|
Mratibu wa mbio za Rock City Marathon 2013, Bw. Mathew Kasonta (kulia) akipokea mfano wa tiketi ya ndege kutoka kwa Mkurugenzi wa Biashara wa Shirika la Ndege la Precision Air (PW), Bw. Patrick Ndekana (kushoto), ambayo itatolewa kwa mshindi wa mwaka huu atakaevunja rekodi ya 1:04:02 iliyowekwa na Kopiro Mwita katika mbio za kilometa 21 za Rock City Marathon mwaka jana. PW pia ni msafirishaji mkuu wa mbio za Rock City Marathon 2013. Wapili kushoto ni Mkuu wa Idara ya Masoko na Uhusiano wa Precision Air, Bi. Linda Chiza, na Meneja Matukio wa kampuni ya Capital Plus International Ltd, Bi. Grace Sanga. |
|
Mkurugenzi wa Biashara wa Shirika la Ndege la Precision Air (PW), Bw. Patrick Ndekana (katikati), akizungumza na waandishi wa habari (hawapo pichani) juu ya udhamini wa shirika lake katika mbio hizo kama wasafirishaji wakuu katika mbio hizo na kutoa tiketi bure kwa mshindi wa mwaka huu atakaevunja rekodi ya 1:04:02 iliyowekwa na Kopiro Mwita katika mbio za kilometa 21 za Rock City Marathon mwaka jana. Kulia ni Mratibu wa mbio hizo Bw. Mathew Kasonta aliyetangaza zawadi zilizoboreshwa kwa mshindi wa mwaka huu, na kushoto ni Mkuu wa Idara ya Masoko na Uhusiano wa Precision Air, Bi. Linda Chiza. |
|
Mratibu wa mbio za Rock City Marathon 2013, Bw. Mathew Kasonta (Kulia) akisisitiza jambo wakati wa mkutano na waandishi wa habari kutangaza zawadi za mbio za Rock City Marathon mwaka huu. Kushoto ni Mkurugenzi wa Biashara wa Shirika la Ndege la Precision Air (PW), Bw. Patrick Ndekana ambaye alieleza juu ya udhamini wa shirika lake katika mbio hizo kama wasafirishaji wakuu katika mbio hizo na kutoa tiketi bure kwa mshindi wa mwaka huu atakaevunja rekodi ya 1:04:02 iliyowekwa na Kopiro Mwita katika mbio za kilometa 21 za Rock City Marathon mwaka jana. |
|
Mratibu wa mbio za Rock City Marathon 2013, Bw. Mathew Kasonta (wapili kulia) akisisitiza jambo wakati wa mkutano na waandishi wa habari kutangaza zawadi za mbio hizo kwa mwaka huu. Wapili kushoto ni Mkurugenzi wa Biashara wa Shirika la Ndege la Precision Air (PW), Bw. Patrick Ndekana ambaye alieleza juu ya udhamini wa shirika lake katika mbio hizo kama wasafirishaji wakuu katika mbio hizo na kutoa tiketi bure kwa mshindi wa mwaka huu atakaevunja rekodi ya 1:04:02 iliyowekwa na Kopiro Mwita katika mbio za kilometa 21 za Rock City Marathon mwaka jana. Kushoto ni Mkuu wa Idara ya Masoko na Uhusiano wa Precision Air, Bi. Linda Chiza na kulia ni Meneja Matukio wa kampuni ya Capital Plus International Ltd, Bi. Grace Sanga. |
Zawadi za Rock City Marathon 2013 zatangazwa
Na Mwandishi Wetu.
Waandaji wa mbio za Rock City Marathon 2013, kampuni ya Capital Plus International (CPI) wametangaza kutenga shilingi milioni kumi kama zawadi katika mbio hizo zilizopangwa kufanyika mwezi Oktoba tarehe 27 katika viwanja vya CCM Kirumba mkoani Mwanza.
Katika kunogesha mbio hizo na kuifanya iwe ya ushindani zaidi, shirika la ndege la Precision Air (PW), mbali na kuwa wasafirishaji wakuu wa Rock City Marathon 2013, limetangaza kutoa tiketi ya kwenda na kurudi jijini Dar es Salaam kwa mshiriki atakaevunja rekodi ya muda wa 1:04:02 iliyowekwa na Kopiro Mwita katika kilometa 21 mwaka uliopita.
Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam jana wakati wa kutangaza zawadi hizo, Mratibu wa mbio hizo Bw. Mathew Kasonta alisema zawadi kwa mbio za mwaka huu zimeboreshwa zaidi na kuongeza kuwa washindi katika mbio za kilometa 21 kwa wanaume na wanawake watajinyakulia shilingi milioni 1.5/- kila mmoja, 900,000/- kwa washindi wa pili na 700,000/- kwa washindi wa tatu.
“Tunahamasisha washiriki kujitokeza kwa wingi kwa sababu zawadi kwa mbio za mwaka huu zimeboreshwa baada ya kupata mwitikio mzuri kutoka kwa wadhamini wetu ambao ni NSSF, Africa Barrick Gold (ABG), Precision Air, Airtel, Bank M, PPF, Nyanza Bottling Ltd, New Mwanza Hotel, Sahara Communications, Continental Decoders na Umoja Switch,” alisema Bw. Kasonta.
Kasonta alisema washindi katika kilometa 5 wa mbio maalum kwa wafanyakazi kutoka makampuni mbali mbali, watapatiwa zawadi za kiheshima na fedha wakati washindi kwenye mbio za kilometa 3 ambazo washiriki wake ni wazee na watu wenye ulemavu wa ngozi wataondoka na zawadi ya shilingi elfu 50,000/- kwa mshindi wa kwanza, 30,000/- kwa wa pili na 20,000/- wa tatu.
“Kwa mbio za kilometa 2 kwa watoto kati ya umri wa miaka 7 mpaka 10, mshindi atajinyakulia shilingi elfu 30,000/-, 20,000/- kwa mshindi wa pili na 15,000/- kwa mshindi wa tatu,” aliongeza.
Alisema mbali na zawadi ya fedha taslim, wasindi watakaoshika nafasi ya kwanza hadi ya tatu katika vipengele vyote (wanawake kwa wanaume) watapatiwa vingamuzi vya Continental, isipokuwa washindi wa kwanza wa kilimeta 21.
Aidha, Mkurugenzi wa Biashara wa Shirika la Ndege la Precision Air, Bw. Patrick Ndekana alisema kuwa udhamini wa shirika lake katika mbio hizo unadhihirisha jitihada za shirika lake za kuendeleza michezo nchi nzima.
“Tunafuraha kuwa sehemu ya wadhamini wa mbio za Rock City Marathon 2013 na tunaamini udhamini wetu utasaidia kuendeleza mchezo wa riadha katika mikoa ya kanda ya ziwa na nchi nzima kwa ujumla.
"Tunajivunia kuunga mkono mbio hizi tukiwa kama shirika la ndege la wazawa kwa kufanya upendeleo kwa wananachi wetu katika kukuza vipaji vyao vya michezo, wakiwa ni mabalozi wazuri wa nchi yetu kama Precision Air inavyoendelea kupeperusha vyema bendera ya nchi hii kwa zaidi ya miaka 22 sasa. Mbio hizi pia zinalenga kukuza utalii katika kanda ya ziwa na kwa vile Mwanza ni kitovu cha pili cha biashara ya Precision Air, shirika tayari limejidhatiti kukuza maendeleo ya mkoa huu. Tayari tunasafiri mara 30 kwa wiki, tukiwa na uhusiano madhubuti na watalii wetu kwa kuwapatia usafiri wa uhakika na ulio salama.
“Shirika linatambua umuhimu wa kuunga mkono jititaha za kufufua mchezo wa riadha ambao ulilitetea taifa heshima kubwa siku za nyuma,” aliongeza Ndekana.
Fomu za usajili wa mbio hizo zinapatikana katika ofisi za kampuni ya Capital Plus International jijini Dar es Salaam, Viwanja vya Nyamagana mkoani Mwanza. Fomu pia zinanunuliwa kwa kupitia Airtel Money kwa kutuma fedha kwenye neno fumbo ‘MARATHON’.
“Utakapomaliza muamala huo, utapokea ujumbe ambao utauwakilisha pale utakapochukua fomu yako ya usajili katika ofisi kuu za Airtel jijini Dar es Salaam pamoja na maduka yote ya Airtel yaliyopo Dodoma, Zanzibar, Mbeya, Arusha na Mwanza,” alisema Kasonta.