ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

Saturday, May 22, 2010

USIKU HUU: Inter Milan beat Bayern 2-0 to win Champions League

Inter Milan's forward Diego Milito celebrates after scoring during their UEFA Champions League final football match against Bayern Munich at the Santiago Bernabeu stadium in Madrid.

BRAVOOOO TIME TO PUT SOME ICE INTO THE GLASS.


MADRID, May 22 (Reuters) - Inter Milan beat Bayern Munich 2-0 with a double strike by Argentine Diego Milito to win the Champions League at the Bernabeu Stadium on Saturday. Inter’s win also secured the first season treble by a Serie A club after their Italian league and Cup triumphs.

(Editing by Ken Ferris; To query or comment on this story email sportsfeedback@thomsonreuters.com)

NYUMBA MABANGO KWA MATANGAZO YA BIASHARA. JE! MWENYE NYUMBA ANANUFAIKA?

ZURURA YA KAMERA YANGU LEO IMEAMUA KUTOKA HIVIII... JE! UNALOLOTE?
NO 1
NO 2
NO 3
NO 4
NO 5
NO 6
NO 7

TOKOLALA WAPI?

MSIHOFU JAMANI ALAJII....
NI KAMA KAWA NDANI YA MZALENDO PUB JUMAMOSI HII.
WOTH DJ BONNY LOVE & DJ MAKEY.
JE! WAYAWEZA?
BASI USIKOSE!
SPONSERD BY OVERMEER WINE.

Friday, May 21, 2010

BIHONDO ASOMEWA MASHTAKA LEO.

ULINZI ULIIMARISHWA WAKATI MSTAHIKI MEYA WA JIJI LA MWANZA BW. LEONARD BANDIHO BIHONDO (64)ALIPOWASILI MAHAKAMA KUU YA MKOA WA MWANZA KUSOMEWA MASHTAKA YA TUHUMA ZA MAUAJI YA KADA WA CCM.

KWA KARIBU ZAIDI.

AKIINGIA CHUMBA CHA MAHAKAMA.

LEONARD BIHONDO (64), AMEFIKISHWA KATIKA MAHAKAMA YA HAKIMU MKAZI MKOA WA MWANZA KUSOMEWA MASHTAKA YEYE PAMOJA NA WENZAKE WA3 AMBAO NI JUMANNE OSCAR (30), MKAZI WA KITANGIRI JIJINI MWANZA ANAYEDAIWA KUTOKEA MKOANI KIGOMA, BARTAZAR SHUSHI (47), AMBAYE NI FUNDI MWASHI MKAZI WA MTAA WA NERA JIJINI NA ABDUL AUSI (45), KADA WA CCM ALIYEWAHI KUWA KATIBU MWENEZI WA CCM KATA YA ISAMILO NA MWENYEKITI WA MTAA WA MASHAURI ULIOPO ISAMILO.

MBELE YA HAKIMU MKAZI MKUU MFAWIDHI WA MAHAKAMA KUU YA MKOA WA MWANZA BIBI. EUGINIANIA RUJWAHUKA WAKILI WA SERIKALI BW. STEVEN MAKWEGA AMEWASOMEA WATUHUMIWA SHITAKA LA MAUAJI YA KUKUSUDIA AMBALO NI KINYUME CHA KIFUNGU CHA KANUNI YA ADHABU YA MAKOSA YA JINAI NAMBA 196 SURA 16 YA MWAKA 2002. KESI IMEAHIRISHWA NA ITATAJWA TENA JUNE 4/ 2010.

MAREHEMU BAHATI ALIZIKWA NYUMBANI KWAO KATIKA KIJIJI CHA BUSIRI WILAYANI UKEREWE AMBAPO RAIS JAKAYA KIKWETE ALIWAKILISHWA NA MSAIDIZI WAKE BWANA ALI LUHAVI.

MIAKA 14 YA KUMBUKUMBU YA WALIOZAMA MV. BUKOBA YAADHIMISHWA KIMYA KIMYA.

