NA ALBERT G. SENGO
MWANZA. Kwa mujibu wa Waziri wa Ardhi Nyumba Maendeleo na Makazi Mhe. Angeline Mabula amesema mpaka sasa jumla ya watu 2,700 kati ya 3500 tayari wameshapata viwanja vyao, huku baadhi yao wakiwa na hati walizopata papo hapo na wengine wakisubiri kukamilisha malipo ili wapewe hati zao. Ndani ya viwanja vya Rock City Mall jijini Mwanza watumishi wa vitengo mbalimbali kutoka Ofisi ya Ardhi wilaya ya Ilemela wameweka kambi hapa kutoa huduma zote katika eneo moja. HUDUMA ZINAZOTOLEWA 1. Kwa uuzaji wa viwanja vilivyotangazwa, mnunuzi atakwenda kwenye ramani na kuchagua kiwanja, atapewa bei kupitia mtandao, atalipa na kupewa hati ya kumiliki papo hapo. 2. Kwa wanaotaka kulipa kodi ya ardhi hakuna riba kwa msamaha wa Rais Samia. 3. Huduma zote zinazotolewa na ofisi ya ardhi zinapatikana hapa kwani hii ni One Stop Centre.Saturday, September 10, 2022
Thursday, September 8, 2022
MALKIA ELIZABETH ALAZWA KWA MATIBABU.
Kasri la Buckingham nchini Uingereza limetangaza kuwa kiongozi mkuu wa kimila wa nchi hiyo, Malkia Elizabeth yupo chini ya uangalizi maalumu wa matibabu kwenye kasri la Balmoral nje ya jiji la London kutokana na maradhi ambayo hayakuwekwa wazi.
Taarifa hiyo iliyotolewa leo Septemba 8, imesema madaktari wa Malkia wamependekeza abaki chini ya uangalizi wa matibabu.
“Malkia anaendelea vizuri na yuko Balmoral kwa matibabu na mapumziko," imesema sehemu ya taarifa hiyo.
Hali hiyo imemtokea malkia huyo mwenye umri wa miaka 96 ikiwa ni siku chache tangu akutane na Waziri Mkuu anayeondoka madarakani Boris Johnson kabla ya kumteua waziri mkuu mpya, Liz Truss.
Pia, kutokana na mwenendo wa afya yake malkia Elizabeth alilazamika kuahirisha kikao chake na Baraza la Mawaziri kilichotakiwa kifanyike siku ya jana, Septemba 7, 2022 baada ya kushauriwa na madaktari wake kupumzika.
Nchi hiyo inaongozwa kwa mfumo wa serikali ya kifalme huku makao makuu yake yakiwa kwenye kasri kuu la Buckingham lililopo kwenye jiji la London, hata hivyo kasri lingine ambalo malkia amepelekwa kupumzika lipo Balmoral eneo la Aberdeenshire huko Scotland.
VIDEO TFS WAJA NA MASHINDANO YA MAGARI
Wa kwanza kwenye video ni Mhifadhi mkuu wa shamba la miti la Sao Hill Mufindi Lucas Sabida anayefuata ni mwenyekiti wa Rally Iringa anaitwa Amjad khan
TFS WAJA NA MASHINDANO YA MAGARI "TUNATANGAZA UTALII WA MISITU"
Mhifadhi mkuu wa hamba la miti la Sao Hill Lucas Sabida akiongea na waandishi wa habari juu ya utalii huo mpya wa mchezo wa mbio za magari katika msitu wa shamba hilo.
Na Fredy Mgunda,Iringa.
Wakala wa huduma za misitu Tanzania
(TFS) kupitia shamba la miti la Sao Hill mkoani Iringa wameanzisha utalii wa
michezo ya magari katika shamba hill kwa lengo la kuunga mkono juhudi za
kutangaza utalii wa ndani kama ambavyo Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
alivyofanya kwenye filamu ya Royal Tour.
Akizungumza wakati wa kutangaza kwa
mashindano ya magari katika shamba la miti la Sao Hill, Mhifadhi mkuu wa shamba
hilo Lucas Sabida alisema kuwa wamejipanga kuanzisha utalii katika shamba hilo
ambao utaongeza kipato kwa wananchi na shamba hilo.
Sabida amesema kuwa kwa sasa
wameanzisha utalii wa mchezo wa magari ambao unatarajiwa kufanyika tarehe
11/09/2022 katika shamba la miti la Sao Hill na wananchi wote wanakaribishwa
kwenda kutazama mchezo huo.
