Mashindano ya KAMANDA SIRO CUP yanatarajiwa kufanyika kesho tarehe 16.04.2011 siku ya jumamosi katika uwanja wa CCM Kirumba kuanzia saa 4:00 asubuhi na kuendelea. Kablea ya Bonanza kutakuwa na maandamano ya washiriki kuanzia saa 3:00 asubuhi yatakayoanzia ofisi ya Mkuu wa mkoa wa Mwanza kupitia barabara ya Makongoro hadi CCM Kirumba, maandamano yakiongozwa na Brass band, Waendesha pikipiki, Magari na Watembea kwa miguu.
Kamanda Sirro amewaomba wananchi wa jiji la Mwanza na wageni kujitokeza kwa wingi kushiriki kwenye maandamano hayo wakiwa na nguo za michezo (Track suits)
Mwanamke mmoja wa nchini Uingereza ametumia paundi 20,000 (Karibia Tsh. Milioni 50) kwaajili ya kuandaa harusi ya kifahari na gauni la harusi la kifahari kwaajili ya mbwa wake wa kike. Louise Harris mwenye umri wa miaka 32 alitumbua paundi 20,000 kwaajili ya harusi ya kifahari ya mbwa wake wa kike anayeitwa Lola ambaye aliozeshwa kwa mbwa anayeshikilia taji la mbwa mwenye sura mbaya kuliko wote Uingereza anayejulikana kwa jina la Mugly.Sherehe hiyo ya kifahari ilihudhuriwa na watu 80 ambapo gharama za kuukodisha ukumbi kwaajili ya harusi hiyo ya aina yake ilikuwa paundi 2,500. Mbwa Lola alivalishwa gauni la harusi lenye thamani ya paundi 1,000 ambalo lilitengenezwa maalumu kwaajili yake na duka la vito vya thamani la Swarovski.
Mbwa Lola pia alivalishwa cheni shingoni na kikuku mguuni ambavyo vyote viligharimu paundi 750. Maua ya kupamba ukumbi wa harusi yaligharimu paundi 1,000 wakati wapambaji wa ukumbi walilipwa kitita cha paundi 3,000.
Miongoni mwa gharama za harusi hiyo ni mabaunsa waliokuwa wakilinda usalama kwenye harusi hiyo ambao walilipwa paundi 400, madansa na wacheza shoo waliolipwa paundi 500, gari la kukodisha aina ya Bentley kwaajili ya maharusi liligharimu paundi 500 wakati Dj alilipwa paundi 500.
"Mbwa wangu ni fahari yangu na furaha yangu ni kuwafanyia kila kilicho kizuri", alisema bi Harris.Bi Harris alisema kuwa furaha yake imetimia kwa kuona Lola amefanikiwa kupata mwenza wake wa maisha ambaye amekuwa akicheza naye wakati wote.
kwa hisani ya www.telegraph.co.uk
Real Madrid itakutana na Barcelona katika nusu fainali ya klabu bingwa Ulaya baada ya kuizaba Tottenham Hotspur kwa bao moja kwa sifuri kwenye uwanja wa White Hart Lane.Bao pekee la Ronaldo liliizamisha Spurs huku Real ikisonga mbele kwa jumla ya mabao 5-0.
Inter Milan nayo iliyaaga mashindano hayo baada ya kuzabwa mabao 2-1 na Schalke 04. Schalke inasonga mbele kwa jumla ya mabao 7-3.
Schalke sasa itakutana na Manchester United katika nusu fainali. United ilitinga nusu fainali baada ya kuinyuka Chelsea kwa jumla ya mabao 3-1.
Niliidaka juu kwa juu tu! leo katika mjadala wa kupitisha Hoja moja wapo kuelekea mchakato wa kupata wawakilishi wa Bunge la Afrika kupitia televisheni LIVE na nikakuta Mbunge wa Nyamagana Mh. Ezekiel Wenje ndiye alikuwa amesimama akitoa pendekezo nao wabunge wenzake wakimzodoa.
Mara sauti zikasikika na nilizozinasa ni hizi;
*****-"akanywe kikombe cha babu huyo...!"
*****-"futa kauli!"
*****-"we vipi waambiwa huna maskio!"
*****-"jamani hatuko klabu tuko bu-nge-ni!"
*****-"out!out katuburuza huyo!!"
SPIKA: "jamani naomba utulivu!!"
