|
Waziri Mkuu Mhe. Kassim Majaliwa Majaliwa akikata utepe kama ishara ya kufungua jengo jipya la ofisi ya TRA, Wilaya ya Chato, Mkoani Geita katika ufunguzi uliofanyika leo mjini Chato. |
|
Waziri Mkuu Mhe. Kassim Majaliwa Majaliwa akipiga makofi baada ya kuwa amekata utepe ambao unaashiria kufunguliwa kwa Jengo la mamlaka ya mapato Wilayani Chato. |
|
Waziri Mkuu Mhe. Kassim Majaliwa Majaliwa akihutubia wananchi wa Chato wakati wa ufunguzi wa jengo la TRA wilayani humo mkoani Geita leo. |
|
Jengo la mamlaka ya mapato(TRA)Wilayani Chato. |
|
Waziri Mkuu,akiwapongeza na kutoa zawadi kwa kwaya ya Mwagazege ambao walikuwa wakiimba nyimbo ya kuipongeza serikali ya awamu ya Tano kwa kuendelea kutekeleza Ilani ya chama cha mapinduzi(CCM) |
|
Waziri Mkuu Kassimu Majaliwa pamoja na Mkuu wa Mkoa wa Geita Meja Jenerali Mstaafu Ezekiel Kyunga wakipongeza kikundi cha Kwaya kwa wimbo mzuri. |
|
Mkuu wa Wilaya ya Chato,Shaaban Ntarambe akitambulisha wageni ambao walikuwepo kwenye viwanja hivyo. |
|
Waziri Mkuu Kassimu Majaliwa akiagana na Mkuu wa Mkoa wa Geita. |
|
Waziri Mkuu Kassimu Majaliwa na Mkuu wa Wilaya ya Chato. |
|
Mbunge wa Chato ambaye pia ni Naibu waziri wa Nishati na Madini,Dk Medadi Kalemani akizungumza na wananchi. |
|
Kamishna Mkuu wa TRA Charles Kichere akitoa maelezo ya mradi wa ujenzi wa ofisi ya TRA katika uzinduzi wa ofisi hiyo uliofanyika leo katika wilaya ya Chato, mkoa wa Geita |
Waziri Mkuu
Kassimu Majaliwa, amesema kuwa kila mwananchi wa Tanzania anawajibika kulipa
kodi kwaajili ya ujenzi wa Taifa na kwamba uchumi utajengwa na watanzania kwa kufanya kazi kwa
bidii na kwa uadilifu mkubwa kwani kufanya hivyo itawaza kusaidia upatikanaji
mkubwa wa kodi.
Kauli hiyo
ameitoa leo wakati wa zinduzi wa Jengo la mamlaka ya mapato nchini(TRA)Wilayani
Chato Mkoani Geita, ambalo ujenzi wake umeghalimu kiasi cha Sh ,Bilioni 1.4.
Waziri
Mkuu amesisitiza kuwa Kila mwananchi ambaye anastahili kulipa kodi
la lazima alipe bila ya kushurutishwa kwani ni jambo la kawaidia na kwamba nchi
ambazo zimeendelea ni kutokana na wananchi wake kujenga destuli ya ulipaji wa
kodi
Pia ameendelea kueleza kuwa Kutokana na maelekezo ya Ilani,Katika Mwaka 2016/17 Kuanzia Mwezi Julai,2016 hadi kufikia mwezi Aprili ,2017 Serikali imefanikiwa kukusanya Shilingi Trilion 20.7 Sawa na Asilimia 70.1 na kwa lengo la mwaka walijiwekea malengo ya kukusanya Sh,Trilion 29.5,Kati ya makusanyo hayo mapato ya ndani ya kodi yalikuwa ni Sh,Trilioni 11.6 Sawa na Asilimia 77.1 ya lengo la kukusanya Sh,Trilion 15.1
Aidha Waziri Mkuu ametoa Wito kwa Kila mwananchi kuakikisha anadai na kupewa Risiti ya manunuzi ya bidhaa alizonunua na kwamba TRA ihakikishe kila mfanyabishara anakuwa na mashine za kielektroniki.
Kamishina wa mamlaka ya mapato TRA Charles
Kichere amesema kuwa Pamoja na kuboresha miundo mbinu ya majengo Mamlaka imeanzisha
mifumo ya ukusanyaji mapato kwa njia za kielekitroniki ambazo zitaunganishwa na ofisi hiyo ili kutoa huduma kwa urahisi kama ilivyo
kwenye ofisi zingine kote nchini.
"Baadhi ya huduma zitakazotolewa hapa
ni kama; Utoaji wa Namba ya Utambulisho wa Mlipakodi (TIN), utoaji
wa leseni za udereva, huduma za usajili wa magari, ukusanyaji wa kodi za
majengo, na kodi zinginezo ambazo zinasimamiwa na Mamlaka ya Mapato Tanzania
kwa mujibu wa Sheria"Alisema Kichere.
"Haya yote yanafanyika kwa lengo la kuhakikisha kodi na tozo
mbalimbali zilizopitishwa na Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
zinakusanywa kikamilifu ili kufikia lengo la makusanyo yanayokusudiwa katika
mwaka ujao wa Fedha na kuendelea"Aliseongeza Kichere.
Jengo hilo ambalo limefunguliwa leo lilianza kujengwa mnamo
tarehe 13 Julai, 2016 na kumalizika tarehe 12 Juni, 2017 ambapo kazi ya ujenzi
ilihusisha ujenzi wa jengo la ghorofa moja kama ambalo lina nafasi
ya kutosha kutoa huduma zote za kodi pamoja na huduma za kibenki ili
kuwapunguzia adha walipakodi kwa kupata huduma zote mahala pamoja.
Kampuni ambayo imejenga jengo hilo ni Wakala
wa Majengo Tanzania (TBA)na mjenzi ni kampuni ya Mayanga Constructions ambapo
katika ujenzi huu zimetumika kiasi cha Takriban
Shilingi Bilioni 1.4.
IMEANDALIWA NA MADUKA ONLINE