ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

Saturday, April 20, 2019

VYOMBO VYA HABARI VYATAKIWA KUWAJIBIKA KWA WANANCHI WAKATI WA UCHAGUZI.

Na George Binagi-GB Pazzo, BMG
Vyombo vya habari nchini Tanzania vimepewa changamoto ya kufanya kazi kwa weledi katika kipindi cha uchaguzi wa Serikali za Mitaa pamoja na Uchaguzi Mkuu kwa kuripoti habari zinazowasaidia wananchi kufanya maamuzi sahihi wakati wa kupiga kura.

Mkurugenzi wa taasisi ya Vyombo vya Habari Kusini mwa Afrika (MISA) tawi la Tanzania, Sengiyumva Gasirigwa aliyasema hayo kwenye warsha ya kuwajengea uwezo viongozi wa vyombo vya habari na taasisi za uchaguzi katika kuangalia na kuripoti habari za uchaguzi, iliyofanyika jijini Dodoma kwa siku tatu kuanzia Machi 15, 2019.

Gasirigwa alisema waandishi wa habari/ vyombo vya habari wanapaswa kuzingatia sheria katika kutekeleza majukumu yao wakati wa uchaguzi ili kuhakikisha kunakuwa na uchaguzi wenye amani hivyo warsha hiyo itawasaidia wakati ambao Tanzania inaelekea kwenye uchaguzi wa Serikali za Mitaa mwaka huu pamoja na Uchaguzi Mkuu hapo mwakani.

Akiwasilisha mada kwenye warsha hiyo, Makamu Mwenyekiti wa MISA Tanzania, wakili James Marenga alisema ipo haja vyombo vya habari kufanya kazi kwa kushirikiana vyema na mamlaka za uzimamizi wa uchaguzi hususani Tume ya Taifa ya Uchaguzi NEC hatua itakayosaidia kuondoa changamoto ambazo zimekuwa zikijitokeza ikiwemo waandishi wa habari kuzuiliwa kuingia kwenye vyumba vya kupigia kura.

“Jukumu la vyombo vya habari ni kuripoti kwa uwazi mchakato wote wa uchaguzi hivyo kuwazuia waandishi wa habari kuingia kwenye vyumba vya kupigia kura inaweza kuibua hofu kwa wananchi wakidhani hakuna uwazi kwenye uchaguzi huo” alisema wakili Marenga.

Baadhi ya washiriki wa warsha hiyo iliyoandaliwa na MISA Tanzani kwa kushirikiana na Ubalozi wa Marekani, akiwemo Joyce Shebe kutoka Clouds Media Group walisema itawasaidia kutambua sheria mpya za vyombo vya habari na hivyo kufanya kazi kwa welezi katika kuripoti habari za uchaguzi, kutambua maswali sahihi ya kuuliza yatakayojibu kiu ya wananchi na hivyo kufanya maamuzi sahihi wakati wa kupiga kura.
Mkurugenzi wa taasisi ya Vyombo vya Habari Kusini mwa Afrika (MISA) tawi la Tanzania, Sengiyumva Gasirigwa akizungumza wakati wa warsha hiyo.
Wakili wa Mahakama Kuu Tanzania ambaye pia ni Makamu Mwenyekiti wa Misa Tanzania, Wakili Jmaes Marenga akiwasilisha mada kwenye warsha hiyo.
Mmoja wa washiriki wa warsha hiyo akichangia mada.
Baadhi ya washiriki wa warsha hiyo.
Washiriki wakifuatilia kwa umakini warsha hiyo.
Baadhi ya viongozi wa vyombo vya habari Tanzania wakifuatilia warsha hiyo.
Mkuu wa Idhaa ya Kiswahili ya Sauti ya Amerika (V.O.A), Dkt. Mwamoyo Hamza (katikati) akichangia mada kwenye warsha hiyo.
Mhariri Mtendaji wa kampuni ya Jamhuri Media, Deodatus Balile (kushoto) pamoja na Kaimu Msemaji wa Serikali, Zamaradi Kawawa (kulia) wakifuatilia kwa umakini warsha hiyo.

NGUMI KUPIGWA JUMAPILI YA PASAKA CCM MWINYI MKUU MAGOMENI

Bondia Vicent Mbilinyi kushoto akitunishiana misuli na Rojas Masamu baada ya kupima uzito kwa ajili ya mpambano wao utakaofanyika CCM Mwinyi Mkuu magomeni Mapipa katikati ni Promota wa mpambano uho Rajabu Mhamila 'Super D' kutoka SUPER D BOXING PROMOTION
Promota wa mchezo wa masumbwi nchini Rajabu Mhamila 'Super D' kutoka Super D Boxing Promotion akiwainu mikono juu bondia Vicent Mbilinyi kushoto na Rojas Masamu baada ya kupima uzito kwa ajili ya mpambano wake wa Pasaka utakaofanyika CCM Mwinyimkuu Magomeni Mapipa

