ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

Friday, June 7, 2019

THAILAND: WAZIRI MKUU AHUKUMIWA MIAKA MIWILI JELA.

Waziri Mkuu wa zamani wa Thailand, Thaksin Shinawatra amelihukumiwa  kifungo cha miaka miwili gerezani, adhamu hiyo ilitolewa siku ya jana na Mahakama kuu nchini humo.

Bwana Thaksin Shinawatra  ametiwa hatiana kwa kosa la kuzindua bahati nasibu haramu ya serikali zaidi ya miaka kumi iliyopita na kuisababishia serikali hasara.

Majaji wa mahakama kuu ambao ni wasimamizi wa kesi za kisheria dhidi ya makosa ya jinai ya wanasiasa walimhukumu waziri mkuu wa zamani kwa kumpata na hatia ya kuhusika katika uzinduzi wa bahati nasibu haramu ya serikali ambayo inadaiwa ilisababisha hasara ya dola za Marekani milioni 53.8 kati ya mwaka wa 2003 na 2006.

TUSEME SEHEMU SALAMA CLUB - RUNGU LA KUTOKOMEZA VITENDO VYA UKATILI


Watoto ni zawadi kutoka kwa Mungu, na kila mzazi hufurahia kuona watoto wake wanaishi katika mazingira mazuri yanayowawezesha kupata haki  za msingi na kuwa raia wema katika kulitumikia taifa na kuleta maendeleo katika vizazi vijavyo.

Watoto wanatakiwa wajisikie salama wakiwa nyumbani, shuleni na kwenye jamii inayowazunguka. Lakini katika maeneo mengi ukatili dhidi ya watoto hufanyika na wakati mwingine kutoka kwa watu ambao wanawaona kila siku. Kwa watoto wengi suala la kufanyiwa ukatili linaonekana zaidi katika sura ya kifamilia.

Suala ukatili dhidi ya watoto linatokea kila mahali kwa sura tofauti tofauti kulingana na mazingira anayoishi mtoto. Hata kwenye nchi ambazo zimepiga hatua kubwa ya maendeleo bado wanakabiliwa na tatizo hili.

Wadau wa Shirika la Elimu, Sayansi na Utamaduni la Umoja wa Mataifa (UNESCO) wakishirikiana na FAWE Tanzania wameendesha mafunzo kwa Klabu za wanafunzi wa Shule za Sekondari wilayani Sengerema, shuhudia walichojifunza.


RAIS MAGUFULI AFUNGUKA WAFANYABIASHARA WANAVYOKWEPA KODI.


Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. John Pombe Magufuli amesema baadhi ya wafanyabiashara wamekuwa wakitengeneza vitabu vya hesabu ili kukwepa kupeleka kodi kubwa ya ongezeko ya thamani Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA).

Amesema linapofika suala la kuwasilisha asilimia 18 ya VAT wengi wamekuwa wakibaki nayo kama mtaji badala ya kuipeleka serikalini huku akibainisha wamekuwa wakitengeneza vitabu tofauti.

“Kimoja ni cha benki chenye mahesabu ya kweli yenye faida na kitabu kingine ni cha TRA. Kwa kawaida kile kinachopelekwa benki kinakuwa cha kweli lakini kinachoenda TRA ni kidogo wakati mwingine kinaonyesha hasara,” amesema Rais Magufuli leo katika mkutano kati yake na wawakilishi wa wafanyabiashara kutoka wilaya zote nchini unaojadili changamoto wanazokutana nazo na kuzitafutia majibu.

“Nataka nitoe mfano wa kampuni tatu, moja ya kampuni (Jina linahifadhiwa) ina vitabu vitatu na fedha zake ni hatari ukiangalia, nina uhakika huyo mfanyabiashara ataenda akairudishe hiyo hela iliyokuwa inatakiwa,” amesema Rais Magufuli .

