ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

Saturday, August 4, 2018

ZITTO, BASHE NA DR MASHINJI WASEMA HAYA BAADA YA KIGWANGALLA KUPATA AJALI.


Baada ya Waziri wa Maliasili na Utalii, Dkt. Hamisi Kigwangalla kupata ajali asubuhi hii akitokea mkoani Arusha kuelekea Manyara karibu na eneo la Magugu mkoani humo na Ofisa wa habari, Hamza Temba amefariki dunia.

Mbunge wa Kigoma Mjini (ACT Wazalendo), Zitto Kabwe kupitia akaunti yake ya twitter ameyasema “Ndugu yetu @HKigwangalla amepata ajali. Nimeongea na msaidizi wake aliyekuwa kwenye gari iliyopata ajali na ameniambia Waziri ameumia kidogo na anapata matibabu Kwa sasa.


Mwana Habari wa Wizara amefariki ( inna lillah ). Hali ya Waziri inaendelea vizuri. Tuendelee kumwombea dua”

Katibu Mkuu wa Chadema, Dk Vincent Mashinji amesema haya kupitia twitter
”Pole sana Mh. Kigwangala na wote mliopatwa na madhira haya. Tunawaombea afya njema majeruhi wote. Pia, roho ya marehemu ipumzike kwa amani! A comprehensive and integrated plan to mitigate RTA is critical. It is not all about speed but also road signs etc are necessary for safety!”

MBUNGE wa Nzega Mjini, (CCM), Hussein Bashe amesema amesema haya kupitia twitter
”It is Sad news ⁦@HKigwangalla⁩ amepata ajali maeneo ya Magugu this morning hali yake sio Nzuri na mtu mmoja amefariki Let us Pray for him”

Friday, August 3, 2018

HIKI NDICHO KISHINDO CHA KONGAMANO LA KANISA LA METHODIST JIJINI MWANZA.



NA ZEPHANIA MANDIA WA G.SENGO TV
KONGAMANO LA KANISA LA METHODIST LENYE MAKAO YAKE MAKUU NCHINI KENYA LIMEFANYIKA MKOANI MWANZA NCHINI TANZANIA KWA MAFANIKIO MAKUBWA.

NI KATIKA UWANJA WA NYAMAGANA KONGAMANO HILO LIMEFANYIKA IJUMAA YA TAREHE.03.08. 2018.  

MICHEZO MBALIMBALI IMEHUSISHWA NAO WASHIRIKI WAKIWA WANAUME KUTOKA NCHI ZA JUMUIYA YA AFRIKA MASHARIKI.

UKWELI KUHUSU GARI LA MISS LAKE ZONE 2018




GSENGOtV
NI ZENGWE TU..! UKAGUZI WAFANYIKA KUHUSU UBORA ZAWADI YA MISS LAKE ZONE 2018 

Wakati Siku nzima ya ijumaa ya tarehe ya leo tarehe 3 mwezi Agasti 2018, mitandao mbalimbali ya kijamii, redio na televisheni zikisheheni habari ILIYOTIKISA juu ya shaka ya ubora wa gari analokwenda kutunukiwa Miss Lake Zone 2018, Gsengo Tv ikaona isiwe tabu na hapa inakusogezea ukweli kuhusu shaka iliyotanda.

Shwali kuu Jeh GARI AINA YA PASSO ALILOKUWA ANAKWENDA KUTUNUKIWA MSHINDI LILIKUWA LINAUBORA AU?

Wakati ukaguzi ukiwa umekamilika Mwenyeji wako mwanahabari Mansour Jumanne wa Gsengo Tv hapa ana fanya mahojiano ana kwa ana na Msimamizi Mkuu Kamati ya Miss Tanzania Basila Mwanukuzi.

BREAKING NEWS:-
KAMATI Miss Lake Zone 2018 imghairi kulitoa gari hilo lenye picha zake mitandaoni (licha ya kukaguliwa na kuonekana bora na lenye viwango) na sasa watatoa gari jingine JIPYA ambalo picha zake kuwajia hivi punde.

MWANDOSYA AFUNGUKA WATU KUHAMA VYAMA VYA SIASA.





