ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

Saturday, January 16, 2016

MWILI WA MWANAFUNZI ALIYE SOMBWA NA MAFURIKO MWANZA WAPATIKANA.

Askari wa jeshi la polisi mkoa wa Mwanza wakitoka eneo la  Kamanga Feri jijini hapa, huku wakiwa wameubeba mwili wa mtoto Janeth James (6), mwanafunzi wa darasa la kwanza shule ya msingi Mabatini uliopatikana mara baada ya wavuvi kuuona ukielea kando kando ya ziwa Victoria eneo la Kamanga Feri. 
Juzi Marehemu Janeth alisombwa na maji wakati akivuka eneo dogo la mfereji unaotiririsha maji na kuingia mto mirongo na maji yake kuelekea Ziwa Victoria, wakati akiwa ameongozana na baba yake mzazi kutoka shule ambako ilikuwa ni mara yake ya kwanza kuhudhuria mara baada ya kujiandikisha.

Wavuvi hao wanaeleza kuwa waliuona mwili wa mtoto huyo ukielea, na kutokana na taarifa za kuzama kwake walizozipata kutoka kwenye vyombo vya habari mbalimbali jijini Mwanza ikiwemo Jembe Fm, pamoja na taarifa za wasimamizi wao kibiashara kwenye mwalo huo nao hawakusita kutoa taarifa haraka kwa jeshi la polisi kwaajili ya hatua zaidi.
Licha ya jitihada kubwa za wananchi na majirani wenye mapenzi mema kuhakikisha kuwa mtoto huyo anapatikana mapema tangu siku alipo sombwa na maji na kuzama kufuatia mvua kubwa zinazoendelea kunyesha, lakini juhudi hizo ziligonga mwamba hatimaye leo ikiwa ni siku ya tatu mwili wa mtoto huyo unaibuka kando kando ya Ziwa Victoria.

TCRA YAVIFUNGIA VITUO 21 VYA RADIO NA 6 VYA TELEVISION KWA MUDA WA MIEZI 3 KUANZIA JUMATATU TAREHE 18

TCRA yavifungia vituo 21 vya Radio na 6 vya Television kwa muda wa miezi 3 kuanzia Jumatatu tarehe 18.
NI VITUO VIFUATAVYO>-
1. Sibuka fm 2. Breez fm 3. Country fm 4. Ebony fm 5. Hot fm 6. Impact fm 7. Iringa manicipal Tv 8. Kiss fm 9. Kitulo fm 10. Kifimbo fm 11. Mbeya city municipal Tv 12. Radio 5 13. Radio free Afrika 14. Musa Television network 15. Pride fm radio 16. Radio huruma 17. Radio uhuru 18. Star Tv 19. Rock fm radio 20. Standard fm radio 21. Sumbawanga municipal Tv 22. Tanga City Tv 23. Top radio fm limited 24. Ulanga fm

Vituo hivi vimefungiwa kutoa huduma kwa muda wa miezi 3 kwa sababu ya kutolipa ada/kodi
Mwezi July 2015 ilitolewa taarifa kwa umma na TCRA kwamba baadhi ya radio na Televisheni zipatazo 40 zinadaiwa ada na tozo mbalimbali.
Septemba 28 vyombo hivyo vikapewa onyo la mwisho kwamba hadi Tar 31 dec wawe wamelipa ada zao ambapo wengine walilipa Jan 4. Wengine wakakausha.
Kwa mujibu wa sheria unapokua hujalipa kodi TCRA wanakuchukulia kuwa wewe hu exist.
TCRA wanasema hata miezi 3 ya adhabu ikiisha na bado haujalipa further actions kama kunyang'anywa leseni kunaweza kutokea.
Ni vituo 11 tu kati ya vituo vilivyokuwa vinadawa na mamlaka vilitii.
Sasa basi TCRA wanasema kuanzia Jumatatu tar 18, Radio 21 na TV 6, vituo hivi havitatakiwa kuwa hewani kufanya kazi kutokana na tamko la mkurugenzi wa TCRA

MAMANTILIE MWANZA WAPEWA SIKU 3 KUFANYA MAREKEBISHO MAENEO YAO YA HUDUMA ZA CHAKULA.

Mama na baba lishe Mwanza wapewa siku 3 kufanya marekebisho katika maeneo wanayotolea huduma zao za chakula.

