ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

Saturday, October 19, 2013

MAN U IKIAMBULIA SARE, ARSENAL HIYOO KILELENI.

Goli la pili la kichwa la Mesut Ozil. 
Ushindi wa Arsenal dhidi ya Norwich umeiwezesha kwendelea kuongoza ligi kuu ya premier ya England.
Mesut Ozil amefunga mabao 2 miongoni mwa 4-1 yaliyofungwa na Arsenal kwenye uwanja wao wa Emerates.
Goli la kwanza limefungwa na Jack Wilshere kwa ustadi mkubwa kunako dakika ya 17 ya mchezo.Mesut Ozil amepiga la pili kunako dakika ya 57 kabla ya Norwich kupata bao lao lililoingizwa na Jonathan Howson dakika 10 baadae.
Aaron Ramsey amepachika goli la 3 la Arsenal kwenye dakika ya 82 na Ozil kufunga kazi dakika 3 kabla ya kipenga cha mwisho kulia.
Kwa ushindi huo Arsenal inaendelea kuongoza msimamo wa ligi ikiwa na alama 19 baada ya mechi 8 zilizokwisha chezwa.inafwatiwa na Chelsea yenye alama 17 sawa na Liverpool,lakini wanatofautiana kwa magoli.
Mchezo baina ya Newcastle na Liverpool umemalizika kwa matokeo ya sare ya 2-2, The Magpies wakitangulia kulisalimia mara mbili lango la Liverpool lakini Steven Gerrard na Daniel Sturride walihakikisha kushea pointi za leo.
Wachezaji wa Southampton wakishangilia goli la kusawazisha dhidi ya Manchester United.
Jahazi la Manchester United limezidi kujaa maji baada ya kugawana pointI na Southampton ambao walirejesha goli kunako dakika za majeruhi mpira ukaisha kwa sare ya 1-1.
Wakati kocha Moyes wa Man U akiendelea kupata presha kwa timu yake kufanya vibaya Chelsea ambao waliikaribisha Cardiff darajani pale Stamford, wamenyakuwa ushindi wao wa tano kwa msimu huu kwa ushindi wa bao 4-1. Matokeo yanayo iweka timu hiyo nafasi ya pili nyuma ya washika bunduki.
In the other 3pm games, Everton beat Hull at Goodison Park, Swansea trashed Sunderland and Stoke vs West Brom finished goalless.
In the late kick-off Sergio Aguero struck twice as Manchester City picked up three vital points away at West Ham.

