ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

Saturday, July 7, 2018

DIAMOND PLATNUM ACHAGULIWA NA WERRASON SASA MIPANGO YAJA



GSENGOtV

Mara baada ya kupiga show Jijini Dar es salaam mwanamuziki mahiri wa muziki wa dansi kutoka nchini Congo Werrason ametua hapa nchini kwa lengo la kufanya show katika jiji la Mwanza na macho yake akiyaelekeza kufanya Kolabo na wasanii mbalimbali akiwemo Diamond Platnumz ambaye anamtaja kuwa ni mmoja kati ya wale anao waelewa.

WERRASON AHAIDI KUPIGA BONGE MOJA LA SHOW KWA WAKAZI WA MWANZA

GSENGOtV
Baada ya kupiga show jijini Arusha mwanamuziki nguli toka Jamhuri ya Demokrasia ya Kongo Werrason Ngiama Makanda usiku wa leo anatarajiwa kupiga show ndani ya Rock City Mall. PICHANI akiwa na waandishi wa habari wa jijini Mwanza wakipiga selfie.

Akiongea na waandishi wa habari mapema leo asubuhi mara baada ya kutua jijini hapa, Werrason amesema kuwa amekuja kamili na wanamuziki wake 26 kwaajili ya kutimiza ahadi yake ya awali iliyoyeyuka kwenye ziara yake aliyoifanya mapema mwaka huu na kupangwa kufanya ndani ya mikoa kadhaa hapa nchini (ikiwemo Mwanza) lakini ikaathiriwa na mvua kubwa zilizokuwa zikiendelea kunyesha nchini.

Karibu sana Mwanza ni kauli ya Afande Jose kulia katika picha akimpa mkono Werrason
We...ndani ya Mwanza.
Werrason na mmoja wa waandishi wa habari kutoka Mwanza.
Radio washirika E Fm nao ndani.
Mwanamuziki nguli barani Afrika Werrason Ngiama Makanda akiwa katika picha ya pamoja na mwandishi Sitta Tuma wa Gazeti la Mtanzania Daima.

DKT TIZEBA AKABIDHIWA TUZO YA HESHIMA KWA KUIMARISHA SEKTA YA USHIRIKA NCHINI

 Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe Kassim M. Majaliwa (Mb) akimkabidhi tuzo ya heshima Waziri wa Kilimo Mhe. Dkt Charles Tizeba kwa kuimarisha sekta ya ushirika nchini wakati wa kilele cha siku ya ushirika Duniani kwenye dhifa iliyofanyika katika uwanja wa Furahisha Jijini Mwanza, Leo 7 Julai 2018. 

 Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Kassim M. Majaliwa (Mb) amemkabidhi tuzo ya heshima Waziri wa Kilimo Mhe. Dkt Charles Tizeba kwa kazi kubwa aliyoifanya na anayoendelea kuifanya katika kuimarisha sekta ya ushirika nchini katika kipindi cha muda mfupi tangu alipoteuliwa kuhudumu katika nafasi hiyo.

 Tuzo hiyo imetolewa Leo 7 Julai 2018 wakati wa kilele cha siku ya ushirika Duniani na Mhe. Waziri Mkuu kwa niaba ya wanaushirika ambao ndio wameandaa Tuzo hizo ikiwa ni heshima na Utumishi mkubwa kwa Waziri Tizeba katika kipindi kifupi kwa kurudisha imani ya ushirika kwa wananchi waliokuwa wamepoteza matumaini kutokana na baadhi ya viongozi wabadhilifu kujinufaisha na Ushirika kinyume na utaratibu.

Tuzo hiyo kwa Dkt Tizeba inatolewa wakati ambapo ni siku moja pekee imepita tangu Waziri huyo wa kilimo kutangaza Kiama kwa viongozi na baadhi ya watendaji wa vyama vya ushirika wanaofanya ubadhilifu wa Mali za wanaushirika kwa manufaa yao pekee pasina kuwanufaisha wanachama wote.

 Kwa msisitizo mkubwa hapo jana Julai 6, 2018 Mhe. Dkt Tizeba alieleza kwa ukali kuhusu ubadhilifu wa rasilimali za ushirika unaofanywa na baadhi ya viongozi na watendaji wa vyama vya ushirika kwenye hafla ya ufunguzi wa Kongamano la Kitaifa la wanaushirika Tanzania linalofanyika kwa siku mbili katika uwanja wa Furahisha Jijini Mwanza.

Kongamano hilo liliambatana na maonesho ya bidhaa na shughuli zinazofanywa na vyama hivyo vya ushirika kote nchini ambapo wanachama wamepata fursa ya kubadilishana uzoefu, na kujadili mafanikio na changamoto wanazokabiliana nazo katika uendeshaji wa sekta ya ushirika nchini na kutoa maoni yao kwa serikali.

Dkt Tizeba amesisitiza kuwa serikali inafanya juhudi mahususi kwa kushirikiana na wadau mbalimbali ili kuhakikisha wananchi wengi zaidi wanahamasishwa na hatimae kujiunga kwenye vyama vya ushirika kulingana na shughuli zao za kiuchumi ili kuondoa dhana kuwa vyama vya ushirika ni kwa ajili ya Kilimo cha Mazao ya biashara ya nchi za nje.