LEO NI TAREHE 21 MEI 2010 UKIRUDI NYUMA MIAKA 14 ILIYOPITA HADI TAREHE 21 MEI 1996 KUTIZAMA YALIYOTOKEA, HAKIKA SIKU HII, SIYO SIKU YAKUTAMANIKA KWANI NI SIKU YA HOFU, SIKU YA HUZUNI NA MAJONZI.
NILIWASILI ENEO LA MAKABURI LILILOKO IGOMA NJE KIDOGO YA MJI WA MWANZA KIASI CHA SAA 4:30 NAKUKUTA VIJANA WAKIFANYA USAFI, HUKU WENGINE WAKIPAKA RANGI YA CHOKAA KUKARABATI MAKABURI HAYO.

KIJANA EMASON MGANYIZI BYENGOZI AKIWEKA SHADA LA MAUA KTK KABURI LA BABA YAKE MZAZI MGANYIZI BYENGOZI MMOJA WA ABIRIA ALIYEKUFA MAJI KWENYE AJALI HIYO.

ALIELEKEZWA TU NA NDUGU ZAKE KWAMBA ATAKUTA LIMEANDIKWA JINA..NILIMSHUHUDIA KIJANA HUYU AKIPATA WAKATI MGUMU KULIPATA KABURI LA BABA YAKE HASA MARA BAADA YA USAFI KUKUTA UMEFANYIKA SAMBAMBA NA UPAKAJI RANGI, NAE HAKUWAHI KUFIKA KATIKA ENEO HILI KWANI ALIKUWA MDOGO KIPINDI HICHO CHA AJALI. HAPA KIJANA EMASON AKIWASILIANA NA NDUGU ZAKE KUWATAARIFU KUFANIKIWA KULIPATA KABURI HILO BAADA YA JUHUDI ZA KUKWANGUA RANGI KABURI HADI KABURI.

SEHEMU YA MAKABURI.

CHAMA CHA MTUME WA SALA YA MOYO WA IMAKULATA PAROKIA YA BUGANDO WALIOJITOKEZA KUWAOMBEA MAREHEMU HAO KTK SIKU HII YA KUMBUKUMBU.

MTANGAZAJI WA RADIO FREE AFRIKA AKIFANYA MAHOJIANO NA MWANACHAMA WA CHAMA CHA UTUME WA SALA MAMA WINFRIDA DAMIANI AMBAYE NAE ALIONDOKEWA NA MTOTO WA DADA YAKE PAMOJA NA JIRANI YKE BW. KABADI AMBAYE ALIKUWA MKUU WA MAGEREZA BUKOBA.

HATIMAYE NILIONDOKA ENEO HILO HUKU NIKIACHA FAMILIA NYINGINE ZIKIWASILI MAHALA HAPO.

PICHANI KWA MBALI ENEO LA MAKABURI HAYO.
CHAKUSIKITISHA MPAKA KAMERA HII INAONDOKA ENEO LA TUKIO HAKUNA KIONGOZI YEYOTE WA SERIKALI ALIYEFIKA ENEO LA HILO WALA HAKUKUWA NA MPANGO WOWOTE WA TAARIFA ZA MAADHIMISHO.
HAKIKA WAANDISHI WA HABARI TUNAYO DHAMANA KUBWA KUELIMISHA UMMA JUU YA UMUHIMU WA SIKU HII + SERIKALI NAYO ITENGE WIKI YA MAADHIMISHO YA MV BUKOBA AMBAPO HUMO TUKUMBUSHANE YOTE YALIYOTUKIA.

Thursday, May 20, 2010

KUHUSU MAUAJI KAMANDA SIRO ANASEMA......

KAMANDA WA POLISI MKOA WA MWANZA SIMON SIRO Akisema:-
“Jana jioni majira ya saa 10 pale uwanja wa ndege wa Mwanza tuliweza kumkamata mh. Leonard Bandiho Bihondo ambaye ni mstahiki meya wa jiji la mwanza ana umri wa miaka 64 kwa tuhuma hii ya mauaji ya Bi Bahati Stephano aliyekuwa katibu wa ccm isamilo jijini Mwanza, hii imekuja mara baada ya kufanya mahojiano na watuhumiwa wote watatu ambao tayari tumekwisha wakamata, wote wamekuwa wakimtaja kwamba ndiye anaye husika katika tukio hili. Kwahiyo mahojiano yanafanyika ili tuweze kujua ukweli wa tuhuma hizi na kama tutathibitisha bila mashaka kwamba anahusika na mauaji haya either kwa kula njama au kwa njia nyingine basi tutampeleka mahakamani na sheria kuchukua mkondo wake. Lakini niombe kwamba bado tunahitaji taarifa nyingine nyingi maana tunajua suala la kesi ya mauaji ni kubwa na linahitaji ushahidi ulio mkamilifu toka pande zote mbili kwa lengo la kuhakikisha kwamba hatutomwonea mtu yeyote ili kulinda haki ya kila mtu na kuhakikisha kwamba hakuna mtu aliyeko juu ya sheria.”
****Tukio la mauaji ya Bahati lilizua mjadala mkubwa huku mauaji hayo yakihusishwa na masuala ya kisiasa.