Alisema kuwa wao kama Shamba mbali na
kujihusisha na shughuli za mazao ya isitu lakini pia wanafanya shughuli za
utalii wa michezo ambapo kwa mara ya kwanza wameanza na utalii wa Mbio za
Magari ambayo yatafanyika September 11 Mwaka huu.
"Leo tumekutana kwa lengo la
kujiridhisha na kuangalia maandalizi hatua ambayo tumefikia hadi sasa sanjari
na kukagua njia zote ambazo zitatumika kwa ajili ya mchezo huo kwa sababu ni
zoezi ambalo halijawahi kufanyika katika historia ya shamba letu hivyo ni kitu
kipya." Amesema Sabida
Sabida alisema kuwa katika Shamba
hilo kuna barabara ambazo wamekuwa wakidhihifadhi ambazo zinaurefu wa
kilometer 1500 hivyo ni fursa ya kipekee ya kutumiwa kwa utalii wa michezo
ambayo ni mchezo mpya
kwa upande wake Mwenyekiti wa
Mbio za Magari kwa Mkoa wa Iringa Amjad Khan amesema kuwa Sao hill na wao
kwa pamoja wameshirikiana kuandaa Mashindano hayo madogo ya magari ambayo
huitwa sprint kwa ajili ya kujifunza kuhusu Shamba hilo
" Hadi sasa tumejipanga vizuri
na maandalizi yamefikia asilimia 99 kwa sababu tulijipanga vizuri ili
kuhakikisha Mashindano hayo yanafanikiwa kwa sababu tulianza kujiandaa
mwezi mmoja na nusu kabla ya siku hii ambayo tunazungumza na waandishi
ikiwa kila kitu kimekamilika." Amesema Khan
Amesema kuwa Mashindano hayo ni fursa
nzuri kwao ya kushirikiana na Serikali kuweza kutangaza msitu huo ili watu
waweze kuelewa zaidi pamoja na kuunga mkono juhudi za Serikali kutangaza
masuala ya utili ikiwa utalii wa michezo.
"Malengo ya Mashindano hayo ya
magari ni kutangaza msitu wa sao hill hivyo Iringa motorsports Club
tumepata fursa hii hivyo .. Sisi kama club tumefurahi sana... Kwa bahati ambayo
tunaipata na tumeipokea kwa mikono miwili na tunajisikia furaha
sana." Amesema Khan
Naye Mchezeshaji wa mchezo huo
wa magari John Makeo alisema asilimia kubwa wamepata ushirikiano mkubwa
kutoka kwa shamba kwakuwa ni mara ya kwanza kushiriki michezo huo katika Shamba
hilo.
"Watu wengi wa Mafinga walikuwa
wanakuja Iringa kwa ajili ya kuangalia Mashindano hayo lakini September
11 yatafanyika katika Msitu wa shamba la Sao hill ambapo wataweza kujionea
fursa zilizopo na kuzitangaza ikiwemo utalii wa nyuki pamoja na gundi zipo
katika msitu hii" Amesema Makeo
Hata hivyo katika Mashindano hayo
jumla ya madereva zaidi ya 20 wanatarajiwa kushiriki katika mchezo huo
ambapo hadi sasa wanajumla ya washiri 14 ambao wamekubali kushiri kwenye mchezo
huo watazungumza mizunguko minne ambayo Sawa na kilometer 6.
Sabida amesema kuwa SAO HILL MISITU AUTO CROSS ni zao jipya la Utalii ndani ya Shamba la Miti SaoHill Mafinga TFS wanasema utalii wa aina hii ni mara ya kwanza kufanyika ndani ya Shamba la Miti SaoHill
Wednesday, September 7, 2022
UONGOZI WA AZIMIO WAMWIDHINISHA KALONZO KUWANIA USPIKA WA SENETI KENYA.
Kalonzo Musyoka.
Kiongozi wa Wiper Kalonzo Musyoka mnamo Jumatano, Septemba 7, alijitosa kwenye kinyang'anyiro cha spika wa Seneti baada ya kujiondoa katika kile cha spika wa Bunge la Kitaifa. Kalonzo Musyoka akizungumza na wanahabari hapo awali.
Kalonzo alipewa msukumo na Muungano wa Azimio One Kenya unaoongozwa na aliyekuwa Waziri Mkuu Raila Odinga na Rais anayeondoka Uhuru Kenyatta.
Katika kinyang'anyiro hicho, kinara wa Wiper anatazamiwa kumenyana na aliyekuwa Gavana wa Kilifi Amason Kingi ambaye anaungwa mkono na mrengo wa Kenya Kwanza.