Bondia Vicent Mbilinyi akipimwa Afya na DOKTA Dolnad Madono

Bondia Ramadhani Mbegu 'Migwede' akipimwa Afya na DOKTA Dolnad Madono

Bondia Saluim Tandu akipimwa Afya na DOKTA Dolnad Madono

Promota wa masumbwi nchini Rajabu Mhamila 'Super D' katikati akiwainua mikono juu mabondia Ramadhani Mbegu 'Migwede' kushoto na Bilali Rashidi baada ya kupima uzito kwa ajili ya mpambano wao utakaofanyika jumapili ya Pasaka katika ukumbi wa CCM Mwinyi Mkuu nagomeni Mapipa

Bondia Ramadhani Mbegu 'Migwede' kushoto akitunishiana misuli na Bilali Rashidi baada ya kupima uzito kwa ajili ya mpambano wao utakaofanyika katika ukumbi wa CCM Mwinyi Mkuu Magomeni Mapipa siku ya sikukuu ya Pasaka

Promota Rajabu Mhamila 'Super D' katikati akiwainua mikono juu mabondia Salum Tandu kushoto na Gelard Mkude ambao watacheza siku ya jumapili ya pasaka April 4 katika ukumbi wa CCM Mwinyimkuu

Bondia Sunday Kiwale 'Moro Best' kushoto akitunishiana misuli na Luckman Ramadhani baada ya kupima uzito kwa ajili ya mpambano wao uakaofanyika jumapili ya Pasaka April 21 katika ukumbi wa CCM mwinyimkuu Magomeni Mapipa katikati ni Promota wa mpambano uho Rajabu Mhamila 'Super D' KUTOKA SUPER D BOXING PROMOTION

Promota wa mchezo wa masumbwi nchini Rajabu MHAMILA 'Super D' kushoto akiwainua mikono juu mabondia Sunday Kiwale 'Moro Best' na Luckman Ramadhani baada ya kupima uzito kwa ajili ya mpambano wao wa Pasaka utakaofanyika katika ukumbi wa CCM Mwinyi Mkuu Magomeni Mapipa

Bondia Bakari Mbede kushoto akitunishiana misuli na Shomari Milundi baada ya kupima uzitio na Afya kwa ajili ya m,pambano wao utakaofanyika siku ya sikukuu ya Pasaka April 21 katika ukumbi wa CCM mwinyi Mkuu katikati ni Promota wa Mpambano uho Rajabu Mhamila 'Super D' KUTOKA sUPER d Boxing Promotion

Promota Rajabu Mhamila 'Super D' katikati akiwangalia mabondia Salum Tandu kushoto na Gelard Mkude  walivyokuwa wakipigiana mikwala mabondia hawo watacheza siku ya jumapili ya pasaka April 4 katika ukumbi wa CCM Mwinyimkuu

Promota wa mchezo wa masumbwi nchini Rajabu Mhamila 'Super D' katikati akiwainua mikono juu mabondia Sandal Nyambala kushoto na Ahmad Kombo baada ya kupima uzito kwa ajili ya mpambano wao wa Pasaka utakaofanyika katika ukumbi wa CCM Mwinyimkuu Magomeni Mapipa

Mabondia Sandal Nyambala kushoto akitunishiana misuli na Ahmad Kombo baada ya kupima uzito kwa ajili ya mpambano wao utakaofanyika siku ya Pasaka katikati ni Promota Rajabu Mhamila 'Super D' 

WAKRISTO WAKUMBUSHWA KUSAMEHEANA.


Dar es Salaam. Watanzania wametakiwa kutumia Sikukuu ya Pasaka kutoa msamaha kwa wote waliowakosea ili kuendeleza amani ya nchi kama Yesu alivyoamua kuwasamehe waliomkosea wakati aliposulubiwa msalabani.

Akihubiri katika kanisa la Jehovah Mercy Ministry, Chanika Jijini Dar es Salaam, Nabii kiongozi wa kanisa hilo, Richard Godwin amesema njia pekee ya kuendeleza amani kwenye taifa lolote ni watu wake kusamehe wanapokoseana wao kwa wao. Amesema watu wengi wamepata magonjwa yasiyo ya kuambukiza yakiwemo ya moyo na hata kupoteza maisha kwa sababu ya kutosamehe.

“Usibebe mzigo mkubwa moyoni, unamshikilia mtu miaka nenda rudi hutaki kutoa msamaha kabisa. Wewe ndiye unayejiumiza na ili upate amani ya moyo wako lazima ujue kusamehe,” amesema nabii huyo na kuongeza kuwa msamaha wa kweli pia lazima uendane na utoaji wa haki.

Amesema wananchi wanaweza kuwa na amani, furaha na kusamehe ikiwa nao wanatendewa haki na mamlaka husika.

“Nikisema haki namaanisha kuna wizara inayohusika ya Sheria na Katiba ambayo mahakama ipo chini yake lakini pia, ulinzi kwa raia kupitia wizara ya ulinzi,” amesisitiza Godwin.

