NA.ZEPHANIA MANDIA WA G.SENGO TV
Wakati biashara haramu ya ukahaba ikishamiri katika baadhi ya maeneo nchini kutokana na ukatili dhidi ya mtoto wa kike na umaskini wa kipato, mashirika mbalimbali yametakiwa kubuni mbinu za kuwakomboa watoto wa kike, ili kutokomeza vitendo hivyo kutokana na changamoto hiyo, Dorocella Reuben kupitia Shirika la Foundatio Dart Tanzania, ameamua kutatua kilio hicho.
Jiji la Mwanza ni moja kati ya Majiji yanayokuwa kwa kasi kubwa hapa nchini, kutokana na ongezeko la idadi ya watu, lakini changamoto kubwa iliyopo ni biashara haramu ya ukahaba inayofanyika hasa nyakati za usiku katika baadhi ya kumbi za starehe kutokana na biashara hiyo zikiwemo sababu za umaskini wa kipato cha familia, ndoto za watoto wengi wa kike hupotea ambapo kwa kutambua thamani yao, Shirika la Foundation Dart limeamua kuanzisha elimu ya ujasiriamali na kuwasomesha, ili kuwakomboa watoto wa kike.
Miriam Nzogi ni mmoja kati ya watoto walioto kakatika familia duni, leo anaelezea mafanikio yake, baada ya kuchukuliwa na shirika hilo na kisha kusomeshwa, Dorocella Reuben ni mkurugenzi wa Shirikala Foundation Dart Tanzania, lililopo kata ya Bwiru wilayani Ilemela Jijini Mwanza na Rotalinda Mhagama ni mwanafunzi wa kitivo cha sharia, katika chuo kikuu cha mtakatifu Agustino (SAUT).
Akimwakilisha kamanda wa Polisi mkoa wa Mwanza Jonathan Shana, wakati wa hafla ya kuwatunuku vyeti watoto hao vya kuhitimu elimu ya ujasiriamali, mkuu wa Polisi wilaya ya Ilemela Ndagile Makubi, amesema Jeshi hilo halifumbia macho vitendo vya mmomonyoko wa maadili.
Mbali na kuwatukunuku vyeti watoto hao vilevile wamepatiwa medali mbalimbali, baada ya kudhihirisha vipaji vyao katika elimu wanazopatiwa na shirika hilo, zinazohusiana na stadi za maisha.
NAIBU KATIBU MKUU WIZARA YA FEDHA ATETA NA RAIS WA IIA -TANZANIA
-
Na. Josephine Majura, WF, Dodoma.
Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha, Bi. Amina Khamis Shaaban, kwa niaba
ya Katibu Mkuu, Dkt. Natu El-maamry Mwamba, ame...
1 hour ago