ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

Saturday, December 31, 2016

VIPORO VYA 2016 NTAVILA 2017 KUNA MBAYA? (IPO SANA)

Gsengo ndani ya chumba cha huduma muhimu ya afya.
*SABABU ZA MAGOJWA YA FIGO JIHADHARI NA ONYEKA!.*
 Raia wa Ghana wanazidi kufa kwa matokeo ya ugonjwa wa Figo. 
*JINSI YA KUONDOKANA NA JANGA HATARI LA UGONJWA WA FIGO:*

*1.Usichelewe kwenda HAJA.*
Kutunza mkojo kweye kibofu chako  kwa muda mrefu ni wazo baya.                    
Kibofu kikijaa kinaweza kusababisha uharibifu.                  
Mkojo ambao unakaa kwenye kibofu  huzidisha bakteria haraka.

Mara mkojo unaporudi nyuma ya njia na Figo, sumu dutu husababisha  maambukizi ya figo, pia njia ya mkojo na "nephritis", pamoja na "uremia". Wakati wito asili (unahisi mkojo) fanya hivyo haraka iwezekanavyo.

*2. Kula Chumvi kupita kiasi.*
Inatupasa kula Chumvi isiyozidi 5.8 gramu kwa siku.

*3. Kula nyama kupita kiasi.*
Protini ikizidi sana katika mlo wako inadhuru figo zako.
Mmeng'enyo wa Protini unazalisha amonia-  sumu dutu ambayo ina uharibifu mkubwa kwa figo zako. Nyama nyingi  inaleta uharibifu zaidi wa figo.

4. *Unywaji mwingi wa "Caffeins".*
Caffein hutokana na vinywaji vya Soda na vinywaji vingine laini kama Kahawa, Redblue n.k.             Hupandisha shinikizo la damu na figo zako kuanza mateso. Unapaswa kupunguza kiwango  cha Coke, Pepsi, Red Bull, nk ambavyo hunywa kila siku.

*5. Kutokunywa maji.* 
Figo zetu lazima zichakatwe vizuri kutekeleza majukumu yake vizuri.  Endapo hatunywi ya kutosha, sumu dutu inaweza kuanza kukusanyika katika damu, kama hakuna kimiminika cha  kutosha kutoa kwa njia ya figo.                    

*** Kunywa zaidi ya bilauri 10 za maji kila siku.
     Kuna njia rahisi ya kuangalia kama  unakunywa maji ya kutosha:                      
Angalia rangi ya mkojo wako; Wepesi wa rangi, ndiyo vzuri.

*6. Kuchelewa matibabu.*
Tibu matatizo yako yote ya kiafya kwa uhakika na uwe unachunguza afya yako mara kwa mara.       Wapendwa na wapenzi wangu, hebu tujisaidie wenyewe... Shirikisha wengine, kama unajali.               ----------------

*Pia epuka vidonge hivi, ni hatari sana:* 
D- baridi*
Vicks Action- 500*
Actified*
Coldarin*
Cosome*
Nice*
Nimulid*
 Cetrizet- D
Hivi vidonge vina Phenyl propanol- amide PPA ambayo husababisha stroke na ni marufuku Marekani.

 MWISHO... Tafadhali, kabla ya kufuta, msaidie rafiki yako kwa kumpitishia hii..!
*Inaweza kumsaidia mtu!*

*Maonyo muhimu ya Afya*
1. Jibu (pokea) simu wito na sikio  la kushoto.
2. Usinywe  dawa zako kwa maji baridi.... 
3. Usile milo mizito baada ya saa 11 jioni. 
4. Kunywa maji vuguvugu mengi asubuhi na kiasi usiku. Usinywe maji baridi kamwe.
5. Muda bora wa kulala ni kutoka saa 4 usiku hadi saa 10 Alfajiri.
6. Usilale mapema baada ya kumeza dawa au baada ya mlo. Usiku, Kula chakula laini.
7. Usipokee simu yako ikiwa haina chaji. Wakati huo mionzi huwa ina nguvu mara 1000 .
 Je, unaweza kuwasambazia watu unao wajali?
Mimi nimeshafanya kwako....!!.

