NETWORK YAFANA!!

Photo Shoot.

Cat walk.

Cat walking ikiendelea.

Model Kutoka Ethiopia katika miondoko ya Cat walk.

Tina (Katikati)Akiwa na SEE LI kutoka kushoto na Mdau.

Sanam zinazo tembea.

Model, Stylist Na Make up artist wakila pozi baada ya kupiga show

Live perfomance.

Frank akila Pozi Na Robert DeNiro

Wadau wakibadillishana mawazo kabla ya show.

URBAN PULSE CREATIVE na MISS JESTINA BLOG wanakuletea picha za London Model Network show iliyofanyika jijini London ijumaa tarehe 30 septemba 2011 ndani Ukumbi wa AURA uliopo MAYFAIR ikiwashirikisha warembo kutoka pande zote za Dunia, Make up Artist, Stylist, na Designers.


Mojawapo Wageni Rasmi walikuwa ni Celebrities Superstar Robert DeNiro na Rebbeca Black.

Show Hii iliandaliwa na SEE LI

Asanteni,
URBAN PULSE Wakishirikiana Na Miss JESTINA BLOG

Monday, October 3, 2011

TUME YA UCHAGUZI YASHINDWA KUTIMIZA AHADI IGUNGA - MATOKEO Eti BAaaaaaaaaaDO!!!!!!

Kazi ya kujumlisha kura uchaguzi mdogo jimbo la Igunga bado inaendelea huku vyama viwili vinavyochuana kwa karibu CCM & CHADEMA macho yakiwa yamevimba makavu kwa kukosa usingizi kila mmoja akidai kutolala mpaka kieleweke. Hayo yanatoke wakati Tume ya Taifa ya Uchaguzi ikiwa imeshindwa kabisa kutimiza ahadi yake iliyoiweka kwamba matokeo yangetangazwa mara tu ya zoezi la upigaji na uhesabu kura kumilika siku husika ya uchaguzi hasa ukizingatia kura ni za jimbo moja tu, lakini holaaa!! mpaka kunakucha hakijaeleweka.

Baadhi ya matokeo ambayo mpaka sasa yamekwisha toka kwenye Kata za Igunga ni Kituo cha Bigadilele ambako CCM ilipata kura 135 na Chadema (96), Choma Bwangamila CCM (193) na Chadema (58).

Katika katika kata ya Nanga, yanaonyesha CCM kupata kura 845 dhidi ya 915 za Chadema, CUF 45 ,DP sita, AFP moja, Sau mbili, UPDP tatu na Chausta mbili.

Kwa upande wa matokeo yaliyojumlishwa kwa Kata ya Nkinga yanaonyesha kuwa CCM imepata kura 1,266, Chadema 1,205, CUF 64 Chausta mbili na AFP mbili.

Matokeo ya Kata ya Bukoko yanaonyesha CCM imepata kura 828, Chadema 726, CUF kura saba, wakati vyama vya SAU, DP, CHAUSTA, AFP na UPDP vikiwa havikupata kitu.

Katika Kata ya Sungwizi, CCM kilikuwa na kura 1,318 huku Chadema kikiwa na kura 671 na CUF kikiambulia kura 14.

Katika Kata ya Simbo, Chadema kinaonekana kuwa mbele kwa kupata kura 861 huku CCM kikiwa na kura 553, CUF 268 na SAU kura moja.

Kwa ujumla, hali ya upigaji kura imekuwa shwari licha ya kuwapo kwa baadhi ya watu waliodai kuyakosa majina yao kwenye vituo.

Mgombea UPDP hakupiga kura
Mgombea ubunge kupitia UPDP, Hemedi Ramadhani Dedu hakupiga kura kwa kuwa hakujiandikisha katika Jimbo la Igunga.

“Sikupiga kura ndugu yangu kwa sababu sikujiandikisha hapa, nimejiandikisha Dar es Salaam.”

Sunday, October 2, 2011

KASEBA BINGWA NGUMI ZA KULIPWA BONGO

Mbunge wa Jimbo la Kinondoni Iddy Azani akimvisha mkanda wa ubingwa unaotambuliwa na chama cha mchezo wa ngumi za kulipwa PST bondia Japhet Kaseba baada ya kumtwanga Maneno Oswald kwa Point jijini Dar es salaam jana.(picha na www.superdboxingcoach.blogspot.com)

Mabondia Japhert Kaseba 9kushoto) akipambana na Maneno Oswald wakati wa mpambano wao wa ubingwa wa PST uliofanyika Dar es salaam jana Kaseba alishinda kwa pointi..(picha na www.superdboxingcoach.blogspot.com)

MBWEMBWE ZA THE NEW STONE CLUB MWANZA

Mkurugenzi wa New Stone Club Mwanza Bw. Jack Fish (shoto) akiongozana na Meneja mauzo wa TBL Mwanza Mr. Mbwambo katika kukata utepe ishara ya ufunguzi..
Ukumbi mzima uligonga kitu cha Chiaaaazzz!!!
Ze crowd kabla ya kukata utape kuzindua dansing flow ya Ze Jiwe..
H Baba akisanukisha...
Ma-Member.
Katika Ming'aro ya kukwaitika... Supa Dadaz.
Diamond...
H. baba
The Platnum along side shosti.
Meza ndefu.
Sisters.com
Ze nyomi.
Together we can...
Mie, Kabago na Stoper.
Round table ya wadau.
WochaZz!
Ni maraha ya kwanza kabisa ya Kiwanja kilicho On 'New Stone Club' yaliyofana, ngoma iliyopigwa Ijumaa ya tarehe 30 Sept 2011 nakupendeza ile NOWMAaaa!!.