"Ufafanuzi katika mkutano wa Azimio Parliamentary Group (PG) kuhusu nani atawania Uspika katika Bunge la Kitaifa na seneti.
Kenneth Marende.
"Mhe. Kenneth Marende atawania spika wa Bunge la Kitaifa na Mhe Kalonzo Musyoka kuwa spika wa Seneti," Philip Etale, Mkurugenzi wa Mawasiliano wa ODM, alitangaza.
Hapo awali, Kalonzo alikuwa kwenye kinyang'anyiro cha spika wa Bunge la Kitaifa lakini akaamua kujiondoa kwa kuhofia kudhalilishwa kwenye uchaguzi uliopangwa kuandaliwa Alhamisi, Septemba 8.
Aliyekuwa Makamu wa Rais chini ya Muungano wa Azimio La Umoja alikuwa amejitupa katika kinyang'anyiro cha kumkabili Moses Wetangula kutoka Muungano wa Kenya Kwanza kuwania kiti cha spika.
Wakati akitoa uamuzi wake, Baraza Kuu la Kitaifa la Chama cha Wiper lilimtaka kiongozi wake kuanza kujenga chapa yake baada ya mgombea urais anayempendelea, Raila Odinga, kukosa kunyakua kiti hicho.
Kalonzo, mnamo Jumatatu, Septemba 5, aliripotiwa kuchagua karatasi za uteuzi katika Bunge la Kitaifa na Seneti, akitaka kuwashawishi wanachama waliochaguliwa kuunga mkono azma yake katika mabunge yote mawili.
Uamuzi wa kujiondoa ulijiri baada ya makubaliano ndani ya Azimio kutaka kinyang'anyiro cha spika wa Bunge la Kitaifa kushikiliwa na aliyekuwa Spika Kenneth Marende.
Marende pia alikuwa amechagua karatasi zote mbili za uteuzi kwa Bunge la Kitaifa na Seneti. Mbunge mteule wa eneo bunge la Dadaab Farah Maalim alichaguliwa kuwa naibu wa Marende katika bunge la kitaifa baada ya mwenzake wa Rarieda kuamua kujiondoa.
"NITASTAAFU LAKINI KIONGOZI WANGU NI BABA" RAIS UHURU ASEMA.
Rais Uhuru Kenyatta amesema yuko tayari kumkabidhi naibu wake William Ruto mamlaka baada yake kuibuka mshindi wa uchaguzi wa urais.
Akiongea katika kikao na wabunge wa muungano wa Azimio katika mkahawa wa Maasai Lodge, Uhuru amesema ni wajibu wake kikatiba kufanya hivyo.
Katika kile huenda kikazua hisia mseto, Rais alisema atafanya hivyo lakini kiongozi wake atasalia kuwa aliyekuwa mgombea wa urais kwa Azimio. "… nitapeana mamlaka nikiwa natabasamu kwa sababu ni wajibu wangu kikatiba kufanya hivyo, lakini mimi kiongozi wangu ni Baba Raila Odinga," Uhuru amesema.
Rais amewakosoa Wakenya kwa kumchagua Ruto akisema wamekataa nafasi ya kuleta umoja nchini. "Mmekataa nafasi ya kuleta umoja humu nchini.
Si Raila mmenyima nafasi," alisema Rais wakati wa kikao hicho Amewataka viongozi wa Azimio la Umoja kusalia ngangari huku akiwashtumu wale ambao wanaungana na Kenya Kwanza. "Jameni msiwekwe mfuko," alisema akiashiria viongozi ambao wameamua kufanya kazi na muungano wa Ruto.
Rais alikuwa akiunga mkono Raila kuwa rais wa tano wa kitaifa baada yake kukosana na naibu wake. Wakati wa kikao hicho, alipigia debe Kalonzo Musyoka kuwa Spika wa Seneti akisema wakifaulu kufanya hivyo watakuwa na nafasi ya kuendeleza ajenda za Azimio.
Sasa Kalonzo watamenyana na aliyekuwa gavana wa Kilifi Amason Kingi ambaye anaungwa mkono na Kenya Kwanza. Katika bunge, Kenneth Marende naye amependekezwa na Azimio huku Kenya Kwanza nao wakiunga mkono Seneta Moses Wetangula.
Ruto aliibuka mshindi wa uchaguzi wa urais baada ya kujizolea kura 7.1M dhidi ya Raila aliyepata 6.9M.