*****-"hatoki mtu nje!!"
*****-"tutatoka wote....!!!"
*****- "tufunge mlango tupigane!!...!!"
(***)-"naona mnafanya mnada badala ya kuendelea na bunge"
*****-"msitumie wingi wenu kutuburuza!!"
SPIKA: "watu mmechaguliwa na kura za wananchi kwanini mwafanya mambo ya kitoto hivi hamjui kuwa tunaonwa na wananchi?...!
Ndipo atilisti utulivu ukapatikana uchaguzi wa Pan Africa Parliament ukaendelea....
Wednesday, April 13, 2011
HABARI
“CCM inatakiwa kujengwa upya kabisa na ili hayo yaweze kufanikiwa, kuna kila sababu za kuwa na watu safi, hivyo mimi nawataka ndugu zangu wasimame katika misingi ya zamani tuliyokuwa nayo katika chama chetu,” alisema Mukama na kuongeza:“Nawataka wote wenye tuhuma za rushwa na ufisadi ndani ya chama waanze kujiuzulu mapema ili kulinda heshima yao, kwani tunaingia kujenga chama sio kukibomoa.”
JUU YA CHAMA KUJENGWA UPYA:
"Ili tuweze kufanikiwa katika hilo mimi nitasimamia maamuzi ya Kamati Kuu ya CCM ya kukirudisha chama kwa wanachama ngazi ya chini ili wao ndio wakafanye maamuzi.”
Mukama ambaye alikuwa akizungumza kwa kujiamini alisema atasimamia kikamilifu itikadi ya Ujamaa na Kujitegemea, kwa kuwa ndio sera kubwa ya CCM tangu kuanzishwa kwake.
Jambo lingine alilosisitiza kiongozi huyo ni pamoja na kukiongoza chama katika kupata ushindi ambao hautakuwa ukitiliwa mashaka na watu wengine.“Jambo kubwa na la msingi hapa ni kukiongoza chama katika kufikia malengo makubwa ya kupata ushindi usiokuwa na manung’uniko, kwani mbinu za kivita hupatikana katika medani sio uwanja wa vita,” alitamba Mukama. Hata hivyo, alisifia hatua ambayo imechukuliwa na chama ambayo imesaidia kukijenga hadi sasa.
Aliyataja mafanikio ya hatua hiyo kuwa ni pamoja na kuwa viti vingi bungeni, kwani zaidi ya asilimia 78 ya wabunge wanatoka CCM.
ABEZA NGUVU YA UPINZANI:
Akizungumzia nguvu za upinzani, Mukama alibeza na kusema hilo haliwezi kumsumbua yeye wala kumfanya asilale usingizi, kwani anatambua ni wapi panatakiwa kusimamiwa na ni wapi panatakiwa kutolewa maelekezo yake.
“Kwenye siasa hata siku moja ni kubwa sana huwezi kuidharau. Leo tutazungumzia miaka minne ili tuingie katika Uchaguzi Mkuu mwingine, hivyo bado kuna muda mzuri na wa kutosha kufanya maandalizi, ndio maana siwezi kutaja moja kwa moja chama kinachonipa tabu bali kitajulikana mbele ya safari,” alitamba Mukama
MAKONGORO NYERERE AMCHOCHEA JK:
Mtoto wa Baba wa Taifa ambaye pia ni Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Mara, Makongoro Nyerere, amemshauri Mwenyekiti wake Rais Kikwete, kuwabwaga wote wanaotuhumiwa kwa ufisadi hata kama ni maswahiba wake kisiasa ili kukinusuru chama.
Kwahisani ya www.mwananchi.co.tz
Aliyekuwa Waziri Mkuu wa Tanzania kwa vipindi viwili (3 Februari 1977 na 7 Novemba 1980) na(24 Februari 1983 to 12 Aprili 1984), Hayati Edward Moringe Sokoine, anakumbukwa leo. SOKOINE alifariki kwa ajali ya gari huko Dakawa, Morogoro tarehe 12 Aprili 1984 na sasa yapata miaka 26 tangu tukio hilo lililozua simanzi kutokea. Kutakuwa na misa ya kumbukumbu ya kifo chake katika kanisa la Mt Joseph jijini leo jioni iliyoandaliwa na familia ya kiongozi huyo wa zamani aliye heshimika sana nchini.
