ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

Friday, May 19, 2017

SAUTI:- HII NDIYO FIRST 11 KWA YANGA YA MSANII MBOTO HAJI DHIDI YA MBAO FC JIJINI MWANZA.

Msanii muigizaji wa uchekeshaji (Comedy) nchini Tanzania Mboto Haja (kulia) ambaye ni Shabiki maarufu wa Yanga Africans akiwa katika picha ya pamoja na Mtangazaji wa kipindi cha michezo SPORTS RIPOTI cha Jembe Fm Mwanza.
BOFYA PLAY KUMSIKILIZA.

POLISI WAUA MAJAMBAZI JIJINI MWANZA.

Jeshi la polisi mkoani Mwanza limepambana na watu wanaosadikika kuwa ni majambazi ambapo katika mapambano hayo, wapo waliouawa.
Tazama video hapo chini

BENKI YA CRDB YAWAPA SEMINA WANAHISA WAKE, JIJINI ARUSHA LEO


Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya CRDB PLC, Dk. Charles Kimei akizungumza wakati wa ufunguzi wa semina ya Wanahisa wa Benki hiyo, iliyofanyika leo kwenye katika Ukumbi wa Simba uliopo ndani ya Kituo cha Mikutano cha Kimataifa cha AICC, Jijini Arusha.Semina hiyo, itafuatiwa na Mkutano Mkuu wa 22 wa Wanahisa wa Benki hiyo, utakaofanyika kesho Mei 20, 2017.
Mwenyekiti wa semina ya Wanahisa wa Benki ya CRDB, Mwasajuni akiongoza semina hiyo
Meja kuu ikifatilia mada mbalimbali zilizokuwa zikiwasilishwa kwa wanahisa.
Muwasilisha Mada ya iliyohusu Mambo yananoathiri Thamani na Bei za Hisa katika Soko, Laurian Malauri kutoka Orbit Securities akisisitiza jambo wakati akiwasilisha mada yake hiyo.
Katibu wa Benki ya CRDB, John Rugambwa akipitia moja ya vitabu vya mada mbalimbali zilizokuwa zikiwasilishwa kwenye semina ya Wanahisa wa Benki hiyo, iliyofanyika leo kwenye katika Ukumbi wa Simba uliopo ndani ya Kituo cha Mikutano cha Kimataifa cha AICC, Jijini Arusha.
Mkurugenzi wa Masoko, Utafitii na Huduma kwa Wateja wa Benki ya CRDB PLC, Tully Mwambapa akifatilia mada mbalimbali zilizokuwa zikiwasilishwa kwenye semina ya Wanahisa wa Benki hiyo, iliyofanyika leo kwenye katika Ukumbi wa Simba uliopo ndani ya Kituo cha Mikutano cha Kimataifa cha AICC, Jijini Arusha.
Naibu Wakurugenzi  Watendaji wa Benki ya CRDB PLC,  Saugata Bandyopadhyay (kulia) na Esther Kitoka wakiteta jambo, wakati wa ufunguzi wa semina ya Wanahisa wa Benki hiyo, iliyofanyika leo kwenye katika Ukumbi wa Simba uliopo ndani ya Kituo cha Mikutano cha Kimataifa cha AICC, Jijini Arusha.

























WIKI YA ELIMU SENGEREMA 19/5/2017



Maadhimisho ya wiki ya  Elimu yamefanika katika halmashauri ya wilaya ya sengerema ikiwa na kauli mbiu ya (UWAJIBIKAJI KWA ELIMU BORA NA JUMUISHA )
Maadhimisho hayo yamefanyika katika viwanja vya Nyatukala Jeshini ikiwa na lengo la kuhamasisha wananchi katika maendeleo ya elimu .

Akizungumza na waadishi wa habari mratibu wa elimu kata ya Nyatukala mwalimu Jesca Manyanga  amesema wananchi wanatakiwa kushiriki katika swala la maendeleo ya elimu ikiwemo ujenzi wa vyumba vya madarasa na kuacha kuitegemea Serikali. 