CHANZO/MWANANCHI
Dar es Salaam. Wakati kukiwa na wimbi la wanasiasa kuhama vyama vya siasa na kuhamia vingine, waziri wa zamani katika Serikali za awamu ya tatu na nne, Profesa Mark Mwandosya amesema ‘hamahama’ hiyo inatokana na vyama kukosa itikadi, dira na sera inayotakiwa na jamii.
Profesa Mwandosya ameyasema hayo ikiwa ni siku chache tangu wabunge wawili wa Chadema kujiuzulu nyadhifa na uanachama wao na kuhamia CCM.
Wabunge waliohama ni Julius Kalanga wa Monduli na Mwita Waitara wa Ukonga. Pia wapo madiwani zaidi ya 50 wa CUF, ACT-Wazalendo na Chadema waliohamia chama hicho tawala hivi karibuni wakidai kuunga mkono juhudi zinazofanywa na Rais John Magufuli.
Akizungumza na Mwananchi jana, Profesa Mwandosya alisema hamahama ya vyama inatokana na changamoto inayovikabili vyama vya siasa barani Afrika na nchi zinazoendelea.
Pia alisema kuhama huko kwa wanasiasa kunatokana na vyama kukosa itikadi inayovisimamia, kwa maana ya mwelekeo na dira pamoja na aina ya jamii ambayo nchi husika zingependa kuijenga.
“Akikaa huko (katika chama alichomo), anaamua kurudi na kupokewa kwa shangwe (katika chama cha awali) mithili ya mtoto aliyepotea katika vitabu vitakatifu. Na kwa sababu anakohamia wanatafuta kuongeza namba, basi inaeleweka kwa nini anapokelewa kwa shangwe,” alisema.
Profesa Mwandosya alifafanua kuwa katika mazingira hayo ni vigumu kutoa sababu za msingi za kiitikadi na kiimani za wanasiasa kurudi katika vyama vya awali, bali mara nyingi ni za kibinafsi zaidi.
Alisema kibaya zaidi mwanasiasa anakorudi kuna watu ambao hata katika mazingira aliyoyaeleza wameendelea kubaki na kukitumikia chama anachohamia.
Alisema watu anaowakuta ndani ya chama husika wanaona “walioasi” wanarudi na kupanda ngazi haraka.
“Jambo hilo limekuwa dhahiri sana baada ya mwisho wa vita vya baridi kati ya nchi za Magharibi na za Mashariki,” alisema mwanasiasa huyo aliyewahi kujitosa kuomba kuteuliwa na CCM kugombea urais mwaka 2005.
Profesa Mwandosya alisema kujenga aina ya jamii inayotakiwa kunahitaji ufafanuzi wa itikadi na sera za uchumi zinazoambatana na itikadi hiyo. Alisema awali sera hizo zilijikita katika ukabaila au usoshalisti.
“Na kila nchi zilitafsiri nini maana ya itikadi na sera hizo katika mazingira yake. Lakini ilivyo sasa, mfumo wa kiuchumi unaongozwa kwa misingi ya soko. Kinachofanyika ni kujaribu kupata itikadi kutokana na mfumo wa uchumi badala ya itikadi kuongoza mfumo wa uchumi,” alisema.
“Vyama vimejikuta katika ombwe la tafakuri hiyo kiasi cha kwamba kushika dola kunakuwa ndio msingi wa kuwepo kwa vyama. Kinachotokea ni kwamba wananchi na wenye nchi hawaoni tofauti za vyama kwa misingi niliyoelezea.”
Alieleza kuwa kutokana na sababu hizo viongozi na wanachama wanaweza kuhama wakati wowote kwenda chama chochote.
“Kwani bila misingi ya kiitikadi, imani ya msingi haipo na masilahi yanakuwa kiini cha maamuzi. Katika hali hii mtu anatoka chama kimoja anaenda kingine, tena kwa jeuri kabisa,” alisema.
Aliongeza kuwa, “sina uhakika kwa kuwa wao ni binadamu wataridhika na hali hiyo. Kwa kawaida, hapo zamani wanaorudi kundini wangepita kwanza kwenye mafunzo au madarasa ya itikadi ili kuwapima kwanza.”
Alisisitiza kuwa ombwe lililopo linatokana na changamoto ya kiitikadi inayoendelea na si kwa Tanzania tu, bali nchi nyingi zinazoendelea.
Miongoni mwa wanasiasa waliohama vyama vyao katika siku za karibuni ni pamoja na aliyekuwa mbunge wa Singida Kaskazini (CCM), Lazaro Nyalandu aliyehamia Chadema.
Wengine ni aliyekuwa mbunge wa Kinondoni (CUF), Maulid Mtulia na wa Siha, Dk Godwin Mollel (Chadema) ambao walihamia CCM, kisha wakateuliwa na chama hicho kugombea tena ubunge katika majimbo hayo na kushinda tena.

