|
Mbunge wa Kwimba Mansoor amepata mapokezi makubwa jimboni kwake. |
|
Akiwa ameambatana na Katibu wa mkoa wa Mwanza Bw. Miraji Mtaturu, Mbunge huyo amekabidhi kadi 1600, mifuko ya saruji 600 yenye thamani ya shilingi milioni 12 na kuviwezesha vikundi mbalimbali zaidi ya shilingi milioni 5. |
|
Mbunge wa Kwimba Mansoor akihutubia watu wa jimbo lake ambapo kubwa zaidi alizungumzia suala la kuboresha elimu na nini mikakati ya baadaye kuhusu kukamilisha miradi ya maji.. |
|
Kusanyikoni. |
|
Katibu wa mkoa wa Mwanza Bw. Miraji Mtaturu naye alipata fursa ya kuzungumza na waanci wa Jimbo la Kwimba akatia msisitizo. |
|
Wanachama wapya. |
|
Kusanyiko.PICHA ZOTE NA ZEPHANIA MANDIA |
MBUNGE MANSOOR, JIMBO LA KWIMBA LIMEBADILIKA NA KUPIGA HATUA YA MAENDELEO KWA VITENDO.
NA PETER FABIAN, KWIMBA.
MBUNGE wa Jimbo la Kwimba, Shanif Mansoor,ametamba kuwa wananchi wa jimboni humo wajivune kwa kushirikiana nae kuleta maendeleo kwa vitendo na kulibadilisha badala ya kusikiliza uzushi wa baadhi ya wapinzani wake kisiasa wanaoendekeza ukabila.
Pia amekuwa akichangia miradi ya maendeleo ambapo metoa kiasi cha shilingi milioni 17 za kutekeleza ahadi zake za maendeleo na Ilani ya Uchaguzi ya CCM kwa vitendo katika Jimbo lake.
Mansoor alikabidhi saruji mifuko 600 katika Kata za Mhande, Fukalo, Ngudu na Bupamwa kwa ajili ya kusaidia ujenzi kwenye shule za msingi, zahanati na sekondari pamoja na kuchangia fedha na vifaa vya Kompute kwenye baadhi ya sekondari na Chuo cha Afya cha Ngudu mjini.
Mbunge Mansoor akizungumza na mamia ya wananchi waliofurika kwenye mkutano wa hadhara juzi uliofanyika katika viwanja vya stendi mjini Ngudu, alisema kwamba saruji hiyo aliyoitoa katika Kata ya Bupamwa kwenye vijiji vya Dodoma, Kiliwi na itegamatwi kwa ujenzi wa vyumba vya madarasa shule za msingi.
Katika Kata ya Fukalo alitoa saruji katika vijiji vya Sanga, Msongwa, Chibuji kwa ajili ya kusaidia ujenzi wa vyumba vya madarasa katika shule za msingi, Kata ya Mhande ni kijiji cha Gurumwa kwa ajili ya kusaidia pia ujenzi wa shule ya msingi na milioni tatu kwa maabara ya sekondari na Kata ya Ngudu mjini alitoa fedha kiasi cha shilingi milioni mbili sekondari ya Bujiku Sakila na shilingi milioni moja Ngudu mjini.
Maeneo mengine aliyochangia ni Chuo cha Afya Ngudu mjini shilingi milioni 2 kwa ajili ya ujenzi wa choo na kutoa Komputa tatu(sh. 1.8 mil), kuchangia saruji mifuko 50 kanisa la Romani (RC) na mifuko 50 kanisa la Afrika Iniland Charch Tanzania (AICT) katika kijiji cha Kilyaboya na kikundi cha ujasilimali Ngudu mjini kilipata shilingi laki tano.
Mansoor aliwaeleza wananchi kuwa katika fedha hizo za kuchangia maendeleo hazihusiani na Mfuko wa Jimbo la Kwimba bali kutokana na nguvu yake kwa lengo la kuwasaidia wananchi ili kupiga hatua ya maendeleo, ambapo al katika Kata ya Ngudu mjini alichangia saruji pia vijiji vya Gudula (shule) na Chamela (jengo la Kiliniki).
“Thamani ya saruji ambayo leo nimeitoa kusaidia wananchi katika vijiji hivyo ni shilingi milioni 12 na jumla ya fedha zilizokabidhiwa ni shilingi milioni tano tasilimu hivyo hapa misaada yote imegharimu kiasi shilingi milioni 17 jambo ambalo ni la kujivunia kwa wananchi kwa kuwa na Mbunge anayetambua maendeleo,”alisema.
Mansoro alitamba kuwa kwa kipindi chake cha uwakilishi kwa wananchi amefanya mambo makubwa kusimamia ikiwemo, usambazaji umeme vijijini katika Kata, kupigania maji safi kutoka chanzo cha Ziwa Victoria cha Ihelele, Shinyanga- Kahama ambayo huduma imefika na barabara ya Hungumalwa, Ngudu-Magu kwa kiwango cha lami ambayo tayari upembuzi yakinifu utaanza hivi karibuni.
Mbunge huyo alitoa wito kwa wananchi wa Jimbo la Kwimba kumpatia ushirikiano kutekeleza yale aliyoahidi kwao na kutekeleza Ilani ya CCM kwa vitendo na kuwapuuza baadhi ya wanasiasa wachache walioanza kupitapita huku wakimchafua na kuanza kuhamasisha ukabila jambo ambalo alisema wananchi wanapashwa kutafakari na kuwataka wapinzani wake waeleze sela na hoja zitakazowashawishi kuwachagua.