Kanda ya video inayomuonyesha mtu anayedaiwa kuwa kiongozi wa kundi la Boko Haram imetolewa akikana madai ya jeshi kwamba amefariki.
Katika kanda hiyo,Abubakr Shekau anasema kuwa wapiganaji wake waliitungua ndege ya wanajeshi wa angani iliotoweka wiki tatu zilizopita.
Wiki iliopita jeshi lilidai kuwa mtu anayejionyesha katika kanda ya video ya Boko Haram aliuawa na mwezi Agosti 2013 likadai kwamba huenda Shekue amefariki.
Wachanganuzi wametilia shaka kuhusu uthabiti wa madai hayo ya jeshi.
|
Wapiganaji wa Boko Haram. |
Mwandishi wa Nigeria Ahmad Salkida ,ambaye ana mawasiliano mazuri na Boko Haram alisema kuwa katika mtandao wake wa Twitter wiki iliopita ana hakika kwamba Shekue yu buheri wa afya na kwamba hajafariki.
Haijabainika ni lini ama wapi kanda hiyo iliopatikana na shirika la habari la AFP ilitengezwa.
Lakini muhariri wa Idhaa ya BBC ya Hausa, Mansur Liman ,amesema kuwa mtu aliyezungumza katika kanda hiyo ya video alikuwa Abubakr Shekue yule yule anayeonekana katika kanda nyengine za video za kundi la Boko Haram.
CHANZO: BBC SWAHILI.