Amesema Pasaka ndio kipindi pekee ambacho Wakristo wanaungana pamoja kupokea wokovu unaoambatana na msamaha toka kwa mwokozi wao Yesu Kristo.

“Biblia inasema aliyabeba madhaifu yetu na kwa kupigwa kwake sisi tumepona. Ina maana aliteseka kwa ajili yetu maana yake tumepokea msamaha bure kabisa. Samehe ndugu yangu, uwe mtu wa haki usimuonee yeyote yule,” amesisitiza.

Mchungaji mwingine wa kanisa hilo, Paul John ‘Master Kinga’ alisema kanisa hilo limeendesha semina ya siku saba kwa waumini wake kwa ajili ya kuipokea Pasaka.

“Watu wamejua kwa nini Yesu alikufa na siku ya tatu alifufuka na wanawezaje kupokea msamaha alioutangaza?” amesema.

ALICIOUS ANAPENDA SIASA - AMTAJA MAGUFULI - ATUA MWANZA


Eyoo... Chungulia kichupa kina maelezo yote.
Mwanamuziki Mkongo anayeishi nchini Kenya wakuitwa Alicious (katikati) akibadilishana mawazo na Meneja wa Burudani na Matukio, Ramadhani Maganga wa Villa Park Resort ya jijini Mwanza mahala ambapo inakwenda kushushwa burudani ya kutakata katika sikukuu ya Pasaka Tarehe 21 April 2019. Kulia ni mwanahabari toka Jembe Fm Mwanza Albert G. Sengo ambaye pia ni CEO wa Gsengo blog

Friday, April 19, 2019

ZANTEL YAPATA VYETI VYA KIMATAIFA VYA ISO VYA MAZINGIRA, AFYA NA USALAMA MAHALI PA KAZI


Kampuni ya mawasiliano ya Zantel, imepata vyeti 2 vya ubora wa kimataifa (ISO), kutokana na kukidhi vigezo vya kimataifa katika  kutekeleza kwa ufasaha kuendesha biashara zake kwa kuzingatia utunzaji wa mazingira  (ISO 14001:25),na cheti kipya cha utekelezaji wa  mifumo ya Afya na Usalama mahali pa kazi (ISO 45001:2018).

Mafanikio haya ni mwendelezo, mwaka jana mwishoni baada ya kufanyiwa ukaguzi ilipata cheti cha kimataifa cha ISO kutokana na kukidhi vigezo vya utekelezaji mifumo ya Afya na Usalama Mahali pa Kazi kwa ufasaha (OHSA 18001:2007).

Kutokana na ukaguzi huo, ilibainika inatekeleza vizuri mifumo ya Afya na Usalama, wakaguzi walipendekeza ZANTEL ibadilike kutoka cheti cha zamani cha OHSA 18001:2007 na kupatiwa cheti kipya cha ISO ambacho kimeanza kutolewa kwa makampuni yanayokidhi vigezo mwaka jana.

Akiongelea mafanikio haya ya kampuni kupata vyeti vya kimataifa vya ISO,Mkuu wa kitengo cha Teknolojia  Mawasiliano wa Zantel,John Sicilima alisema “Tunayo furaha kukidhi viwango vya ukaguzi na kupewa vyeti vya ubora vya kimataifa.Hatua hii inadhihirisha umakini wetu tunavyozingatia suala la afya na Usalama kuanzia kwa wafanya kazi ,wadau mbalimbali tunaoshirikiana nao  na  katika mazingira tunayofanyia shughuli zetu,kama malengo yetu tuliojiwekea mojawapo ni kuendesha shughuli zetu tukiwajibika kulinda usalama wa jamii katika maeneo tunayofanyia biashara sambamba na kuongeza hadhi ya kampuni yetu”.

Alisema baada ya kupata vyeti vya kimataifa vya ISO, Zantel itahakikisha inafanikisha dhamira yake katika maeneo ya afya na tahadhari katika usalama, athari za mazingira, Kutekeleza kanuni za usalama kwa vitendo, mifumo ya uharibifu wa mazingira wa sauti na kuhakikisha tahadhari zaidi na athari zinadhibitiwa ipasavyo.

“Utekelezaji wa maelekezo yanayoendana na vyeti hivi yatawezesha taswira ya Zantel kuwa nzuri zaidi, kuongeza uhusiano mzuri na jamii na kupanua wigo wa masoko ya biashara zetu na wadau wengine,” aliongeza Sicilima.

Cheti cha kimataifa cha ubora cha ISO 45001 taasisi yenye kuwa nacho, inapaswa kuwa inatekeleza mifumo ya Afya na Usalama kwa ufasaha, lengo kuu likiwa ni kulinda Afya na usalama kwa wafanyakazi na watu wengine.