CRDB WAPANDA MITI 1000 HOSPITALI YA RUFAA BUGANDO

Mkuu wa mkoa wa Mwanza Evarist Ndikilo (wa pili kutoka  kushoto) akishiriki zoezi la kupanda miti katika hospitali ya Rufaa Bugando ambapo Benki ya CRDB imehisani shughuli hiyo ya upandaji miti 1000 kwaajili ya kutunza mazingira ya hospitali hiyo, wengine katika picha kutoka kushoto ni Mkurugenzi wa Hospitali ya Bugando Dr. Charles Majinge, Mkurugenzi Mtendaji wa CRDB Dr. Charles Kimei na Mkuu wa Wilaya ya Nyamagana Baraka Konisaga.
Mkuu wa mkoa wa Mwanza Evarist Ndikilo akipanda mti kuhifadhi mazingira ya Hospitali ya Rufaa Bugando jijini Mwanza, zoezi lililohisaniwa na Benki ya CRDB.
Mkurugenzi Mtendaji wa CRDB Dr. Charles Kimei na Mkuu wa Wilaya ya Nyamagana Baraka Konisaga wakipanda miti kuhifadhi mazingira ya Hospitali ya Rufaa Bugando jijini Mwanza, Benki hiyo imeweka mikakati ya kuitunza miti hiyo mpaka itakapokuwa.
Mkurugenzi wa Hospitali ya Rufaa Bugando Dr. Charles Majinge (kulia) akiteta jambo na Mkuu wa Mkoa wa Mwanza Injinia Evarist Ndikilo huku wadau wa CRDB na wahudumu wa hospitali hiyo wakifurahia zoezi hilo.
Ni wakati wa umwagiliaji sasa.
Wadau wa Benki ya CRDB nao walishiriki zoezi hilo kuhakikisha miti 1000 inapandwa katika Hospitali ya Rufaa Bugando jijini Mwanza.
Zoezi la upandaji miti lilikuwa kubwa kwani miti 1000 siyo mchezo.. kutoka kushoto ni Mkuu wa Wilaya ya Ilemela Bi. Amina Masenza, Mkuu wa Mkoa Injinia Ndikilo na Mkurugenzi wa CRDB Charles Kimei.
Wadau wa CRDB wakipanda miti na maua kuhakikisha BMC panakuwa mahali safi kimazingira.
Pamoja na upandaji miti, pia Mkuu wa Mkoa Injinia Evarist Ndikilo aliongoza zoezi la upakaji rangi jengo la Hospitali ya Bugando ambapo benki ya CRDB inahisani mpango huo. Kulia ni Mkurugenzi Mtendaji wa CRDB Charles Kimei. 
Kamanda wa Polisi Ernest Mangu akishiriki upakaji rangi jengo la Hospitali ya Rufaa Bugando anayefuata ni Mkuu wa Wilaya ya Ilemela Bi. Amina Masenza.
Burudani toka Bujora Dance.
Ngoma Boys.
Mkurugenzi Mtendaji wa CRDB Charles Kimei akiwapongeza wafanyakazi wa CRDB Mwanza kwa kusimamia shughuli nzima kwa ufanisi.
Kamati.

BLOGGER SEIF KABELELE KUZINDUA KITABU KUHUSU MAISHA NA CHANGAMOTO

Blogger mkongwe katika game Seif Kabelele anasema kuwa atazindua kitabu kuhusu maisha yake, itakuwa ni siku ya tarehe 4 mwezi Novemba 2013. 
Kaa mkao wa kula.........!

TIMU YA TAIFA POOL TABLE YAKABIDHIWA BENDERA KUELEKEA MALAW

Naibu waziri wa habari utamaduni na Michezo, Amos Makalla akimkabidhi bendera ya Taifa nahodha wa timu ya Taifa ya Safari Pool, Charles Venance wakati wa kuagwa rasmi wakielekea kwenye mashindano ya mchezo huo ya Afrika yanayotarajiwa kufanyika nchini Malawi Octoba 23-26,2013. Makabidhiano hayo yalifanyika Mkoani Morogoro jana.Kulia ni Makamu mwenyekiti wa chama cha Pool Taifa, Fredy Mushina baadhi ya wachezaji wa timu hiyo.

Na Mwandishi Wetu.Morogoro
NAIBU waziri wa habari utamaduni na Michezo Amos Makalla ameikabidhi timu ya taifa ya pool table bendera ya taifa kwaajili ya kwenda kuiwakilisha nchi kwenye  michuano  ya afrika mashariki nchini Malawi,ambapo aliwataka kwenda kuitangaza nchi kwa mema.

 Makala alikabidhi bendera  hiyo jana mjini Morogoro na kuwahimiza wachezaji hao kuhakikisha wanakuwa raia wema ili wengine waweze kuiga kutoka kwao sambamba na kuonyesha umoja na ushirikiano.

Alisema Serikali imeanza kuutambua mchezo huo na kuupa ushirikiano hivyo kuipongeza kampuni ya TBL kupitia bia yake ya safari lager ambao ndiyo wadhamini wakubwa wa mchezo huo.

“ Hongereni TBL kwa kazi nzuri mnayoifanya huu mchezo ulikuwa haufahamiki kabisa na sasa unajulikana na kupendwa ni kazi kubwa ambayo mmeifanya inayostahili kuigwa na makampuni mengine” Alisema Naibu Waziri huyo.

