Baba na mama yake mzazi Veronica Stima (kutoka kulia) wakicheza nyimbo ya kikabila la Kifipa. |
Wakwe wa bibi harusi mtarajiwa wakiingia ukumbini kwa madaha. |
Bi Harusi mtarajiwa Veronica Stima akiwa na kaka na dada zake aliomsindikiza katika sherehe yake ya send off iliyofanyika ukumbi wa Student Centre, Tabora. |
Bibi Harusi Mtarajiwa Veronica Stima akimlisha mtarajiwa wake Bw. Allen Mnene |
Wachanga nao hawakuwa nyuma kuonyesha umoja wao na ule wimbo wao wa kushikana mikono. |
Bwana harusi mtarajiwa Allen na mkewe mtarajiwa Veronica Stima wakienda mbele kwa ajili ya utambulisho. |
...akilishwa keki na mtarajiwa wake |
Bibi harusi mtarajiwa akiaga wazazi wake, kujitayarisha kuungana na mwenzake |
...hapa bibi harusi mtarajiwa alikuwa akitoa keki kwa mama mkwe wake mtarajiwa huku kaka yake akiwa amemsindikiza. |
Mzee Prosper Stima ambaye ni baba bibi harusi mtarajiwa akitoa machache. |
Mama Catherine Stima ambaye ni mama mazazi wa bibi harusi nae alipata wasaa wa kutoa machache kwa mwanae. |
Kaka mkubwa John Stima akiongea machache kabla ya kumkabidhi dada yake kwa shemeji zake. Alisema, 'Nawakabidhi dada yangu mpendwa, hana hata doa... nawaombeni msije mkanyanyasa'. |
...mara baada ya kuongea machache kaka mkubwa alikabidhiwa begi la nguo za bibi harusi, tayari kwa maandalizi ya harusi. |
Aha... Bwana na Bibi Cathbert Angelo nao walikuwepo kuhakikisha kila kitu kinaenda sawa. |
Bibi harusi mratajiwa (wapili kutoka kulia) akiwa na dada zake. |
Muda wa kupata show ulifika na mambo yalikuwa kama unavyopna mwenyewe. |
Picha ya kumbu kumbu kwa wake na watoto wao. Nguzo zote za shughuli hiyo zimedizainiwa na na kushonwa na mwanamitindo Manju Msita |