ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

Saturday, June 3, 2023

NSSF YAMSHUKURU RAIS DKT SAMIA SULUHU KUPANUA WIGO KWA WANACHAMA WAO

 

Meneja wa Mfuko wa Taifa wa Hifadhi za Jamii (NSSF) Mkoa wa Tanga Audrey Claudius akizungumza na waandishi wa habari wakati wa maonyesho ya 10 ya Biashara na Utalii yanayoendelea kwenye viwanja vya Mwahako Jijini Tanga
Afisa Mwandamizi wa Shirika la Hifadhi ya Jamii (NSSF) Pangani Haji Sultan kushoto akimpatia kadi kwa mwanachama Grace Poul (kulia)  wakati wa maonyesho ya 10 ya biashara na utalii yanayoendelea kwenye viwanja vya Mwahako Jijini Tanga
Afisa Mwandamizi wa Shirika la Hifadhi ya Jamii (NSSF) Pangani Haji Sultan akitoa elimu kwa wananchi waliofika kwenye banda lao wakati wa maonyesho ya 10 ya biashara na utalii yanayoendelea kwenye viwanja vya Mwahako Jijini Tanga


Na Oscar Assenga,TANGA

MFUKO wa Taifa wa Hifadhi za Jamii (NSSF) Mkoa wa Tanga amesema wanamshukuru Rais Dkt.Samia Suluhu kwa kutoa sapoti ya kupanua wigo kwa wanachama wao.

Hayo yalisema na Meneja wa Mfuko wa Taifa wa Hifadhi za Jamii (NSSF) Mkoa wa Tanga Audrey Claudius wakati wa maonyesho ya 10 ya Biashara na Utalii yanayoendelea kwenye viwanja vya Mwahako Jijini Tanga.

Alisema baada ya Serikali kuona wananchi wengi wanafanya biashara lakini hawana mfuko rasmi wa kuweka mafao yao na kutunza fedha zao kwa ajili ya matumizi ya baadae hivyo waliona waanzisha mfumo mpya wa Niss.

Aidha alisema kupitia mfumo huo wanachama wanaweza kujitunzia akiba zao kila mwezi na hivyo kuwa na sifa ya kupata mafao yao baadae lakini ili waweze kuwa mwanachama wa National Informal Sector Scheme (NISS) lazima waandikishwe wapate namba ya uanachama.

Meneja huyo alisema kwamba wakishapata namba ya uanachama naa akishaanza kuchanga kila mwezi kuna mafao wanayotoa kama mafao ya mateniti kwa wakina mama na mafao ya uzee baada kila kazi kuna mwisho wa ajira.

Hata hivyo alisema kwamba wameendelea kuboresha huduma zao na hivyo kuwezesha waajiri kuweza kufanya malipo ya michango ya wafanyakazi wao wakiwa ofisini au majumbani.

Alisema kwa sababu wanaweza kulipa kupitia mifumo ya kieletroniki ikiwa na Portal kufanya malipo kwa wafanyakazi wako pia mwanachama anaweza kuangalia salio lake akiwa nyumbani kwa kutumia simu yake ya mkononi.

“Sio hivyo tu wale waliofungua madai anaweza kuangalia mchakato wa faili lake limefikia wapi”Alisema

Hata hivyo Meneja huyo alisema kwamba wameamua kushiriki kwenye maonyesho hayo ya ili kutoa elimu inayohusiana na hifadhi ya jamii na kutoa huduma kwa wanachama wao.

Alisema kwamba wanatoa elimu kwa wafanyakazi walioajiriwa na waliojiajiri wenyewe kutokana na kwamba mfuko huo wameanzisha huduma kwa wanachama ambao wanajiingizia kipato wao.