Naye Mwalimu anaeinoa  timu hiyo alisema anaishukuru timu hiyo kwa kuwa imekuwa ikionesha nidhamu ya hali ya juu tangu wakiwa kambini, nakwamba timu imejiandaa vya kutosha na wanauhakika wakurudi na ushindi.

Kwa upande wake Makamu Mwenyekiti wa chama cha mchezo  wa pool table Tanzania (TAPA) Fredy Mushi aliiomba serikali iuangalie mchezo huo badala ya kungalia michezo mingine, nakwamba kufanya hivyo kutawawezesha wachezaji kuwa na ari ya kufanya vyema zaidi wakati wamashindano kama haya.

Aidha wachezaji wanaokwenda kushiriki michuano hiyo nchini Malawi ni , Kampten watimu hiyo Vernace Charles, Omary Akida, Festo yohana, Mohamed Idd, Mercxedek Amedius,Godfrey Swai, Abdala Husein, na Patrick Mnyanguzi.

Mashindano hayo ambayo yanataji kuanza kutimua vumbi Oktoba 23 hadi 26 yanatarajia kushirikisha nchi 14 kutoka afrika  ambazo ni Kenya , Tanzania,Afrika ya Kusini,Zambia, Lesotho,Kongo, Swazland, Ghana,,Nigeria, Misri, Morocco, Namibia, Msumbiji, na Mwenyeji Malawi.

TANZIA

Familia ya Marehemu Joel Mwendamaka wa Dodoma, wanasikitika kutangaza kifo cha ndugu Chaka (Joseph) Joel Mwendamaka, kilichotokea jana Alasiri,Hazina Mkoani Dodoma.

habari ziwafikie ndugu, jamaa na marafiki wote popote walipo Dar es Salaam, Tanga, Dodoma, Mwanza, Arusha, Kigoma, Iringa, Mbeya, Uongozi na Wafanyakazi wote wa Dodoma Hotel. 

Mazishi yatafanyika Jumatatu Mchana Mkuzi, Muheza Tanga. Bwana ametoa na Bwana ametwaa jina lake lihimidiwe. 

- Amen

Taarifa imetolewa na Peter Joel Mwendamaka na Mwani Nyangassa

Friday, October 18, 2013

AKUMAKI WAOMBA UFADHILI KUNUSURU MAZINGIRA YA MJI WA PANGANI

Hii ni sehemu moja wapo ya ufukwe wa bahari katika eneo la wilaya ya Pangani mjini katika eneo la makutano ya mto Pangani na bahari ya Hindi.
Hali ya ufukwe ni mbaya sana na hatarishi kwa maisha ya wakazi wa mji wa Pangani.

Ufukwe huo unaathirika na mmomonyoko wa udongo kwa fukwe hiyo ya bahari, uharibifu wa mazingira na kuanguka kwa miti aina ya Mivinjea na Mikoche katika sehemu hiyo.
Uharibifu mwingine unasababishwa na kuzagaa taka ngumu zikiwemo chupa za plastiki, mifuko ya nailoni na taka nyingine zinazotupwa na wapitanjia wakiwemo wasafiri watumiao usafiri wa majini pamoja na wakazi wa mji wa Pangani ambao hutupa taka hizo baharini nazo mwisho wa siku zikizagaa ufukweni.
Wana AKUMAKI pamoja na wataalamu  wa Halmashauri ya mji wa Pangani wakiwa katika ukaguzi wenye madhumuni ya kufanya jitihada za kunusuru hali hiyo ya uharibifu wa mazingira katika ufukwe wa bahari ya mji wa Pangani.
AKUMAKI wanawaarifu wadau wengine kushirikiana kwa pamoja katika kutoa elimu ya kutosha juu ya suala zima la kuhifadhi mazingira na usafishaji wa fukwe zetu zote hapa nchini Tanzania ikiwa ni pamoja na upandaji miti ya asili yenye kuhifadhi mazingira yakiwemo majani aina ya Mla kasa.
Hali ya mazingira inatatanisha, mti mmoja baada ya mwingine unapuputika kuukaribisha ukame nayo bahari kukosa ulinzi.
Kwa kukosa miti ardhi inatafunwa (inamomonyoka) na kupoteza rutuba yake.