“Kampuni nyingine namba mbili (Jina linahifadhiwa) taarifa ya benki inaoyesha mwaka 2017 inaonyesha faida ilikuwa Sh958 milioni lakini iliyopelekwa TRA ni Sh20 milioni kwenye kitabu cha pili, kampuni namba tatu mwaka 2017 taarifa ya benki inaoyesha faida ilikuwa Sh501 milioni lakini TRA iliambiwa kuwa imepata faida ya Sh72 milioni.”


Wednesday, June 5, 2019

SOKO KUU MWANZA KUBOMOLEWA MWEZI AGOSTI MWAKA HUU.


IFIKAPO mwezi Agosti mwaka huu 2019 Halmashauri ya Jiji la Mwanza inategemea kuanza kulivunja Soko kuu la jijini hapa.

Hayo yamesemwa na Mkurugenzi wa Halmashauri ya jiji la Mwanza Kiomoni Kibamba mapema leo asubuhi wakati akipokea msaada wa vifaa vya kufanyia usafi na uzoaji vilivyotolewa na Benki ya Biashara na Mikopo ya 'Akiba Commercial' katika Maadhimisho ya Siku ya Mazingira duniani iliyo adhimishwa  ndani ya viunga vya soko hilo tegemeo kwa huduma za uuzaji jumla na rejareja mazao ya chakula na bidhaa mbalimbali lililopo kata ya Pamba wilayani Nyamagana.

Zaidi ya shilingi bilioni 23 zitatumika kwenye ujenzi wa soko hilo la kisasa ambalo tayari mkandarasi wake amekwisha patikana, nalo likitarajiwa kukamilika ndani ya miezi 18.
 Hafla ya kukabidhi vifaa hivyo imeambatana na zoezi la kufanya usafi katika maeneo mbalimbali ya Soko Kuu jijini Mwanza ambapo wafanyakazi wa benki ya Akiba wamejumuika pamoja na wafanyabiashara sokoni hapo kufanya usafi huo.
Meneja wa benki ya Akiba tawi la Mwanza, Herieth Bujiku amesema lengo ni kuhakikisha kunakuwa na zoezi endelevu la kufanya usafi katika soko hilo na kuweka mazingira katika hali ya usafi ili kuzuia magonjwa ya milipuko huku akitoa pongezi kwa Serikali kuzuia matumizi ya mifuko ya plastiki.
Mkurugenzi wa Jiji la Mwanza, Kiomoni Kibamba aliyepokea vifaa hivyo kwa niaba ya Mkuu wa Mkoa Mwanza, John Mongella na kuvikabidhi kwa uongozi wa Soko Kuu jijini Mwanza, amesema vifaa hivyo vina umuhimu mkubwa wa kuimarisha usafi na hivyo wafanyabiashara kufanya shughuli zao katika mazingira safi na salama kiafya.

HAAFISA WAANDAMIZI UHAMIAJI WAULA....

Taarifa ya uteuzi na Kupandishwa vyeo kwa Maafisa waandamizi wa uhamiaji.

WAZIRI MKUU: TUITUMIE SIKU YA EID KWA KUTENDA MEMA.

WAZIRI MKUU, Kassim Majaliwa amewataka waislamu wote nchini watumie siku kuu ya Eid el Fitr kwa kutenda matendo mema pamoja na kuwakumbuka yatima na wajane.

“Leo ni siku kubwa na muhimu waislamu wanahitimisha mfungo wa Mwezi Mtukufu wa Ramadhani na kusherehekea siku kuu ya Eid El Fitr, hivyo tuendeleze matendo mema.”

Waziri Mkuu ameyasema hayo leo (Jumatano, Juni 5, 2019) wakati aliposhiriki swala ya Eid El Fitr katika msikiti wa Anwar uliopo Msasani jinini Dar es Salaam.

Waziri Mkuu amesema wakati huu ni mzuri kwa kuimarisha mshikamano miongoni mwenu na madhehebu mengine, hivyo hakikisheni mnayaendeleza mambo mema yote.