WAFANYAKAZI WAANDAMANA KILOMETA 3 KUMFUATA WAZIRI KITWANGA KUMUELEZA KERO YAO MISUNGWI

Baadhi ya wafanyakazi wa Kiwanda cha kuzalisha kokoto na mawe cha Kampuni ya Nyanza Road Ltd kilichopo kijiji cha Nyang'homango Kata ya Usagara Wilaya ya Misungwi mkoani Mwanza wakiwa kwenye maandamano ya kukimbia kilometa 3 ili kwenda kumuona Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Charles Kitwanga (Mbunge wa Jimbo la Misungwi) kwenye mkutano wa hadhara na wananchi uliokuwa ukifanyika Katani humo.
Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Charles Kitwanga(kulia) mbaye ni Mbunge wa jimbo la Misungwi(CCM),akimtaka Kaimu Afisa Ardhi wa Wilaya ya Misungwi, Julius Karumuna (kushoto) kutoa majibu kwa wananchi na wenyeviti wa vijiji vitano vya Kata ya Usagara kufatia kulalamikiwa kuvamia na kupima maeneo ya mashamba yao bila kuwashirikisha kisha kuwagawia wawekezaji, Kitwanga alipoga stop maafisa ardhi kupima bila kutoa taarifa na kuwashirikisha viongozi na wananchi husika.
Sehemu ya wafanyakazi wa Kiwanda cha kuzalisha kokoto na mawe cha Kampuni ya Nyanza Road Ltd kilichopo kijiji cha Nyang'homango Kata ya Usagara Wilaya ya Misungwi mkoani Mwanza wakiwa na mabango kwenye mkutano wa hadhara wa Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Charles Kitwanga, katani humo wakiomba awasaidie walipwe mapunjo ya mishahara na kueleza unyanyasaji wanaofanyiwa na uongozi wa kiwanda hicho.
PETER FABIAN, MISUNGWI.
 
WAFANYAKAZI zaidi ya 50 wa Kiwanda cha kuzalisha kokoto cha Kampuni ya Nyanza Road Ltd cha Jijini Mwanza juzi wameandamana umbali wa kilometa 3 kwenda Usagara kuonana na Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Charels Kitwanga ambaye ni Mbunge wa Jimbo la Misungwi wakipinga unanyasaji wanaofanyiwa na uongozi wa Kiwanda hicho.
 
Wafanyakazi hao waliokuwa wakiimba nyimbo mbalimbali za “tumechoka, tunataka haki zetu, Kitwanga mwambie Tingatinga wetu na Jembe letu Rais Dk John Magufuli atuokoe tumechoka , tumechoka kunyanyaswa watulipe mishahara na kutupatia mikataba ya ajira, wakiwa wanakimbia misili ya mchakamchaka shuleni.
 
Mmoja ya wafanyakazi hao ambaye hakutaka jina lake kuanikwa kwa kuhofia usumbufu na kufukuzwa kibarua, alisema kwamba wameamua kufuata Waziri Kitwanga ambaye pia ni Mbunge wao baada ya kusikia kuwa atakuwa na mkutano na wananchi wa Kata ya Usagara kwenye hadhara.
 
“Tumetoka kijiji cha Nyang’homango kilometa 3 kilipo Kiwanda cha kuzalisha Kokoto na lengo  nataka kumueleza na atufikishie ujumbe kwa Rais Dk Magufuli na kwa Waziri wa Kazi na Ajira, Jenista Mhagama kuwa Kampuni hii inatunyanyasa na imekuwa ikikiuka sheria na taratibu za ajira kwa kushindwa kutoa mikataba, kuwapunja mishahara, kufukuzwa, kunyimwa likizo na kutolewa lugha za matusi pamoja na kunyimwa usafiri.
 
Akiwa katika mkutano na wananchi wa Kata ya Usagara, Kitwanga aliona vijana wakiwa na sale za kiwanda wakiwa na mabango yenye ujumbe mbalimbali na kuomba askari polisi kuwaruhusu ili kufika eneo la mkutano na kasha kumuomba mmoja wao kusema kero yao ambapo baada ya kuelezwa huku  wananchi wakishangilia.
 
Kitwanga aliwaeleza kuwa amepokea malalamiko hayo na kuwaahidi kushughulikia suala hilo ambapo aliwataka vijana hao kurejea kazini na kwamba Januari 23 mwaka huu atakutana na Uongozi wa Kiwanda hicho pamoja na Mkurugenzi wa Kampuni ya Nyanza Road wakiwepo wafanyakazi hao ili kulimaliza suala hilo.