RC Pwani aziagiza halmashauri kubuni vyanzo vipya vya mapato
Mkuu wa Mkoa wa Pwani Alhaj Abubakari Kunenge akizungumza na wajumbe mbali mbali wa kikao hicho cha kazi. Baadhi ya wajumbe wa kikao hicho cha kazi wakisikiliza mada mbali mbali zilizokuwa zikitolewa.
Na Victor Masangu,Pwani
BENKI YA CRDB YAZINDUA ATM YA KUWEKA PESA HADI MILIONI 100
Wateja wa Benki ya CRDB sasa kupata huduma ya kuweka fedha masaa 24 kupitia ATM za kisasa za kuweka pesa. Hayo yameelezwa leo na Afisa Mkuu Uendeshaji wa Benki hiyo, Bruce Mwile wakati akizindua huduma hiyo katika tawi la Benki ya CRDB Mlimani City.
Akizungumza na Waandishi wa Habari, Mwile alisema mashine hiyo inatumia teknolojia ya kisasa ambayo inawawezesha wateja kuweka pesa wenyewe bila usaidizi kwa urahisi, usalama, na unafuu. Mwile alisema mashine hizo zinauwezo wa kupokea hadi shilingi milioni 100 kwa mara moja.
“Tunatambua zipo biashara ambazo zinaendeshwa nje ya muda wa kazi wa kawaida ambapo matawi ya Benki na hata CRDB Wakala wanakuwa wamefunga, mashine hii inakwenda kutatua changamoto hii kwani huduma ya kuweka pesa sasa itapatikana masaa 24 kwa urahisi na usalama zaidi,” alisisitiza.
Pamoja na msisitizo wa mifumo ya kidijitali, ukweli ni kuwa matumizi ya fedha taslimu ‘noti na sarafu’ bado ni makubwa. Hii inaifanya huduma ya kuweka pesa “deposit” kuwa moja ya huduma muhimu za kibenki. Mashine hii ya kisasa ya kuweka pesa iliyozinduliwa na Benki ya CRDB inatarajiwa kuleta mapinduzi makubwa ya kihuduma.
Akieleza namna ya kutumia mashine hiyo Mwile alisema: “Mteja atatakiwa kuchagua lugha anayopenda kati ya kiswahili na kingereza, kisha ataweka TemboCard yake na kuingiza namba ya siri. Mteja ataweka pesa hadi noti 200 na kisha kubonyeza kitufe cha ‘Weka Pesa’, kisha utapokea taarifa kupitia ujumbe mfupi.”
Mwile aliongezea kuwa pamoja na kuzindua mashine hiyo katika tawi la Mlimani City, Benki ya CRDB pia inatarajia hadi ifikapo mwishoni mwa mwezi Oktoba itazindua mashine nyengine za kisasa zaidi katika miji na sehemu zote zenye biashara kubwa kote nchini ikiwemo Mwanza, Arusha, Dodoma.
Benki ya CRDB inatajwa kuwa Benki kiongozi nchini ikiongoza katika ubunifu wa huduma na bidhaa zinazokidhi mahitaji halisi ya wateja. Benki ya CRDB inaongoza kwa kuwa na mtandao mpana zaidi wa utoaji huduma kupitia matawi zaidi ya 260, CRDB Wakala zaidi ya 22,000, ATMs zaidi ya 550, na vifaa vya manunuzi (PoS) zaidi ya 2,500.
Benki ya CRDB pia inaongoza kwa ubunifu wa mifumo ya kidijitali ya utoaji huduma ikiwamo SimBanking, SimAccount, Internet Banking, na TemboCard. Mtandao wa Benki hiyo umevuka mipaka hadi Burundi ambapo ina kampuni tanzu, na hivi karibuni inatarajia kuingia katika nchi ya Jamhuru ya Kidemokrasia ya Congo.
Mkuu wa Kitengo cha Uwakala wa Kibenki wa Benki ya CRDB, Erick Willy (wapili kulia) akiweka taarifa zake katika mashine ya kuweka pesa ( Deposit ATM) wakati wa hafla ya uzinduzi wake uliofanyika kwenye tawi ya Benki ya CRDB, Mlimani city jijini Dar es salaam.
Meneja wa Benki ya CRDB tawi la Mlimani City, Zaituni Manoro akizungumza katika hafla fupi ya uzinduzi wa mashine mpya na ya kisasa ya kuweka pesa ( Deposit ATM) iliyofanyika kwenye tawi ya Benki ya CRDB, Mlimani city jijini Dar es salaam.
MAMA KOKA KULETA MAGEUZI YA KIUCHUMI KWA WANAWAKE WA UWT KIBAHA MJI.