HIVI MAJUZI:-
Serikali ya Mkoa wa Morogoro kwa kushirikian na Wilaya ya Mvomero, tayari zimetenga Sh bilioni 12 kwa ajili ya mradi wa ujenzi wa Shule ya Sekondari ya juu itakayokuwa na Kidato cha Tano na Sita eneo la Kijiji cha Wami Ruhindo, alipofia aliyekuwa Waziri Mkuu, Edward Moringe Sokoine.
Shule hiyo imepewa jina la Sokoine Memorial High School, ambapo ujenzi wa awamu ya kwanza iliyotengewa kiasi cha sh bilioni tatu unatarajia kuanza Mei, 2011 na kukamilishwa Desemba 2011 na wanafunzi wa kwanza wa kidato cha tano wanatarajia kuanza mapema Februari 2012.
SWALI:-
Je! VIONGOZI WETU WANAENZI VIPI MAWAZO YAKE KATIKA KUSIMAMIA RASLIMALI ZA TAIFA LETU?
Tuesday, April 12, 2011
BANGO
Tuesday, April 12, 2011
HABARI
Kiongozi wa Ivory Coast Laurent Gbagbo ametiwa kizuizini mjini Abidjan na kuwekwa chini ya ulinzi wa polisi wa Umoja wa Mataifa.Alikamatwa wakati majeshi ya kiongozi anayetambulika kimataifa kuwa Rais wa nchi hiyo Alassane Ouattara na vifaru vya Ufaransa kuingia kwenye makazi yake. Bw Gbagbo alikuwa akikataa kukabidhi madaraka, akisema alishinda uchaguzi wa Rais wa mwezi Novemba. Ufaransa ilisema majeshi yanayomwuunga mkono Ouattara yalimkamata, lakini washirika wa Bw Gbagbo walisema ni majeshi maalum ya Ufaransa.
Majeshi ya kutunza amani ya umoja huo yaliyashutumu majeshi yanayomwuunga mkono Bw Gbagbo kwa kuhatarisha maisha ya raia na kuiomba Ufaransa, ambalo lilikuwa koloni lake, kuondosha silaha nzito za kiongozi huyo.Kumekuwa na madai ya ukatili kufanywa na wote wafuasi wa Gbagbo na Ouattara, na umoja huo una taarifa ya zaidi ya watu 1,000 kuuawa na takriban 100,000 kukimbia nchi hiyo.
Wawakilishi wa kudumu wa Umoja wa Mataifa wa Ivory Coast, Youssoufou Bamba, walisema Bw Gbagbo atashtakiwa. Mjini London, Waziri wa mambo ya nje wa Uingereza William Hague alisema kama atafunguliwa mashtaka, basi ashtakiwe kwa kuzingatia njia zinazostahili.
Waziri wa mambo ya nje wa Marekani Bi Hillary Clinton alisema mjini Washington kwamba kukamatwa kwa Bw Gbagbo kumepeleka ujumbe kwa "madikteta" ambao "hawatopuuza sauti za watu wao katika uchaguzi wa haki na huru."
**OUATTARA AOMBA UTULIVU.
Rais wa Ivory Coast anayetambulika na jamii ya kimataifa, Alassane Ouattara, ametoa wito wa kuwepo kwa hali ya utulivu baada ya kumkamata mpinzani wake Laurent Gbagbo.
Kwa hisani ya bbc swahili
Pozi namba moja - 'kacha'
Pozi namba mbili - 'kacha'
Pozi namba tatu - 'kacha'
'asanteni kwa kunisikiliza'
Mfanyabiashara wa Marekani Stan Kroenke ameongeza hisa zake katika klabu ya Arsenal na kufikia asilimia 62.89, na pia kukubali kutaka kununua hisa zote zilizosalia za klabu hiyo.
Hamu ya kununua hisa zote ilikuja baada ya kampuni ya Kroenke (KSE) kununua hisa za Danny Fiszman asilimia 16.1 na za Lady Nina Bracewell-Smith asilimia 15.9. Makubaliano yamefikiwa pia na kununua mtaji wa hisa uliosalia, huku Arsenal ikikadiriwa kuwa na thamani ya Pauni milioni 731.
MAKAO YA TAJIRI HUYO JUU YA JENGO LA DENVER'S PEPSI CENTER.