Wana AKUMAKI wana karibisha makampuni mbalimbali yenye malengo ya kurejesha faida kwa jamii katika kufadhiliwa miti nao wakiwatayari  kufanya zoezi hilo kwa kujitolea. 

Ufukwe ni  moja ya vivutio kwa wageni kama inavyoonekana katika picha, watalii wakiwa baharini katika mji wa Pangani eneo la ufukwe wa Funguo (PAndedeco) wakifurahia maadhari.

Je wewe wafurahia wageni kama hawa wakute sehemu zetu adimu zikiwa duni. 
Mazingira na yatunzwe.

MISS UNIVERSE TANZANIA AKABIDHIWA BENDERA LEO


PRESS RELEASE
MISS UNIVERSE TANZANIA AKABIDHIWA BENDERA LEO
Mrembo wa Miss Universe Tanzania 2013 Betty Boniface Omara amekabidhiwa bendera leo na waziri wa mali asili na utalii mheshimiwa Kagasheki.

Zoezi hili limefanyika katika ukumbi wa mkutano wa wizara hiyo tayari kwa safari yake ya kwenda kwenye mashindano ya Miss Universe yatakayofanyika Moscow nchini Urusi mapema mwezi Novemba.

Akimkabidhi bendera huku akimpongeza waziri Kagasheki pia amemtakia mafanikio mema huko aendako.

Betty pia aliwaahidi watanzania kuwa mbali na kurudi na ushindi lakini pia ataenda kuitangazia dunia kuacha kutumia nakshi(Mapambo) yanayotumia pembe za ndovu ili kumaliza tatizo la ujangili nchini.

Zoezi la kukabidhiwa bendera lilifanyika likishuhudiwa na Mkurugenzi wa Kitaifa Miss Universe Tanzania Maria Sarungi Tsehai.


Mashindano ya Miss Universe Tanzania 2013 yamedhaminiwa na hifadhi ya Taifa Tanapa na Mrembo Betty Boniface ameshaanza kutangaza hifadhi hizi kwa njia mbalimbali hapa nchini na nje ya nchi.

WATEJA WA MALIPO YA MWEZI (POSTPAID) AIRTEL SASA KULIPIA ANKRA ZAO KUPITIA HUDUMA YA AIRTEL MONEY

Akizindua huduma ya Airtel money. Kulia ni Mkurugenzi wa kitengo cha  Airtel huduma kwa wateja adriana Lyamba akiongea na waandishi wa wa habari wakati wa uzinduzi wa huduma mpya ya Airtel Money leo. ambapo sasa inawawezesha wateja wake wa huduma ya malipo ya baadayekulipia bili zao za kila mwezi kupitia huduma ya Airtel money popote walipo. Kushoto ni afisa wa Airtel kitengo cha huduma ya malipo baadae Pauline Shoo akifuatilia uzinduzi huo leo.
Afisa malipo ya huduma kwa wateja wa malipo baadae Bi Pauline Shoo akielezea jinsi huduma hiyo inavyofanya kazi kupitia (Menu) au Orodha ya huduma ya Airtel Money. huduma hii inawawezesha wateja wa Airtel  wa malipo ya baadaye kulipia bili zao za kila mwezi kupitia huduma ya Airtel money popote walipo 
Kushoto ni Mkurugenzi wa huduma kwa wateja Adrina Lyamba na ofisa huduma kwa wateja wa malipo baadae bi Pauline Shoo wakiwa wameshikilia vipeperushi vya huduma mpya inayowawezesha wateja wake wa huduma ya malipo ya baadaye kulipia bili zao za kila mwezi kupitia huduma ya Airtel money popote walipo. Kushoto ni afisa wa Airtel kitengo cha huduma ya malipo baadae bi Pauline Shoo
Wateja wa malipo ya mwezi (POSTPAID)  Airtel sasa kulipia Ankra zao kupitia  huduma ya Airtel Money

Dar es Salaam 17, 2013 katika mwendelezo wa kutoa suluhisho na kuboresha huduma za kifedha,  Airtel Tanzania sasa inawawezesha wateja wake wa huduma ya malipo ya baadaye kulipia bill zao za kila mwezi kupitia huduma ya Airtel money.