Na Victor Masangu,Kibaha
Monday, September 5, 2022
TBS YAWANOA MAAFISA BIASHARA NA AFYA PWANI
Na Victor Masangu,Pwani
RUTO ASHINDA KESI YA UCHAGUZI, NDIYE RAIS ANAYESUBIRI KUAPISHWA.
Philomena Mwilu (kushoto) na Martha Koome wakati wa moja ya mikutano ya kusikilizwa kwa kesi ya urais. |
Jaji Mkuu wa Mahakama ya Upeo Martha Koome hatimaye ametangaza kuafiki uamuzi wa ushindi wa Rais Mteule William Ruto, kwenye kesi iliyowasilishwa na muungano wa Azimio la Umoja.
Akitoa uamuzi huo siku ya Jumatatu, Koome alisema kwamba makamishna wanne waliojitenga na kutangazwa kwa matokeo ya mwenyekiti wa IEBC Wafula Chebukati hawakuwa na ushahidi kwamba uchaguzi wa Agosti 9 ulitiwa doa.
Vile vile Jaji Mkuu alidokeza kuwa ushahidi wa John Githingo haukuafikia viwango vinavyotakikana.
Wakati huo huo mgombea urais wa Azimio Raila Odinga ameposti picha akifuatilia mwenendo wa kesi hiyo ya uchaguzi kwa njia ya television. |
Raila alikuwa amesema kuahirishwa kwa chaguzi hizo ulikuwa ni njama ya mahasimu wake kwa ushirikiano na mwenyekiti, kusababisha watu wasijitokeze kumpigia kura katika maeneo hayo ambayo ni ngome yake.
Tayari shamrashamra zimeanza kulipuka, huku baadhi ya television zikionesha matukio mbalimbali toka viunga tofauti tofauti kwa wananchi wa taifa hilo wakishangilia ushindi wa bwana Ruto.
KISINDA APIGWA STOP USAJILI YANGA.
Taarifa kutoka Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF)
MAKOSA YA UONGOZI WA YANGA AU TFF? CHANZO:- JUMA AYO
✍kama yanga walikuwa wameshakamilisha idadi ya wachezaji 12 wa kimataifa alafu ghafla wakamuongeza Kisinda jumla wanakuwa na wachezaji 13 kama walikuwa na option ya kumtoa mchezaji mmoja ii kisinda achukue nafasi lazima wavunje mkataba wa huyo mchezaji au wamuuze kwenda timu A au wamtoe kwa mkopo ili usajili wake ufutwe kwenye orodha.
✍Lakini kama yanga walikuwa wanatoa jina tu la mmoja ili kisinda aingie kwenye system na huyo mchezaji anakuwa hajafutwa kwenye mipangi ya klabu bado wanakuwa na wachezaji 13 kinyume na kanuni.
Huu ndio utaratibu ninavyojua mimi.
✍Maswali ya msingi
Je yanga walipokuwa wanaomba mabadiliko ya wachezaji walianisha kama wanamtaka mchezaji fulani acheze kimataifa au waliomba mchezaji abadilishwe kwasababu Kuna mmoja ana majeraha??
✍Kanuni ya wachezaji wa kigeni ndani ya nchi ni 12 tu na hakuna klabu inapswa kuvuka idadi hii....yanga wanayo room ya kwenda kwenye kamati lakini hakuna usajili wa mchezaji 13 inapswa kutolewa pia tukumbuke kabla dirisha kufungwa kuna dirisha la CAF ambayo klabu zote zilishatuma idadi ya wachezaji wake ambao ni 12 na tff ndio wanatuma majina hayo CAF mapema.
LIVE: SUPREME COURT JUDGMENT ON PRESIDENTIAL ELECTION PETITION
Mahakama hiyo inatarajiwa kushikilia au kubatilisha ushindi wa Rais Mteule William Ruto katika chaguzi za Agosti 9.
Azimio pia walidai kuwa IEBC haiwezi kuhesabu kura 250,000, bila kujumuisha kura zilizopigwa.
Raila na mgombea mwenza waliitaka mahakama kuu kuwatangaza rais mteule na naibu rais mteule mtawalia.
Raila pia alitaka ukaguzi wa kina na wa kitaalamu wa vifaa na teknolojia zote zilizotumiwa na tume ya uchaguzi katika uchaguzi wa urais.
MWENGE WA UHURU UMEZINDUA MIRADI MITANO YENYE THAMANI YA SH.BILIONI 1.6 IRINGA
Na Fredy Mgunda, Iringa.