WAZIRI KITWANGA AWAPIGA STOP MAAFISA ARDHI KUVAMIA NA KUPIMA MAENEO YA WANANCHI WILAYANI MISUNGWI

Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Charles Kitwanga ambaye ni Mbunge wa jimbo la Misungwi(CCM), akizungumza na wananchi kwenye mkutano wa hadhara katika Kata ya Usagara kusikiliza kero na changamoto zilizopo pamoja na kutoa ufafanuzi wa matatizo yao.
Na PETER FABIAN, MISUNGWI.
WAZIRI wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Charles Kitwnga ambaye pia ni Mbunge wa Jimbo la Misungwi amewapiga stop Maafisa Ardhi kwenda kwenye Vitongoji, Vijiji na Kata kuvamia na kupima maeneo bila kuwashirikisha viongozi na wamiliki wa maeneo hayo wilayani Misungwi mkoani Mwanza.
Kauli hiyo ameitoa juzi kwenye mkutano wa hadhara na wananchi wa Kata ya Usagara waliomuomba kusikiliza kero zao ambazo alikubali na kuagiza Mkurugenzi wa Halmashauri na wataalamu wa Idara zote kuhudhulia mkutano huo ili kutoa ufafanuzi na majibu ya kero na hoja mbalimbali za wananchi.
Kitwanga kwanza aliwataka wananchi hao kuwa huru kumuelezea kero zao ili kuwezesha watalamu wa Halmashauri akiwemo nay eye kuanza kuzitolea ufafanuzi na majibu ambapo Mariam Makwaya mkazi wa kijiji cha Sanjo alihoji lini vijiji vya Sanjo na Usagara vitapatiwa maji safi na salama. 

Huku Samwel Malongo akiwatuhumu maafisa ardhi kuvamia kwa kufika katika mashamba yao na kuanza kupima viwanja bila kuwashirikisha na kuwapa taarifa ambapo wamekuwa wakija na watu ambao huwatambulisha kuwa Wawekezaji jambo ambalo limeonekana kulalamikiwa na wananchi wengi .
Kitwanga  alimwomba Kaimu Afisa Ardhi aliyekuwepo katika mkutano huo, Julius Karumuna, kujibu hoja hiyo na alipoanza kujibu wananchi walidai wamefanya hivyo bila kuwashirikisha na hatua ambayo wenyeviti wa vijiji vitano nao waliunga mkono na kudai kuwa husikia tu tayari wakiendelea na upimaji.
Kitwanga alisimama na kumwamuru Kaimu Mkurugenzi wa Halmashauri hiyo, Lucas Kulliani na Kaimu Afisa Ardhi, Karumuna kuacha mara moja kuvamia na kupima mashamba ya wananchi kwa kisingizio cha wawekezaji bila kuwashirikisha wananchi ikiwemo kuwalipa fidia inayostahiki kabla ya kuwagawia wawekezaji.
“Kuanzia leo hii ni marufuku kwenda kwenye maeneo na mashamba ya wananchi na kuanza kupima viwanja kwa kisingizio cha kuwagawia Wawekezaji lakini hebu wapeni taarifa viongozi wa vitongoji, vijiji na Kata pia muwashirikishe wenye maeneo yao kabla ya kufanya upimaji mkikubaliana basi mwendelee na uwepo ushahidi,”alisema.
Kitwanga aliahidi wananchi hao kuwa mradi mkubwa na wa uhakika wa maji safi na salama utatekelezwa kama ilivyoahidiwa na Rais Dk  John Magufuli, wakati wa kampeni  katika Mji wa Misungwi ambapo utafika hadi Kata ya Usagara, lakini pia amewataka wananchi kuendelea kumpatia ushirikiano ili kutekeleza ahadi zake na Ilani ya CCM kwa wao pia kuhudhulia mikutano ya Mbunge na Madiwani.

BOSI WA MAMLAKA YA ANGA ASIMAMISHWA KAZI, SERIKALI YASIMAMISHA UMILIKI MASHAMBA YA KATANI TANGA.

Bosi wa mamlaka ya anga asimamishwa kazi, Serikali yafuta umiliki wa mashamba ya katani Tanga. Pata dondoo za magazeti ya leo hapa.

Friday, January 15, 2016

NAIBU WAZIRI WA WIZARA YA MAMBO YA NDANI YA NCHI ATEMBELEA MAMLAKA YA VITAMBULISHO VYA TAIFA (NIDA)

Naibu Waziri wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi,Hamad Masauni (kushoto), akiongozana  na Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Vitambulisho vya Taifa(NIDA),Dickson Maimu (kulia), wakati wa ziara ya kutembelea moja ya ofisi za mamlaka hiyo,iliyopo barabara ya Ali Hassani Mwinyi,jijini Dar es Salaam. Naibu Waziri aliweza kupata fursa ya kuangalia jinsi utengenezaji wa kitambulisho cha Utaifa unavyofanyika.
Naibu Waziri wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi,Hamad Masauni, akiwa katika kikao na viongozi mbalimbali wa Vitengo vya Mamlaka ya Vitambulisho vya Taifa(NIDA),wakati wa ziara iliyoanzia Makao Makuu ya Mamlaka hiyo,jijini Dar es Salaam.Wa kwanza kulia ni Mkurugenzi Mkuu wa mamlaka hiyo, Dickson Maimu.
Afisa Msajili wa Mamlaka ya Vitambulisho vya Taifa(NIDA), Emmanuel Joshua(kushoto), akitoa maelezo jinsi taarifa za muombaji wa kitambulisho cha Taifa zinavyohakikiwa kwa Naibu Waziri wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi,Hamad Masauni(katikati),wakati wa ziara ya Naibu Waziri kwenye mamlaka hiyo,jijini Dar es Salaam.
(Picha zote na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi)

Imeandaliwa na Kitengo cha Mawasiliano Serikalini-Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi

MFAHAMU NABII EMMANUEL MAGAYA.


