ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

Saturday, March 24, 2012

KAMPUNI YA ALLIANCE ONE TANZANIA YAWAELIMISHA WAHARIRI WA VYOMBO VYA HABARI JUU YA ZAO LA TUMBAKU

Mkurugenzi wa Alliance One Tanzania Ltd Bw. Mark Mason akizugumza katika mkutano na wahariri wa vyombo mbali mbali vya habari jijini Dar es Salaam. Mkutano huo uliandaliwa kwa ajili ya kuwapa taarifa juu ya maendeleo ya tumbaku na mambo mbali mbali wanayoyafanya katika kuisaidia jamii. Kampuni hiyo inafanya shughuli za Tumbaku huko Kinglowila, Morogoro.

Meneja Uhusiano wa Alliance One Tanzania Ltd, Bw. Hamis Liana akiwaeleza wahariri juu ya miradi mbali mbali ya kijamii inayotolewa na kampuni yao kupitia zao la tumbaku ambalo wanashughulikia huko mkoani Morogoro. Mkutano huo ulifanyika leo jijini Dar es Salaam.

Wahariri kutoka The African Bw. Shermax Ngahemera, Uhuru Bw. Damas na Bethuel Kinyori wa Corporate Digest na Meneja Uhusiano wa Silverbullet PR Nadine Kapya wakiwa katika mkutano na Alliance One Tanzania Ltd jijini Dar es Salaam.

Friday, March 23, 2012

PICHA YA WIKI

Kuelekea sokoni..

HAPPY BIRTHDAY REUBEN NDEGE, DJ BONNY LOVE & MAULID KITENGE

Mzeiyaa wa soso fresh, jamaa mwenye kipaji kinachoongea toka moyoni almaarufu kwa jina 'Ncha Kali' amezaliwa siku kama ya leo tarehe 23 march.

sIKu hii njema kwake imeangukia ijumaa ambapo mida ya night kuanzia saa nne kamili mara baada ya Sports Extra, huwa anahusika hewani na madizaini tofauti tofauti kila wiki katika Soso Fresh kupitia Radio ya watu....

jEh leo atafanya kipi cha Udiferenti????!!!!?????






Dj Bonny love, mtayarishaji wa muziki akiwa long time kwenye game, sambamba na Dj Elly Big Daddy mwalimu wangu wa mixxing', Bonny Love alinitich engo za maujanja na siri za ziada kwenye moja na mbili.

Makamu Mwenyekiti wa TASWA Maulid Kitenge ambaye vilevile yu mtangazaji wa Radio One Stereo naye leo ni siku yake.

.HAPPY BIRTHDAY 2 YOU ALL.

WAMACHINGA MWANZA WAPEWA SOMO.

James Kajugusi.
Wilaya tatu za Geita, Kwimba na Sengerema mkoani Mwanza zimeteuliwa kuingia katika mpango mahsusi wa kuwawezesha vijana wajasiriamali kupata ruzuku ya kuendesha shughuli zao.

Hayo yamebainisha katika taarifa ya mafunzo ya siku tatu ya ujasiriamali kwa wafanyabiashara ndogondogo maarufu kama wamachinga yaliyofanyika jijini Mwanza.

Kwa mujibu wa Kaimu Mkurugenzi wa Maendeleo ya Vijana katika Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo, James Kajugusi amesema kuwa katika awamu ya kwanza ni wilaya ya Magu pekee kutoka mkoani Mwanza ndiyo iliyoteuliwa kuingia katika mpango huo unaoofadhiliwa na Shirika la Kazi Duniani (ILO), lakini katika awamu hii ya pili zimeongezwa wilaya tatu.

Pia imebainishwa kuwa vijana wajasiliamali kutoka katika wilaya hizo, watapata fursa ya kuwasilisha mipango yao ya kibiashara ambayo itashindanishwa na watakaofanya vizuri watapatiwa ruzuku ya kati ya Dola 5,000 hadi 25,000 za Marekani.

Mwenyekiti wa Jumuiya ya Wamachinga jijini Mwanza, Liberatus kabaila akitoa maelezo katika siku ya kwanza muda mfupi kabla ya kuanza kwa mafunzo ya ujasiliamali yaliyowashirikisha zaidi ya wamachinga 100.

