Mfadhili wa michuano ya kombe la Ng'ombe ambaye pia mkurugenzi wa kampuni ya East Link Tanzania Ltd,Kim Fute wapili kutoka kushoto akibadilishana mawazo na baadhi ya vijana waliofika kushuhudia michuano hiyo ,michuano hiyo itahitimishwa mapema siku ya jumapili wiki hiii katika uwanja wa shule ya msingi Sinoni ambapo Timu ya Zamzam na Nyota watachuana(Habari picha na Pamela Mollel wa jamiiblog)
Taswira ya muonekano wa mlima Meru unavyoonekana pichani,hii ilikuwa juzi katika uwanja wa shule ya msingi Sinoni jijini Arusha
Baadhi ya wachezaji wa klabu ya Zamzam FC wakimwangalia mlinda mlango wao ,Seleman Casillas mara baada ya kuanguka na kulalamika kuua mguuni juzi katika mechi baina yao na Parrot katika kombe la Ng"ombe iliyochezwa katika uwanja wa shule ya msingi Sinoni jijini Arusha,klabu ya Zamzam ilifanikiwa kutinga fainali katika mchezo huo ambapo itakutana na Nyota siku ya jumapili
SOKA ni mchezo wa ajabu embu sikia hii mlango wa klabu ya Parot FC,Sacrifice Adam juzi alijikuta akiangua kilio uwanjani mara baada ya kushuhudiwa timu yake ikitolewa katika michuano ya kombe la ng’ombe linaloendelea kuwaka moto katika uwanja wa shule ya msingi Sinoni jijini Arusha.
Adam,aliangua kilio wakati alipokuwa akishuhudia timu yake ikiondolewa na klabu ya Zamzam FC juzi katika viwanja hivyo katika hatua ya matuta baada ya timu yake kuchapwa kwa jumla ya penati 5 kwa 4.
Hatahivyo,hapo awali Adam alifanikiwa kuokoa mipira mingi ya hatari iliyokuwa ikipigwa na washambuliaji wa klabu ya Zamzam hususani wakati timu hizom zinakkwenda kumalizia kipindi cha pili.
Kwa hatua hiyo klabu ya Zamzam sasa imefanikiwa kukata tiketi ya kuingia katika hatua ya fainali ambapo itakutana na Nyota siku ya kesho (jumapili) katika viwanja hivyo ambapo mgeni rasmi anatarajiwa kuwa mdau wa michezo jijini Arusha na mkurugenzi wa kampuni ya East Link Tanzania Ltd,Kim Fute.
Hatahivyo,jambo la kuvutia katika mechi hiyo ni pale paliposhuhudiwa watu wa kada zote wanafunzi,wanawake,wazee pamoja na watoto wadogo walipokusanyika kwa pamoja kushuhudia mchezo huo jambo lililoashiria kwamba mchezo wa soka bado unachukua nafasi ya kupendwa kwa kiasi kikubwa kupendwa tofauti na michezo mingine.
Tupe maoni yako
0 comments:
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.