Je waijua ardhi takatifu inayofanya ukombozi na kuvunja nguvu za giza na kukuacha huru kupitia jina la Yesu? Jionee ukombozi hapa

Panapo mkono wa Bwana umbali hauwezi kuzua mkono wake kutenda maajabu, Shuhudia Nabii Magaya akiwafungua waliofungwa kwa njia ya simu. 

POLISI MKOANI PWANI YAPIGA MARUFUKU WANANCHI KUKESHA KWENYE VILABU VYA POMBE

NA VICTOR MASANGU,  PWANI
KATIKA kukabiliana na wimbi la uharifu Jeshi la Polisi Mkoa wa Pwani limepiga marufuku kwa watu wenye tabia ya kukesha katika vilabu vya pombe usiku kucha, na kucheza pool kuanzia asubuhi mpaka usiku wa manane ,hali ambayo  ndio imekuwa ikichangia kwa kiasi kikubwa kuwepo kwa vitendo vya wizi, unyang’anyi pamoja na ujambazi.
 Akizungumza na waandishi wa habari  ofisini kwake kuhusiana na mikakati waliyojiwekea katika kupambana na uharifu Kamanda wa Polis Mkoa wa Pwani kamishina msaidizi Boniventura Mushongi amesema kwamba kwa sasa wameanza kufanya msako mkali katika maeneo ya Mkoa wa Pwani ya kuwasaka watu ambao wanajihusiha na vitendo vya ujambazi.
Kamanda Mushongi alisema  kwamba  tabia ya baadhi ya watu kukesha katika maeneo hayo ya  vilabu vya pombe  wamebaini wanajihusisha na uchezaji wa kamali, uuzaji wa  bangi hivyo kupelekea kufanya matukio ya uporaji  wa mali za watu katika nyakati hizo za usiku kwa wapiti njia na wale ambao wamekwisha pumzika majumbani kwao
"Jamani waandishi kwa sasa sisi kama jeshi la polisi Mkoa wa Pwani tumejipanga vilivyo na tutafanya msako katika maeneo mbali mbali yote hii ni kuhakikisha wimbi la uharifu linapungua na kwa sasa hatutaki kuona watu wanakesha baa kwani wao ndio chanzo vha kusababbisha kutokea kwa uharifu,”
“Maana kuna baadhi ya watu wanakesha katika vilabu vya pombe kumbe wengine wanavuta muda wa usiku ndipo waanza kufanya matukio yao ya uharifu kwa hiyo hatutakio kuona mtu yoyote anashinda katika vilabu hivyo sambamba na kucheza pool kuanzia asubuhi mpaka saa nane za siku ni marufuku kwanza ni kinyume cha sheria na taratibu ,”alisema Kamanda.
Aidha Kamanda huyo aliwataka wananchi wa Mkoa wa Pwani kwa kushirikiana na wazazi kkuachana na uwogo na badala yake sasa wahakikishe wanashirikiana na jeshi la polisi katika kuwafichua wahalifu bila ya kuwa na uwoga wowote na pindi watakapoona wana mashaka na mtu watoe taarifa katika vyombo husika.
Katika hatua nyingine Kamanda huyo alibainisha, sababu nyingine zinazochangia kwa kisi kikubwa kutokea kwa  wimbi la uharifu ni kutokana na baadhi ya watu kunywa ombe kupita kiasi pamoja na madereva wa pikipiki kushirikiana na waharifu katika kufanya matukio hayo ya uporaji.
 Kufuatia kaluli hiyo iliyotolewa na Kamanda wa Polisi Mkoa wa Pwani Tanzania daima iliweza kuzungumza na baadhi ya madereva wa pikipiki akiwemo Hussen Ally pamoja na Nassoro Bala ambao walisema kwamba  kuna baadhi ya madereva wa pikipiki wanavunja sheri kwa makusudi ikiwemo kunywa pombe wakati wanaendesha chombo cha moto.
Walisema kwamba wakati mwingine matukio ya uharifu yanajitokeza bila ya wao kujua kwani wakati mwingine wanaweza kupakia abiria zaidi ya mmoja kumbe wote waliopanda ni waharifu na matokeo yake wanapofika njiani wanaipora pikipiki hiyo na kumjeruhi dereva au wakati mwingine wanaamua kumuuwa.
Hata hivyo uchunguzi uliofanyuwa na Mwandishi wa habari hizi  uliweza kubaini katika Mkoa wa Pwani kwa sasa bado unakabiliwa na wimbi la uharifu kutokana na baadhi ya vijana wengi wa mitaani kutokuwa na kazi hivyo kujiingiza katika uharifu hali ambayo imekuwa ni tishio sana kwa wananchi  hasa katika eneo la maili moja , lililopo Wilaya ya Kibaha, pamoja na eneo la Kiluvya  lililopo Wilaya ya Kisarawe hivyo kuhahitajika juhudi za makusudi kwa jeshi la  polisi kukabiliana na hali  hii.