Thursday, August 2, 2018

WANAFUNZI WAIBUKIA KWENYE MKUTANO WA MBUNE WA BUKOMBE.

Mbunge wa jimbo la Bukombe mkoani Geita, Mhe.Doto Mashaka Biteko (CCM) ambaye pia ni Naibu Waziri wa Madini ameendelea na ziara yake katika Kata mbalimbali jimboni humo ili kuwaeleza wananchi utekelezaji wa ahadi zake za maendeleo pamoja na serikali ya awamu ya tano.

Akiwa katika Kata ya Butinzya jana, wanafunzi wa shule ya sekondari katika Kata hiyo waliibuka kwenye mkutano wake wa hadhara na kumuuliza maswali kuhusu changamoto zinazoikabili shule yao na namna atakavyowasaidia kuzitatua. 

Na George Binagi, Bukombe

VIDEO:- WAKUU WAPYA WA WILAYA ZA MKOA WA MWANZA WAAPISHWA AUGUST 02/2018.



GSENGOtV
Mkuu wa Mkoa wa Mwanza John Mongella  amewaapisha Wakuu wa Wilaya wapya wanne baada ya kuteuliwa Rais Dk. John Magufuli hivi karibuni.

Mongella amewaapisha wakuu hao wa wilaya leo mapema katika viwanja vya ofisi ya mkuu wa mkoa, ambapo waliokula kiapo ni Mkuu wa Wilaya ya Ilemela Dk. Severin Mathias, Mkuu wa Wilaya wa Nyamagana Dk. Philis Nyimbi, Mkuu wa Wilaya Magu Philemon Sengati na Mkuu wa Wilaya Ukerewe Kanali Lucas Magembe.

Pia Mongella aliwaomba wakuu hao wa Wilaya kuwa waadilifu katika kazi waliyopata sambamba na  kuongoza wananchi vyema ikiwemo kutatua kero zao bila woga.

"Kupata cheo cha kuwa Mkuu wa Wilaya siyo lazima uwe msomi sana bali ni utendaji kazi wako mpaka Rais akuone wewe amekuamini ndio mana hamjatuma vyeti kwa ajili ya kuomba cheo hichosambamba na uwezo wa Mungu," amesema.


Aidha Mongella amewataka wakuu hao wapya kusimamia ukusanyaji wa mapato kwa lengo la kuinua uchumi wa mkoa ambayo inashika nafasi ya tano kati ya majiji sita nchini.



Mbele ya Mkuu wa Mkoa wa Mwanza Mhe. Hohn Mongella ni Mkuu wa Wilaya ya Nyamagana Dr. Philis Micheck Nyimbi akila kiapo cha utumishi tayari kuwatumikia wananchi wa wilaya yake.
Mbele ya Mkuu wa Mkoa wa Mwanza Mhe. Hohn Mongella ni Mkuu wa Wilaya ya Magu, Dkt Philemon Sengati Lugumiza akila kiapo cha utumishi tayari kuwatumikia wananchi wa wilaya yake.
Mbele ya Mkuu wa Mkoa wa Mwanza Mhe. Hohn Mongella ni Mkuu wa Wilaya ya Ukerewe Cornel Lucas Magembe akila kiapo cha utumishi tayari kuwatumikia wananchi wa wilaya yake.
Mbele ya Mkuu wa Mkoa wa Mwanza Mhe. Hohn Mongella ni Mkuu wa Wilaya ya Ilemela Dr. Severine Mathias Latika akila kiapo cha utumishi tayari kuwatumikia wananchi wa wilaya yake.
Kiapo kwa pamoja.
Kiapo kwa wakuu wa wilaya za Ukerewe, Magu, Nyamagana na Ilemela mkoa wa Mwanza.
Mbela wanasa matukio taswira ya zoezi la kula Kiapo kwa wakuu wa wilaya za Ukerewe, Magu, Nyamagana na Ilemela mkoa wa Mwanza.
Mkuu wa Mkoa wa Mwanza John Mongella akiendesha utaratibu katika kusanyiko la kuwaapisha wakuu wa wilaya za Nyamagana, Ukerewe, Ilemela na Magu shughuli iliyofanyika katika viwanja vya Ofisi yake.
Aliyekuwa Mkuu wa Wilaya ya Nyamagana Marry Tesha alipata fursa ya kuaga na kutoa shukurani kwa viongozi na wadau wenzake aliofanya nao kazi.
Shukuran......
Viongozi.
Aliyekuwa Mkuu wa Wilaya ya Magu, mama Khadija Nyimbo akitoa neno mara baada ya kustaafu.
Kutoka kushoto ni wakuu wa wilaya za Ukerewe, Nyamagana Magu, na Ilemela.
 Mkuu wa Wilaya ya Nyamagana Dr. Philis Micheck Nyimbi.
Mkuu wa Wilaya ya Ilemela Dr. Severine Mathias Latika.
Mkuu wa Wilaya ya Magu, Dkt Philemon Sengati Lugumiza.
Mhe. Mongella.
Viongozi wa dini na madhehebu mbalimbali.
Familia nazo zimehusika kwa ukaribu tukioni.
Mhe. Mongella akichapa neno.
Wasimamizi wa shughuli za ulinzi na usalama.
Kusanyiko la uapisho.
Wazee wa Siasa.