Akiongea juu ya huduma hii mpya, Mkurugenzi wa kitengo cha huduma za wateja wa baadaye bi Adriana Lyamba alisema "Airtel Leo tunayo furaha kuwafahamisha wateja wetu wa malipo ya mwezi (postpaid) kuwa malipo ya ankra zao za simu za kila mwenzi yamerahisishwa zaidi kwa kupitia huduma ya Airtel money ambapo kwa sasa hakuna haja ya kwenda benki au kwenye ofisi za Airtel kulipia bill zao,  wateja wote wanaweza kufanya malipo kwa kupitia huduma ya Airtel money.

Tunao wateja wa mashirika ya binafsi , Umma, serikali, UN agencies, NGO na mashirika madogo madogo SME  kutoka katika mikoa mbalimbali nchini wanaotumia huduma zetu za  malipo ya mwisho wa mwenzi yaani huduma ya Postpaid

Tumeanzisha huduma ya kulipia bill kwa kupitia Airtel money  ili kuweza kukabili changamoto mbalimbali tulizokuwa nazo huku tukiongeza mapato katika ukusanyaji wa madeni na kuwaondelea wateja wetu usumbufu wa kutembea umbali mrefu kufanya malipo na kutoa rahisi katika huduma zetu.

Bi Adriana Lyamba alisema, Tunaamini huduma hii italeta ufanisi mkubwa katika huduma zetu na kuongeza wigo mpana wa malipo ya anka zao. Na nachukua fulsa hii kuwashukuru wateja wetu kwa kutumia huduma zetu mbalimbali katika kuendesha shughuli za kibiashara, kiuchumi na kijamii

Akiongea jinsi ya kulipia ankra za simu Afisa huduma za baada Bi Pauline Shoo  alisema Kupata huduma hii ni rahisi , piga *150*60#  na kuunganishwa na menu ya Airtel money, kisha bonyesha kulipia bill, andika neno la biashara postpaid - malipo ya mwenzi, ingiza kiasi , number ya account yako ya post paid kisha bonyeza ok na mojakwamoja utapa uthibitisho wa malipo yako.

huduma ya Airtel money yaani pesa mkononi ni huduma ya kifedha inayotolewa na Airtel ikiwa na lengo la kurahisisha malipo ya anka mbalimbali na kuwezesha upatikanaji wa pesa yaani  kutuma na kutoa fedha kuwa rahisi na uhakika mahali popote nchini

kwa sasa Airtel kupitia promosheni yake ya hakatwi mtu hapa inawawezesha wateja wake nchi nzima kutuma na kutoa pesa BURE bila makato yoyote .

Thursday, October 17, 2013

MASHABIKI WA SIMBA NA YANGA MWANZA WANAVYO UZUNGUMZIA MCHEZO WA JUMAPILI.

Baadhi ya  wanachama wa kijiwe cha kahawa cha Bendera mbili mtaa wa Rufiji jijini Mwanza.
MSISIMKO wa mchezo wa watani wa jadi wa soka nchini Tanzania SIMBA NA YANGA, unazidi kuongezeka wakati tukiendelea kuyahesabu masaa yanayoteketea kuufikia mchezo huo utakao chezwa jumapili hii ya tarehe 20 October 2013 kwenye dimba kuu la Taifa jijini Dar es salaam.