“Tumeona utulivu uliojitokeza katika mwezi mtukufu, na jambo hili limesisitizwa na viongozi wa dini. Tuendelee kuwa wamoja, tuimarishe mshikamano na tuvumiliane.”

Pia, Waziri Mkuu amewakumbusha wazazi na walezi kuwaongoza watoto kwa kuwapa mafundisho ya dini yatakayowawezesha kumjua Mwenyezi Mungu na kuwa raia wema.

Awali, Imamu wa msikiti huo, Sheikh Mhina alisema waislamu wanatakiwa kuitumia siku ya leo kwa kuhamasisha Amani pamoja na kuwasaidia watu wasiokuwa na uwezo.

Pia amewasisitiza wayaendeleze mema yote waliyoyafanya katika kipindi cha mwezi Mtukufu wa Ramadhani ikiwa ni pamoja na kuwaheshimu na kuwajali wazazi wao.

 (mwisho)
IMETOLEWA NA:
OFISI YA WAZIRI MKUU,

Tuesday, June 4, 2019

RAIS MAGUFULI KUZUNGUMZA NA WAFANYABIASHARA WADOGO 1,000

Dar es Salaam. Miezi mitano baada ya kukutana na wachimbaji wadogo wa madini, Rais John Magufuli anatarajia kuzungumza na takriban wafanyabiashara wadogo 1,000 Ijumaa ya wiki hii.Miezi mitano baada ya kukutana na wachimbaji wadogo wa madini, Rais John Magufuli anatarajia kuzungumza na takriban wafanyabiashara wadogo 1,000 Ijumaa ya wiki hii.
Kwa mujibu wa tangazo lililotolewa na Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (Tamisemi), kila halmashauri (zipo 186) inatakiwa kuwaalika wafanyabiashara watano ambao watahudhuria mkutano huo utakaofanyika kuanzia saa 2:00 asubuhi katika ukumbi wa mikutano wa Kikwete, Ikulu jijini hapa.
Agizo hilo lililotolewa Mei 31, liliwataka wakuu wa mikoa yote Tanzania Bara kuwasilisha majina hayo hadi Juni 2. “Orodha hiyo ionyeshe jina, aina ya biashara na namba ya simu ya mfanyabiashara husika, iwapo katika wilaya husika kuna mfanyabiashara ambaye pia ni kiongozi wa kisiasa au mtendaji wa Serikali wasisite kumpendekeza na wafanyabiashara hao wajigharamie,” inasomeka sehemu ya barua hiyo.
Akizungumza Mwananchi kuhusu mkutano huo, Waziri wa Viwanda na Biashara, Joseph Kakunda alisema ajenda kuu ni kusikiliza kero na malalamiko kutoka kwa wafanyabiashara wanaowahudumia wananchi.
Kama alivyokutana na wachimbaji wadogo mapema Januari, Kandege alisema hii ni mara ya kwanza kukutana na kundi hilo, mara zote huzungumza na wenye viwanda vikubwa na wafanyabiashara wa kimataifa.
Alifafanua kuwa kazi ya kuwakusanya wafanyabiashara hao watano kutoka katika kila wilaya itaratibiwa na halmashauri husika chini ya uangalizi wa wakuu wa wilaya.
CHANZO: MWANANCHI

Monday, June 3, 2019

SARE NA PAMBA DIMBA LA NYAMAGANA, KAGERA YAJIWEKA PAZURI


TIMU ya Kagera Sugar imejiweka kwenye nafasi nzuri ya kubaki Ligi Kuu ya Tanzania Bara baada ya kulazimisha sare ya 0-0 na wenyeji Pamba SC jioni ya leo Uwanja wa Nyamagana mjini Mwanza.

Mchezo huo wa kwanza wa mchujo wa kuwania kubaki na kupanda Ligi Kuu, ulikuwa mkali na wa kusisimua na Pamba SC watajilaumu wenyewe kwa kushindwa kutumia nafasi walizotengeza.