WANASWA KWA TUHUMA ZA WIZI WA MAFUTA YA MWENDOKASI.


JESHI la Polisi mkoani Morogoro, linawashikilia watuhumiwa tisa kwa tuhuma za wizi wa mafuta ya dizeli lita 570, mali ya kampuni zinazoshughulika na ujenzi wa reli ya kisasa (SGR) zilizopo Ngerengere mkoani hapa.

Kwa mujibu wa Kamanda wa Polisi mkoani Morogoro,  Willibrod Mutafungwa, watuhumiwa hao walikamatwa Julai 17 majira ya jioni saa 10 jioni ilipoanza operesheni maalum ya Jeshi la Polisi na kwamba msako unaendelea mkoani hapa.

Kamanda Mutafungwa alisema, watuhumiwa hao walikamatwa na mafuta hayo yakiwa kwenye madumu ya lita 20 na lita 40 kila moja.

Alisema majina ya watuhumiwa hao yamehifadhiwa  kwa ajili ya kuepusha uwezekano wa kuvuruga upelelezi unaoendelea.

Wakati huo huo Anna Selestin (30), mfanyabiashara na mkazi wa Manzese Manispaa ya Morogoro, anashikiliwa na polisi kwa tuhuma za kukamatwa na dawa zinazidhaniwa ni za kulevya aina ya Heroin kete 47 zikiwa kwenye kikopo cheusi.

Kamanda huyo alisema tukio hilo lilitokea Julai 30 majira ya mchana katika eneo la Manzese na kwamba vitu vingine alivyokutwa navyo ni bangi puli 15, kete za bangi 20 na misokoto 160.

Kamanda Mutafungwa aliongeza kuwa uchunguzi zaidi unaendelea, huku taratibu za kumfikisha mahakamani zikiendelea.

MASAUNI ZIARANI WILAYANI BUNDA KUKAGUA NA KUSHUGHULIKIA CHANGAMOTO ZA ASKARI POLISI

Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani  ya  Nchi, Mhandisi Hamad Masauni, akikagua mojaya makazi ya askari polisi   katika   kijiji cha Makongoro B,   kilichopo wilayani Bundawakati wa ziara ya kikazi ya kukagua na kushughulikia changamoto za makazi ya askaripolisi   ambapo jumla ya nyumba mia nne   za askari polisi zinatarajiwa kujengwa nchinzima.Picha na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi


Naibu  Waziri wa   Mambo   ya Ndani    ya     Nchi,   Mhandisi   Hamad   Masauni,   akisomamaelezo ya mmoja ya mtuhumiwa  aliyemkuta katika chumba cha mahabusu katika Kituocha   Polisi   Bunda   wakati   wa   ziara   ya   kikazi   ya   kupitia   shughuli   za   utekelezaji   wamashtaka ya mahabusu walioko katika vituo vya polisi nchini.Wapili kulia ni Mkuu waWilaya ya Bunda, Lydia Bupilipili na wengine ni viongozi waandamizi wa kamati yaUlinzi na Usalama wilayani  Bunda.Picha na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi
Afisa Mnadhimu wa Polisi mkoa wa Mara, Mrakibu Mwandamizi ,Jeremiah Shila  akitoamaelezo ya mwenendo wa mashtaka ya watuhumiwa walioko katika Kituo cha PolisiBunda   kwa  Naibu   Waziri   wa   Mambo   ya   Ndani   ya   Nchi,   Mhandisi   HamadMasauni(wapili kulia) na   Mkuu wa Wilaya ya Bunda, Lydia Bupilipili(watatu kulia),wakati   wa   ziara   ya   naibu   waziri     kupitia   shughuli   za   utekelezaji   wa   mashtaka   yamahabusu walioko katika vituo vya polisi nchini. Picha na Wizara ya Mambo ya Ndaniya Nchi