Kwaupande wa waalimu wamesema mzazi anatakiwa kutoa ushirikiano kwa kufatilia maendeleo ya mwanafunzi. Nao wanafunzi wamesema mzazi anatakiwa kumpeleka mtoto shule ili kumpa msingi bora kwa maisha ya baadae. BOFYA PLAY KUSIKILIZA.

MHASIBU BILIONEA WA TAKUKURU KUFIKISHWA MAHAKAMANI MUDA WOWOTE.

ALIYEKUWA Mhasibu Mkuu wa Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (Takukuru), Godfrey Gugai, ambaye anadaiwa kukutwa na mali za thamani zaidi ya Sh. bilioni 3.5 sasa anaweza kufikishwa mahakamani wakati wowote.

Chanzo cha uhakika kimeiambia Nipashe kuwa mojawapo ya kosa litakalompeleka mahakamani kigogo huyo wa zamani wa Takukuru, ni kosa la kujilimbikizia mali kinyume cha maadili ya utumishi wa umma. Pia mali hizo zinahusishwa na tuhuma za rushwa.

Kwa mujibu wa tangazo la Takukuru jana, mali za mhasibu huyo wa zamani ni pamoja na nyumba saba za maghorofa zilizopo katika maeneo ya Wilaya ya Kinondoni jijini Dar es Salaam; nyumba tisa za kawaida zikiwamo zilizopo kwenye maeneo mbalimbali ya majiji ya Dar es Salaam na Mwanza na pia Musoma mkoani Mara; viwanja 37 vikiwamo vya kwenye maeneo ya karibu mwa bahari ya Bagamoyo, Ununio, Mbweni na Kigamboni; magari matano na pikipiki moja ambavyo kwa pamoja, thamani yake inakadiriwa kuwa zaidi ya Sh. bilioni 3.5.

Chanzo hicho ndani ya Takukuru kiliiambia Nipashe jana kuwa taratibu zinakamilishwa na mtuhumiwa huyo atafikishwa mahakamani kujibu mashtaka yake wakati wowote kuanzia sasa.

“Yuko mbioni kushtakiwa. Na ndiyo maana lile tangazo limetolewa kwenye magazeti… ukiona tangazo kama lile ujue huyo mtu karibu anashtakiwa,” alisema mtoa taarifa huyo kwa sharti la kutotajwa jina.

“Siwezi kusema ni lini hasa atafikishwa mahakamani. Lakini naweza kukuthibitishia kuwa siku si nyingi… ni suala la kusubiri tu,” chanzo kilisema na kuongeza:

“Mahakama haiwezi kutoa oda ya kuzua mali ya mtu kama hujaishawishi. Lazima uishawishi mahakama kwamba mtu unayemtuhumu yuko mbioni kushtakiwa na ndipo wanakupa oda ya kuzuia mali zake. Kwa hiyo hilo ndilo lililopo kwa sasa. ”

Mei 9 mwaka huu, Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu ilitoa amri ya zuio la mali za Gugai ambaye anakabiliwa na tuhuma za limbikizo la mali kinyume cha Sheria ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa, Namba 11 ya mwaka 2007.

Amri ya zuio la mali za Gugai imetolewa na mahakama hiyo kufuatia ombi la Mkurugenzi wa Mashtaka Nchini (DPP) chini ya kifungu namba 38(1)(a) na (b) cha sheria ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa Namba 11 ya mwaka 2007 katika shauri namba 13 la 2017.

Kufuatia maombi ya DPP, mahakama imeamuru mali zilizotajwa kuwa za Gugai ziwe chini ya zuio la mahakama.

Pia mawakala wake na watu wengine wote wanaomwakilisha wamezuiwa kuuza au kuhamisha umiliki au kuweka dhamana mali zote zilizowekewa zuio.
Aidha, msajili wa hati ameagizwa kusajili zuio hilo kama kizuizi dhidi ya mali zote zilizotajwa.

Pia Msajili Msaidizi wa magari ameagizwa asiruhusu uhamishaji wa umiliki wa vyombo vya moto vilivyowekewa zuio mpaka mahakama itakapoelekeza.

