
Timu hizo mbili zitakutana katika mchezo wa kwanza wiki ijayo na kurudiana baada ya wiki mbili.
Motema Pembe kwa sasa imekwenda mjini Goma kucheza mechi za kirafiki za kujiandaa kupambana na Simba huku timu hiyo kwa sasa ikifundishwa na aliyekuwa kocha msaidizi Andy Fulila.

Uongozi wa DC Motema Pembe umesema umemuachisha kazi kocha huyo raia wa Ubelgiji, kwa sababu alishindwa kufanya kazi na wasaidizi wake, na pia kushindwa kufanya vyema katika ligi ya nyumbani. Motema Pembe ilifungwa na Ndo Mbosco ya Lubumbashi na TP Elima ya Matadi, kusini mwa Jamhuri ya Kidemokrasi ya Kongo.
Kocha Nabi ameviambia vyombo vya habari vya mjini Kinshasa kuwa klabu haijamlipa mshahara wake katika kipindi ambacho walikuwa wakijadili suala lake. Amesema amesikitishwa na uongozi wa klabu hiyo, kwa kuwa alikuwa na mipango mizuri ya kuiongoza klabu hiyo hadi fainali ya Kombe la Shirikisho.
Mchezo wa kwanza kati ya DC Motema Pembe na Simba utachezwa jijini Dar Es Salaam.
Tupe maoni yako
0 comments:
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.