Pia, alisema kuwa Ilani ya Chama Cha Mapinduzi kupitia serikali ya awamu ya tano inayoongozwa na Mhe. Dkt John Pombe Magufuli- Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania inatambua na kuthamini mchango wa ushirika wa Taifa katika kuyafikia malengo ya milenia na malengo mbalimbali ya nchi kama uimarishwaji wa sekta ya viwanda, Kilimo, Mifugo, uvuvi na biashara na kuchangia katika ongezeko la kipato kwa wananchi na hatimaye kuchangia katika ukuaji wa pato la Taifa.

Tuzo hiyo ya kuimarisha sekta ya ushirika nchini pia imetolewa kwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt John Pombe Magufuli sambamba na Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe Kassim M. Majaliwa (Mb).
 Waziri wa Kilimo Mhe. Dkt Charles Tizeba akitoa salamu za Wizara ya Kilimo kwa Waziri Mkuu wakati wa kilele cha siku ya ushirika Duniani kwenye dhifa iliyofanyika katika uwanja wa Furahisha Jijini Mwanza, Leo 7 Julai 2018.

 Baadhi ya viongozi waliojumuika kwenye Mkutano wa kilele cha siku ya Ushirika Duniani
 Baadhi ya viongozi waliojumuika kwenye Mkutano wa kilele cha siku ya Ushirika Duniani
 Baadhi ya wananchi wakifatilia Mkutano wa kilele cha siku ya Ushirika Duniani
 Baadhi ya wananchi wakifatilia Mkutano wa kilele cha siku ya Ushirika Duniani







 Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe Kassim M. Majaliwa (Mb) akiwatunza wadau wa ngoma asili wakati wa kilele cha siku ya ushirika Duniani kwenye dhifa iliyofanyika katika uwanja wa Furahisha Jijini Mwanza, Leo 7 Julai 2018. 
 Michezo mingine ina watu wake.
 Picha ya pamoja.
Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe Kassim M. Majaliwa (Mb) akipungia mkono wananchi na wadau mbalimbali kuwaaga mara baada ya kumalizika kwa kilele cha siku ya ushirika Duniani kwenye dhifa iliyofanyika katika uwanja wa Furahisha Jijini Mwanza, Leo 7 Julai 2018. 

SIRRO ATOA ONYO KALI KWA WALE WOTE WANAOJIHUSISHA NA UHARAMIA KWENYE MAZIWA NA BAHARI HAPA NCHINI


GSENGOtV

Jeshi la Polisi nchini limetoa onyo kali kwa watu wanaofanya vitendo vya uhalifu katika bahari, maziwa na mito mikubwa hapa nchini kuacha mara moja kwa kuwa wamejipanga kuhakikisha wavuvi wanakuwa salama wakati wanapofanya shughuli zao.
Kauli hiyo imetolewa na IGP Simon Sirro Jijini Mwanza wakati wa ufungaji wa mafunzo ya askari polisi wanamaji yaliyokuwa yakifanyika katika Chuo cha Polisi Wanamaji kilichopo Jijini humo.

Aidha IGP Sirro amewataka wazazi kuwakanya watoto wao kutojihusisha na vitendo vya uhalifu kwa kuwa serikali ya awamu ya tano haina mchezo na wahalifu.

IGP Sirro yupo ziarani katika Mikoa ya Kanda ya Ziwa kukagua utendaji kazi wa Polisi na kuzungumza na wananchi waishio katika visiwa ili kuimarisha usalama hususani kwa wavuvi.

VIDEO;- MWANZO HADI MWISHO ILIVYOKUWA MISS MWANZA 2018 NA JINSI ALIVYOPATIKANA

GSENGOtV
Hatimaye Miss Mwanza 2018 imefikia tamati kwa mshindi kupatikana.
Kinyanganyiro cha Shindano la kumsaka mrembo wa shindano hilo kilizaa matunda mnamo majira ya saa nane na nusu za usiku wa kuamkia jumamosi ya tarehe 7 ndani ya Rock City Mall Mwanza kwa mrembo Sharon Headlom kuibuka kidedea baada ya kuwabwaga wenzake 13.
Mepal Management ndio waandaaji wa Shindano hilo lililokuwa na mvuto wa aina yake.

Mgeni rasmi wa Miss Mwanza 2018 Mkuu wa Wilaya ya Nyamagana Bi. Marry Tesha akifungua shindano hilo kwa mwaka huu katika viwanja vya ukumbi wa Rock City Mall jijini Mwanza.
Mkurugenzi wa Mepal Management Bi. Pamela akitoa shukurani kwa muitikio wa wakazi wa Mwanza na wageni.
Vazi la ubinifu. 
Mrembo ndani ya kitenge.
Muonekano wa nyuma kwa vazi lake.
Majaji wa usiku wa kumsaka Miss Mwanza 2018 ndiyo hawa.
Vazi la usiku kwa warembo.
Pigo la usiku.
Muonekano maridadi.
Warembi katika vazi la usiku.
Minato.
Mikogo.
Kwa kwa kwa.......
Safu ya washiriki wote 14 kinyang'anyiro cha kumsaka Miss Mwanza 2018.
Engo nyingine.
Hamissa Mobetto akivuta pumzi kuwataja Top 5 Bora.
14 wote ndiyo hawa hapa.
Hatimaye Top 5 ya Miss Mwanza 2018 ikapatikana kuelekea kumpata mshindi.

TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI KUTOKA JESHI LA ZIMAMOTO NA UOKOAJI

Kamishna Jenerali wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji, Thobias Andengenye.