MALI ZENYEWE
Orodha ya mali zilizowekewa zuio la mahakama ni pamoja na nyumba nne za ghorofa moja zilizoko kiwanja na 64 Kitalu B, Ununio, Kinondoni; nyumba tatu za ghorofa moja zilizoko kiwanja na 150 Kitalu 8 Bunju, Kinondoni na nyumba nne zilizoko kiwanja namba 225 kitalu 6, Mbweni JKT, Kinondoni.

Nyingine ni nyumba zilizoko kwenye kiwanja namba 62 na 63 kitalu C, Kinondoni; nyumba iliyoko kiwanja namba 29 kitalu L, Majita, Musoma mkoani Mara; nyumba namba 713 PPF Kiseke, Mwanza na nyumba iliyoko kwenye kiwaja namba 438 kitalu D, Nyegezi, Mwanza.

Aidha, viwanja ni pamoja na kiwanja namba 14 kitalu J, Bunju, Kinondoni; kiwanja namba 47 kitalu B, Mwongozo, Kigamboni; kiwanja namba 184 kitalu B, Buyuni,Temeke; kiwanja namba 103 kitalu L, Kaole, Bagamoyo; kiwanja namba 104 kitalu L, Kaole, Bagamoyo na kiwanja namba 209 kitalu B, Kibaha.

Vingine ni kiwanja namba 195 kitalu 3, Kihonda, Morogoro; kiwanja namba 993 kitalu L, Kiegeya, Morogoro; kiwanja namba 868 kitalu Q, Lukobe, Morogoro; kiwanja namba 34 kitalu K, Kisasa B, Dodoma; kiwanja namba 32 kitalu N, Itega, Dodoma; kiwanja namba 39 kitalu M, Itega, Dodoma; kiwanja namba 24 kitalu B, Chidachi, Dodoma; kiwanja namba 64 Nzuguni, Dodoma; kiwanja namba 230 kitalu B, Nyegezi, Mwanza na kiwanja namba 439 kitalu D, Nyegezi, Mwanza.

Viwanja vingine ni kiwanja namba 275 Kitalu 2, Nyamhongolo, Mwanza; kiwanja namba 277 kitalu 2 Nyamhongolo, Mwanza; kiwanja namba 296 kitalu 2, Nyamhongolo, Mwanza; kiwanja namba 297 kitalu 2, Nyamhongolo, Mwanza; kiwanja namba 286 kitalu G, Nyamagana, Mwanza, kiwanja namba 287 kitalu G, Nyamagana, Mwanza; kiwanja namba 90 kitalu 5, Bugarika, Mwanza; kiwanja namba 126 kitalu A, Makoko, Musoma; kiwanja namba 622 kitalu A, Gomba, Arusha; kiwanja namba 621 na 623, kitalu A, Gomba, Arusha; kiwanja namba 737 kitalu C, Mwambani, Tanga; Kiwanja namba 1,2 na 3 kitalu J,
Mwambani,Tanga; kiwanja namba 4 kitalu J Mwambani, Tanga; kiwanja namba 5 kitalu J, Mwambani Tanga; kiwanja namba 18 kitalu J, Mwambani, Tanga; kiwanja namba 79 kitalu J, Mwakidila, Tanga; na kiwanja namba 11 13 kitalu J, Mwakidila, Tanga.

Magari yaliyozuiwa ni matano, ambayo ni gari namba T 180 DBQ, Mitsubish Canter; gari namba T 581 BQU, Toyota Hillux; gari namba T 814 CSC , Nissan Murrano; gari namba T 679 ASD Toyota RAV 4; gari namba T 913 DHE Suzuki na pikipiki namba MC 837BCL.

Thursday, May 18, 2017

TANZANIA MACHO YAO YOTE LEO YAELEKEZWA GABON.

GABON:- Timu ya soka ya vijana ya Taifa leo Alhamisi inatarajiwa kukata kiu ya Watanzania kwenye mchezo wake wa pili katika mashindano ya Afrika.

Mchezo wa kwanza, Serengeti Boys iliishangaza Mali baada ya kutoka suluhu ya 0-0.

