Dar es Salaam 17, 2013 katika mwendelezo wa kutoa suluhisho na kuboresha huduma za kifedha, Airtel Tanzania sasa inawawezesha wateja wake wa huduma ya malipo ya baadaye kulipia bill zao za kila mwezi kupitia huduma ya Airtel money.
Akiongea juu ya huduma hii mpya, Mkurugenzi wa kitengo cha huduma za wateja wa baadaye bi Adriana Lyamba alisema "Airtel Leo tunayo furaha kuwafahamisha wateja wetu wa malipo ya mwezi (postpaid) kuwa malipo ya ankra zao za simu za kila mwenzi yamerahisishwa zaidi kwa kupitia huduma ya Airtel money ambapo kwa sasa hakuna haja ya kwenda benki au kwenye ofisi za Airtel kulipia bill zao, wateja wote wanaweza kufanya malipo kwa kupitia huduma ya Airtel money.
Tunao wateja wa mashirika ya binafsi , Umma, serikali, UN agencies, NGO na mashirika madogo madogo SME kutoka katika mikoa mbalimbali nchini wanaotumia huduma zetu za malipo ya mwisho wa mwenzi yaani huduma ya Postpaid
Tumeanzisha huduma ya kulipia bill kwa kupitia Airtel money ili kuweza kukabili changamoto mbalimbali tulizokuwa nazo huku tukiongeza mapato katika ukusanyaji wa madeni na kuwaondelea wateja wetu usumbufu wa kutembea umbali mrefu kufanya malipo na kutoa rahisi katika huduma zetu.
Bi Adriana Lyamba alisema, Tunaamini huduma hii italeta ufanisi mkubwa katika huduma zetu na kuongeza wigo mpana wa malipo ya anka zao. Na nachukua fulsa hii kuwashukuru wateja wetu kwa kutumia huduma zetu mbalimbali katika kuendesha shughuli za kibiashara, kiuchumi na kijamii
Akiongea jinsi ya kulipia ankra za simu Afisa huduma za baada Bi Pauline Shoo alisema Kupata huduma hii ni rahisi , piga *150*60# na kuunganishwa na menu ya Airtel money, kisha bonyesha kulipia bill, andika neno la biashara postpaid - malipo ya mwenzi, ingiza kiasi , number ya account yako ya post paid kisha bonyeza ok na mojakwamoja utapa uthibitisho wa malipo yako.
huduma ya Airtel money yaani pesa mkononi ni huduma ya kifedha inayotolewa na Airtel ikiwa na lengo la kurahisisha malipo ya anka mbalimbali na kuwezesha upatikanaji wa pesa yaani kutuma na kutoa fedha kuwa rahisi na uhakika mahali popote nchini
kwa sasa Airtel kupitia promosheni yake ya hakatwi mtu hapa inawawezesha wateja wake nchi nzima kutuma na kutoa pesa BURE bila makato yoyote .
Tupe maoni yako
0 comments:
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.