Saturday, June 11, 2011
huzuni
Sala ya maziko ya mama Albertina Sisulu, mfuasi mashuhuri wa mapambano dhidi ya ubaguzi wa rangi Afrika Kusini, imehudhuriwa na watu wengi Soweto pamoja na watu mashuhuri wa nchi hiyo na nje akiwemo rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mh. Jakaya Mrisho Kikwete.
Rais Zuma alitaka Bibi Sisulu apewe mazishi ya kitaifa ambapo majenerali walibeba jeneza la mama Sisulu katika ibada hiyo iliyofanywa kwenye uwanja mkubwa wa michezo wa Soweto, ambako Rais Jacob Zuma aliongoza maombolezi.
Alisema: "Enzi imemalizika, na taifa limeondokewa; lakini tuna fahari kwamba tukimjua Mama Albertina Sisulu.
Baadhi ya wakazi wa soweto waliohudhuria mazishi ya mpigania uhuru Albetina Sisulu yaliyofanyika katika kitongoji cha Soweto leo (picha na Freddy Maro)
Tunamzika shujaa na mama wa taifa. ambaye alikuwa jabari na imara katika kupambana na ukandamizi wa ubaguzi wa rangi, huku akiwa na huruma kwa maskini na wanyonge.
Hapo awali, Nelson Mandela alisema Bibi Albertina Sisulu alikuwa mmoja kati ya wazalendo wakubwa wa Afrika Kusini. Bwana Mandela alikuwa mpambe kwenye harusi ya Bi Albertina na hayati Walter Sisulu - ambaye alimshawishi Mandela ajiunge na chama cha ANC..
I know you have travelled the world and this might not really be of any interest, but to me a first timer, felt to share with you some experiences of while in Europe. I am officially destined to Germany but have had the opportunity to travel to neighbouring countries Holland and Denamark. Joseph Sekiku akiwa mpakani mwa Ujerumani na Denmark.
1. The borders are entirely free (hakuna cha afisa uhamiaji, hakuna cha polisi, hakuna cha passipoti, hakuna chochote). Labda vibao vinavyokuonyesha ..sasa unaingia mfano Uholanzi, au Denmark au Ujerumani.
Nikiwa katika ziara hii nimejiuliza maswali mengi.. sisi africa kuna nini? Hata baada ya kuwapo na umoja wa afrika mashariki, kitabu cha pasipoti hujaa mihuri, ukifika katika mipaka yetu, belia kibao.
Nakumbuka kwetu Karagwe (mkoa wa kagera) kwenda Uganda: Unapofika Kyaka kuna belia, na unapofika Mtukula, niliacha belia 3 upande wa Tanzania, na kuingia Uganda, kuna belia 2. Impression ya kwanza, ni kama unapokwenda hapaendeki. Tofauti ambayo nimeiona tuu denmark, wao wanatumia DK Kronners ingawa wamepokea Euro niliponunua chakula katika mgahawa. Hivyo nakutumia picha chache.
Wind turbine kwa ajili ya umeme wa upepo.
2. Nishati: Ninaposikia sakata la umeme nchini kwetu, najiuliza maswali mengi? Mbona huku ulaya wanazima mitambo yao ya kufufua umeme na kuwekeza katika nishati endelevu ya upepo na umeme wa jua?
Solar panel katika majengo
Kwa nini TANESCO au SERIKALI (wizara husika) isiwekeze katika umeme kama huu wa jua au upepo. Nikiangalia tuna bahari na coastline ndefu sana. Je tungeliwekeza katika umeme wa upepo, tusingepata umeme mwingi? Mbona hawa wameweza jamani? Nakuletea picha hizi chache uone huku wanavyoweza...
Inverter za kubadilisha umeme sola kuwa umeme wa AC
Sisi mara Richmondi, mara Songeshaz' mara nini,... hatutafika popote. Jua tunalo la kutosha, upepo tunao wakutosha.