Katibu wa CCM
Vijana wakiwa ndio kundi kubwa la Watanzania wanahitaji kuhakikishiwa maisha bora kwa kupewa mafunzo ya biashara nafuu.

"Inafurahisha kuwa tayari mmejifunza namna ya kujitambua hivyo tunaamini kuwa mtafika mnapotaka" by Mkufunzi kutoka Tanzania Youth Capacity building Organization Daniel Zenda.

Aidha katika kukabiliana na suala la ukosefu wa mitaji kwa wajasiliamali, Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo nchini inakusudia kuanzisha mchakato wa kuanzisha Benki ya Taifa ya Vijana ambayo itatoa mikopo yenye masharti nafuu kwa vijana.

Thursday, March 22, 2012

ZURUZAZzzz.KOM

Vyuma chakavu dili mpaka kesho.

Kituo kidogo cha polisi Pasiansi wilaya ya Ilemela jijini Mwanza.

Mbao dugu yake gogo.

Picha ya ukutani Uwanja wa CCM Kirumba.

Ground la mpira wa kikapu.

Ekacliff Building.

JENGO LA CM PLAZA LAZINDUA TEKNOLOJIA MPYA YA KUFANYA USAFI IITWAYO ROPE ACCESS

Mkurugenzi wa kampuni ya Equilibrium Rope Access Bw. Abdulkarim Tumba akipanda juu kwa ajili ya kusafisha vioo kwa kutumia teknolojia ya Rope Access ambayo ni mpya kwa hapa nchini. Amesema kuwa ni vyema Watanzania wenye majengo wakaitumia teknolojia hii ambayo ni salama. Na leo kwa mara ya kwanza tokea teknolojia hiyo imeingia nchini Tanzania wameifanya katika Jengo la CM Plaza lililopo jijini Dar es Salaam.

...Akielekea juu kwa ajili ya kuanza kusafisha jengo hilo; ambapo usafi unafanyika kwa ustadi kabisa.

Muonekano wa jengo huku akionekana Bw. Abdulkarim Tumba akiendelea na usafi.

Hapa akiendelea na usafi ambapo haitaji vifaa vingi wala umeme na ni haraka na salama.

Jengo la CM Plaza kama linavyoonekana wakati likifanyiwa usafi.
PICHA NA Cuthbert Angelo.

KULA NGOMA TOKA MWANA WA ROCK CITY.

Ni mwanamuziki mpya kabisaaaa katika tasnia ya muziki wa kizazi kipya, long time akijihusisha na kusimamia hafla mbalimbali na sherehe kama Mc ndani ya Rock City. Baada ya watu kukiona kipaji chake hawakusita kumshauri kutinga kona hii nyingine ya maburudani, mtu mzima kafyatua kitu 'MACHEPELE'.
Muite Mc Mziwanda.
Chekshia kideo.

CHEKA VS MAUGO WAONESHWA MKANDA WA UBINGWA LEO

WAANDAAJI wa pambano la ubingwa wa IBF kati ya Francis Cheka na Mada Maugo leo Wametyambulisha rasmi mkanda huo ambao utashindaniwa Aprili 28 mwaka huu katika ukumbi wa PTA, Dar es Salaam.
Francis Cheka (kushoto) na Mada Maugo (kulia)

Pambano hilo linatarajiwa kuwa katika uzito wa kg 75 la raundi 12 la Kimataifa ambapo linatarajiwa kuwa chini ya Kamisheni ya Kamisheni ya ngumi za kulipwa Tanzania (TPBC huku majaji wa pambano hilo wakitegemewa kutoka nje ya nchi.

Akizungumza Dar es Salaam leo, Mratibu wa pambano hilo, Kaike Siraju alisema kuanikwa kwa mkanda huo kutaashiria kupamba moto kwa ambano hilo ambalo linatarajia kuwa katika ngazi ya Kimataifa ili kuweza kupatikana kwa mshindi wa halali na pia itafuta hisia za kuwepo na ubabaishaji katika pambano hilo.

Alisema, maandalizi kwa ujumla ya pambano hilo yanaendelea vizuri na zawadi ya gari kwa mshindi iko pale pale ambapo mshindi atakabidhiwa siku hio hio ya pambano baada a kutangazwa mshindi na kupewa mkanda itafuatiwa na zawadi hiyo ya gari.