CCM KIRUMBA YACHUKUWA HATUA KUKOMESHA MAJI YANAYOHARIBU TASWIRA NJIA ZIINGIAZO UWANJANI HAPO.

Ndugu wadau wa Michezo Mkoa wa Mwanza na Tanzania kwa ujumla!
Uongozi wa Uwanja wetu wa CCM kirumba, umeanza kuchukua hatua za kukomesha maji yanayoharibu taswira ya uwanja wetu kwa kushirikiana na wadau mbalimbali, zaidi wananchi waliokuwa wakilima katika eneo la Uwanja kwa kuamua kujitolea kuchimba Mkondo wa maji waliouathiri wao kwa shughuri zao za kilimo.
Tumepata ahadi ya Mifuko 10 ya Cement kutoka kwa Wajasiliamali na Mafundi Garage wa eneo la uwanja na jirani, uhitaji ni Mifuko 100 ya Cement, Mawe trip 20, Kokoto trip 3 na Mchanga trip 10, tunaamini kuwa vifaa hivi vikipatikana tutaanza ujenzi haraka wa Mkondo wa Maji ulioathiriwa na Shughuri za Binadamu (Kilimo).
Pamoja na Changamoto nyingi zilizopo, tunaamini kadri siku zinavyosonga tutaendelea kuongeza bidii na maarifa kukabiliana nazo ikiwezekana kuziondoa kabisa au kuzipunguza sana.
Ombi letu kwa wadau wa Soka, tushikirikiane kwa hali na mali kuziondoa changamoto hizo, ili kukifanya kiwanja chetu kuendelea kuwa sehemu muhimu na Salama kwa Michezo.
"Tunaamini katika uwajibikaji na Weredi katika kuwatumikia"
Ndimi Mtumishi wenu:-
S.E.Shija Meneja CCM Kirumba Stadium

KIPINDI CHA TAARABU 'SEGA LA LEO' TOKA JEMBE FM CHASABABISHA TABASAMU KWA WATOTO WAISHIO MAZINGIRA MAGUMU FOREVER ANGEL.

