
Wilaya tatu za Geita, Kwimba na Sengerema mkoani Mwanza zimeteuliwa kuingia katika mpango mahsusi wa kuwawezesha vijana wajasiriamali kupata ruzuku ya kuendesha shughuli zao.
Hayo yamebainisha katika taarifa ya mafunzo ya siku tatu ya ujasiriamali kwa wafanyabiashara ndogondogo maarufu kama wamachinga yaliyofanyika jijini Mwanza.
Kwa mujibu wa Kaimu Mkurugenzi wa Maendeleo ya Vijana katika Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo, James Kajugusi amesema kuwa katika awamu ya kwanza ni wilaya ya Magu pekee kutoka mkoani Mwanza ndiyo iliyoteuliwa kuingia katika mpango huo unaoofadhiliwa na Shirika la Kazi Duniani (ILO), lakini katika awamu hii ya pili zimeongezwa wilaya tatu.
Pia imebainishwa kuwa vijana wajasiliamali kutoka katika wilaya hizo, watapata fursa ya kuwasilisha mipango yao ya kibiashara ambayo itashindanishwa na watakaofanya vizuri watapatiwa ruzuku ya kati ya Dola 5,000 hadi 25,000 za Marekani.


Vijana wakiwa ndio kundi kubwa la Watanzania wanahitaji kuhakikishiwa maisha bora kwa kupewa mafunzo ya biashara nafuu.


Tupe maoni yako
0 comments:
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.