Utoaji wa cheti kipya cha ISO 45001, umeanza mwezi Machi mwaka 2018, kuhakikisha kanuni za Afya na Usalama zinapewa kipaumbele duniani kote. Taasisi ya Kimataifa ya Kusimamia Ubora (ISO) imelenga kuhakikisha matukio ya ajali na magonjwa yatokanayo na shughuli za kazi yanapungua sambamba na kuwezesha umri wa kuishi kuogezeka.

Kutokana na kuanza kutolewa kwa cheti cha ubora cha kimataifa cha ISO 45001, taasisi ambazo zilikuwa katika mfumo wa cheti cha zamani cha ISO ikiwa ni pamoja na cheti cha OHSAS 18001 yanapaswa kubadilika na kupata cheti kipya kabla ya kufikia mwezi Machi mwaka 2021.

AJALI YA HIACE IGOMBE MWANZA YAUWA WAWILI


WAKATI zikiwa zimesalia siku tatu tu wakristo nchini na kwingineko duniani wapate kujumuika katika maadhimisho ya kufa na sikukuu ya kufufuka kwa Bwana Yesu Kristo, ajali mbaya ya gari la abiria linapata ajali na kuuwa watu wawili papo hapo huku wengine 17 wakijeruhiwa. 

Thursday, April 18, 2019

BODABODA 8 WASHIKILIWA POLISI KWA TUHUMA ZA MAUAJI YA ASKARI.


Na, Clavery Christian Bukoba.

Jeshi la Polisi mkoani Kagera linawashikilia waendesha pikipiki 8 maarufu bodaboda kwa kumshambulia kwa kipigo kikali MG.433651 Steven Sospeter kilichopelekea kupoteza maisha.
Kamanda wa polisi mkoa wa Kagera amesema hayo wakati akiongea na waandishi wa habari Ofisini kwake ambapo amesema kuwa MG Steven Sospeter mhaya, miaka 37 ambaye alikuwa askali mgambo na mkaazi wa Gera alifariki dunia wakati akipatiwa matibabu baada ya kushambuliwa kwa kupigwa na fimbo, mawe, ngumi na mateke sehemu mbalimbali za mwili wake na kundi la bodaboda baada ya marehemu kutuhumiwa kuiba pikipiki MC.799 BZY aina yaBajaji Boxer rangi nyekundu mnamo tarehe 15/04/2019 majira ya saa 21:00 usiku.

Malimi amesema kuwa Steven na wenza ke wawili wakiwa kazini eneo la kizuizi barabarani iliyopo kijiji cha Gera walimkamata Justine Jackson mhaya miaka 20 ambaye ni bodaboda na mkazi wa kyakakombo akiwa na pikipiki hiyo MC 799 BZY akiwa anasafirisha mkaa gunia mbili kwenda bukoba mjini bila kibali ambapo walimkamata na kumpa maelekezo ya kulipia faini ambapo kijana huyo alikosa pesa ya kulipia faini na kuamua kukaa na pikipiki hiyo mpaka asubuhi na ilipofika asubuhi ya tarehe 16/04/2019 ambapo marehemu alichukua pikipiki hiyo na kuonda nayo kwa ajiri ya kwenda kuikabidhi bunazi kwenye ofisi ya wakala wa mistu na ndipo alipovamiwa na bodaboda hao akiwa amefika eneo la kajunguti na kumrudisha hadi eneo la mto nkenge na kuanza kumpga hadi kupoteza fahamu ambapo polisi walikuja kumuokoa.

Kamanda Malimi amesema kuwa Polisi walimpeleka kituo cha polisi kyaka na kufungua kesi ya kujeruhi kisha kumpeleka katika kituo cha afya BUNAZI na kulazwa lakini hali yake ilizidi kuwa mbaya na hatimaye Aprili 17 mwaka huu alifariki dunia ambapo amesema kuwa chanzo cha tukio hilo ni bodaboda kujichukulia sheria mkononi.

INAOGOFYA - UNYANYASAJI NA VITENDO VYA UKATILI HUANZIA NYUMBANI...!!?PAMOJA na kuwacha huru watoto wao kujiamulia na kufanya wanavyofanya, ni kwanini wenzetu mataifa ya mbele wameliweza suala la kuwadhibiti watoto wao kimaadili nasi tunaowabana na kuwachunga tukashindwa? 

Kila siku tunasema na kufundisha namna mtoto akipata tatizo shuleni au mtaani mahala sahihi pa kukimbilia ni kwa wazazi, walezi au kwa waalimu lakini tunasahau kumwelekeza mtoto huyo huyo, wapi pa kukimbilia pale anapopata tatizo linalichangiwa na wazazi, walezi au familia.

Jeh wazazi wanapata changamoto gani katika kutoa elimu kwa watoto wetu?