Naibu   Waziri   wa   Mambo   ya     Ndani     ya     Nchi,   Mhandisi   Hamad   Masauni   (watatukushoto),   akifuatilia   wakati   mpelelezi   akifunua   jalada   la   mmoja   wa     mahabusualiyemkuta katika chumba cha mahabusu katika Kituo cha Polisi Bunda wakati wa ziaraya kikazi ya kupitia shughuli za utekelezaji wa mashtaka ya mahabusu walioko katikavituo vya polisi nchini.Wapili kulia ni Mkuu wa Wilaya ya Bunda, Lydia Bupilipili nawengine   ni   viongozi   waandamizi   wa   kamati   ya   Ulinzi   na   Usalama   wilayaniBunda. Picha na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi

Serikali Kujenga Nyumba 400 za Askari  Polisi Na Mwandishi WetuSerikali imetenga kiasi cha shilingi bilioni kumi kwa ajili ya ujenzi wa nyumba zaaskari polisi kote nchini, ikiwa ni kukabiliana na changamoto ya makaazi ya askarina uchakavu wa vituo vya polisi ili kuwawezesha askari hao kutekeleza majukumuyao kwa ufanisi. 

Hayo yamesemwa     na Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, MhandisiHamad  Masauni alipotembelea   kijiji   cha  Makongoro   wilaya  ya   Bunda  mkoaniMara   kuona   changamoto   wanazokutana   nazo   askari   polisi   katika   kutekelezamajukumu yao ya ulinzi na usalama.

Alisema wizara iko katika mpango maalumu wa kuboresha makazi ya askari polisinchini huku akitoa  wito na nafasi kwa  wadau wa maendeleo pia  kujitokeza nakuunga  mkono  juhudi  za  Rais   Dk.John  Magufuli kuboresha makazi  ya  askaripolisi “Katika kukabiliana na changamoto ya askari nchi nzima tayari tushaanza kujengamakazi ya askari wetu tukianza na nyumba za polisi Kusini Pemba na tutaendeleana ujenzi huo wa nyumba 400 katika mikoa mingine nchini na kutokana na haliniliyoiona   hapa   Bunda   basi   tutatoa   kipaumbele   hapa”Alisema   Naibu   Waziri Masauni Akizungumza wakati wa ziara hiyo

Mkuu wa Wilaya ya Bunda, Lydia Bupilipili, ametoa rai kwa wananchi kuhakikisha wanashirikiana na serikali katika ujenzi wamakazi ya askari polisi wilayani humo huku Mwenyekiti wa Kijiji hicho Mussa Masilu akiongeza   kuwa nyumba hizo ni chakavu na zinashusha hadhi ya Askari Polisi.

Hadi sasa serikali imeshaanza taratibu za awali ikiwemo tathmini ya ujenzi wanyumba hizo mia nne za askari polisi nchini ambapo mikoa mbalimbali itanufaikana  ujenzi huo utakaotekelezwa kwa awamu tofauti ukienda sambamba na ujenzina ukarabati wa vituo vya polisi. ……………………………......................MWISHO………………………………………..