Meneja wa BOA Bank Tawi la Mwanza Bi. Lilian (kulia) akikabidhi mchango wake kwa wadau wanachama wa kipindi cha muziki wa taarab 'Sega la Leo' kutoka Jembe Fm  ili ukabidhiwe kwa kituo cha kulea watoto cha Forever Angel kilichopo Bwiru wilayani Ilemela mkoani Mwanza
 Meneja msaidizi wa Vipindi Jembe Fm Mr. G. Sengo (wa pili kutoka kushoto) akikabidhi mchango wa Kipindi cha KAZI NA NGOMA  kwa mwenyekiti wa Wadau na wanachama wa kipindi cha muziki wa taarab 'Sega la Leo' kutoka Jembe Fm  wanajiita 'TEAM SEGA' Bi. Fatuma Salum ili ukabidhiwe kwa kituo cha kulea watoto cha Forever Angel kilichopo Bwiru wilayani Ilemela mkoani Mwanza, wa kwanza kushoto ni mweka hazina Nasra Hassan, na kulia ni katibu wa kikundi Ayoub Said.
Mwenyekiti wa Wadau na wanachama wa kipindi cha muziki wa taarab 'Sega la Leo' kutoka Jembe Fm  wanajiita 'TEAM SEGA'  ambaye ni msikilizaji mahiri Bi. Fatuma Salum akikabidhi baadhi ya zawadi za msimu wa sikukuu kwa kituo cha Forever Angel.
Mwenyekiti wa Wadau na wanachama wa kipindi cha muziki wa taarab 'Sega la Leo' kutoka Jembe Fm  wanajiita 'TEAM SEGA'  ambaye ni msikilizaji mahiri Bi. Fatuma Salum akimkabidhi unga wa ngano Bw. Hassan ambaye ni Meneja wa kituo cha kulea watoto wadogo cha Forever Angel kilichopo Bwiru wilayani Ilemela Mkoani Mwanza kama sehemu ya kusherehekea msiku wa sikukuu za krismasi na mwaka mpya 2017.
'TEAM SEGA' na zawadi zao.
Mwenyekiti wa nidhamu Mustapha Kinkulah Master ambaye pia ni mtangazaji wa Jembe Fm akiongoza shughuli za ukabidhi wa zawadi ambao umefanyika chini ya usaidizi wa wadau mbalimbali akiwemo Mkuu wa mkoa wa Mwanza Mhe. John Mongela, Kampuni ya Startimess, BOA Bank, na wadau wengine wengi walioguswa.
Meneja wa BOA Bank Tawi la Mwanza Bi. Lilian akitoa neno la shukurani jinsi gani alivyoguswa kujitoa kwaajili ya watoto wakituo hicho.
Marafiki wa Jembe Fm wa ndani na nje ya nchi nao hawakubaki nyuma kushiriki nasi kuhakikisha watoto wanaifurahia siku yao.
Keki yakuukaribisha mwaka kituo cha kulea watoto wadogo iliyoandaliwa na TEAM SEGA kwa hisani ya Jembe Fm 93.7
Jiografia ya eneo la tukio.
Kila mdau wa TEAM SEGA alijibidiisha na mtoto wake.
Sasani muda wa kukata keki.
Nilishe nikulishe ya viongozi.
Mwenyekiti wa Wadau na wanachama wa kipindi cha muziki wa taarab 'Sega la Leo' kutoka Jembe Fm  wanajiita 'TEAM SEGA'  ambaye ni msikilizaji mahiri Bi. Fatuma Salum akimlisha keki Meneja wa BOA Bank tawi la Mwanza Bi. Lilian.
Sasa ni zamu yamama mlezi.
Wadau marafiki wa Jembe Fm na TEAM SEGA.
Tamu..........
Mwenyekiti wa Wadau na wanachama wa kipindi cha muziki wa taarab 'Sega la Leo' kutoka Jembe Fm  wanajiita 'TEAM SEGA'  ambaye ni msikilizaji mahiri Bi. Fatuma Salum akimlisha keki Meneja wa kituo cha Forever Angel Mr. Hassan.
Mwenyekiti msaidizi wa TEAM SEGA ambaye ni mtangazaji Johari Ngassa akimlisha keki mmoja wa watoto wa kituo.
Upendo wa dhati 
Sasa ni zamu ya G Sengo.
PAMOJA SANA.
Ni raha tele kituoni hapa kwa siku ya leo.
Mazingira ya ndani kituoni.
MSOSI TIME.






Tunawashukuru wadau wote kwa kutumia muda wenu na nafasi zenu kuhakikisha hili linafanikiwa kwa kiwango kikubwa.

WAANDISHI KARIBU 100 WA HABARI WAMEUAWA MWAKA HUU WA 2016

Federesheni ya Kimataifa ya Waandishi Habari (IFJ) imetangaza kuwa, waandishi habari 93 wameuawa kwa makusudi au katika machafuko yaliyotokea kwenye maeneo mbalimbali ya dunia katika mwaka huu unaomalizika leo wa 2016.
IFJ imesema kuwa, waandishi hao wa habari wameuawa katika nchi za Afrika, Asia, Pasific, America na Ulaya. 
Federesheni ya Kimataifa ya Waandishi Habari imesema matukio mabaya zaidi kwa waandishi habari katika mwaka huu unaomalizika leo ni vifo vya maripota 20 wa Brazil baada ya ndege waliyokuwamo kuanguka katika mji wa Medellin nchini Colombia na vifo vya maripota 9 wa Russia wakati ndege iliyokuwa na nambari ya usajili Tu-154 ilipoanguka katika Bahari Nyeusi, mwezi huu wa Disemba. 
Maandamano dhidi ya mauaji ya waandishi habari Ufilipino

Mwaka uliopita wa 2015 waandishi habari 112 waliuawa kote duniani katika matukio mbalimbali. 
Federesheni ya Kimataifa ya Waandishi Habari ambayo iliasisiwa mwaka 1926, ndiyo jumuiya kubwa zaidi ya waandishi habari duniani. Jumuiya hiyo ina wanachama laki sita katika nchi 140 na lengo lake kuu ni kuimarisha na kuboresha haki na uhuru wa waandishi wa habari.