Kwa kuliona hilo Shirika la Umoja wa Mataifa la elimu, sayansi na utamaduni, UNESCO kwa kushirikiana na Wizara ya Elimu ya Tanzania na mashirika mengine ya Umoja wa Mataifa UnfPA pamoja na UN WOMEN wameandaa semina ya siku tatu kwa walimu wa shule za sekondari na msingi wilayani Sengerema kuwafundisha mbinu na namna ya kuwasaidia watoto wanaokabiliana na changamoto za vitendo vya ukatili kutoa elimu ya Afya kujitambua kwa jinsi na jinsia kwa wanafunzi wa darasa la 2 hadi wanafunzi wa sekondari kidato cha 4.

ASASI YA LSF YATEUA OFISA MKURUGENZI MKUU MPYA.


Lulu Ng’wanakilala Ofisa Mkurugenzi Mkuu wa LSF kuanzia Mei 1 2019

Na Mwandishi Wetu

Shirika la Legal Services Facility (LSF) jane limetangaza rasmi uteuzi wa Bi Lulu Ng’wanakilala kama Ofisa Mkurugenzi Mkuu mpya. Katika kutekeleza kazi hii, anachukua nafasi ya Bw Kees Groenendijk, ambaye ameongoza asasi hii tangu kuanzishwa kwake mwaka 2011.

Bi Ng’wanakilala, ambayeana Shahada ya Pili katika Sheriaya Kimataifa na Haki za Binadamu kutoka Chuo Kikuu cha Livraserpool nchini Uingereza na Shahada ya Kwanza ya Sheria kutoka Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, pamoja na mambo mengine, amedhamiria kufanya mabadiliko ya kitaasisi lengo kuu likiwa ni kuifanya LSF kupanua wigo utoaji wa msaada wa kisheria kwa mamilioni ya wanaume na wanawake maskini Tanzania wenye matatizo mbalimbali ya kisheria.

Anachukua uongozi wa asasi isiyo ya kiserikali ambayo imewezesha uwepo wa wasaidizi wa kisheria Tanzania Bara na Zanzibar, wanaotao msaada wa kisheria kwa watanzania wenye matatizo ya kisheria na kuwawezesha kupata haki zao.

Akitoa mtazamo wake, Afisa Mkurugenzi anayemaliza muda wake, Bw. Mkurugenzi Bw Groenendijk, anasema: “Tangu mwanzoni kwa msaada wa washirika wa maendeleo DANIDA naDfID, LSF imefanya kazi kubwa ya kuweka mazingira yaliyowezesha upatikananji wa huduma za kisheria kwa watu maskini hasa wanawake, kuwa rahisi na wakuaminika.”

Kwa kupitia mtandao mkubwa wa takriban wasaidizi wa kisheriahai 3,000 nchi nzima, “tumeweza kuleta mabadiliko chanya kwa maisha ya watu maskini, mpaka kwa wale waishio wa pembezoni. Kwa umuhimu unaofanana ni ukweli kwamba LSF inafanya kazi na asasi zingine za kiraia na serikali kuwezesha mabadiliko ya sera na sheria kwa lengo la kuhakikisha haki inabakikuwa sifa muhimu ya maisha ya kila siku ya mamilioni ya Watanzania. Ofisa Mkurungenzi Mkuu mpya atakuta misingi bora yenye lengo la kutekeleza maono yake, na hatimae kukuboresha misingi na maono hayo zaidi na zaidi.”

“Ng’wanakilala analeta nguvu na kasi mpya ya uongozi wenye mawazo mapya, uzoefu na maarifa mapana aliyonayo katika taaluma na nyadhifa mbalimbali alizoshika  ambazo ni muhimu katika kuipeleka LSF mbele na kuwawezesha maelfu ya wananchi kuendelea kupata na kutambua hakizao,” anaongezaBw Groenendijk.

Akimkaribisha Ofisa MkurugenziMkuumpya, Mwenyekiti wa Bodiya LSF, Dk Benson Bana anasema: “Huduma za kutoa msaada wa kisheria ni kiini kinachoelezea kazi ya LSF. Kwa miaka hii michache asasi hii imebadilisha maisha ya watu wengi wa kawaida kwa kutilia mkazo kuwainua wanawake ambao kwa mfumo dume uliopo wamekuwa hawafaidiki sana. LSF, kwa ushirikiano kutoka serikalini, inaendelea kuwezesha upatikanaji wa huduma za msaada wa kisheria kila siku bila malipo yoyote. Ofisa Mkurugenzi Mkuu anayekuja ataunganisha vizuri watu hawa na kwa kutumia utajiri wa uzoefu wake ataweza kuiwezesha LSF kukuza fursa kwa watu wengi zaidi kunufaika na kujitoa kwetu kwa upatikanaji wa haki.”

Kablayauteuzi wake LSF, Ms Ng’wanakilala alishika nyadhifa mbalimbali, ikiwa ni pamoja na kuwa mwenyekiti wa Mtandao wa UtepeMweupe kwa Uzazi Salama Tanzania (WRATZ), mjumbe wa KamatiyaUtendajiyaMradiUnaoongoza wa Uamzi Salama (LSC), Mkurugenzi wa BodiyaWanawake wa Mafanikio Tanzania (TWA) namwanzilishinamjumbe wa BodiyaKituo cha MawasilianonaMaendeleo Tanzania (TCDC).