Timu hiyo mpaka sasa imefikisha pointi moja na matokeo mazuri ya leo inaweza kuifanya kusogea hadi nafasi ya kwanza kwenye kundi B.
Picha kwa hisani ya Wapenda soka.

Macho na masikio ya Watanzania yataelekezwa kwenye runinga zao, huku wakiiombea dua ili iweze kushinda ili kusonga mbele katika mashindano hayo yanayoendelea nchini Gabon.

WANACHAMA MWANZA WAANDAA SHEREHE YA UBINGWA VILLA PARK MWANZA KUIPONGEZA YANGA AFRICANS


PICHA KUTOKA MAKTABA:- Aliyekuwa Mstahiki Meya wa jiji la Mwanza Stanslaus Mabula (ambaye ni mbunge sasa wa Jimbo la Nyamagana) wakati akikabidhiwa na wanachama wa Yanga Kombe la Ubingwa lililonyakuliwa na timu hiyo katika msimu wa 2012-2013 kama ishara ya kombe hilo kuingia jijini Mwanza ni katika uwanja wa CCM Kirumba ambapo kulikuwa na mechi ya kirafiki baina ya Mabingwa Yanga na Mabingwa KCC ya Uganda. Matokeo timu hizo zilitoka sare ya bao 1-1.
Na PETER FABIAN, MWANZA.
WANACHAMA na mashabiki wa timu ya Yanga Africans Jijini Mwanza wameandaa sherehe na chakula cha usiku baina yao, wachezaji na viongozi wa juu wa Klabu hiyo watakaoambatana na timu eneo la Villa Park Resort baada ya mchezo wa mwisho wa Ligi kuu ya Vodacom (VPL) utakaopigwa uwanja wa CCM Kirumba jijini hapa. BOFYA PLAY KUSIKILIZA.
Akizungumza na GSENGO BLOG Mjini Mwanza, msemaji wa tawi la Mwanza lililopo mtaa wa Rufiji, Sele Yanga  maarufu kama 'Lialia' alisema kwamba uamuzi huo umefikiwa na wanachama na mashabiki wa timu hiyo ikiwa ni sehemu ya kuwashukuru wachezaji, benchi la ufundi na viongozi kwa ushirikiano na umoja uliowezesha kutwa ubingwa wa Ligi kuu kwa mara ya tatu mfululizo.


Sele alisema kwamba baada ya sherehe hiyo siku ya Jumapili wachezaji, benchi la ufundi na viongozi walioambatana na timu jijini Mwanza watashiriki katika uzinduzi wa matawi mawili ya Mwanza mjini na Mecco majanini lililopo Nyakato ikiwa ni sehemu ya pili ya mashabiki kupiga picha na wachezaji wa timu na viongozi sanjari na kuongeza hamasa na kuwaaga kabla ya kurejea jijini Dar es salaam.


“Tunataraji kuwa na mapokezi makubwa pale uwanja wa ndege wa Mwanza siku timu itakapowasili kuja kucheza na timu ya Mbao FC ya Jijini Mwanza katika mechi ya mwisho ya kufunga msimu wa Ligi kuu ya VPL 2016/2017 ambayo Yanga Africans inatwa taji la Uchampioni kwa mara ya tatu mfululizo, rai yangu kwa wanachama na mashabiki wajitokeze kwa wingi siku ya Jumamosi katika uwanja wa CCM Kirumba,”alisema.


Naye Meneja wa Burudani wa Villa Park Resort, Ramadhan Maganga alikiri kuwa na program ya kuandaa chakula cha usiku (Dinner) kwa viongozi, wachezaji, benchi la ufundi, wanachama na mashabiki wa timu ya Yanga Africans ambapo kwa wanachama na mashabiki watakaotaka kujumuika kwa chakula na wachezaji na viongozi watachangia gharama kidogo.


Maganga alisema kutakuwa na eneo maalum limeandaliwa kwa ajili ya kutoa fursa kwa mashabiki na wanachama ya kupiga picha ya pamoja na wachezaji na viongozi ambapo mlangoni wataingia kwa kuchangia Sh 3,000/- na kutakuwa na burudani ya muziki kutoka katika bendi ya Villa Park ya Super Kamanyola .