Friday, June 2, 2023

KASI YA MAPAMBANO DHIDI YA FISTULA HOSPITALI YA BUGANDO YAKABIDHIWA VIFAA TIBA

 NA ALBERT G. SENGO/MWANZA

Hospitali ya Rufaa Kanda Bugando jijini Mwanza imepokea vifaa tiba vya upasuaji wa ugonjwa wa fistula ya uzazi kutoka shirika la Americares, vyenye thamani ya shilingi milioni 234.2 vitakavyosaidia utoaji huduma ya matibabu ya ugonjwa huo. Akizungumza Juni 01, 2023 kwenye hafla ya makabidhiano ya vifaa hivyo, Mkuu wa Wilaya ya Nyamagana Amina Makilagi amesema vitasaidia kutoa huduma ya matibabu kwa akina mama wanaougua fistula ya uzazi na hivyo kuzuia vifo vitokanavyo na ugonjwa huo.

Thursday, June 1, 2023

BRELA WATUMIA MAONYESHO YA 10 YA BIASHARA NA UTALII KUTOA ELIMU JUU YA MIFUMO WANAYOISIMAMIA

 

 


Afisa Usajili wa Wakala wa Usajili wa Biashara na Leseni nchini (BRELA) Julieth Kihwelu akizungumza na waandishi wa habari leo kuhusu huduma wanazotoa katika banda lao
Maafisa wa Wakala wa Usajili wa Biasharaa na Lesni nchini (Brela) wakitoa huduma kwa wananchi waliofika kwenye banda lao


Na Oscar Assenga, TANGA.

WAKALA wa Usajili wa Biashara na Leseni nchini (BRELA) wamesema kwamba wameshiriki kwenye maonyesho ya biashara na utalii ya 10 ili kuweza kutoa elimu juu ya matumizi ya mifumo wanayosimamia kwa sasa ambao ni ORS na Tanzania Nationali Business Portal.

Hayo yalibainishwa na Afisa Usajili wa Wakala huo Julieth Kihwelu wakati akizungumza na waandishi wa habari katika banda lao lililopo eneo la Mwahako Jijini Tanga kunakoendelea maonyesho hayo ambapo wameamua kushiriki ili kusogeza karibu huduma kwa wakazi wa mkoa wa Tanga na mikoa ya kanda ya kaskazini.

Alisema kwamba mifumo hiyo ni mikuu pendwa ambayo mwombaji anatakiwa kutumia kuwasilisha ombi lake huku akieleza wanatoa huduma ya kuwafundisha namna ya kutumia mfumo huo kuweza kujisajili.

“Katika mifumo hii mwombaji anatakiwa awe na kitambulisho na Taifa,barua pepe aweze kujisaijili na nitoe wito kwa wajasiriamali nchini kuendelea kusajili alama za biashara zao kwa kuwa alama moja inamtumbisla mtu mmoja”Alisema

Afisa usajili huyo alisema kwamba wasiposajili alama zao wanaweza kutegeneza bidhaa ambayo kuna mtu mwengine anayo na amesajili kwa mujibu wa sheria kwa alama za biashara na huduma.

Hata hivyo aliwashauri wakazi wa Tanga na mikoa ya jirani waenda kupata huduma ya papo kwa papo ambapo kwa sasa wanaendelea kutoa huduma hiyo katika maeneo hayo.

“Tokea 28 mei mpaka Mei 31 tumekwisha kuwahudumia wananchi 35 na tukilinganisha mwaka jana na mwaka huu kuna utofauti na tunategemea kufikia watu wengi kwa kuwatembele kwenye mabanda hususani wajasiriamali kuweza kuwapa ushauri namna ya kuweza kusajili alama za biashara “Alisema Afisa huyo.

Hata hivyo aliwataka wajasiriamali na wafanyabiashara kufika kwenda banda lao kupata elimu na kufanyiwa usajili alama zao za bidhaa zao.