Meli hiyoooo
3. Miundo mbinu: Natoka mkoa wa Kagera na usafiri wa maji tulionao umebaki meli moja tu ya Mv Victoria, ambayo imesafiri katika ziwa hili kwa zaidi ya miaka 40? Na juzi nimetembelea mji wa Panerbug ilipotengenezwa meli ya MV Liemba iliyoko katika mji wa Kigoma, nikakuta sasa wao wameisha fikia uwezo wa kutengeneza meli kubwa sana duniani. Nakuletea picha hapa Angalia meli hiyo ukubwa wake.
Barabara chini ya Ardhi
4. Miundo mbinu, usiseme. Na kwa upande wa barabara, nilikuwa najiuliza ili kasumba na tararatibu za BOMOA BOMOA, nimejiuliza nikasema kuwa, kama watu tayari wanaishi katika mazingira, na sasa unataka kutengeneza barabara, kwa nini barabara hiyo isipite katika maeneo ambayo hayana makazi? si lazima kusumbua utarataibu na makazi ya watu. Barabara kuu inarahisisha uchukuzi.. si miji hata ikibaki pembeni, inaweza kuunganika na barabara kuu kuliko, kubomoa nyumba za watu, n.k?
Samahani kaka kwani picha ni nyingi kidogo na labda hauna bandwidth ya kutosha.
Wako,
Joseph Sekiku
Ujerumani
Mtangazaji mahiri wa Star Tv Yahaya Mohamed (kushoto) akiongoza mada ndani ya kipindi cha asubuhi Tuongee, pembeni yake ni Bw. Mohamed Moledina Mfanyabiashara, Diwani mstaafu na mwanahabari Albert G. Sengo.
Utashi wa viongozi, uwezo duni wa wasimamizi, viongozi kujali maslahi binafsi na kuweka kando maslahi ya Umma ni moja kati ya mambo yaliyojitokeza na kutiliwa mkazo leo hii kwenye kipindi cha 'Tuongee Asubuhi' kupitia Star Tv ambapo mada kuu ilikuwa ni kuijadili Hotuba ya Bajeti ya Serikali ya Mwaka 2011/2012 iliyotolewa jumatano (trh 8 juni) na waziri wa fedha na Uchumi Bw. mustapha Mkulo.
Safari mezani.
Nimefurahishwa na sms nilizokutana nazo kwenye simu yangu moja ikisema 'Pombe, sigara na mvinyo hata vikipanda kwa asilimia ngapi, kiwango chochote mimi na wanywaji wenzangu tutaendelea kunywa tu hadi kieleweke kwani wanywaji hawana bajeti'
Tangu enzi za hayati Mwalimu Julius K.Nyerere wakati huo bia ikiuzwa Tshs 50 kwa chupa hadi leo awamu ya nne ya Jakaya ambapo chupa moja inauzwa kuanzia Tshs. 1,500 katika baa za kawaida hadi Tshs. 3,000 kwenye mahoteli makubwa watumiaji wanakunywa kwa kiwango kilekile na zaidi na zaidi wengine maelfu na makumi matatu wakiongezeka na wala hatujashuhudia watu wakiandamana kudai haki ya punguzo.
Mtunza bustani akiwa bize kuihudumia moja ya engo za bustani ya makao ya Sahara Communication Mwanza.
TAKWIMU ZA BAJETI:
Mfumuko wa bei hadi April 2011......8.6%
Pato la Mwananchi hadi 2010..........sh.770,463
Akiba ya Dola hadi desemba 2010.....$milioni 3,948
Ukuaji wa uchumi mwaka 2010.........7%
Riba katika mabenki mwaka 2009......13.4%
Shilingi kuporomoka mwaka 2009......8.5%
Thamani ya Shilingi kwa dola ...........$1=1432
Uuzaji biashara nje umekuwa 2009....24%
Akaunti katika mabenki...................4,241,610
Matawi ya benki nchini yamefikia.......475
ATM nchi nzima zimefikia.................966
Mapato ya ndani (2010)yameongezeka..8.7%
Deni la Taifa limekuwa hadi..............$millioni 11,380
Nguvu kazi ya Taifa 22,661,280.........52.7%
Wenye ajira milioni 8......................35.3%
Ni mjengo unaoteka hisia zangu kila mara ninapopita eneo hili... Mjengo uliojengwa miaka hiyooo ya zamani muundo wa meli, mali ya Shirika la nyumba la Taifa (NHC) liko mkabala na Ofisi za Tanesco Mwanza.