Inadaiwa kuwa hivi sasa makundi yanayohasimiana ndani ya CCM yanachuana kwa ajili ya uchaguzi mkuu unaotarajiwa kufanyika Oktoba 31, mwaka huu.

Waliokwisha kukamatwa ni pamoja na Jumanne Oscar (30) ambaye anatuhumiwa kumchoma Bahati kwa kisu sehemu za tumboni na kwenye titi na kusababisha kifo chake. Oscar alikamatwa muda mfupi baada ya mauaji hayo.

Watuhumiwa wengine waliokamatwa kabla ya kukamatwa kwa Bihondo jana, ni Baltazar Shushi ambaye mwaka 2009 aligombea uenyekiti wa mtaa wa Isamilo Kaskazini B kwa tiketi ya CCM na kubwagwa na mgombea wa Chadema.

Kada mwingine aliyekamatwa kwa kuhusishwa na mauaji hayo ni pamoja na Abdul Ausi aliyewahi kuwa Katibu Mwenezi wa CCM Kata ya Isamilo kabla ya uchaguzi wa 2007.

BREAKING NEWS: MAUAJI YA KATIBU WA CCM ISAMILO MEYA WA JIJI LA MWANZA ATIWA NGUVUNI.


MSTAHIKI MEYA WA JIJI LA MWANZA BWANA LEONARD BIHONDO PICHANI AMEKAMATWA NA JESHI LA POLISI KWA MADAI YA KUHUSISHWA NA TUHUMA ZA MAUAJI YA KATIBU WA CCM ISAMILO BI BAHATI STEPHANO ALIYEFARIKI HIVI MAJUZI MARA BAADA YA KUCHOMWA KISU KATIKA ENEO LA OFISI YAKE.
INASEMEKANA MEYA HUYO NDIYE ALIYEPANGA MAUAJI HAYO NA SHUGHULI ZOTE ZA MALIPO KWA MTEKELEZAJI WA MAUAJI HAYO JUMANNE OSCAR.
WAKATI WA MAZISHI YA MAMA HUYO, WAZIRI WA MAMBO YA NDANI AMBAYE PIA NI MBUNGE WA WILAYA YA NYAMAGANA MH. LAWRENCE MASHA ALIKITAJA KIFO CHA BI BAHATI KUWA SI CHA MAPENZI YA MUNGU BALI MKONO WA MTU, NA KUAHIDI KWA KUSEMA KUWA JESHI LAKE LITAWASAKA WALE WOTE WALIOHUSIKA NA MAUAJI HAYO NA KUWAFIKISHA MAHAKAMANI HARAKA IWEZEKANAVYO.

TAARIFA KAMILI ITATOLEWA LEO SAA SABA MCHANA NA KAMANDA SIRO WA JESHI LA POLISI MWANZA. NAYO ISIKILIZE KWA KINA ZAIDI KATIKA JAHAZI CLOUDS FM.
Dk. Asha-Rose Migiro akitunukiwa hadhi ya kuwa Diwani wa Halmashauri ya Jiji la Mwanza. Alipewa tuzo hiyo na Meya wa Jiji, Leonard Bihondo (anaye valisha joho).

HATUKUPANGA IMETOKEA TU!

JUMANNE 11/MEI/2010 ILIKUWA HIVI.

THEN:-
KUTOKA KUSHOTO G, KATAHIGWA NA HUPHREY WA CLOUDS FM MWANZA. HAWA JAMAA WALISTUANA NINI ASUBUHI KWA SIMU, KWAMBA LEO WATOKE HIVI?