SASA NI ZAMU YA MIUNDO MBINU.

Waziri mkuu Mhe. Kassim Majaliwa amewataka watanzania kujikita katika kuimarisha miundombinu ili kukuza uchumi wa nchi.

Thursday, January 14, 2016

WIZARA YA NISHATI NA MADINI YATOA UFAFANUZI MRADI WA UMEME WA KINYEREZI II

Mkuu wa Mawasiliano Serikalini, Wizara ya Nishati na Madini, Badra Masoud, akizungumza na waandishi wa habari, Dar es Salaam, wakati alipokuwa akitoa ufafanuzi kuhusu mradi wa umeme wa Kinyerezi Awamu ya Pili, akielezea kuhusu habari zilizoandikwa kimakosa katika moja ya magazeti ya kila siku nchini jijini leo. Kulia ni Ofisa Habari Mwandamizi wa Idara ya Habari-Maelezo, Magreth Kinabo. (Picha na Kassim Mbarouk-www.bayana.blogspot.com)


Na Nyakongo Manyama- MAELEZO
14/01/2016
WIZARA ya Nishati na Madini  imekanusha habari iliyopotosha umma kuhusu   mradi wa umeme wa Kinyerezi II kuwa bado haujaanza na gharama zilizoandikwa si za kweli.

Wizara hiyo imekanusha habari hiyo, iliyoandikwa katika gazeti la Mtanzania la leo Januari 14, mwaka huu toleo namba8063,  lenye kichwa cha habari “ Harufu ya Jibu Mradi wa Umeme.”

Habari hiyo  ambayo ilieleza kwamba mradi huo ulizinduliwa na Rais Mstaafu wa  Serikali ya Awamu ya Nne, Mhe. Dkt.Jakaya Kikwete uligharimu Sh. trilioni 1.6 na kwamba fedha za ujenzi wa mradi huo zimetokana ubia kati ya Serikali ya Tanzania na Japan,ambapo Serikali ya Tanzania itakuwa na hisa ya asilimia 40 na kampuni ya SUMITOMO ya Japan asilimia 60. 

 Aidha habari hiyo ilidai kuwa Serikali inachangia fedha za ndani kwa asilimia 12 na zilizobaki zikiwa na mkopo kutoka benki ya Japan na kwamba gharama za mradi huo ziko juu ikilinganishwa miradi mingine akitolea mfano Kampuni ya TALLAWARA Power Station ya nchini Australia anayodai ilitaka kujenga mradi huo kwa dola za Marekani milioni 350.

Hayo yamesemwa leo na  Mkuu wa Mawasiliano Serikali  wa wizara hiyo,  Badra  Masoud alipokuwa akizungumza  na waandishi wa habari kuhusu habari hiyo katika ukumbi wa Idara ya Habari (MAELEZO) jijini Dar es Salaam. 

“Serikali  ya Tanzania  iliingia makubaliano na Serikali ya Japan  ya mkopo wa masharti nafuu  wa dola za Marekani  milioni 292  kwa ajili ya kutekeleza mradi wa  kuzalisha umeme wa Megawati 240 utakaojengwa na kampuni ya SUMITOMO kama mkandarasi wa “EPC contractor” na sio kama mbia wa Serikali yaTanzania kama ilivyodaiwa.

“Mradi huo unamilikiwa na Serikali kwa asilimia 100 kupitia TANESCO  na hakuna mwekezaji mwingine katika mradi huo.Hivyo si kweli kwamba Serikali ya Tanzania na kampuni ya SUMITOMO zinawekeza kwa ubia wa asilimia 40 (kwa Serikali ya Tanzania) na asilimia 60 kwa SUMITOMO. Kwa maana hiyo, hatutauziwa umeme utakaozalishwa na mradi huu kwani ni mali yetu na hakuna gharama yoyote ya ziada kama alivyodai mwandishi wa habari hiyo,” alisema Badra.

Aidha Badra alisema mwandishi huyo alidai kwamba mradi huo ulizinduliwa na Rais wa  Serikali ya Awamu ya Nne Mhe. Dkt. Jakaya Kikwete, wakati ni  kwamba mradi huo haujazinduliwa bado na sasa upo katika maandalizi ya kuwekwa katika jiwe la  msingi.

 Akizungumzia kuhusu gharama za mradi huo, alieleza kuwa unatekelezwa kwa dola za Marekani milioni 344 sawa na Sh. bilioni 740 zikiwa ni mkopo wa masharti nafuu wa asilimia 85 sawa  na dola za Marekani 292 na mchango wa Serikali ya Tanzania kwa asilimia 15 sawa na dola za Marekani milioni 52 na sio asilimia 12 kama ilivyodaiwa na mwandishi huyo. 
“Mwandishi wa habari hii amejaribu kufananisha uwekezaji huu na uwekezaji wa TALLAWARA Power Station ya Australia na kudai kwamba gharama yake ingekuwa ndogo kuliko gharama ya mradi huu. 