Amefanya kazi kubwa katika mabadilikoya sera na kwenye vikundi vya kitaalamu vinavyoratibu, wezesha na ameshiriki katika hatua mbalimbali za utekelezaji, ikiwani pamoja na Mkakati wa Kukuza Uchumi na Kupungu za Umaskini Tanzania (Mkukuta). Bi Ng’wanakilalanimwanachama pia wa Chama cha WanasheriaTanganzania Bara (TLS).

Uteuzi wa Bi Ng’wanakilalaunaanzarasmi Mei 1, 2019.

Wednesday, April 17, 2019

WAZIRI MPINA AWATANGAZIA NEEMA WANAOKULA SAMAKIWAZIRI wa Mifugo na Uvuvi, Luhaga Mpina amezindua mafunzo kwa wavuvi yenye lengo la kuzifahamu zana za uvuvi zinazoruhusiwa kwa mujibu wa sheria na kutambua fursa zilizopo katika sekta ya uvuvi hali itakayoleta tija kwa maisha yao na ukuaji wa uchumi wa Taifa.

Amesema licha ya Tanzania kuwa na eneo kubwa la uvuvi katika kipindi cha mwaka 2016/ 2017 Tanzania ilitumia jumla ya sh. bilioni 56 ambapo mwaka 2017/ 2018 imefikia sh Bilioni 150 kwa ajili ya kuagiza samaki kutoka nje ya nchi fursa ambayo ingetumiwa na wavuvi wa Tanzania kukuza uchumi wao.

Akizindua mafunzo hayo kitaifa kwa wavuvi katika mwalo wa Kilindoni, Wilaya ya Mafia mkoani Pwani, Waziri Mpina amesema kufuatia wavuvi wengi na sekta ya uvuvi kwa ujumla kukumbwa na changamoto nyingi ndio iliyoisukuma wizara yake kuanzisha mafunzo hayo ili kujenga uelewa wa pamoja na kuondoa kasoro zilizopo.

Mpina alisema pia watafundishwa juu ya matumizi ya zana bora za kisasa za uvuvi, watafundishwa namna ya kuandaa samaki na kuwahifadhi ili kupunguza hasara ya mavuno pamoja na fursa za masoko, utunzaji wa mazingira ili kulinda ikolojia na bioanuai zilizopo majini ili kuwa na uvuvi endelevu.

HIKI HAPA KITUO CHA AFYA KILICHOWEZA KUENDANA NA KASI YA JPMUkitaka kipimo halisi cha kasi ya Serikali ya awamu ya tano ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Joseph Magufuli basi video hii ni kielelezo tosha.

Timu yangu imeniomba nisitie neno zaidi  ya kutoa fursa kwako kusikia na kuona kilichomo. KARIBU 

Tuesday, April 16, 2019

NAIBU MEYA MANISPAA YA IRINGA APIGA MARUFUKU KUNUNUA CHAKI NJE YA KIWANDA DUSTLESS SMART CHALK

Naibu meya wa manispaa ya Iringa Joseph Lyata akiwa kiwandani hapo na kupiga marufuku kwa shule zote za manispaa ya Iringa kununua chaki kutoka nje ya kiwanda Dustless Smart Chalk kilichopo manispaa ya Iringa kwa kuwa kiwanda hicho kinatengeneza chaki zilizo bora
Naibu meya wa manispaa ya Iringa Joseph Lyata akiandika kwa kutumia chaki zinazotengenezwa na kiwanda Dustless Smart Chalk kilichopo manispaa ya Iringa kinachotengeneza chaki zilizo bora
Naibu meya wa manispaa ya Iringa Joseph Lyata akipata maelezo ya jinsi gani chaki hizo zinavyotengenezwa katika kiwanda Dustless Smart Chalk kilichopo manispaa ya Iringa
Hizi ni baadhi ya chaki zinazotengenezwa katika kiwanda Dustless Smart Chalk kilichopo manispaa ya Iringa
 NA FREDY MGUNDA,IRINGA.
 
NAIBU meya wa manispaa ya Iringa Joseph Lyata amepiga marufuku kwa shule zote za manispaa ya Iringa kununua chaki kutoka nje ya kiwanda Dustless Smart Chalk kilichopo manispaa ya Iringa kwa kuwa kiwanda hicho kinatengeneza chaki zilizo bora na zinazofaa kutumiwa katika shule zote.

Akizungumza na blog Naibu meya,alisema kuwa kiwanda cha chaki kilichopo katika manispaa ya Iringa kinatengeneza chaki zilizo na kiwango bora cha kutumiwa na walimu wakati wa kufundisha ili kuinua uchumi wa kiwanda hicho.