Meneja huyo alisema kwamba tayari wameisha toa taarifa kwa barua kwa viongozi wa Klabu hiyo Makao Makuu na kupewa rukusa hiyo ambapo watashirikiana na viongozi na wanachama wakiwemo baadhi ya mashabiki kuanda shughuli hiyo na kutoa wito kwa mashabiki kuzikiliza utaratibu kupitia vituo mbalimbali vya redio na magazeti kujua nini watafanya kabla ya kujumuika na wachezaji na viongozi katika sherehe.

WANANCHI MTAA WA MTAA WA KAGOMU MAHINA WATAKA MKURUGENZI KUTEKELEZA AGIZO LA WAZIRI WA ARDHI

Na PETER FABIAN, MWANZA.
WAKAZI wa Mtaa wa Kagomu na maeneo ya Kata ya Mahina Wilaya ya Nyamagana wamemtaka Mkurugenzi wa Jiji la Mwanza, Kiomon Kibamba kuacha kutengeneza migogoro ya ardhi katika maeneo yao na badala yake apeleke watalaam wake kupima maeneo yao kama alivyoagizwa na Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi hivi karibuni alipokuwa katika ziara yake ya kikazi.

Hayo yalijitokeza jana wakati wa mkutano wa hadhara wa Diwani wa Kata ya Mahina, James Bwire (CCM) ambaye ni Meya wa Jiji la Mwanza uliofanyika katika mtaa wa Kagomu wakimuomba Meya huyo afatilie agizo la Waziri William Lukuvi alilolitoa wakati alipofanya mkutano wa hadhara kwenye viwanja hivyo kutokana na muda aliotoa wa upimaji shirikishi kuwa mdogo ili hali bado wataalamu awajafika kuwapimia.

Martine Magoma akihoji wakati wa maswali kwa Diwani Bwire alisema kwamba muda uliotolewa na Waziri Lukuvi wa Jiji kupima maeneo ya wananchi ni mdogo ambapo mwisho ni Juni 6 mwaka huu lakini hadi sasa wataalamu wa Idara ya Mipango Miji kitengo cha upimaji hawajawahi kuonekana na wananchi hawajui nini kinaendelea na wananchi wako tayari kulipia gharama za Sh 150,000/- za upimaji shirikishi.

Akijibu maswali ya wananchi Meya Bwire alisema kwamba atalifikisha kwa Mkurugenzi ili wataalam wafike kuja kuwapimia na kinachotakiwa ni kujiandaa kulipia gharama hizo kwa kuwasiliana na wenyeviti wa mitaa yenu na Mtendaji wa Kata na hili litasaidia kuanza utaratibu wa kumilikishwa maeneo ya makazi yenu kama alivyoagiza Waziri Lukuvi.

Meya akihutubia wananchi wa mtaa huo alikataa la Mwenyekiti wa mtaa wa Igelegele, Dancan Nyamgoncho (CHADEMA) kwa kuwa ni Mjumbe wa Kamati ya Maendeleo ya Kata (WDC) na maswali yake anatakiwa kuuliza huko na kumtaka akaye chini awachie wengine, akieleza  kusikitishwa kwake na Mkurugenzi wake wa Jiji kutaka kutengeneza mgogoro wa ardhi hilo akitumia mwenyekiti mmoja (hakumtaja) kudai eneo langu ninalojenga Hospitali kuwa ni mali ya wananchi.

 “Kuna mambo yanaendelea pale Jiji ambayo baadhi ya wataalam na watumishi wamekuwa na tabia ya kutafuna fedha za Halmashauri ikiwemo kufanya mambo ya hovyo, sasa tangu nimechaguliwa kuwa Meya nilikaa na Madiwani wenzangu na kukubaliana kukataa Jiji letu kuwa shamba la bibi kwa kuchotwa fedha za walipa kodi kutumika kinyume cha utaratibu kamwe hili sitokubaliana nalo,”alisema.