OFISI YA KIJIJI YACHOMWA MOTO.

Nyaraka za kijiji cha Mtangimbole  mkoani Ruvuma zimeteketea kwa moto baada ya ofisi ya kijiji hicho kuchomwa moto na watu wasiojulikana. 

10 WAUAWA KWA RISASI KATIKA MAENEO TOFAUTI NCHINI MAREKANI.

Polisi ya Marekani imetangaza habari ya kuuawa hivi karibuni watu kumi katika maeeo tofauti ya nchi hiyo.

Polisi hiyo imesema watu wengine 7 wamejeruhiwa katika matukio hayo ya ufyatuaji risasi katika pembe tofauti za nchi hiyo. Kwa mujibu wa ripoti ya polisi hiyo, ufyatuaji risasi huo ulitokea katika majimbo ya North Carolina,Tennessee, mji wa Chicago katika jimbo la Illinois, Sacramento katika jimbo la California, Phoenix katika jimbo la Arizona, Frankfort katika jimbo la Kentucky, Trenton katika jimbo la New Jersey mji wa San Francisco mji wa Belle Glade katika jimbo la Florida na katika mji wa San Antonio katika jimbo la Texas.

Ufyatuaji risasi mjini Florida, Marekani
Kwa mujibu wa ripoti ya Kituo cha Twakwimu za Ufyatuaji Risasi cha Marekani, kesi 57,371 za ufyatuaji risasi zimeripotiwa tokea mwanzo wa mwaka huu hadi kufikia tarehe 9 mwezi huu wa Disemba ambapo watu 859,000 wameuawa na wengine 315,000 kujeruhiwa.

SEKUNDE 48 ZATOSHA KWA AMANDA NUNES KUMCHAKAZA RONDA ROUSEY.

Ronda Rousey hakuweza kuhimili makonde mazito toka kwa Mbrazil, Amanda Nunes aliyemchakaza kwenye pambano la UFC 207 la ubingwa wa bantamweight, lililofanyika Las Vegas, asubuhi ya Jumamosi kwa saa za Afrika Mashariki.
Pambano lilianza kwa Nunes kurusha makonde mfululizo kwa Rousey yaliyomwelemea na kuchakazwa ndani ya sekunde 48 tu za pambano hilo na kumfanya mwamuzi, Herb Dean asitishe pambano.

Rousey hakuamini kama angeweza kudundwa katika muda huo mfupi na kuna wakati alitaka kuanguka wakati amesimama kutafakari kilichotokea ndani ya sekunde chache tu.

 Hilo linakuwa pigo jingine kubwa katika ungwe ya upambanaji wa bondia huyo ambaye mwaka uliopita alipoteza tena pambano jingine dhidi ya Holly Holm kwa fedheha kubwa.
 Swali ambalo watu wengi wanajiuliza sasa ni iwapo Ronda ataendelea tena ngumi ama ataamua kustaafu kabisa.
Referee Herb Dean stepped in and stopped the contest after less than a minute following a brutal onslaught from Nunes
Referee Herb Dean alijongea na kulisimamisha pambano hata kabla ya pambano kufikisha dakika moja baada ya Ronda kupelekewa makonde ya haja.
Rousey never troubled Nunes inside the ring before the contest was stopped in the interest of her own safety
Kamwe katika usiku huo Rousey hakumpa kabisa wakati mgumu Nunes ndani ya ulingo zaidi ya kujitahidi kuzuia na kukwepa makonde ya mpinzani wake ambaye hata hivyo ilimchukuwa sekunde 48 tu kudhihirisha ubabe wake.
Rousey was helped away from the octagon by her mother, AnnMaria, after losing to Nunes in rapid time on Friday night
Rousey akisaidiwa kuondoshwa kwenye ulingo na mama yake, AnnMaria, baada ya kupoteza pambano mapema katika mpambano ulioganyika ijumaa usiku saa za Marekani na alfajiri saa za Afrika Mashariki.
Nunes celebrated wildly with her entourage at the conclusion of the contest in which she retained her bantamweight title
Nunes akisherehekea ushindi na safu yake ya mafunzo na uwezeshaji mara baada ya kutajwa kuwa yu mshindi wa pambano mkanda wa UFC.

