ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

Saturday, January 16, 2016

WAFANYAKAZI WAANDAMANA KILOMETA 3 KUMFUATA WAZIRI KITWANGA KUMUELEZA KERO YAO MISUNGWI

Baadhi ya wafanyakazi wa Kiwanda cha kuzalisha kokoto na mawe cha Kampuni ya Nyanza Road Ltd kilichopo kijiji cha Nyang'homango Kata ya Usagara Wilaya ya Misungwi mkoani Mwanza wakiwa kwenye maandamano ya kukimbia kilometa 3 ili kwenda kumuona Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Charles Kitwanga (Mbunge wa Jimbo la Misungwi) kwenye mkutano wa hadhara na wananchi uliokuwa ukifanyika Katani humo.
Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Charles Kitwanga(kulia) mbaye ni Mbunge wa jimbo la Misungwi(CCM),akimtaka Kaimu Afisa Ardhi wa Wilaya ya Misungwi, Julius Karumuna (kushoto) kutoa majibu kwa wananchi na wenyeviti wa vijiji vitano vya Kata ya Usagara kufatia kulalamikiwa kuvamia na kupima maeneo ya mashamba yao bila kuwashirikisha kisha kuwagawia wawekezaji, Kitwanga alipoga stop maafisa ardhi kupima bila kutoa taarifa na kuwashirikisha viongozi na wananchi husika.
Sehemu ya wafanyakazi wa Kiwanda cha kuzalisha kokoto na mawe cha Kampuni ya Nyanza Road Ltd kilichopo kijiji cha Nyang'homango Kata ya Usagara Wilaya ya Misungwi mkoani Mwanza wakiwa na mabango kwenye mkutano wa hadhara wa Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Charles Kitwanga, katani humo wakiomba awasaidie walipwe mapunjo ya mishahara na kueleza unyanyasaji wanaofanyiwa na uongozi wa kiwanda hicho.
PETER FABIAN, MISUNGWI.
 
WAFANYAKAZI zaidi ya 50 wa Kiwanda cha kuzalisha kokoto cha Kampuni ya Nyanza Road Ltd cha Jijini Mwanza juzi wameandamana umbali wa kilometa 3 kwenda Usagara kuonana na Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Charels Kitwanga ambaye ni Mbunge wa Jimbo la Misungwi wakipinga unanyasaji wanaofanyiwa na uongozi wa Kiwanda hicho.
 
Wafanyakazi hao waliokuwa wakiimba nyimbo mbalimbali za “tumechoka, tunataka haki zetu, Kitwanga mwambie Tingatinga wetu na Jembe letu Rais Dk John Magufuli atuokoe tumechoka , tumechoka kunyanyaswa watulipe mishahara na kutupatia mikataba ya ajira, wakiwa wanakimbia misili ya mchakamchaka shuleni.
 
Mmoja ya wafanyakazi hao ambaye hakutaka jina lake kuanikwa kwa kuhofia usumbufu na kufukuzwa kibarua, alisema kwamba wameamua kufuata Waziri Kitwanga ambaye pia ni Mbunge wao baada ya kusikia kuwa atakuwa na mkutano na wananchi wa Kata ya Usagara kwenye hadhara.
 
“Tumetoka kijiji cha Nyang’homango kilometa 3 kilipo Kiwanda cha kuzalisha Kokoto na lengo  nataka kumueleza na atufikishie ujumbe kwa Rais Dk Magufuli na kwa Waziri wa Kazi na Ajira, Jenista Mhagama kuwa Kampuni hii inatunyanyasa na imekuwa ikikiuka sheria na taratibu za ajira kwa kushindwa kutoa mikataba, kuwapunja mishahara, kufukuzwa, kunyimwa likizo na kutolewa lugha za matusi pamoja na kunyimwa usafiri.
 
Akiwa katika mkutano na wananchi wa Kata ya Usagara, Kitwanga aliona vijana wakiwa na sale za kiwanda wakiwa na mabango yenye ujumbe mbalimbali na kuomba askari polisi kuwaruhusu ili kufika eneo la mkutano na kasha kumuomba mmoja wao kusema kero yao ambapo baada ya kuelezwa huku  wananchi wakishangilia.
 
Kitwanga aliwaeleza kuwa amepokea malalamiko hayo na kuwaahidi kushughulikia suala hilo ambapo aliwataka vijana hao kurejea kazini na kwamba Januari 23 mwaka huu atakutana na Uongozi wa Kiwanda hicho pamoja na Mkurugenzi wa Kampuni ya Nyanza Road wakiwepo wafanyakazi hao ili kulimaliza suala hilo.

Tupe maoni yako

0 comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.