Kroenke alinunua asilimia 9.9 za hisa za Arsenal kwa mara ya kwanza mwaka 2007. "Tumefurahia nafasi hii na kujihusisha zaidi na kuonesha nia na Arsenal," amesema Kroenke mwenye umri wa miaka 63, ambaye kampuni yake pia inamiliki timu ya mpira wa kikapu ya Denver Nuggets inayocheza ligi ya NBA, na pia timu ya Colorado Avalance ya ligi ya NHL, na St Louis Rams ya ligi ya NFL, na Colorado Rapids inayocheza ligi kuu ya soka Marekani.
Hisa nyingi zilizosalia ambazo Kroenke huenda akazinunua zinamilikiwa na bilionea wa Urusi Alisher Usmanov.
Kiungo wa Yanga, Nurdin Bakari aliyetupia bao la kisigino lililotosha kufuta ndoto ya Simba ya kutetea ubingwa wake pamoja na timu hiyo ya mtaa wa msimbazi kupata karamu ya mabao 4-1 dhidi ya Majimaji.Mkuu wa mkoa wa Mwanza Abbas Kandoro akimkabidhi kombe la ubingwa Tanzania bara nahodha wa Yanga Shadrack Nsajigwa.
Kikosi kazi Yanga Afrika kilichoifunga Toto 3-0.
Abbas Kandoro akisalimiana na Kipa wa Yanga, Yaw Berko ambaye kama kawaida yake alitumia mbinu zote nyavu za goli lake zisitikisike kwani katika mchezo huo alipewa kadi ya njano dakika 22, baada ya kudaka mpira nje ya 18, baada ya kurudishiwa pasi fupi, lakini aliweza kuokoa faulo hiyo.
Kwa makiiini'' na nasaha za kuu wa mkoa wa Mwanza.
Hadi kipindi cha kwanza kinaisha hakuna aliyeweza kuchungulia goli la mwenzake lakini alikuwa kiungo Nurdin Bakari ndiye aliyeipatia Yanga bao la kuongoza dakika ya kwanza ya kipindi cha pili, kwa mpira wa adhabu nje ya eneo la 18, ile kuanza tu mchezo....'KITUuu!!' Nalo goli la pili likafungwa nae Davis mwape.
Nurdin akiwa amelipa mgongo goli alipokea mpira uliokuwa ukizagaa kwenye eneo la 18, kupiga kisigino na kumwacha kipa wa Toto Afrika, Hussein Tade aliyeingia kuchukua nafasi ya Wilbert Mwate akiruka uelekeo mwingine na mpira ukipenya kwa sataili ya aina yake hivyo kuipa Yanga bao la tatu.
Wachezaji wa Yanga mara baada ya goli la Nurdin Bakari (jezi no.5) wengine ni Jerry Tegete (10), Chacha Marwa (24) na Idd Mbaga (22). Kipa Tade aliingia uwanjani dakika ya 83 kuchukua nafasi ya Mweta aliyekuwa kikwazo kikubwa kwa Yanga, mara baada ya kupata maumivu ya paja.
Mabingwa hao wapya walianza mchezo huo taratibu na kuifanya Toto kutawala sehemu kubwa ya kipindi cha kwanza, lakini mambo yalibadilika nusu ya pili na kufanikiwa kupata mabao matatu muhimu.
Kombe la ligi kuu ya Vodacom Tanzania bara lilipokuwa tayari kwa mabingwa wapya 2010-2011.
Yanga wakilionesha kombe lao kwa mashabiki waliofurika katika dimba la CCM Kirumba.
Tegete juu kwa juu na mashabiki wa Yanga, Timu hiyo imekuwa bingwa baada ya kufikisha pointi 49 sawa na timu ya Simba lakini imetawazwa bingwa baada ya kuwa na uwiano wa magoli 25 na 24 dhidi ya mahasimu wao Simba.
Mashabiki wa Yanga jijini Mwanza walifanya maandamano toka uwanja wa CCM Kirumba kupitia barabara ya makongoro hadi katikati ya jiji na hatimaye sikujuwa ila nauhakika ilikuwa either majumbani kwao ama sehemu za maraha kwani ilikuwa shangwe kwa ngoma, matrarumbeta na kupeperusha bendera.
ORODHA YA MABINGWA 2000-2011
2000 - Yanga
2001 - Simba
2002 - Simba
2003 - Simba
2004 - Simba
2005 - Yanga
2006 - Yanga
2007 - Simba
2008 - Yanga
2009 - Yanga
2010 - Simba
Na hatimaye ubingwa kwa mwaka..2011 = Yanga