The Brazilian, nicknamed 'the lioness' was in dominant form at Las Vegas's stunning T-Mobile Arena on the main strip
Mpiganaji huyo wa ki-Brazil almaarufu 'Simba Jike' alikuwa na ari kubwa na kila dalili ya ushindi maratu sekunde za awali zilipoanza za pambano hilo lililofanyika mjini Las Vegas's stunning T-Mobile Arena.

TRUMP AMSHUKURU PUTIN KWA KUTOWAFUKUZA WANADIPLOMASIA WA MAREKANI.

Donald Trump, Rais mteule wa Marekani jana Ijumaa kupitia ujumbe wa Twitter alimshukuru Rais Vladimir Putin wa Russia kwa kutolipiza kisasi kitendo cha kufukuzwa wanadiplomasia wa nchini hiyo huko Marekani ambacho kilichukuliwa na serikali ya Washington siku ya Alkhamisi, na kusema kuwa daima amekuwa akimtambua Putin kuwa ni kiongozi anayetumia busara.
Huku akitoa radiamali yake kufuatia hatua ya serikali ya Washington ya kuwafukuza wanadiplomasia 35 wa Russia kwa madai ya nchi yao kuathiri matokeo ya uchaguzi mkuu wa Marekani, Rais Putin amesema kuwa amesikitishwa mno na hatua ya Rais Barack Obama wa nchi hiyo kumaliza kipindi chake cha miaka minane ya uongozi kwa njia hiyo, lakini akaongeza kuwa hatalipiza kisasi kwa kuwafukuza wanadiplomasia wa Marekani wanaohudumu Russia. Akitoa radiamali yake kuhusiana na hatua hiyo ya Putin, Trump amesema kuwa hatua hiyo ya Putin ni nzuri na ya kuvutia sana.
Trump
Katika hali ambayo hatua hiyo ya Putin kutolipiza kitendo hicho cha serikali ya Washingtion haikutarajiwa na wengi katika ngazi za kiaisa za Marekani, lakini hatua ya Trump ya kusifu hatua hiyo imewashangaza hata zaidi na kuwafanya wamtuhumu kuwa anahatarisha maslahi ya kitaifa ya Marekani. 

Ni wazi kuwa huo unaweza kuwa ni mwanzo wa changamoto mpya katika kipindi cha uongozi wa Trump na chama cha Warepublican ambao walimpa madaraka ya kuongoza nchi hiyo. Katika hatua ya hivi karibuni kabisa ya uadui wa Marekani dhidi ya Russia, serikali ya Rais Barack Obama imechukau hatua ya kuwafukuza Marekani wanadiploamasia 35 na kuwawekea vikwazo maafisa sita pamoja na mashirika matano ya Russia kama jibu kwa madai ya nchi hiyo kuhusika na shambulio la kimtandao dhidi ya Marekani.