Wednesday, May 19, 2010

KIPATO SHILINGI MOJA MATUMIZI SHILINGI MBILI, DOLA YA MAREKANI ILEEE.

WAKATI WAFANYAKAZI WA TANZANIA WAKILILIA NYONGEZA KTK KIMA CHA CHINI CHA MSHAHARA NA HATIMAYE KUGOMEA MGOMO WA KUGOMA DOLLAR YA MAREKANI LEO IMEPANDA BEI HADI KUFIKIA SHILINGI 1,480/= KUIPATA DOLA MOJA AU SHILINGI 1,430/= KUIUZA.
BEI ZA BIDHAA MUHIMU KAMA MAFUTA NA CEMENT TAYARI ZIMERIPOTIWA KUPANDA

ZUHURA NA KUMBUKUMBU YA MV BUKOBA.

mv bukoba ikizama yapata miaka 14 iliyopita.

MSANII WA MUZIKI WA KIZAZI KIPYA MWANADADA ZUHURA KWA HIVI SASA YUKO MAPUMZIKONI NYUMBANI KWAO JIJINI MWANZA, AMBAPO PAMOJA NA KUSALIMIA NDUGU PIA ANATUMIA MAPUMZIKO HAYO KUFANYA SHUGHULI MBALIMBALI ZA KIJAMII KUPITIA MIALIKO MBALIMBALI YA MASHIRIKA BINAFSI ROCK CITY. SHOTO DJ GEORGE, KULIA KABAGO.
ZUHURA MWIMBAJI AMBAYE VILE VILE YU MWANAMITINDO ANAMPANGO WA KUUNGANA NA WANANCHI WOTE WATAKAO KUSANYIKA PAMOJA KATIKA SIKU YA KUWAKUMBUKA WATU WALIOFARIKI DUNIA KWA AJALI MBAYA YA MELI YA MV BUKOBA 21 MWEZI HUU KTK VIWANJA VYA IGOMA JIJINI MWANZA.

VAGI LAZUKA LEO KATI YA MGAMBO WA JIJI NA MACHINGA MWANZA.

<-kioo cha ghorofa ya pili jengo la seif plaza kilichotobolewa na risasi.

LEO MAJIRA YA SAA 5 ASUBUHI IMETOKEA VURUGU BAINA YA MACHINGA NA MGAMBO WA JIJI PAMOJA NA ASKARI POLISI WANAOANDAMANA NA MGAMBO HAO WA JIJI KATIKA ZOEZI LA KAMATAKAMATA.

HALI YA HEWA ILICHAFUKA GHAFLA NA AMANI KUTOWEKA KWA MUDA AMBAPO MADUKA YALIFUNGWA, BIASHARA ZILISIMAMA KWA MUDA KTK MITAA YA MAKOROBOI NA SEHEMU KTK BARABARA YA NYERERE MADUKA YALIFUNGWA HUKU WANANCHI WAKIHAHA KUKIMBIA HUKU NA HUKO ALIMURADI TU KUTOWEKA ENEO LA TUKIO KWANI HATA WALE AMBAO WALIKUWA NDANI YA DALADALA NA VYOMBO VINGINE VYA USAFIRI VILIVYOKUWA VIKINGOJA RUKSA YA TAA ZA BARABARANI KTK BARABARA YA NYERERE ILIWALAZIMU KUSHUKA KUKIMBIA KUTAFUTA PA KUJISITIRI.

SABABU KUBWA YA YOTE HAYA NI LILE ZOEZI LA KAMATA KAMATA SAFISHA JIJI LINALOFANYWA KAMA ADA NA MGAMBO WA JIJI DHIDI YA MACHINGA WANAOCHUUZA BIDHAA NDOGONDOGO IWE KWA KUTEMBEZA AU KWA KUTANDAZA BIDHAA KATIKA MITAA YA JIJI LA MWANZA.