Kikosi cha Pamba SC kilikuwa; Deus Tilusubya, Hassan Kabailo, Amos Ikuzungura, Alex Joseph, John Mtobesya, Salum Ally, Yussuf Dunia, Salum Juma, Shija Mkina, Elias Seth/Kelvin John dk69 na Ally Rajab/David Richard dk84. 
 Kagera Sugar; Ramadhani Chalamanda, Mwaita Gereza, David Luhende, Juma Nyosso, JUma Shemvuni, Peter Mwalyanzi, Suleiman Mangoma, Ally Ramadhani, Ramadhani Kapera, Paul Ngalyoma/Jerson Tegete dk68 na Venende Ludovic/Japhet Makalai dk53.
John Mongella ndiye aliyekuwa mgeni rasmi wa mchezo huo kati ya Pamba Sc iliyokaribisha Kagera Sugar dimba la Nyamagana jijini hapa akisalimiana na benchi la ufundi pamoja na wachezaji wa akiba wa timu ya Kagera Sugar. 

Hadi mwisho timu hizo zilitoshana nguvu kwa sare ya 0-0.
Sasa Kagera Sugar wanarejea nyumbani Bukoba kujipanga kwa mchezo wa marudiano Jumamosi ya tarehe 8 mwezi huu Juni 2019 katika dimba la  Kaitaba, wakihitaji ushindi ili kusalia Ligi Kuu.
Kagera Sugar wameangukia katika Play-Off baada ya kumaliza nafasi ya 18 kwenye Ligi Kuu ya Tanzania Bara, wakati Pamba SC ilimaliza nafasi ya pili kwenye Kundi B.
Baada ya mchezo huo tumezungumza na wadau wa vikosi vyote tukianzia na benchi la ufundi la klabu ya Wanakawekamo Tupuisant Lindanda al-maarufu Pamba Sports Club kuahirishwa kwa mchezo huu jana kumeathiri chochote?

UCHAGUZI MKUU MAALUM MPC "WENGI WATEMWA, WACHACHE WAREJEA"

Mwenyekiti mpya wa Chama cha Waandishi wa Habari Mkoa Mwanza, Edwin Soko (katikati) akitoa salamu zake za shukrani baada ya wajumbe wa Mkutano Mkuu Maalum uliofanyika jana Juni 01, 2019 katika ukumbi wa Nyanza jijini Mwanza kumchangua kushika nafasi hiyo hadi hapo mwakani 2020 uchaguzi mkuu utakapofanyika.

GB Pazzo, BMG
Wajumbe wa Mkutano Mkuu Maalum wa Chama cha Waandishi wa Habari Mkoa Mwanza (MPC) uliofanyika jana jumamosi Juni 01, 2019, wamewaondoa viongozi waliokuwa madarakani na kuwachagua viongozi wapya watakaokaa madarakani hadi mwakani 2020 utakapofanyika Uchaguzi/ Mkutano Mkuu.

Hatua hiyo ilijiri huku tayari tayari baadhi ya nafasi kama vile Mwenyekiti na Katibu Mkuu zikiwa wazi baada ya kujiuzulu mwanzoni mwa mwezi Mei mwaka huu 2019 kufuatia mashinikizo kutoka kwa wanachama waliokuwa wakiwalalamikia kutotimiza vyema majukumu yao.

Katika uchaguzi huo, Edwin Soko alichaguliwa kuwa Mwenyekiti, Makamu Mwenyekiti Albert Gsengo, Katibu Mkuu Magreth Kusekwa (akipanda kutoka Katibu Mkuu Msaidizi), Katibu Mkuu Msaidizi Projestus Binamungu, Mweka Hazina Paulina David (akitetea nafasi yake). Aidha mkutano huo pia uliwachagua wajumbe watano wa Kamati Tendaji MPC ambao ni George Binagi, Gloria Kiwia, Nashon Kennedy, Sitta Tuma pamoja na Philmon Malili (akitetea nafasi yake).