Friday, December 30, 2016

MAABARA YA KISASA YAZINDULIWA MASHARIKI YA KATI NA SHIRIKA LA NDEGE LA ETIHAD

Katika hafla ya uzinduzi wa maabara ya Lantal katika Kitengo cha Uhandisi cha Shirika la Ndege la Etihad mjini Abu Dhabi. Wanaoshuhudia tukio hilo (toka kushoto kwenda kulia), Peter Baumgartner, Ofisa Mtendaji Mkuu wa Shirika la Ndege la Etihad, Dkt. Urs Rickenbacher, Ofisa Mtendaji Mkuu wa  Lantal, Bernhard Randerath ambaye ni Makamu wa Rais, Upangaji, Uhandisi na Ubunifu katika Kitengo cha Uhandisi cha Shirika la Ndege la Etihad, Heiko Nüssel,  Mdau mwenza, mtendaji makamu wa rais, udhibiti na uhakiki, Lantal; Shevantha Weerasekera,  Mkuu wa Uhandisi, Kitengo cha Uhandisi cha Shirika la Ndege la Etihad, Jeff Wilkinson na Balozi mdogo wa Uswisi, Jürg Metz.
SHIRIKA la Ndege la Etihad kupitia Kitengo chake cha Uhandisi (Etihad Airways Engineering) kwa kushirikiana na Lental Textiles AG wamezindua maabara ya kipekee ya kwanza Mashariki ya Kati kwa ajili ya wateja wa kanda hiyo walio sekta ya anga na waendeshaji mashirika ya uzalishaji na ubunifu.

Maabara hiyo ambayo ipo ndani ya kituo cha uhandisi cha Shirika la Ndege la Etihad karibu kabisa na Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Abu Dhabi itakuwa inatoa huduma mbalimbali   ikiwemo vipimo vya kuwaka kwa moto, joto, moshi n.k.

Aidha, maabara hiyo itaenda sambamba na hadhi ya ubora wa Kimataifa ISO 17025  na vipimo vyote vitafanyika kwa mujibu wa Kanuni za Anga za imataifa FAR/CS25.853.

Kwa mujibu wa Ofisa Mtendaji Mkuu wa Kitengo cha Uhandisi cha Shirika la Ndege la Etihad Jeff Wilkinson alisema, “Tunatoa huduma zilizotukuka kwenye matengenezo ya ndege na ufumbuzi wa kiuhandisi katika soko la anga duniani na kwa ajili ya aina zote za ndege za kibiashara.

“Kupitia ushirikiano wetu huu na Lantal, itakuwa rahisi sasa na haraka kwa kwa wateja wa sekta ya anga katika Ukanda kupata huduma bora za vipimo katika kituo chetu cha Abu Dhabi,” alisema.

Naye Ofisa Mtendaji Mkuu wa Lantal, Dkt. Urs Rickenbacher alisema, “Maabara yetu ya Lantal kwa ajili ya vipimo nchini Uswisi inajulikana vema kwa huduma zake bora na haraka.  Kwa sasa tunalo soko kubwa barani Ulaya na sasa maabara yetu hapa Abu Dhabi tukishirikiana na Kitengo cha Uhandisi cha Shirika la Ndege la Etihad (Etihad Aiways Engineering) litatuwezesha kutoa huduma kwa ukaribu zaidi na wateja wetu wa Mashariki ya Kati,”.

CHID BENZ AYARUDIA MADAWA.

Leo nimeona picha ya kushoto na nyinginezo kadhaa zikimuonesha alivyo hivi sasa zikisambaa mitandaoni katika hali ya wengi kusikitishwa na hali hiyo iliyomkumba kijana mwenzetu, Msanii wa bongofleva aliyekuwa na uwezo mkubwa wa kughani jukwaani kwa madaha na stail ya aina yake iliyowavutia wengi.

Chid Benzii hali yake kwa sasa inasikitisha sana anahitaji msaada mkubwa kwa namna yoyote ile, Shime watanzania naamini tunaweza kumrudisha na kumjenga Chid Benz na kurejea katika hali yake,ingaawaje inaweza kuchukua muda sana, lakini si haba kijana mwenzetu akaendelea na maisha yake maZuri aliokuwa nayo hapo mwanzo.

Wasanii popote pale mlipo mkae mkijua athari ya Madawa ya Kulevya ni mbaya,mbaya sana, ni vema mkajiepusha na janga hilo kungali mapema,kama ulikuwa unatumia, unataka kuanza kutumia unaendelea kutumia, Tafadhali achana nayo ni hatari kwa afya na maisha yako.
!!!CHUNGA SANA!!!