Anaitwa Anthony Weiner,ni representative aka mbunge wa chama cha Mr Obama hukoo unyamwezini. Huyu mbunge baada suala la Osama kuuawa hivi karibuni kwa sasa ndio anashikilia vichwaa vya habari na mabreking nyuzi huko huko Obama bay(marekani). Juzi kati amekumbwa na kisanga cha ufuska baada ya kugundulika kupitia ma-facebook na ma-twitter kuwa alikuwa akimmuvuzishia binti mmoja kigori wa chuo kimoja mapicha ya ngono yenye kutia hamasa. Mtoni nako kama bongo tu, wambeya, wanafki, vishanshuda si wakazikamata bwana hizo picha!? ikawa noma kwenda mbele hadi sasa! Sasa kazi kwenu nyie wapenzi wa mafacebook na matwitter yenu....
''Bado kidogo tu ningekuwa nimejazia kama Rambo ama anodi shozniga'', of coz kwa kifua hiki ntakutuliza..teh teh teh. Ndivyo kichwani alichokuwa akiwaza bwana Weiner kabla hajazisongesha picha zake kwa mdafada Gennette.
Chunguza mjomba utabaini' Ichekshie vizuri hii pic,: Ni boxer nyeupe iliyo kwenye bodi ya Gavana huyo, huku ze@#$%^&*@ dot jogoo.maungo ni kokolikooooo mbaya. Hiyo ndio kazi ya kujifotoa aliyokuwa akiifanya mbunge Weiner akiwa chumbani kwake. Sijui alikuwa akimvizia mkewe akiwa anaoga bafuni ndo anafanya huu usanii? Sijui''
''Kwa jina naitwa Gennette Cordova, nasoma katika chuo cha Seattle college, ile mipicha ya mbunge yuko kifua wazi pamoja na ile amevaa kile ki-boxer ndani yake nanihiiii #@%%#@ inaonekana ndio zilikuwa zinakuja kwangu, najuuuuuta kumfahamu mbunge Weiner''.
Huma Abedin, (pichani kulia) ndiye mke wa mbunge Anthony Weiner. Huyu mama sio tu kwamba ni msomi bali bata lake ni noomaaa, kwa taarifa yako huyu mama ni mmoja wa wasaidizi wa juu sana wa Hillary Clinton ambaye ni secretary of state huko mbelembele.
kwa msaada wa Bongo shega
Wednesday, June 08, 2011
HABARI
Macho na masikio ya mamilioni ya Watanzania na wadau wa nje, leo yameelekezwa Dodoma ambako Bajeti ya Serikali kwa mwaka wa fedha 2011/12 imesomwa. Wananchi wengi wakiwa na shauku ya kujua mwelekeo wa bajeti hiyo hasa katika kipindi hiki ambacho wanakabiliwa na hali ngumu ya maisha iliyotokana na kupanda kwa bei vyakula na bidhaa za mafuta.Mwananchi akifuatilia hotuba ya bajeti.
::BAJETI::
Serikali imepandisha bei katika vinywaji baridi, bia, sigara, mvinyo, vinywaji vikali, tumbaku, faini kwa makosa ya usalama barabarani (notification).
Serikali itasamehe VAT kwenye vipuri vya zana za kilimo; chakula cha kuku; nyuzi zinazotumika kutengeneza nyavu za kuvulia samaki; kwenye vipuri vya mashine za kunyunyiza na kutifua udongo na mashine za kupanda nafaka.
Waziri wa Fedha na Bajeti 2011/12.
Mkulo amesema inapendekezwa kufanyiwa marekebisho ya kupunguza ushuru wa bidhaa kwenye mafuta mazito ya kuendeshea mitambo kutoka Sh 80 hadi Sh 40 kwa lita, ili kupunguza gharama za uzalishaji wa bidhaa nchini:- Bidhaa hizo ni vinywaji baridi kutoka Sh 63 kwa lita hadi Sh 69 kwa lita; bia inayotengenezwa na nafaka ya nchini na ambayo haijaoteshwa, kutoka Sh 226 kwa lita hadi Sh 249 kwa lita.