Taarifa hii haina ukweli wowote kwa sababu gharama ya dola milioni 344 zinazotarajiwa kutumika mkatika mradi huu iko chini kuliko dola milioni 350anazodai mwandishi kwamba zingetumiwa na kampuni TALLAWARA.

“Aidha, kampuni ya TALLAWARA haijawahi kuomba au kuonesha nia ya kuwekeza katika mradi wowote wa kufua mradi wa umeme nchini. Pia ni muhimu ifahamike kwamba makubaliano ya mkopo huu yalikuwa yanakwenda sambasamba na utekelezaji wa mradi wenyewe (EPC with Financing).  
   
Badra aliongeza kwamba pamoja na kwamba gharama za uwekezaji wa mradi huo wa kwanza wa aina ya “Combined Cycle” nchini zinawiana na gharama za miradi mingine ya aina hiyo duniani, gharama za uwekezaji zinaweza kutofautiana kutegemeana na mazingira ya nchi na nchi, teknolojia iliyotumika na aina ya mitambo.

Hivyo sio suala la kulinganisha gharama ya mradi mmoja na mwingine.

Wizara hiyo imeshauri waandishi wa habari kufuata miiko na maadili ya uandishi wa habari kwa kuandika habari  zenye ukweli na sahihi na zilizozingatia pande zote mbili kwa kuwa ipo na tayari kujibu maswali ya waandishi wakati wowote.

MVUA YAUA MTOTO JIJINI MWANZA: HALI TETE KWA BARABARA ZA MWANZA

Mvua kubwa iliyonyesha kwa zaidi ya saa nne jijini hapa leo, imesababisha kifo cha mwanafunzi na uharibifu wa mali zenye thamani ya mamilioni ya fedha.

Wananchi wamedai kuwa mvua hiyo, iliyonyesha kuanzia saa 4:00 asubuhi hadi saa 9:00 alasiri, haijawahi kushuhudiwa kwa kipindi cha zaidi ya miaka minne iliyopita.

Mwenyekiti wa Mtaa wa Mabatini, Ntobi Ntobi pamoja na kaimu kamanda wa kikosi cha Zimamoto jijini Mwanza, Hamidu Nguya walithibitisha kutokea kwa kifo cha mtoto huyo, Jenipher Joseph (6), aliyekuwa mwanafunzi wa Shule ya Msingi Mabatini.

Kamanda Nguya alisema mtoto huyo alisombwa na maji na baba yake, James Joseph walipoteleza na kuangukia mtoni wakati wakivuka daraja la Mto Mirongo uliokuwa umefurika.

Mvua Yauwa Mtoto 1 Mwanza

Fuatilia taarifa hii iliyoandaliwa na Star TV. Mwanza.


Mkazi wa Mabatini jijini Mwanza akijiokoa kwa
Mkazi wa Mabatini jijini Mwanza akijiokoa kwa kupanda juu ya bati, baada ya eneo lao kukumbwa na mafuriko ya maji kutokana na mvua iliyonyesha jana jijini humo.  Picha na Michael Jamson.
Huku wengine wakivuka katika eneo la daraja maarufu kama Daraja la Wakoma lililopo barabara ya uhuru wilayani Nyamagana jijini hapa, Kikosi cha Zimamoto na Uokoaji pamoja na wadau wa Idara ya maji safi na maji taka Mwanza MWAUWASA wanaendelea na juhudi ya msaka mtoto aliyezama.
Miongoni mwa waliopoteza mali ni pamoja na Juma Said, mmiliki wa duka la vifaa vya shule na ofisi zenye thamani ya zaidi ya Sh7.5 milioni.

Licha ya ubovu wa miundombinu, eneo la Mabatini hukumbwa na mafuriko ya mara kwa mara kutokana na ujenzi holela uliobana kingo za Mto Mirongo.

Hadi saa wakati tunatoka eneo la tukio, Kikosi cha Zimamoto na Uokoaji kilikuwa kikiendelea na juhudi za uokoaji na kutafuta miili ya watu wanaodhaniwa kuwa wamesombwa na mafuriko hayo.


Huu mchanga na tope umejikita hapa na kusababisha barabara kupitia kwa shida.
Kingine ambacho kimekuwa changamoto kubwa kwa watendaji wa sekta mbalimbali za uokoaji ni suala la ukosefu wa vitendea kazi., hakukuwa na vitendea kazi madhubuti vya uokoaji zaidi ya fimbo na miti kwaajili ya kuzibua taka zinazojikita kwenye kingo za daraja hilo.
Hali tete juhudi zimekwama.....
Mitaani nako si salama.