Awali mabondia hao walishakutana mara mbili ulingoni ambapo katika pambano la kwanza lilofanika PTA Cheka alishinda kwa pointi ambapo Maugo hakukubali matokeo hao na kuandaliwa pambano la marudiano lilofanyika Uwanja wa Jamuhuri Morogoro ambapo Cheka aliibuka mshindi tena kwa kumtwanga kwa pointi.

Baada ya kumalizika kwa pambano hilo kila bondia aligoma kucheza na mwenzake tena lakini baada ya kuandaliwa pambano hilo la ubingwa kila mmoja alibadilisha nia na kuamua kurudi ulingoni kuwania mkanda huo. Mbali na kuwepo mapambano ya ngumi kutakuwa na uuzwaji wa DVD zenye mapambano ya mabingwa wa Dunia akiwemo Manny Paquaio, Floyd Maywherth, Roy Jones na wengine kiba DVD hizo zilizoandaliwa kwa ubora wa hali ya juu zitakuwa zikiuzwa kwenye mpambano huo na Kocha Rajabu Mhamila 'Super D', alisema kuwa kutakuwa na DVD ili kuweza kuwauzia mashabiki kwa ajili ya kujifunza Kanuni na Sheria za mchezo huo.

"Ninatarajia kuwapelekea DVD mashabiki wa ngumi watakaokuwepo katika pambano la Cheka na Maugo ili kuweza kujifunza mambo mbalimbali ikiwa ni pamoja na sheria za mchezo wa ngumi", alisema Super D.

MUAMBA ALIFARIKI KWA DAKIKA 78

Fabrice Muamba ''alifariki'' kwa dakika 78 baada ya kuzirai uwanjani, amebainisha daktari wa klabu yake ya Bolton Wanderers' Jonathan Tobin.

Lakini Dr Tobin amesema ameshangazwa na jinsi mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 23 alivyoweza kuponyoka hadi wakati huu.

Katika mahojiano yenye makiwa, Dr.Tobin amesema hatukua na hakika, fikra zetu ziliwaza mengine kabisa hatukutazamia kufikia hali hii ya afuweni kiasi hiki. Ni ajabu. Muamba alizirai kutokana na kukwama kwa mishipa ya moyo wakati wa mchuano wa Kombe la FA kwenye uwanja wa White Hart Lane jumamosi iliyopita.

Alisema kua Muamba alipewa vifaa viwili vya kumsaidia kuikunjua mishipa ya moyo mara ya kwanza uwanjani mara ya pili wakati akipitishwa uwanjani na mara nyingine 13 kwenye gari la wagonjwa kuelekea hospitali lakini ajabu ni kwamba hakuna hata moja lililofanikiwa.

Saa mbili baada ya leo kurejesha fahamu, nilimsogelea na kumuuliza jina lake, akajibu,Fabrice Muamba. Nikasema nasikia wewe ni mchezaji mzuri wa mpira' akasema'Najitahidi' Nilijihisi chozi likinitoka.'' Mtaalamu ameongezea kusema kua: "singependa kuahidi muujiza kwa wakati huu lakini kwa hali ilivyo maisha yake hayamo hatarini tena.

Bado ni mapema mno kusema kwa uhakika kama atarudi kucheza mpira au la. Dr Sam Mohiddin, mshauri wa masauala ya magonjwa ya Moyo anayemuangalia Muamba kwa sasa, alisema kua Fabrice amezidi kuonyesha dalili nzuri za kupona.

Matokeo yake yamekua ya ajabu kutokana na utunzaji usio wa kawaida. Hali ya afya yake imetushangaza sana. "Jambo la muhimu ni jinsi alivyotunzwa mara tu alipoanguka na kuzirai uwanjani, huduma ya haraka na hasa majaribio ya kuamsha moyo wake uwanjani White Hart Lane na wakati wa kusafirishwa kuelekea hospitali.

Kwa sasa kurejelea maisha yake ya kawaida ni jambo lenye uwezekano mkubwa.