Bia nyingine zote, kutoka Sh 382 kwa lita hadi Sh 420 kwa lita; mvinyo uliotengenezwa kwa zabibu inayozalishwa nje ya nchi kwa kiwango kinachozidi asilimia 25, kutoka Sh 1,223 kwa lita hadi Sh 1,345 kwa lita.
Mvinyo uliotengenezwa kwa zabibu inayozalishwa nchini kwa kiwango kinachozidi asilimia 75, utatozwa Sh 420 kwa lita; vinywaji vikali kutoka Sh 1,812 kwa lita hadi Sh 1,993 kwa lita.
Kurekebisha viwango vya ushuru wa bidhaa kwenye sigara ambavyo ni sigara zisizo na kichungi na zinazotengenezwa kutokana na tumbaku inayozalishwa nchini kwa kiwango cha angalau asilimia 75, kutoka Sh 6,209 hadi Sh 6,830 kwa sigara 1,000.
Sigara zenye kichungi na zinazotengenezwa kutokana na tumbaku inayozalishwa nchini kwa kiwango cha angalau asilimia 75 kutoka Sh 14,649 hadi Sh 16,114; sigara nyingine zenye sifa tofauti na hizo za awali kutoka Sh 26,604 hadi Sh 29,264 kwa sigara 1,000.
Tumbaku ambayo iko tayari kutengeneza sigara kutoka Sh 13,436 hadi Sh 14,780 kwa kilo na ushuru wa siga unabaki asilimia 30. Kwa mujibu wa Mkulo, hatua hiyo inatarajiwa kuongeza mapato ya Serikali kwa kiasi cha Sh milioni 99,521.5.
Kuendelea kutoa msamaha wa ushuru wa forodha kwenye mnagari ya mizigo yenye uwezo zaidi ya tani 20; kutoza ushuru wa forodha wa asilimia 10 badala ya 25 kwenye mabasi yanayoingizwa kwa ajili ya mradi wa mabasi ya Jiji la Dar es Salaam, na kutoa msamaha wa ushuru wa forodha kwenye pikipiki maalumu za kubeba wagonjwa.
Hatua hizo za kodi zinazopendekezwa zitaanza kutekelezwa kuanzia Julai mosi, isipokuwa pale ilipoelezwa vinginevyo. jumla ya Sh bilioni 13,525.9 zinahitajika kutumika katika kipindi hicho cha mwaka 2011/12
Uongozi wa klabu ya DC Motema Pembe ya Jamhuri ya Kidemokrasi ya Kongo umetangaza kumuachisha kazi kocha wao Mohamed Nashridine Nabi huku wakiwa katika maandalizi na ya mchezo dhidi ya Simba ya Tanzania kwa ya kuwania nafasi ya kushiriki katika raundi ya makundi ya kombe la shirikisho la Africa.DC Motema Pembe
Timu hizo mbili zitakutana katika mchezo wa kwanza wiki ijayo na kurudiana baada ya wiki mbili.
Motema Pembe kwa sasa imekwenda mjini Goma kucheza mechi za kirafiki za kujiandaa kupambana na Simba huku timu hiyo kwa sasa ikifundishwa na aliyekuwa kocha msaidizi Andy Fulila.
Simba Sc.
Uongozi wa DC Motema Pembe umesema umemuachisha kazi kocha huyo raia wa Ubelgiji, kwa sababu alishindwa kufanya kazi na wasaidizi wake, na pia kushindwa kufanya vyema katika ligi ya nyumbani. Motema Pembe ilifungwa na Ndo Mbosco ya Lubumbashi na TP Elima ya Matadi, kusini mwa Jamhuri ya Kidemokrasi ya Kongo.
Kocha Nabi ameviambia vyombo vya habari vya mjini Kinshasa kuwa klabu haijamlipa mshahara wake katika kipindi ambacho walikuwa wakijadili suala lake. Amesema amesikitishwa na uongozi wa klabu hiyo, kwa kuwa alikuwa na mipango mizuri ya kuiongoza klabu hiyo hadi fainali ya Kombe la Shirikisho.
Mchezo wa kwanza kati ya DC Motema Pembe na Simba utachezwa jijini Dar Es Salaam.