Bwire alieleza kuwa nachojua Mkurugenzi ni Mtendaji siyo mwanasiasa hivyo ache kutuingilia wanasiasa na kutufatafata kwa kutaka kutuchonganisha na kuturetea migogoro ya ardhi badala yake afanye kazi ya kupima maeneo yetu kama alivyoagizwa na Waziri na kama anahitaji eneo langu basi anilipe fidia na kulichukua awape watu anaowahitaji lakini siyo kuanza kutengeneza visa baada ya kumkatalia ulaji kule Jiji.

Naye Mwalimu Steven Machunda akijitokeza katika mkutano huo na kueleza kuwa eneo analojenga Meya Hospitali ni eneo lake halali kwa kuwa baba yake mzazi na yeye waliamua kumuuzia mwaka 2009 ili kupata fedha wakati anashinda kwenda Chuo cha Ualimu Mrutunguru kutokana na kukosa fedha mwanzoni ndipo familia ikamua kumuuzia kihalali na kumukabidhi nyaraka zote.

Machunda alisema kwamba hata baada ya kumaliza Chuo na kupata ajira  amekuwa akipata msaada kutoka Meya kama mtu ambaye alimpatia mwanga hivyo kama kuna mtu anadai eneo hilo ni lake ajitokeze hapa ili ni muone na kumuhoji hali iliyoibua shangwe kwa wananchi na kumuonya mkurugenzi huyo kuacha kumchonganisha na kiongozi huyo mpenda maendeleo na badala yake atafute njia nyingine ya kumchafua.

MAKAMU WA RAIS WA TANZANIA AWATAKA POLISI WANAWAKE KUCHANGAMKIA FURSA.

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania amewataka askari polisi wanawake kutoka kwenye Shirikisho la Majeshi la Polisi Kusini mwa Afrika (SARPCCO) washiriki kikamilifu katika oparesheni mbalimbali ambazo zinafanyika kwenye ukanda huo kama hatua ya kukabiliana na vitendo vya uhalifu.

Samia Suluhu Hassan, amesema hayo wakati akifungua mafunzo ya siku tatu ya polisi wanawake kutoka nchi wanachama wa SARPCCO katika Ukumbi wa Kimataifa wa Mikutano wa Mwalimu Julius Nyerere jijini Dar es Salaam Tanzania.

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania pia amewahimiza askari polisi wanawake kufanya kazi kwa bidii na kujituma, hatua ambayo itawasaidia kupanda vyeo kama askari wanaume katika maeneo yao ya kazi, na kusisitiza kuwa, muda wa kulalamika kuwa hawapandishwi vyeo umeshapitwa na wakati bali kwa sasa wachape kazi na waonyeshe kuwa wanaweza majukumu yao wanayopangiwa ili waweze kupanda vyeo.
Hamad Masauni, Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani wa Tanzania
Kuhusu utendaji kazi wa polisi wanawake, Makamu wa Rais Bi Samia Suluhu Hassan amewataka polisi hao kutumia mkutano huo wa siku tatu kujadili kwa kina namna ya kuondoa changamoto hizo zinazorudisha nyuma utendaji wao wa kazi.
 
Amesema kama polisi wanawake wataacha majungu na kujenga umoja na mshikamano miongoni mwao watafikia malengo yao haraka hasa katika kushiriki kikamilifu katika mapambano dhidi ya vitendo vya uhalifu ikiwemo biashara ya dawa za kulevya.

Kwa upande wake, Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani Hamad Masauni amesema ana imani kubwa kuwa mafunzo hayo yatasaidia kwa kiasi kikubwa polisi hao wanawake kuimarika ipasavyo katika utendaji wao wa kazi

TADB KUCHANGAMKIA FURSA ZANZIBAR

 aibu Katibu Mkuu wa Wizara hiyo anaeshughulikia Kilimo na Maliasili Bibi Maryam Juma Abdullah (aliyesimama) akiwakaribisha ugeni kutoka Benki ya Maendeleo ya Kilimo ya Tanzania (TADB). 
  