Kutokana na sifa za wachezaji waliosajiliwa kwa timu hizo kwa msimu huu mpya ambao unazikutanisha timu hizo kwenye duru ya kwanza na kwa mara ya kwanza, kila shabiki amekuwa na lake la kujivunia,. 

Kwa kuliona hilo SPORTS XTRA ya Clouds Fm ilipata fursa kutembelea kijiwe maarufu cha kahawa kinacho kutanisha mashabiki wa ukweli wa SIMBA na YANGA kinachojulikana kwa jina la Bendera mbili kilichopo mtaa wa Rufiji jijini Mwanza na kuteta na wadau hao, 

Bofya play uwasikilize ... 

VILLA SQUAD Fc YATEMBEZA BAKULI

Villa Squad yatembeza bakuli
Kujiimarisha kurejea ligi kuu Bara

Na Mwandishi Wetu
TIMU ya Soka ya Villa Squad Fc  ya Magomeni Kinondoni,  Jijni Dar es salaam inayo shiriki  michuano ya Ligi Daraja la Kwanza Tanzania Bara (FDL), imewaangukia wadau wa soka kuwapiga tafu ili kuweza kurejea ligi kuu Tanzania Bara.

Akitoa taarifa Mweka hazina wa Villa,  Alwan Geyash alisema  kuwa hadi sasa klabu hiyo inaukata mkubwa hali inayopelekea kuvunjika nguvu hata hivyo wanawaomba wadau kujitokeza na kuichangia kufikia malengo yake kwani wanaamini ikiwezeshwa itaweza kurejea ligu kuu.

“Timu ina uwezo na molali wa kutosha, lakini mifuko imekauka  kiasi tunachopata cha kuchangishana viongozi  wenyewe kwa wenyewe ni kidogo, tunaomba wadau wa soka kujitokeza na kutuchangia kuongeza nguvu zaidi ya kufanya vizuri” alisema Alwan.

Na kuongeza kuwa,  kwa wadau watakao guswa wanaweza kufika katika klabu hiyo iliyopo Magomeni Mtaa wa Kionga ama kuchangia  kupitia akaunti  ya benki ya DTB namba 0704757001 (villa squad football club)au kupitia  tigo pesa 065269999 kwa jina la mweka hazina wa klabu hiyo.

Alwan pia alisema kwa wadau wenye vitu vya kuchangia wanakaribishwa ikiwemo vifaa vya mazoezi, maji ya kunywa,madawa ya michezo na pesa kwa ajili ya posho za wachezaji  ambapo wanaweza kufika kwenye mazoezi  wanakofanyia uwanja wa Garden Kinondon.

Aidha, kwa upande wake Katibu Mkuu wa Villa, Mbarouk  Kassanda  alisema watahakikisha wanajituma kurejea ligi kuu ya Tanzania Bara msimu ujao licha ya kuwa kwenye kundi la kifo.
“Tumefikisha pointi saba na tupo nafasi ya nne, tunahakika kupanda hadi kileleni  tutakapo fanya vizuri kweye michezo yetu iliyobaki” alisema Kassanda.

Villa ipo kundi B, ikiwa na timu za Ndanda (Mtwara),  African Lyon, Friends Rangers, Green Warriors , Polisi DSM, Tessema  na Transit Camp zote za Dar es Salaam.

Ligi hiyo yenye kushirikisha jumla ya timu 24, iliyo kwenye makundi matatui huku kwa kila kundi ikitakiwa kutoa timu moja kupanda ligi kuu.

Makundi mengine ni  kwa kundi A linaundwa na timu za Burkina Moro ya Morogoro, JKT Mlale (Ruvuma), Kimondo SC (Mbeya), Kurugenzi Mufindi (Iringa), Majimaji (Ruvuma), Mkamba Rangers (Morogoro), Polisi (Iringa) na Polisi (Morogoro).

 Kwa upande wa kundi la mwisho  C,  lina timu za JKT Kanembwa (Kigoma), Mwadui (Shinyanga), Pamba (Mwanza), Polisi (Dodoma), Polisi (Mara), Polisi (Tabora), Stand United (Shinyanga) na Toto Africans (Mwanza). 