SHESHE LILIANZA PALE MGAMBO WALIPO KAMATA MALI ZA MOJA WA MACHINGA AMBAYE ALIKUWA AKICHUUZA BIDHAA ZAKE PALE KTK MITAA MAARUFU YA KIBIASHARA MAKOROBOI...
MACHINGA KATU HAKUKUBALI MALI ZAKE ZIENDE "AMA ZANGU AMA ZAO LABDA KAMA MGAMBO WANASAIDIA KULISHA FAMILIA YANGU" MACHINGA HUYO ALISIKIKA AKISEMA.

HATUA CHACHE MVUA YA MAWE IKAANZA NA KUONGEZEKA KADRI MUDA UKISONGA, WAFANYABIASHARA WADOGO WAKE KWA WAUME WAKIWARUSHIA MAWE MGAMBO HAO KUWAONDOA WASIWABUGHUDHI KATIKA VIUNGA VYAO VYA KUJITAFUTIA.

POLISI KUONA HALI IMEZIDI KUWA TETE, WAKACHUKUA JUKUMU LA KUFYATUA RISASI HEWANI, RISASI KADHAA ZIKALIA MWISHO WA SIKU PILISI WAKAFANIKIWA KUTAWANYA WAFANYABIASHARA HAO NA KUKAMATA KADHAA WANANAOTUHUMIWA KUHUSIKA NA VURUGU HIZO.

UHARIBIFU:
KIOO CHA GHOROFA YA KWANZA CHA JENGO JIPYA LA SEIF PLAZA KIMEPUPUTIKA MARA BAADA YA KUTOBOLEWA NA RISASI NA KAMA KUNGELIKUWA NA MTU AKIFUATILIA YALIYOKUWA YAKITOKEA KTK VURUGU HIZO TUNGEKUWA TUNAZUNGUMZA MENGINE.

HALI YA SASA NI TULIVU,
SHUGHULI ZINAENDELEA KAMA KAWAIDA.

NDOMANAKE! 3

ASUBUHI HII NANI ANAKWENDA NYUMBANI? DALADALA ZA KURUDI HAZINA WATEJA KITUO CHA MISHENI MZ.

MITAA YA SELEMANI NERA EH BANA PANAKUJA KWA KASI ILE MBAYA, MIJENGO, BARABARA MPYA NINI NA NINI YAANI FULL SERVICE USWAZI UNATOWEKA TARATIIB

open house in kampala: the full moon party on may 28th


Party people!
Tickets to the Full Moon party are now on sale! For the first time ever in Kampala, Talent 256 brings you the best music and lighting, visuals, and many more surprises - all under the moon and stars!

We’ll have a bus running from central Kampala, and plenty of secure parking at the venue if you prefer to drive. Cash bar and lots of snacks will be available all night, so bring your dancing shoes and prepare for an unforgettable party!
It all goes down on Friday, May 28th at Kamooflage Paintball Munyonyo, next to Speke Resort. Get your tickets now for 25,000 or pay 30,000 at the door.

Call the ticket hotline at 0782 506 684 to get yours!

Tuesday, May 18, 2010

MDAU HEBU TEMBELEA.....


kifupi mimi naitwa Dismas Ten ni mwandishi wa habari na ninapiga mzigo kwenye nyumba ya magazeti pendwa Global Publishers pande za Sinza Dar eS Salaam, Ni hilo tu mkuu kazi njema

akhsante

Dismas Ten

TEMBELEA www.dismas10.blogspot.com

Monday, May 17, 2010

MIE MJUMBE TU!