TASAC YATOA NENO KWA WASAFIRI WANAOTUMIA VYOMBO VYA MAJINI

 

 

Afisa Mfawidhi wa Shirika la TASAC Mkoani Tanga Kapten Christopher Shalua  (kushoto) akitoa maelezo kwa Kaimu Katibu Mkuu wa Wizara ya Uwekezaji,Viwanda na Biashara Conrad Millinga wa kwanza (kulia)ambaye alimwakilisha Waziri wa Wizara hiyo kuhusu namna ya kutumia vifaa vya kujiokolea wakati alipotembelea banda  la TASAC katika maonyesho ya 10 ya biashara na utalii yanayoendelea kwenye viwanja vya Mwahako Jijini Tanga
Afisa Mfawidhi wa Shirika la TASAC Mkoani Tanga Kapten Christopher Shalua  (kushoto) akitoa maelezo kwa Kaimu Katibu Mkuu wa Wizara ya Uwekezaji,Viwanda na Biashara Conrad Millinga wa kwanza (kulia) ambaye alimwakilisha Waziri wa Viwanda wakati alipotembelea banda lao katika maonyesho ya 10 ya biashara na Utalii yanayoendelea kwenye viwanja vya Mwahako Jijini Tanga
Afisa Mfawidhi wa Shirika la TASAC Mkoani Tanga Kapten Christopher Shalua  akizungumza na vyombo vya habari katika Banda lao kwenye  maoanyesho ya 10 ya biashara na utalii yanayoendelea kwenye viwanja vya Mwahako Jijini Tanga
Afisa Masoko Mwandamizi wa Shirika la Uwakala wa Meli Tanzania (TASAC) Martha Kelvin (kushoto) akimkabidhi zawadi Kaimu Katibu Mkuu wa Wizara ya Uwekezaji,Viwanda na Biashara Conrad Millinga (kulia) wakati alipotembelea Banda lao


Na Oscar Assenga,TANGA

SHIRIKA la Uwakala wa Meli Tanzania (TASAC) limetoa wito kwa wasafiri wanaotumia vyombo vya Usafiri majini kuhakikisha wanatumia vyombo vilivyo ruhusiwa kisheria kubeba abiria na sio kupanda vyombo vya kusafirisha mizigo ikiwemo majahazi.

Wito huo ulitolewa leo na Afisa Mfawidhi wa Shirika hilo Mkoani Tanga Kapten Christopher Shalua wakati akizungumza na waandishi wa habari katika maonyesho ya 10 ya biashara na utalii yanayoendelea katika viwanja vya Mwahako Jijini Tanga

Aidha, alisema kwa sababu viwango vya vyombo vipo kwenye madaraja tofauti ni vema kila chombo kikatumika kulingana na matumizi huzika yaliyothibitishwa na amewataka  wananchi wa Tanga kwa ujumla kutembelea Banda lao ili kupata elimu zaidi.

Alisema TASAC imeshiriki maonesho hayo kwa ajili ya kuwafikia wananchi hususani wanaoishi maeneo ya fukwe na kuwaelimisha kuhusu Usalama, Ulinzi na Utunzaji wa Mazingira Majini pamoja na majukumu yanayotekelezwa na Shirika hilo kwa Mujibu wa Sheria. 

Hata hivyo alisema kwamba jukumu lao pia ni kuhakikisha wanasimamia Bandari kuhakikisha wanatoa huduma katika viwango vinavyokubalika kimataifa ili kuweza kuchochea ukuaji wa uchumi nchini .

Wednesday, May 31, 2023

KLABU YA KWANZA YA MKONGE YAZINDULIWA

 

 


Bodi ya Mkonge Tanzania (TSB) kwa kushirikiana na Shule ya Sekondari ya Coastal ya jijini Tanga, zimezindua Klabu ya Mkonge kwa wanafunzi wa shule hiyo ambayo imelenga kuwafundisha vijana kuhusu kilimo cha Mkonge na Sekta ya Mkonge kwa ujumla hatua itakayowawezesha kujiajiri baada ya kumaliza masomo.


Akizindua klabu hiyo, Mkurugenzi Mkuu wa TSB, Saddy Kambona amesema wazo la kuanzisha klabu hiyo lilizaliwa kwenye Mahafali ya kidato ya shule hiyo Machi mwaka huu, lakini baadaye ikaonekana isiwe klabu kwa ajili ya Shule ya Coastal pekee bali ianzishwe klabu itakayoshirikisha shule zote za Tanga na vizazi vinavyokuja kushiriki kwenye uchumi huu wa mkonge.