Wednesday, August 1, 2018

MASWALI MA 5 YA WASHIRIKI MISS LAKE ZONE 2018 KWA JESHI LA POLISI MWANZA



GSENGOtV Washiriki wa Shindano la kumsaka Miss Lake Zone 2018 hii leo wameketi meza moja na baadhi ya maafisa wa jeshi la polisi jijini Mwanza wakiuliza na kujibiwa maswali mbalimbali yaliyokuwa yamejikita katika nyanja tofauti tofauti za rika na staha mbalimbali. Pengine wengi twaweza kuwa na maswali:- JEH kitu gani cha msingi walichofuata kwenye ofisi hizo nyeti za Serikali? GsengoTv imekusogezea maswali ya udadisi na yenye tija kwa jamii yaliyoulizwa na warembo hao.
1. Kuhusu bodaboda na kamatakamata ya kutovaa kofia ngumu.
2. Waoto watukutu wanapokamatwa kwa makosa na kuwekwa sero moja na wakubwa
3. Taratibu za mwendo kasi wa uendeshaji na tochi za barabarani.
4. Kesi za watu wanaoshiriki mapenzi ya jinsia moja kwanini mara nyingi zinaangukia pua.
5. Kesi za uhujumu uchumi
Mkuu wa Kikosi cha Usalama Barabarani (RTO) Mkadam Khamis Mkadam ndiye mwenyeji wa wanyange hao na hapa anasimama kwa niaba ya Kamanda wa Jeshi la Polisi Mkoa wa Mwanza, Ahmed Msangi.


Ni mwendo wa kusababisha tabasamu pichani mchango wa Miss lake Zone 2018 kwa Kituo cha watoto wadogo waishio mazingira magumu cha FKT jijini Ilemela Mwanza.
Kuzungumza nao na hata kujua changamoto zao FKT.
Picha ya washiriki Miss lake Zone 2018 pamoja na Kitengo cha Usalama Barabarani na Makosa ya Jinai Polisi Mwanza.
Picha ya pamoja hapa ni walimu na wasimamizi itifaki Miss lake Zone 2018 na Kitengo cha Usalama Barabarani na Makosa ya Jinai Polisi Mwanza.
Utalii Mwanza unaanzia hapa 'SANGARA MTEMA MAJI'
Utalii na mazingira.
Katikati ya jiji la Mwanza.

Watalii nao wamo....Tukutane Jumamosi hii ya tarehe 4 Sept 2018 Rock City Mall Mwanza.

ANAYEDAIWA KUJITEKA MWANZA AKITAKA KUWAKAMUA PESA NDUGU ZAKE ANASWA NA JESHI LA POLISI



GSENGOtV

Polisi Mkoani Mwanza inamshikilia Prosper lema Mkazi wa Pasiansi na Mfanyabiashara wa kuuza vileo eneo la Pasiansi Wilayani Ilemela kwa tuhuma za kutuma ujumbe mfupi wa maandishi kwenye simu za mkononi akidai kuwa ametekwa katikati ya Jiji na Watu wasiojulikana kisha kuomba atumiwe pesa zaidi ya shilingi milioni 5 ili aweze kuachiwa huru na watu waliomteka.

MABULA KUPELEKA BUNGENI AJENDA YA WAFANYABIASHARA WA FILAMU



ZEPHANIA MANDIA/GSENGOtV

Mbunge wa jimbo la nyamagana mkoani Mwanza, stanslaus Mabula, amesema anakusudia kupeleka ajenda ya wafanyabiashara wa filamu nchini kusaidiwa kutengenezewa leseni za gharama nafuu ili wafanyabiashara hao waweze kujikwamua kiuchumi na kukuza pato la Taifa.

Mabula amesema katika bunge la miswada linalotarajiwa kuanza Septemba mwaka huu jijini Dodoma, moja ya ajenda yake kuu ni kufikisha kilio cha wafanyabiashara wa wadogo wa filamu wanaotembeza filamu mtaani.

Kauli hiyo ameitoa wakati akizungumza na wafanyabiashara zaidi ya 300 wanaouza CD za kudurufiwa mtaani jijini hapa ambao wameitisha mkutano kwa ajili ya kuzungumza na wadau wa filamu kuhusu changamoto zinazowakabili.

MBUNGE JIMBO LA BUKOMBE ALIVALIA NJUGA SUALA LA ELIMU.



Na George Binagi, Bukombe
Wazazi na walezi katika wilaya ya Bukombe mkoani Geita wametakiwa kuweka mkazo katika kuwasomesha watoto ili kuwasaidia kuondokana na utegemezi hapo baadae. Mbunge jimbo la Bukombe, Doto Biteko ametoa rai hiyo wakati akizungumza kwenye mkutano wa hadhara uliofanyika katika Kata ya Iyogelo jimboni hapa. 

RAIS MAGUFULI AWAAPISHA VIONGOZI ALIOWATEUA.



