ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

Friday, December 30, 2016

MAABARA YA KISASA YAZINDULIWA MASHARIKI YA KATI NA SHIRIKA LA NDEGE LA ETIHAD

Katika hafla ya uzinduzi wa maabara ya Lantal katika Kitengo cha Uhandisi cha Shirika la Ndege la Etihad mjini Abu Dhabi. Wanaoshuhudia tukio hilo (toka kushoto kwenda kulia), Peter Baumgartner, Ofisa Mtendaji Mkuu wa Shirika la Ndege la Etihad, Dkt. Urs Rickenbacher, Ofisa Mtendaji Mkuu wa  Lantal, Bernhard Randerath ambaye ni Makamu wa Rais, Upangaji, Uhandisi na Ubunifu katika Kitengo cha Uhandisi cha Shirika la Ndege la Etihad, Heiko Nüssel,  Mdau mwenza, mtendaji makamu wa rais, udhibiti na uhakiki, Lantal; Shevantha Weerasekera,  Mkuu wa Uhandisi, Kitengo cha Uhandisi cha Shirika la Ndege la Etihad, Jeff Wilkinson na Balozi mdogo wa Uswisi, Jürg Metz.
SHIRIKA la Ndege la Etihad kupitia Kitengo chake cha Uhandisi (Etihad Airways Engineering) kwa kushirikiana na Lental Textiles AG wamezindua maabara ya kipekee ya kwanza Mashariki ya Kati kwa ajili ya wateja wa kanda hiyo walio sekta ya anga na waendeshaji mashirika ya uzalishaji na ubunifu.

Maabara hiyo ambayo ipo ndani ya kituo cha uhandisi cha Shirika la Ndege la Etihad karibu kabisa na Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Abu Dhabi itakuwa inatoa huduma mbalimbali   ikiwemo vipimo vya kuwaka kwa moto, joto, moshi n.k.

Aidha, maabara hiyo itaenda sambamba na hadhi ya ubora wa Kimataifa ISO 17025  na vipimo vyote vitafanyika kwa mujibu wa Kanuni za Anga za imataifa FAR/CS25.853.

Kwa mujibu wa Ofisa Mtendaji Mkuu wa Kitengo cha Uhandisi cha Shirika la Ndege la Etihad Jeff Wilkinson alisema, “Tunatoa huduma zilizotukuka kwenye matengenezo ya ndege na ufumbuzi wa kiuhandisi katika soko la anga duniani na kwa ajili ya aina zote za ndege za kibiashara.

“Kupitia ushirikiano wetu huu na Lantal, itakuwa rahisi sasa na haraka kwa kwa wateja wa sekta ya anga katika Ukanda kupata huduma bora za vipimo katika kituo chetu cha Abu Dhabi,” alisema.

Naye Ofisa Mtendaji Mkuu wa Lantal, Dkt. Urs Rickenbacher alisema, “Maabara yetu ya Lantal kwa ajili ya vipimo nchini Uswisi inajulikana vema kwa huduma zake bora na haraka.  Kwa sasa tunalo soko kubwa barani Ulaya na sasa maabara yetu hapa Abu Dhabi tukishirikiana na Kitengo cha Uhandisi cha Shirika la Ndege la Etihad (Etihad Aiways Engineering) litatuwezesha kutoa huduma kwa ukaribu zaidi na wateja wetu wa Mashariki ya Kati,”.

Tupe maoni yako

0 comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.