 Mjumbe wa Bodi ya TADB, Bibi Rehema Twalib ambaye ni Mkuu wa Msafara huo (aliyesimama) akizungumza wakati walipotembelea Wizara ya Kilimo, Maliasili, Mifugo na Uvuvi Zanzibar.
 Mkuu wa Msafara wa TADB, Bibi Rehema Twalib (katikati) ambaye pia ni Mjumbe wa Bodi wa Benki hiyo akihimiza jambo wakati wa ziara hiyo. Kushoto ni Mjumbe wa TADB, Bw. Hussein Mbululo na Naibu Katibu Mkuu wa Wizara hiyo anaeshughulikia Kilimo na Maliasili Bibi Maryam Juma Abdullah (kulia).
 Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa Benki hiyo, Bw. Francis Assenga (aliyesimama) akieleza dhima ya Benki ya Kilimo katika kusaidia juhudi za Serikali katika kuinua ukuaji wa uchumi na kupunguza umaskini Tanzania.

 Mkurugenzi wa Mikopo na Biashara wa TADB, Bw. Augustino Chacha (kushoto) akizungumzia fursa za mikopo inayotolewa na Benki hiyo wakati walipotembelea viongozi na wajumbe wa Bodi ya TADB walipotembelea Wizara ya Kilimo, Maliasili, Mifugo na Uvuvi Zanzibar.
 Mkurugenzi wa Mipango wa Wizara ya Kilimo, Maliasili, Mifugo na Uvuvi Zanzibar, Sera na Utafiti, Bw. Sheha Idrissa Hamdan (aliyesimama kushoto) akizungumza wakati Ugeni wa Benki ya Kilimo ulipotembelea wizarani hapo.

Meneja wa Mikopo wa TADB, Bw. Samuel Mshote (kulia) akizungumza wakati wa kikao hicho.
Na Mwandishi wetu,           
Benki ya Maendeleo ya Kilimo ya Tanzania (TADB) imeanza kuchangamkia fursa za uwekezaji katika sekta ya kilimo na mifugo visiwani Zanzibar kwa kuanza mchakato wa kutoa mikopo kwa wakulima na wakazi wa visiwa hivyo wanaojishughulisha katika uchakataji wa mazao ya kilimo visiwani humo.
Akizungumza wakati wa walipotembelea Wizara ya Kilimo, Maliasili, Mifugo na Uvuvi, visiwani humo Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa Benki hiyo, Bw. Francis Assenga alisema kuwa TADB ikiwa chombo cha Muungano ina wajibu kusaidia juhudi za Serikali katika kuinua ukuaji wa uchumi na kupunguza umaskini nchini Tanzania hasa katika kuchagiza mapinduzi na maendeleo katika Sekta ya Kilimo, ambayo inaajiri zaidi ya asilimia 75 ya watu wenye uwezo wa kufanya kazi nchini na pia kutoa kiasi cha zaidi ya  asilimia 65 cha mali ghafi kwa ajili ya viwanda vya nchi.
“Uanzishwaji wa TADB unatokana na Serikali kutambua umuhimu wa uwekezaji wenye tija kwenye maeneo yote ya sekta ya Kilimo na kuleta mapinduzi ya dhati ya Kilimo ili kuwezesha upatikanaji wa mikopo na mitaji ya riba nafuu  ikiwa ni pamoja na kuhamasisha mabenki na taasisi zingine za fedha nchini kutoa mikopo zaidi kwenye sekta ya Kilimo,” amesema.
Bw. Assenga amesema Zanzibar ina utajiri mkubwa kwenye uzalishaji wa viungo ‘spices’ ambayo ni mojawapo wa minyororo ya thamani ya mwanzo inayopatiwa mikopo kwa ajili ya uongezaji wa thamani mazao mbalimbali na Benki ya Kilimo.
Kwa upande wake Naibu Katibu Mkuu wa Wizara hiyo anaeshughulikia Kilimo na Maliasili Bibi Maryam Juma Abdullah ameishukuru Benki hiyo kwa kuiangalia Zanzibar kuwa sehemu ya kimkakati na kutaka kuanza mikopo visiwani humo.