GSENGOtV

Rais John Magufuli, amewaambia Wakuu wa Mikoa, Makatibu Tawala na Makatibu Wakuu alikaa na majina yao kwa muda wa miezi mine kabla ya kuwateua kushika nafasi hizo.

Akizungumza baada ya kuwaapisha viongozi hao leo Jumatano Agosti Mosi, Ikulu jijini Dar es Salaam, Rais Magufuli pia amewataka viongozi hao kutambua ni Mungu ndiye amewachagua.

“Nimekaa na majina yenu zaidi ya miezi minne, wengine wamepungua wengine wameongezeka.

“Tanzania ni kubwa mno, mimi sikufaa kuwa rais, ni Mungu alitaka na ndiyo sababu siwezi nikasimamam nikajisifu, ni Mungu alitaka vile vile Makamu wa Rais.

“Hata Waziri Mkuu… kwanza hata sijui nilimchaguaje, kwa sababu kuna watu walikwenda Dodoma na suti wameshona ili wawe Waziri Mkuu, lakini Majaliwa (Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa) ni Mungu aliamua awe Waziri Mkuu, vivyo hivyo katika nafasi zenu,” amesema Rais Magufuli.

Aidha, Rais Magufuli pia amesema nafasi hizo kwa viongozi hao, zimepangwa na Mungu ambaye alitaka wazipate ambapo wakiamini hivyo kila mmoja katika nafasi yake atatenda haki kwa wakati wake.

“Wengine wanasema nimechagua wapinzani, nani mpinzani Tanzania hii, Kafulila (David Kafulila, Katibu Tawala wa Mkoa wa Songwe) mtasema ni mpinzani.

“Alipokuwa huko alipigania suala la IPTL, akaitwa tumbili leo umteue useme umeteua mpinzani, huyu si mpinzani ni mpiganaji wa serikali yake,” amesema.

HAKUNA JINSI:- YANGA SASA YATEMBEZA BAKULI KWA MASHABIKI WAKE.



Baada ya hali kiuchumi kuwa ngumu ndani Yanga, uongozi wa klabu hiyo kupitia kwa Kaimu Katibu Mkuu, Omary Kaaya, ametangaza kuomba wanachama mashabiki wa timu hiyo kuichangia fedha.

Kaaya ambaye amechukua nafasi ya aliyekuwa Katibu Mkuu, Charles Boniface Mkwasa ambaye alijiuzulu kufuatia kusumbuliwa na matatizo ya kiafya, amewaomba wanayanga wajitoe ili kuisaidia timu wakati huu wa mpito.

Kaimu huyo amesema kinachofanyika hivi sasa ni kuandaa namba maalum ambazo wanayanga wataweza kuzitumia kwa ajili ya kuichangia fedha ili kuikwamua klabu hiyo na hali ngumu inayopitia kwa sasa.

Yanga imeamua kufikia maamuzi hayo ili kuweza kupata fedha walau za kuweza kujikimu wakati timu ikiwa kambini kwa ajili ya msimu ujao na mashindano mengine ikiwemo ya kimataifa.

Wakati uongozi ukitangaza kuandaa namba hizo za kuchagia, kikosi cha timu hiyi sasa kipo katika maandalizi ya msimu mpya na mchezo wa Kombe la Shirikisho Afrika dhidi ya USM Alger utakaopigwa siku za usoni jijini Dar es Salaam. 


CHANZO AZAM TV

NAIBU MEYA DAR AMWAGA MANYANGA.


"Nimejivua uanachama wa CUF na nafasi zangu zote ndani ya chama ikiwemo ya udiwani katika kata ya Vingunguti pia unaibu meya wa manispaa na nimechukua hatua hii ili kulinda na kutetea maslahi ya wananchi ninaowatumikia hivyo ili niendelee kuteleza majukumu yangu ipasavyo najivua ili kuunga mkono jitihada za rais Magufuli na viongozi wote Serikali kwa ujumla" amsema Kumbilamoto.

Tuesday, July 31, 2018

WAKAZI WA KANDA YA ZIWA SASA KUJISHINDIA MAMILIONI NA PEPSI.




GSENGOtV

Kampuni ya SBC Tanzania Limited, watengenezaji na wasambazaji wa vinywaji baridi aina ya Pepsi, Mirinda, 7up, Mountain Dew na Evervess, Mkoani  Mwanza wanayo furaha kuwaletea  Shindano kabambe litakalojulikana kwa jina la“Jishindie Mamilioni ”  Shindano hili  litahusu  soda aina ya Pepsi, Mirinda Orange, Mirinda Fruity, Mirinda Lemon, 7Up za ujazo wa mililita 350, na Mountain Dew (300ml).