Nimesikitika sana kwakweli na kujiuliza mengi sana,hivi sanaa yetu ya muziki inakwenda wapi jamani??Kama wasanii wetu ndio hawa ambao vichwa vyao ni kama vina mtindio ya ubongo??Mdau weekend hii iliyopita Tanzania yetu ilikuwa na tukio la kihistoria hasa kwa upande wa sanaa hii ya muziki,Kilimanjaro Tanzania Music Awards 2010,ni tukio ambalo kila mpenda burudani alikuwa karibu kuweza kujua kipi ni kipi upande huo na tumeshuhudia mengi,wa kuboronga ukumbini tumewaona na mapungufu yaliyosalia kwa waandaaji wa tuzo tumeyaona pia,leo sitaki kuzungumzia sana juu ya yale ambayo nilipata nafasi ya kuyazungumza kwenye kipindi cha "tupo pamoja" cha TTV kabla ya tunzo zenyewe,leo naomba nizungumze juu ya maoni mbalimbali ya wasanii au wanamuziki wenyewe baada ya tunzo hasa wale waliokuwa katika vipengere(categories) mbalimbali ndani ya tunzo hizi,nimewasikia wengi,lakini mimi naona waandaaji wa tunzo hizi(TBL) katika miaka ijayo wajitahidi kutoa semina juu ya wasanii kukubali matokeo yoyote yatakayopatikana baada ya tunzo zenyewe.Mi naona wasanii wetu wengi hawana upeo kabisa juu ya mambo haya ya tunzo,msanii wa kibongo akishaingizwa kwenye category yoyote tayari anajiona keshachukuwa tunzo,hakumbuki kwamba huu ni ushindani wa yeye na wenzake kibao ambao pia wako katika category hiyo na kati yao wote yeyote anaweza kuchukuwa tunzo hiyo,inapotokea yeye asichukuwe basi inakuwa lawama mtindo mmoja na kutishia kujitoa katika tunzo za miaka inayokuja kitu ambacho mimi naona sio dawa,halafu kitu kingine msanii anatazama jina lake zaidi ya ni nini kilichomfanya aingie katika category fulani,eti kwa sababu yeye ni msanii mwenye kijina kidogo kimuziki basi anataka abebe tunzo zote hata zile ambazo kiukweli ni ngumu kwake kubeba kwa mwaka huo.Mfano naomba nimzungumzie Ali Kiba,nimepata bahati ya kumsikia akihojiwa sehemu fulani akiziponda tunzo na kudai kuwa eti yeye alistahili kuchukua na anashangaa kwanini hajachukua.Ali Kiba alikuwa katika category mbili ambazo ni msanii bora wa kiume wa mwaka na wimbo wake wa "usiniseme" uliingia kwenye category ya wimbo bora wa afro pop.Sasa kimatokeo ni kwamba msanii bora wa kiume wa mwaka alichukua Banana Zorro ambaye kiukweli alistahili tunzo hiyo,Banana kwa mwaka mzima wa 2009 amesimama vizuri kimuziki na hakuna anayeweza kubisha katika hilo,Banana ni mwanamuziki ambaye kwa sasa haimbi kwa playback,anaimba live na anamiliki bendi yake mwenyewe ambapo anatumbuiza sehemu mbalimbali kila weekend,lakini pia Banana mwaka jana ameweza kuhit vizuri na wimbo wake "zoba" sambasamba na B-Band,sidhani kama kweli Ali Kiba alitegemea kumpiku mtu kama Banana katika category hiyo,Ali Kiba bado anaimba kwa kutumia Cd na kupiga vishoo vidogovidogo kwenye sebule za watanzania waishio ulaya na hicho tu si kigezo cha kumfanya awe msanii bora wa kiume wa mwaka.Ushindi wa category ya pili aliyowekwa Ali Kiba ulikwenda kwa wimbo wa Marlow "PiiPii",wimbo ambao hauna ubishi kabisa kustahili kuchukua tunzo hiyo,kwa kudhihirisha hilo basi tunzo hii si tunzo ya kwanza kwa wimbo huo ni tunzo ya pili,ya kwanza ilipatikana toka Kenya,sasa Ali Kiba alitegemea kweli "usiniseme" umfanye yeye achukuwe tunzo hiyo??ni habari ya kuchekesha kidogo,wimbo wenyewe una video mbovu mwanzo mwisho,na video hiyo ilipata airtime sababu yeye ni Ali Kiba na si kingine,na tukizungumzia hit,wimbo wenyewe hauku-hit kivile kama ulivyokuwa "PiiPii" wa Marlow zaidi ya kuhit'ishwa kilazima na wanaojua promo.Kutokana na hilo basi mi naona msanii kama Ali Kiba na wengine wenye vichwa vigumu wanatakiwa wapewe darasa kabla ya kilele cha tunzo zenyewe ili wasizungumze "utumbo" wao wanaouzungumza hivi sasa,kuna mifano mingi lakini kutokana na muda naomba niishie hapa ili mengine mengi wayazungumze wenzangu wanaokerwa na ishu ka' hizi,chiaooo!!!!

SAYS BIZZO 4SHIZO