Itakumbukwa katika uchaguzi wa mwaka 2015, viongozi wa MPC waliochaguliwa walikuwa ni Mwenyekiti Osoro Nyawana (alijiuzulu), Makamu Mwenyekiti Neema Emmanuel, Katibu Mkuu Calvin Jilala (alijiuzulu), Katibu Mkuu Msaidi Magreth Kusekwa, Mweka Hazina Paulina David huku wajumbe wa Kamati Tendaji wakiwa ni Philmon Malili, Martha Lume, Antony Gervas, Shagatta Suleiman (amehamia mkoani Simiyu kikazi) na Neema Mwita (ametangulia mbele za haki).

Viongozi hao walipaswa kukaa madarakani kwa kipindi cha miaka mitatu lakini baadae UTPC ambayo ni taasisi inayolea klabu za waandishi wa habari Tanzania ilibadili Katiba na hivyo kufanya kupindi cha uongozi kwa klabu zote nchini kuwa miaka mitano badala ya mitatu.
Tazama picha na kisha video kujua zaidi yaliyojiri kwenye Mkutano Mkuu Maalum MPC
Makamu Mwenyekiti wa MPC, Albert George Sengo akisisitiza umoja na mshikamano baada ya kuchaguliwa kushika nafasi hiyo.
Katibu Mkuu MPC, Magreth Kusekwa akitoa shukrani zake baada ya kuchaguliwa kushika nafasi hiyo ambapo aliahidi ushirikiano ili kuhakikisha MPC inasonga mbele kimaendeleo.
Katibu Mkuu Msaidizi MPC, Projestus Binamungu akitoa salamu za shukrani ambapo alisisitiza uvumilivu miongozi mwa viongozi na wanachama kwa maslahi mapana ya chama.
Mweka Hazina MPC, Paulina David akiwashukru wajumbe wa Mkutano Mkuu Maalum kwa kumuamini na kumchagua kuitumikia tena nafasi hiyo.
Mmoja wa wajumbe wa Kamati Tendaji MPC yenye wajumbe wa watano akitoa salamu za shukrani baada ya kuchaguliwa kushika nafasi hiyo.
Mjumbe wa Kamati Tendaji MPC, Nashin Kennedy akitoa salamu zake za shukrani.
Mjumbe wa Kamati Tendaji MPC, Philmon Malili akiwashukru wajumbe wa Mkutano Mkuu Maalum kwa kumuamini na kumchagua tena kushika nafasi hiyo kwa mara nyingine.
Mjumbe wa Kamati Tendaji MPC, Sitta Tuma akitoa salamu zake za shukrani baada ya kuchaguliwa kushika nafasi hiyo.
Mjumbe wa Kamati Tendaji MPC, Gloria Kiwia akiwashukru wajumbe wa Mkutano Mkuu Maalum kwa kumchagua kushika nafasi hiyo.
Mkurugenzi wa Muungano wa Klabu za Waandishi wa Habari Tanzania (UTPC), Abubakar Karsan ambaye alikuwa msimamizi wa uchaguzi huo kwa kushirikiana na Hilda Kileo (hayuko pichani), akitoa ujumbe wako kwa wanachama na viongozi wapya MPC.
Mkurugenzi wa UTPC, Abubakar Karsan (katikati) pamoja na baadhi ya wajumbe wa Mkutano Mkuu Maalum MPC wakifuatilia mkutano huo.
Baadhi ya wajumbe wa mkutano huo wakifuatilia mijadala kwa umakini.
Baadhi ya wajumbe wa mkutano huo akiwemo aliyewahi kuwa Mwenyekiti MPC, Deus Bugaywa (katikati) wakifuatilia mawasilisho mbalimbali kwenye mkutano huo.
Viongozi wapia waliochagua kuiongoza MPC hadi hapo mwakani uchaguzi mkuu uakapofanyika kwa mujibu wa Katiba.
Wanachama wa MPC na viongozi wa UTPC wakiwa kwenye picha ya pamoja na viongozi wapya MPC.
Wanachama wa MPC na viongozi wa UTPC wakiwa kwenye picha ya pamoja na viongozi wapya MPC.
Baadhi ya viongozi wapya MPC wakipongezana baada ya uchaguzi.
Maakuli pia yalikuwepo.