“Mimi nimekuwa mwalimu kwa takribani miaka nane katika shule mbalimbali na nimefundisha na kuandikia chaki kutoka katika kampuni mbalimbali ila hizi chaki ambazo zinatengemezwa hapa manispaa ya Iringa zinaviwango vinavyotakiwa” alisema Lyata

Lyata alisema kuwa haiwezekani kunakiwanda cha kutengeneza chaki lakini walimu wanatumia chaki kutoka nje ya manispaa ya Iringa kutasababisha kuua mitaji na viwanda hivi vya vijana wabunifu ambao wapo manispaa hapa.

“Tusipo waunga mkono vijana na kiwanda hiki cha kutengeneza chaki tutakuwa tuaua uchumi wa wananchi wa manispaa ya Iringa hivyo lazima walimu wa manispaa ya Iringa kuwaamuru kutumia chaki zinazotengenezwa na kiwanda chetu kilichopo hapa manispaa ya Iringa” alisema Lyata

Aidha Lyata aliwaomba wadau mbalimbali kuendelea kuwasaidia vijana hao wenye kiwanda cha Dustless Smart Chalk ambacho bado kinahitaji vitu vingi ili kuwa na kiwanga kikubwa zaidi na kuongeza ajira kwa vijana wengine.

“Wadau naombe mjaribu kuwatembelea wale vijana walipo pale Ipogolo SIDO kwa kuwa wanafanya kazi kubwa na ubunifu mkubwa kwa lengo la kufanikiwa kuja kuwa na kiwanda kikubwa ambacho kitasaidia kuongeza ajira kwa vijana wengine” alisema Lyata

Lyata alisema kuwa kiwanda cha Dustless Smart Chalk kinakabiliwa na upungufu wa vifaa na vitendea kazi ambavyo vinarudisha nyuma kazi zao hivyo wadau wanatakiwa kujitokeza na kuwasiadia kununua vifaa pamoja kukiboresha kiwanda hicho kuwa cha kimataifa.

Lakini Lyata alimalizia kwa kusema kuwa chaki hizo zinaubora wa kimataifa kwa kuwa hazina vumbi wala madhara kwa binadamu yeyeto yule hivyo sasa ni muda muafaka kwa walimu kutumia chaki hizo.

Awali akitoa taarifa kwa Naibu meya mmoja wa wanakikundi wa kiwanda cha Dustless Smart Chalk Prisca Masalanga alisema kuwa kiwanda hicho kinakabiliwa na changamoto mbalimbali hasa za vifaa bora vya kuzalishia bidhaa hii ya chaki.

“Tunazalisha chaki zenye kiwango bora lakini tunakumbana na uhaba wa vifaa vinavyopelekea kuanika chaki hizi kwenye meza kwa kuwa hatuna sehemu sahihi ya kuanikia chaki hizi,bado hatuna mashine kubwa bado tunatumia mashine ndogo” alisema Masalanga

Masalanga alisema kuwa changamoto kubwa ambayo wanakumbana nao ni kukosa soko la kudumu la chaki kutoka katika kiwanda hicho cha Dustless Smart Chalk ambacho kinauwezo wa kuazalisha chaki zenye ubora unaotakiwa kufundishia mashuleni.

“Kwa kweli ndugu mwandishi kiwanda chetu bado hatuna soko tunazalisha tu hizi chaki huku tukitafuta soko na kuwaomba wadau kutusaidia kutafuta soko ili tuweze kuuza chaki hizi na kukuza mitaji yetu na kuwa na kiwanda kikubwa ambacho kitaajili vijana wanzetu wengi hapo baadae” alisema Masalanga

MTOTO AMCHOMA KISU NA KUMUUA MTOTO MWENZAKE KISA DENI LA SHILINGI MIA MBILIKutoka eneo la vilima vya mtaa wa Mkudi, Ghana kata ya Nyamanoro B jijini Mwanza mwanafunzi wa darasa la 6 Shule ya msingi Ghana aliyetambulika kwa jina la Saleh Bundala ameuawa kwa kuchomwa shingoni na kitu chenye ncha kali na kijana mwenzake (jina limehifadhiwa) katika ugomvi wa kudai shilingi za kitanzania mia mbili (200/=) 

Kwa mujibu wa vijana waliokuwa karibu na tukio lililotokea juzi Jumapili ya tarehe 14 mwezi April 2019 majira ya saa 9 alasili, wanasema kuwa marehemu alikuwa amesimama pembeni akiwatizama vijana wenzake waliokuwa wakicheza kamari na mshitakiwa alisikika akilalamika kuwadai wenzake shilingi 200/= aliodai wamemdhulumu.

Akiwa na hasira mtuhumiwa alianza kumpiga 'makwenzi' bila sababu mtoto mdogo ambaye alikuwa amesimama pembezoni akishangaa mchezo  huo ndipo marehemu Salehe akauliza kwanini unampiga mdogo wangu? Mvutano ukatokea penye kuamua, kijana mtuhumiwa akamshindilia Salehe Bundala kitu chenye ncha kali shingoni damu zikaanza kutiririka kwa wingi ......hali iliyo sababisha kifo. 