AIRTEL YAZINDUA DUKA LA KISASA JIJINI DAR ES SALAAM.

Afisa huduma kwa wateja wa Airtel, Deogratius Gerald,(wakwanza kulia) akimuonyesha Naibu Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi, na Mawailiano Eng, Edwin Ngonyani jinsi ya kupata taarifa kuhusu huduma mbalimbali za Airtel kupitia komputa zilizoweka katika duka jipya la Airtel Expo wakati wa uzinduzi  rasmi wa duka hilo jana katika ofisi za makao makuu ya Airtel jijini Dar es Salaam. Akishuhudia ni Mkurugenzi Mkuu wa Airtel Bwn Sunil Colaso (nyuma katikati) na Meneja huduma kwa wateja bi, Zakia Omary
Naibu Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi, na Mawailiano Eng, Edwin Ngonyani akiongea wakati wa uzinduzi wa duka jipya la kisasa la Airtel Expo lililopo katika makao makuu ya Airtel Morocco, jijini Dar es Saalam. Pichani ni Mkurugenzi Mkuu wa Airtel Bwn Sunil Colaso akifatiwa na Mkurugenzi wa mawasilino wa Airtel Bi Beatrice Singano Mallya
Naibu Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi, na Mawailiano Eng, Edwin Ngonyani akiongea na waandishi wa habari wakati wa uzinduzi wa duka jipya la kisasa la Airtel Expo lililopo katika makao makuu ya Airtel Morocco,jijini Dar es Saalam.
Naibu Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi, na Mawailiano Eng, Edwin Ngonyani pamoja na mkurugenzi mkuu wa Airtel kwa pamoja wakibonyesha kitufe kuashiria uzinduzi wa duka la Airtel Expo lililopo makao makuu ya Airtel jijini Dar es salaam
Shamrashamra za uzinduzi wa duka la Airtel Expo Morocco, jijini Dar es Saalam
Afisa huduma kwa wateja wa Airtel, Deogratius Gerald,(kwanza kushoto) akimuonyeshaNaibu Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi, na Mawailiano Eng, Edwin Ngonyani vifaa  na simu mbalimbali vinavyopatikana  katika duka jipya la Airtel Expo wakati wa uzinduzi  rasmi wa duka hilo jana katika ofisi za makao makuu ya Airtel  Morocco, jijini Dar es Salaam. Akishuhudia ni Mkurugenzi Mkuu wa Airtel Bwn Sunil Colaso (wa kwanza kulia) akifatiwa  na Meneja huduma kwa wateja bi, Zakia Omary
Airtel yazindua Duka la kisasa jijini Dar es saalam

·    Ni duka lenye muundo na mazingira ya kisasa
Dar es Salaam Alhamisi Januari 14, 2016, Kampuni ya simu za mkononi ya Airtel leo imezindua duka la kisasa jijini Dar es Salaam ikiwa ni mwendelezo wa kutanua wigo wa kutoa huduma zenye ubora tofauti na bidhaa za kibunifu kwa wateja wake

Duka hilo la kisasa liko katika ofisi za makao makuu ya Airtel barabara ya Moroco

Akiongea wakati wa hafla ya uzinduzi Mkurugenzi Mkuu wa Airtel, Sunil Colaso alisema” Tunayodhamira ya kuwa karibu na wateja wetu ili kuwapatia huduma bora zinazokidhi mahitaji yao.  duka letu jipya tulilolizindua leo litakuwa na sehemu maalumu itakayowawezesha wateja wetu kuona bidhaa bora za mawasiliano zikiwemo simu za aina tofuati na kupata nafasi ya kuzijaribu kwanza ili kuona ubora wake na kufanya chaguo la ununuzi. tunaamini wateja wetu sasa wateweza kufurahia huduma zetu kwa kuwa watapata nafasi ya kuchagua aina ya kifaa au simu wanayomudu kuitumia kwa urahisi zaidi”.

“Duka letu la Airtel Expo litakuwa ni sehemu ya maonyesho na ubunifu kwa wateja wale wanaopenda kuishi maisha yanayoendana na technolojia ya kisasa ndani ya sekta ya mawasiliano. Kila atakaetembelea duka hili atafurahia huduma za haraka toka kwa watoa huduma wetu ambao watatatua mahitaji na matatizo yao katika mazingira ya kirafiki zaidi” alieleza Colaso

Akizindua duka hilo, Naibu Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi, na Mawailiano Eng, Edwin Ngonyani alisema “Ninawapongeza sana Airtel kwa kutengeneza duka hili la kisasa na kibunifu litalorahisisha utoaji huduma kwa wateja na watumiaji wa huduma za mawasiliano na kuchochea matumizi ya  technologia ya mawasiliano katika kuendesha shughuli mbalimbali za kijamii na kiuchumi ”

“Natoa wito kwa wakazi wa Dar es saalam na wateja wa Airtel kutembelea duka hili na kufurahia mazingira bora na kuunganishwa na huduma za kifedha na huduma zote za mawasiliano nilizoziona hapa. alimaliza kwa kusema Mh, Ngonyani

Kwa upande wake, Mkuu wa kitengo cha huduma kwa wateja , Adriana Lyamba alisema “Duka letu litakuwa linatoa huduma kuanzia Jumatatu hadi Ijumaa muda saa 3 hadi saa 11 jioni na Jumamosi kuanzia saa 3 hadi saa 7 mchana. Huduma zote muhimu kama Airtel Money, huduma ya intanet, bidhaa za kisasa kwa Intaneti na  vifaa vya Wi-Fi yaani (Home Wi-Fi)  pamoja simu za smartphone za vitapatikana katika duka letu.”