Shindano hili litatangazwa Katika Radio, Magazeti, Mabango na Vipeperushi mbalimbali. Madhumuni ya kuwaletea shindano hili niKuboresha hali ya maisha ya wateja wetu wa kanda ya Ziwa kwa kuwapatia zawadi za fedha taslimu ili kuwawezesha kujikomboa kiuchumi.

Shindano hili litaendeshwa Kwa muda wa wiki sita kuanzia tarehe 01/08/18 hadi 16/09/18 katika mikoa ifuatayo: Mwanza, Shinyanga, Mara, Simiyu, Tabora, Geita, Kigoma na Kagera. 
 Meneja Mafunzo na Uwezeshaji SBC Tanzania Limited Rashid Chenja akionesha moja ya mabango ya kutambulisha shindano la Jishindie Mamilioni.
 Kutoka kushoto ni Phocas lusato Meneja Rasilimali watu SBC, akifuatia Meneja Mafunzo na Uwezeshaji SBC Tanzania Limited Rashid Chenja na Hussein Mkwawa ambaye ni Meneja mauzo Kanda ya Ziwa wakisikiliza vyema maswali ya waandishi wa habari (hawako pichani) katika utambulisho rasmi wa shindano la Jishindie Mamilioni, uliofanyika ukumbi wa mikutano SBC Nyakato jijini Mwanza.
 "Safiiiiii.....!!"

 Balozi wa PEPSI Albert Sengo (kulia) akitoa maelezo kwa wawezeshaji SBC, anayemsikiliza mbele yake ni Meneja Mauzo kanda ya Ziwa Hussein Mkwawa, Meneja Mafunzo na Uwezeshaji SBC Tanzania Limited Rashid Chenja na Meneja Rasilimali Watu Phocas Lusato  katika utambulisho wa shindano la Jishindie Mamilioni, uliofanyika ukumbi wa mikutano SBC Nyakato jijini Mwanza.
 "Hizi ndizo zawadi"
Nikama wakisemezana "Hebu tuone umepata nini ndani ya kizibo chako...." Balozi wa PEPSI Albert (kushoto) Sara Onesmo kutoka Clouds Tv na Johari Shani wa Mwananchi Communication.
 Shindano hili la“Jishindie Mamilioni” litakuana vizibo vya rangi ya Silva. Shindano hili litakua na zawadi nyingi za pesa taslimu kuanzia shilingi za Kitanzania 1,000,000/-, 500,000/-, 10,000/-, 5000/-,  1000/= na SODA YA BURE.

Ili Mteja ajishindie zawadi anatakiwa kununua soda za Jamii ya Pepsi kisha abandue ganda Ndani ya Kizibo akikuta maandishi aidha ya shilingi 1,000,000/-, 500,000/-, 10,000/-, 5,000/- 1000/-  au Free Pepsi (SODA YA BURE), atakua amejishindia zawadi hiyo papo hapo. 

Zawadi za shilingi 10,000/=, 5000/=,1000/=na Soda ya bure zitapatikana hapo hapo kwa aliyekuuzia soda, Gari ya Mauzo au Muuzaji wa Jumla. Vizibo vya zawadi vimeandikwa kwa rangi ya dhahabu, Zawadi za shilingi 1,000,000/-, 500,000/-  zitatolewa kiwandani Mwanza tu, Barabara ya Musoma, Nyakato, Kuanzia saa 4 asubuhi hadi saa 9 jioni siku za Jumatatu hadi Ijumaa (isipokua siku za sikukuu). 
Hii ndio fursa nzuri kwa wanywaji wa soda zetu kujishindia Mamilioni kila siku kwa kunywa Soda zetu, Kuna zawadi nyingi sana, kunywa sasa unaweza kuwa wewe ndio mshindi, ili uboreshe maisha yako.

Tarehe ya mwisho ya kutoa zawadi ni Tarehe 30 Septemba 2018.

Tuna imani utashirikiana nasi  kufanikisha shindano hili na kuboresha maisha yako.

“Jishindie Mamilioni ”


ASANTE SANA  

SBC  TANZANIA  LIMITED