Siku hiyo hiyo ya tukio (juzi Jumapili) mara baada ya kutokea mkasa huo wa kusikitisha na kuogofya KAZI NA NGOMA ya Jembe Fm ilidhuru eneo husika kuzungumza na mashuhuda pamoja na baba mzazi wa marehemu kujua Kisa na Mkasa.......

TAKUKURU YACHUNGUZA MRADI WA MABILIONI YA PESA.


Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU) mkoa wa Njombe inaendelea na uchunguzi wa mradi wa ujenzi wa kituo cha mabasi cha Njombe mjini ambacho kimeshindwa kukamilika kwa wakati na kuchukua zaidi ya miaka 6 mpaka sasa.

Akizungumza na vyombo vya habari ofisini kwake Kaimu Mkuu wa TAKUKURU mkoani hapo, Bw Charles Mulebya, amesema Kuwa.

Taasisi ilianza kufanya uchunguzi juu ya ujenzi wa kituo hicho cha mabasi (stendi) kinachoendelea kujengwa katika halmashauri ya mji wa Njombe, kufuatia taarifa ya ofisi ya Mdhibiti na Mkaguzi wa Hesabu za Serikali (CAG) ilivyosema na kuibua ubadhilifu mkubwa wa fedha katika ujenzi huo.

"TAKUKURU mwanzoni mwa mwezi Machi mwaka huu (2019) tulianza kufanya uchunguzi juu ya ujenzi wa stendi kuu ya mabasi inayoendelea kujengwa katika halmashauri ya mji wa Njombe, kufuatia taarifa ya ukaguzi uliofanywa na ofisi ya mdhibiti na mkaguzi wa hesabu za serikali na kuibua ubadhilifu katika ujenzi huo.” Amesema Bw Mulebya.

Aidha, Bw Mulebya amesema kuwa kutokana na uchunguzi wanaoufanya mpaka Sasa wamefikia katika hatua nzuri na  karibuni utakamilika.

“Ujenzi huu utagharimu shilingi Bil 9.7 hadi kukamilika kwake na uchunguzi upo kwenye hatua nzuri za kukamilika, uchunguzi unafanyika kwa umakini mkubwa ili yeyote aliyehusika akutane na mkono wa sheria kwa kusababisha ucheleweshwaji wa kituo hicho pamoja na ubadhilifu wa fedha ulioibuliwa hivi karibuni.” ameongeza Bw Mulebya.

Mbali na hivyo, Kaimu huyo amebainisha kuwa uchunguzi wa majalada ya mwanzo umebaini makosa chini ya manunuzi ya umma na kanuni zake za mwaka 2013 na mara baada ya kukamilika majalada yatapelekwa makao makuu kwa hatua zaidi.

Katika ziara ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli,  iliyofanyika kwa siku tatu mkoani Njombe, Rais alimuagiza mkurugenzi na mkandarasi wa kituo hicho cha mabasi mjini Njombe kuhakikisha mpaka mei 5  kimekamilika na kuanza kutumiwa.

MKUU WA MKOA, WILAYA ATAE MSWEKA MTU MAHABUSU BILA SABABU KUCHUKULIWA HATUA.


Waziri wa Ofisi ya Rais Utumishi na Utawala Bora, George Mkuchika amesema kuwa Wakuu wa Mikoa na Wilaya wenye tabia ya kuwasweka mahabusu watu wasiokuwa na hatia watachukuliwa hatua.

Mkuchika amesema kuwa mtu nawekwa ndani kama ana hatarisha amani sio watu wanadaiana madeni huko una muweka ndani, mtu asiwekwe mpaka awe amehatarisha amani.

“Mkuu wa mkoa au mkuu wa wilaya wanapotumia Mamlaka yao ya kuweka mtu mahabusu kwa saa 48 na 28 wazingatie sheria ya Tawala za Mikoa, " amesema Mkuchika Bungeni jijini Dodoma.

"Akitekeleza sheria kinyume na utaratibu kinyume na utaratibu anaweza kuchukuliwa hatua ikiwa ni pamoja na yeye mwenyewe kushitakiwa binafsi, Mwanasheria mkuu wa Serikali hatomtetea mtu aliyevunja sheria makusudi kwa kumuweka mtu ndani bila sababu."

Sunday, April 14, 2019

KAZI YA MWANAUME.


#KONGAMANOlaWANAUME

Kwa mara ya kwanza katika jiji la #MWANZA! Karibu tuandike historia mpya katika maisha ya #UWANAUME.

Mwambie MWANAUME nae amwambie MWANAUME mwingine.

 #JISAJILI SASA
+255622 154 848 +255 764 158 007 +255763 396 237
#Tembelea www.menatwork.or.tz

#WanaumeKazini
#CallofDuty
#MenatWorkGlobal
#JukwaLaWanaume