TAKWIMU ZA MIMBA ZAMSHITUA KAMANDA WA POLISI MWANZA "hatuwezi kukubali"


Kamanda wa Polisi Mkoa Mwanza, ACP. Jumanne Muliro akifungua kikao kazi cha wadau mbalimbali wakiwemo viongozi wa Serikali za Mitaa, Ustawi wa Jamii, Dawati la Jinsia, Jeshi la Polisi na wataalamu wa afya mkoani Mwanza.

Kikao hicho kiliandaliwa na shirika la kutetea haki za wanawake na watoto (KIVULINI) la jijini Mwanza ili kuweka mikakati ya kuboresha upatikanaji wa huduma rafiki za afya kwa vijana na wahanga wa ukatili ikiwemo ubakaji na kutokomeza mimba katika umri mdogo.

Hatua hiyo ni sehemu ya utekelezaji wa mradi wa “sauti yangu, haki yangu katika kupunguza mimba za umri mdogo Manispaa ya Ilemela” unaosimamiwa na shirika la KIVULINI.
Na George Binagi-GB Pazzo, BMG
Wanahabari wakinasa matukio kwenye warsha hiyo ya kikazi.
Mkurugenzi wa shirika la KIVULINI, Yassin Ally akifafanua jambo kwenye kikao hicho.
Mwakilishi kutoka jeshi la polisi mkoani Mwanza akiongoza wajumbe wa kikao kazi hicho kuweka mikakati ya upatikanaji wa huduma rafiki kwa wahanga wa ukatili.
Mmoja wa washiriki wa kikao kazi hicho akichangia mada.

NAIBU WAZIRI JULIANA SHONZA AWAASA VIJANA VISIWANI ZANZIBAR KUTHAMINI VIPAJI VYAO

 Naibu  Waziri  wa  Wizara  ya  Habari  Utamaduni  Sanaa  na  Michezo, Juliana Shonza akisalimiana  na  wachezaji  wa  timu  ya Miembeni  kabla  ya  kuanza kwa  mchezo  wa  Nusu Fainali  ya  Kombe  la  Masauni/Jazeera  uliofanyika katika  Viwanja  vya  Tumbaku, Visiwani Zanzibar.
 Naibu  Waziri  wa Wizara ya Habari Utamaduni Sanaa na Michezo, Juliana Shonza  akisalimiana  na wachezaji  wa  timu ya Kundemba, kabla  ya  kuanza kwa mchezo wa Nusu Fainali ya Kombe  la Masauni/Jazeera uliofanyika katika Viwanja  vya Tumbaku, Visiwani  Zanzibar.
 Mbunge  wa  Jimbo la Kikwajuni, Mhandisi  Hamad  Masauni, akizungumza kabla ya kuanza mchezo wa Nusu Fainali wa Mashindano ya Masauni/Jazeera uliofanyika katika Viwanja vya Tumbaku, Visiwani Zanzibar. Kulia ni Naibu Waziri wa Wizara ya Habari Utamaduni Sanaa na Michezo, Juliana Shonza.
Naibu Waziri  wa Wizara ya Habari Utamaduni Sanaa na Michezo, Juliana Shonza  akizungumza kabla  ya  kuanza  mchezo  wa Nusu Fainali wa Mashindano ya Masauni/Jazeera uliofanyika katika Viwanja vya Tumbaku, Visiwani Zanzibar. Kushoto  ni Mbunge wa Jimbo la Kikwajuni, Mhandisi Hamad Masauni.Picha na Mpigapicha Wetu