Amesema kwa muda mrefu imezoelekea kwamba elimu yetu haimuandai mwanafunzi kwenda kujitegemea anapomaliza shule, wengi wamekuwa na mtazamo kuwa kazi ya kuajiririwa ndiyo inafaa.

“Kwa hiyo sisi tulitazama wazo la kuwa na klabu za Mkonge kwa maana kama tunasema Mkonge ni Tanga na Tanga ni Mkonge, basi tunataka mtu akifika Tanga aone kweli kama Mkonge ni Tanga, tunategemea aone kwamba Mkonge ndiyo zao kuu la kibiashara.

“Yaani kuanzia anatua uwanja wa ndege anapotua anaona bidhaa za Mkonge barabarani hadi anapofika hotelini anakutana na mazuria ya Mkonge na bidhaa nyingine. Sasa sehemu ya kuanzia ni kuwa na klabu za kuhamasisha si tu kilimo cha Mkonge bali  pia kuhamasisha matumizi ya bidhaa za Mkonge lakini pia kushiriki kwenye kuzalisha hizo bidhaa.

“Baada ya hayo sasa Bodi inakuwezesha kupata elimu, utaalamu kuanzia shambani kulima Mkonge na uongezaji wa thamani, wataalamu wetu watatoa ujuzi huo kwa vijana wa Tanga na nje ya Tanga ili wanapomaliza shule huko wanakokwenda wakawafundishe na wengine,” amesema.

Naye Mkurugenzi wa Maendeleo ya Zao la Mkonge na Masoko, Olivo Mtung’e akizungumzia faida za Mkonge na somo la kuhamasisha wanachama wa klabu hiyo alisema mahitaji ya Mkonge kwa sasa yameongezeka ndiyo maana wanahamasisha wakulima kulima zao hilo.

“Nchi nyingi sasa zinahitaji Mkonge lakini kiasi ambacho tunakilima kwa sasa ni kidogo ndiyo maana baada ya kuingia kwenye kilimo cha wakulima wadogo sasa tunahamasisha na sisi kwenye familia zetu wenye mashamba ya eka moja hadi tatu walime Mkonge kwa sababu kwa sasa hali ya hewa inatusukuma kuelekea huko kwani zao la Mkonge linahimili hali za hew azote ili kuimarisha uchumi wa familia,” amesema.

Mkurugenzi Mtung’e anasema kutokana na hali hiyo, wahitimu hawana haja ya kutafuta ajira kwa sababu Mkonge wenyewe ni ajira kwani ukishapanda baada ya miaka mitatu unaanza kuvuna hadi kwa muda wa miaka 18.

Kwa upande wake mwanafunzi wa shule hiyo na mmoja wa wanachama wa klabu hiyo, Fatuma Mshashi amesema klabu hiyo yenye wanachama 50 ambao kati yao wavulana ni 23 na wasichana 27, inatekeleza malengo mbalimbali ikiwamo kufanya tafiti kuhusu kilimo cha zao la Mkonge ili kuona faida zake, kutoa elimu kwa wanafunzi, walimu, wadau wa elimu kuhusu umuhimu wa zao hilo, kuhamasisha jamii kutumia bidhaa za mkonge, kuwaandaa wanafunzi ili kuja kuwa wataalamu wazuri na wabobevu katika zao la Mkonge na nyingine nyingi.

“Ili kufanikisha malengo katika Klabu ya Mkonge katika shule yetu, tunaomba ofisi yako kwa kushirikiana na Ofisi ya Mwalimu Mkuu itusaidie kukutanishwa na wataalamu wa zao la Mkonge ili kupata elimu na ujuzi wa zao hili, kuwezeshwa klabu kuwa na shamba darasa ambalo litakuwa la kujifunzia hatua zote za uandaaji hadi uvunaji ambapo shamba hilo mlitakuwa mradi wa klabu,” amesema.