UTAIPENDA...!!

Ni mawe ya jiji la Mwanza na ujembe wa usalama barabarani toka Crown Paints.
Hawa wamejikita hapa.
Kofia ngumu huokoa maisha ya mpanda pikipiki na abiria wake.
Baridiii...
Ni nyumba juu ya jiwe.
Mambo ya ujenzi vilima vya Rock city.
Kama maisha ya ghorofani  vile ambapo vyombo vya usafiri hupaki chini. 
Mama na mwana na ngazi kuelekea nyumbani.
Kwa ukaribu makazi yetu.

Wednesday, October 16, 2013

BONANZA LA MICHEZO KWA WATUMISHI ILEMELA

BONANZA LA MICHEZO KWA WATUMISHI WA HALMASHAURI YA MANISPAA YA ILEMELA LAFANA      
Bonanza la michezo lililojumiuisha zaidi ya  watumishi 200 wa Halmashauri ya Manispaa ya Ilemela kutoka Idara zote kuanzia ngazi ya Shule, Kata na Makao Makuu ya Halmashauri ya Manispaa ya Ilemela lilifanyika siku ya Jumamosi ya tarehe 12.10.2013 katika viwanja vya michezo vya shule ya Sekondari Buswelu na kufunguliwa rasmi na Mstahiki Meya wa Manispaa ya Ilemela Mh. Henry Matata. Bonanza hili lilijumuisha michezo ya mpira wa Miguu (Football) wanaume, mpira wa Pete (Netball) wanawake, mpira wa wavu (Volleyball) kwa wanaume na wanawake na Riadha kwa wanaume na wanawake.

Akisoma risala fupi kwa niaba ya Mkurugenzi wa Manispaa ya Ilemela, Afisa Utamaduni wa Manispaa, Bi. Rosemary Makenke alielezea lengo hasa la Bonanza hili ikiwa ni:
·         Watumishi kujumuika pamoja na kufahamiana.
·         Watumishi kushiriki katika michezo mbalimbali ya Soka, Netball, Volleyball na Riadha ili kujenga afya za miili yao.
·         Kusheherekea kwa njia ya michezo kutimia kwa mwaka mmoja tangu kuanzishwa kwa Halmashauri ya Manispaa ya Ilemela tarehe 01.10.2012.
·         Kupata nafasi ya kuchagua wachezaji watakaounda timu ya Halmashauri ya Manispaa ya Ilemela inayotarajiwa kwenda kushiriki mashindano ya SHIMISEMITA katika Manispaa ya Dodoma kuanzia tarehe 21.10.2013.
Akizungumza wakati wa hotuba yake ya ufunguzi, Mstahiki Meya alisisitiza yafuatayo:
·         Watumishi wote kuanzia wakuu wa Idara na wale wanaowaongoza washiriki katika michezo kwani ni sehemu kubwa ya kufahamiana ambayo huja kuleta ufanisi katika kazi kwani  michezo hutumika kama sehemu ya kupunguza migogoro katika jamii.
·         Atashauriana na Mkurugenzi kutenga bajeti ya kutosha ya michezo ili kuweza kukidhi mahitaji muhimu yanayoitajika kama vile vifaa vya michezo (mipira, jezi na viatu), huduma ya kwanza, maji ya kunywa n.k.

Katika bonanza hili ambalo lilionekana kuwa na upinzani mkubwa na ilidhihirshwa pale timu zilizocheza mchezo wa fainali soka kufikia hatua ya penati, timu shiriki ziliundwa kama ifuatavyo:
1.      Kata ya Bugogwa na Sangabuye.
2.      Kata ya Pasiansi na Ilemela
3.      Kata ya Kirumba, Nyamanoro na Kitangiri
4.      Kata ya Nyakato, Buswelu na Makao Makuu ya Manispaa.