Adriana aliongeza kwa kusema Duka letu la Airtel Expo lina sehemu maalumu kwa ajili ya kuwahudumia wateja watu maalum yaani (Airtel Premeir Custumers)ambapo mteja anaweza kupitia na kusaini mikataba wake au kulipia ankra yake, kurudisha namba iliyopotea, huduma za Airtel Money na nyingine nyingi zitatolewa.”

Kuzindulia kwa duka hili ni muendelezo wa kutimiza dhamira na mkakati wa Airtel wa sasa wa kukamilisha maduka 28 yanayoendelea kutengenezwa na kuzinduliwa nchi nzima hadi ifikapo  Juni mwaka huu.


WAZEE,VIONGOZI WA DINI,WAGANGA WA JADI NA WALEMAVU WAKUTANA NA MZINDAKAYA.

Na Shushu Joel,Busega.
MKUU wa wilaya ya Busega , Mkoana Simiyu Paul Mzindakaya amewataka wananchi wake wa Busega kuweza kuwa mfano wa kuigwa hapa nchini katika suala zima la kupiga hatua katika maendeleo ili  waweze   kujiongezea   kipato katika maisha yao na familia zao.

Hayo yamezungumzwa kwenye kikao chake cha mwanzo wa mwaka na wazee na waganga wa jadi viongozi wa dini  na walemavu wilayani humo, kikao hicho kilikuwa na malengo ya kutatua changamoto mbalimbali zikiwemo changamoto zao zinazowakabili watu hao katika utendaji wa shughuli zao ndani na nje ya wilaya hiyo.

Mkuu huyo wa wilaiya hiyo aliqwataka wazee,waganga wa jadi na walemavu wa aina zote kutoteteleka katika kazi zao kwani sasa ni hivi ni kipindi cha hapa kazi tu ambayo ni kauli mbiu ya Rais wetu inazidi kuwa na kasi ya pekee kwa watanzania, hivyo wale wasiojishughulisha na kazi watakuwa awawezi kuendana na kasi ya wilaya yetu.

Aliongeza kuwa anawataka wazee na viongozi wa dini na wengine ambao ni wakuu wa familiakuweza kuwa wasemaji wakuu kwa vijana wetu ambao wanaonekana kuwa ni gumzo katika jamii yetu hasa katika shughuli za maendeleo yao kwani vijana wengi wamekuwa ni wachezaji wa kamali na wacheza mapuru table kwa muda mwingi hivyo hata kujihusisha na masuala ya maendeleo yao wanashindwa nah ii ni kutokana na tama za kupata mali mapema.

Aidha amewataka vijana wote wa Busega kuweza kuunda vikundi ili Halmashauri iweze kuwapatia mikopo kwa ajili ya shughuli za maendeleo yao ili waweze kujikwamua katika maisha yao hivyo waje ofisini muda wowote ule lakini wawe na masuala ya maendeleo ili wasikae kuwa wanailaumu serikali juu ya ajirana huku wao awataki kujishighulisha na kazi za kawaida.

Kwa upande wake Mzee Petro Mabeyo(87) mkazi wa kata ya kiloleli amempongeza mkuu wa wilaya kwa kutambua umuhimu wa wazee ndani ya wilaya yake, pia tunakushukuru kwa agizo lako la kumtaka mganga mkuu anaanza mara moja kuhakikisha wazee wasiokuwa na vitambulisho vya matibabu bure wanapewa haraka sana ili nao waeze kupata huduma za bure kama wengine.

Na kwa upande wa mwakilishi wa waganga wa jadi Saimon Ndila alisema kuwa kilio chao kwa serikali ni kutokupewa lessen za kuweza kuendeshea kazi zao hivyo wamemtaka mkuu wa wilaya kuweza kuwasaidia ili waweze kupata lessen hizo alisema.

Aliongeza kuwa wanaiomba serikali kuweza kuwa na imani na waganga wa jadi kwani si wote wanaofanya kazi hiyo ni wale wanaowadanganya watu juu ya utajiri mara wapelekapo viungo vya walemavu wa ngozi na kuitaka serikali kuwa punde wanapowabaini waganga wa namna hiyo wachukuliwe hatua kali za kisheria.