Wednesday, March 21, 2012

EPI BAZDEI 'MWANA MWANZA KWANZA' RAJAB

Eh bana kumbe leo ni bazdey ya mshikaji.... So kwa mwendo wa sapulaizz akatukusanya Tivoli pale juu kwa miito ya mialiko mara kabaaa!!! Rajabu akasaidizana na wake mtarajiwa kukata kekizzz.

Mwenye bazdey Rajab akamlisha keki maiwaifu wake.

Sasa ni zamu ya m-bazdeiwa.

Humu ndani kapo zilikuwa mbili tu! so wacha tuzipe mashavu.

The Crew kutoka shoto ni Philbert Kabago, Ezden The Rocker na Phabian Fanuel.

Mc Mziwanda alifanya machejo na matimbwili yake kisha akamalizia kukitumbukiza kipande hiki cha keki kwenye koo la braza..amini usiamini chapati ilizama yote.

Dj John Lyatow (shoto) akibarikisha mvinyo kupitia mikono ya m-bazdeiwa.

Bahati mbaya nilikuwa looo betri lakini ningekuchukulia muvi watu waliogeshwajeeeh mvinyooooo!!!!

kisha chiazzzZZZzz!!!

Mazawadizzz ni mahela mwanawani!!!

WANDISHI WA HABARI MWANZA WATEMBELEA TBL NAO MGAO WA UMEME CHANZO CHA KUPANDA BEI YA BIA

Afisa Mahusiano wa Kampuni ya Bia Tanzania (TBL), Edith Mushi akizungumza na waandishi wa habari kabla ya safari kuanza kutembelea eneo la kiwanda hicho lililopo Ilemela jijini Mwanza, ili kujionea shughuli mbalimbali za uzalishaji.

Mwishoni mwa wiki waandishi wa habari walipata fursa kutembelea kiwanda cha bia TBL mkoani Mwanza kujionea mapinduzi mapya yanayopangwa kufanyika ndani ya kampuni hiyo hasa katika sekta ya uzalishaji.

Meneja wa TBL Mwanza Richard Rymond akitoa maelezo katika kitengo cha mitungi ya kupika bia.

Mfanyakazi wa TBL kikazi zaidi.

Kwamujibu wa meneja wa kampuni hiyo amesema kuwa mgao wa umeme pamoja na kukatikakatika mara kwa mara kwa nishati hiyo ni miongoni mwa sababu zinazochangia kupanda bei kwa bia zinazotengenezwa na kampuni hiyo.

Meneja wa TBL mkoa wa Mwanza Richard Raymond amesema kuwa si lengo la TBL kupandisha bei ya bia kila wakati, lakini wanalazimika kufanya hivyo kutokana na mgawo wa umeme hivyo huamua kutumia majenereta ambayo huzifanya gharama za uzalishaji kuwa juu.

Sababu nyingine inayotajwa ni ongezeko la mara kwa mara la kodi na ushuru katika malighafi zinazotumika kuzalisha bia.

Kitengo cha uchujaji bia kimeboreshwa kwa kufungwa mitambo ya kisasa zaidi na hili ni moja kati ya machujio yaliyopo kwenye mashine hii.

Kidampa kikihamisha bia zilizozalishwa.

Ndipo ukawadia wakati wa SHINDANO LA 'WHO IS THE GREAT TEASTER' (muonjaji bora wa bia).

"Rilaxini' ni zoezi linalotumia ulimi, harufu, rangi ya kinywaji na kisha utulivu" sauti ya dada mdau toka TBL ilisikika.

Mwandishi Emanuel Chacha toka ITV ni mmoja kati ya watu wanne walioingia fainali na hapa zilitengwa glass tatu kwa kila mmoja.

Henry Kavirondo toka Chanel ten ndiye mshindi wa kwanza akigongana na ....

Jackline Wanna mwandishi wa habari wa gazeti la Mzawa na Kasi Mpya naye yu mshindi wa kwanza akigongana na Kavirondo.

Mshindi wa tatu

Emmanuel Chacha wa ITV mshindi wa nne na zawadi yake.

Kampuni ya Bia Tanzania (TBL) tawi la Mwanza sambamba na kufanya upanuzi katika eneo lake la uzalishaji pia imeboresha vitengo vyake vya kuhifadhi malighafi lengo likiwa ni kwaajili ya kukidhi mahitaji ya soko la ndani na nje ya nchi.