Matokeo ya michezo ilikuwa kama ifuatavyo:
MPIRA WA MIGUU (FOOTBALL)
1.      Kata ya Kirumba, Nyamanoro na Kitangiri
2.      Kata ya Bugogwa na Sangabuye.
3.      Kata ya Pasiansi na Ilemela
4.      Kata ya Nyakato, Buswelu na Makao Makuu ya Manispaa.

MPIRA WA PETE (NETBALL)
1.      Kata ya Pasiansi na Ilemela
2.      Kata ya Kirumba, Nyamanoro na Kitangiri
3.      Kata ya Nyakato, Buswelu na Makao Makuu ya Manispaa.
4.      Kata ya Bugogwa na Sangabuye.

MPIRA WA WAVU (VOLLEYBALL) – WANAUME.
1.       Kata ya Bugogwa na Sangabuye.
2.      Kata ya Kirumba, Nyamanoro na Kitangiri
3.      Kata ya Nyakato, Buswelu na Makao Makuu ya Manispaa
4.      Kata ya Pasiansi na Ilemela

MPIRA WA WAVU (VOLLEYBALL) – WANAWAKE.
1.       Kata ya Kirumba, Nyamanoro na Kitangiri
2.      Kata ya Nyakato, Buswelu na Makao Makuu ya Manispaa.


RIADHA:
WANAUME ROUND 1: MITA 100
1.       Samson Msodoki
2.       Mahamba Sebastian
3.       Msema Ernest
WANAWAKE ROUND 1: 100
1.       Frola Masatu
2.       Devotha Bukulu
3.       Kissa Mwakibinga
WANAUME MITA 800 WANAUME

  1. Yusuph Mboje
  2. Joshua Nassari
  3. Antidius Selestin

WANAUME ROUND 2: MITA 100
1.       Albert Mongela
2.       Nyawabu Maganga
3.       Said Wawa
WANAWAKE ROUND 2: 100
1.       Edith Shekifu
2.       Felista Kilasa
3.       Veronika TeshaMATUKIO MBALIMBALI KATIKA PICHA                                                                                         


Mgeni rasmi Mstahiki Meya wa Manispaa ya Ilemela Mh. Henry Matata akihututubia wanamichezo mbele ya waandishi wa habari kutoka TBC, CHANNEL 10, STAR TV, BARMEDAS TV, RFA, CLOUDS FM,METRO FM na AFYA RADIO.
Afisa Michezo wa Manispaa ya Ilemela Ndg. Kizito Bahati akifafanua mbele ya waandishi wa habari malengo ya uanzishwaji wa Bonanza la michezo katika Manispaa ya Ilemela.
Sehemu ya umati wa watumishi wanamichezo wakimsikiliza mgeni rasmi wakati wa ufunguzi waBonanza la Wafanyakazi.
Refarii wa mechi ya ufunguzi Siraji Tuwa  akihesabu hatua za miguu 12 kwa ajili ya penati ya ufunguzi iliyopigwa na mgeni rasmi huku golikipa  Gido Buretta  akijitayarisha kudaka.
Mgeni rasmi Mstahiki Meya, Mh. Henry Matata akisalimia na Wilbard kutoka timu ya Makuu Makuu wakati wa mechi ya ufunguzi rasmi wa Bonanza la Wafanyakazi. 
Baadhi ya wachezaji kutoka Makao Makuu wakiwa katika picha ya pamoja kutoka kushoto ni  Hamis, David, Hashimu, Mutani na Goodluck, 
Mkurugenzi wa Manispaa ya Ilemela Alhaj Zuberi Mbyana akiwa na Shilinde wakiteta jambo wakati wakiangalia mechi ya mshindi wa  3
Baadhi ya picha za timu shiriki katika Bonanza la Michezo la Manispaa ya Ilemela.                                                                                                                                                                                                                                                                               

Imetolewa na:
Kizito I. Bahati

Afisa Michezo - Manispaa ya Ilemela.