ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

Saturday, October 22, 2016

BHUDAGALA - NG'WANAMPELA

Bhudagala ni jina lililo maarufu katika zama za sasa ndani ya kabila la watu wa Sukuma, ukipata nafasi kuingia ndani ya wilaya na vijiji mbalimbali kanda ya ziwa utapata majibu ya hiki ninachokujuza hapa.

Nimewahi kuhudhuria sherehe mbalimbali za wadau kanda ya ziwa ikiwa ni pamoja na matamasha na kupata fursa ya kuzisikia na kushuhudia watu wakizicheza nyimbo za jamaa huyu tena zikiombwa na kurudiwa rudiwa.

Jamaa anajaza show zaidi ya vile unavyodhani tena bila ya promo ya redio wala mitandao.

KISA NA MKASA
Ujumbe unaowasilishwa unaigusa jamii ukielezea maisha halisi ya watu wa kijijini wa hali ya chini na changamoto zao umekuwa kichocheo cha yote hayo, na haiishii hapo lugha nayo imekuwa sababu ya kuusababisha muziki wa jamaa huyu kuvuma sana kwani wengi hasa vijiji vya ndani usukumani hawaijui vyema legha ya kiswahili hivyo kwa mwanamuziki huyu kuimba akitumia lugha mama ya kabila lake imekuwa kichocheo cha kukubalika.

Lakini kingine kikubwa ni uwezo pia katika kuimba na kucheza.

SAKATA LA WANAFUNZI HEWA MWANZA LAFIKIA PAZITO.

Mkuu wa mkoa wa Mwanza aunda kamati kuchunguza tuhuma ya kughushi takwimu za idadi ya wanafunzi katika shule za msingi.

OCTOBER 23 UKUMBI WA CCM MWIJUMA HAPATOSHI.

Kocha wa wa kimataifa wa mchezo wa masumbwi nchini Rajabu Mhamila 'Super D ' katikati akiwa na mabondia Iddi Mkwela kushoto na Issa Nampepeche baada ya kupima uzito kwa ajili ya mpambano wao wa  raundi kumi utakaofanyika siku ya jumapili ya October 23 katika ukumbi wa CCM Mwijuma Mwananyamala Picha na SUPER D BOXING NEWS
Mabondia Iddi Mkwela kushoto akitunishiana misuli na Issa Nampepeche baada ya kupima uzito kwa ajili ya mpambano wao wa jumapili ya Ocober 23 katika ukumbi wa CCM Mwijuma Mwananyamala Picha na SUPER D BOXING NEWS


Kocha wa kimataifa wa mchezo wa masumbwi nchini katikati Rajabu Mhamila 'Super D ' akimtia gumi la kolomelo kocha wa ISSA Nampepeche  Ibrahimu Kamwe wakati wa upimaji uzito baada ya kokosana kauli kila mmoja akidai bondia wake zaidi Super D anamnowa Iddi Mkwela na Kamwe anamfundisha Nampepeche 
Kocha wa wa kimataifa wa mchezo wa masumbwi nchini Rajabu Mhamila 'Super D ' katikati akiwa na mabondia Iddi Mkwela kushoto na Issa Nampepeche baada ya kupima uzito kwa ajili ya mpambano wao wa  raundi kumi utakaofanyika siku ya jumapili ya October 23 katika ukumbi wa CCM Mwijuma Mwananyamala 
Bondia Iddi Mkwela akihojiwa na wana habari nyuma ni kocha wake Rajabu Mhamila 'Super D' 
Bondia Mohamed Kisua akipima uzito kwa ajili ya mpambano wake kesho jumapili
mohamedi kisua
bondia Pius Kazaula akipima uzito
PIus Kazaula
Bondia Iddi Mkwela akipima uzito kushoto ni mpinzani wake Issa Nampepeche
Bondia Rojas Masamu akipima uzito kwa ajili ya mpambano wake na Haidal Raju.

Friday, October 21, 2016

TEKNOMILES - DIANA (OFFICIAL VIDEO)

Teknomiles - Diana [Official Video]
Published on Oct 21, 2016

Tekno drops the official video to his latest single "Diana".
Tekno sure has won the hearts of many after dropping hits back to back and topping them off with amazing videos.

VIJANA WAJASILIAMALI TOKA WILAYA YA MAGU WAVUNJA REKODI KWA MIRADI.

Mkuu wa kitengo cha mawasiliano na huduma za jamii (NHC) Bi. Susan Omari akikabidhiwa Taarifa ya Mradi.
Nyumba zilizofanikiwa kujengwa.
Ufyatuaji matofali.
Taarifa...
Ukaguzi na eneo la mradi.
Moja ya nyumba zilizojengwa kwenye mradi.
Madi ukikamilika hatua kwa hatua.
Mkuu wa kitengo cha mawasiliano na huduma za jamii (NHC) katika picha ya pamoja na wadu wa mradi.
TAREHE 20.10.2016

Zaidi ya vijana 40 wanaounda vikundi vitatu vya ujasiriamali wilayani Magu mkoani Mwanza, vilivyokabidhiwa Mashine moja ya kufyatulia matofali, chini ya mpango wa Shirika la nyumba la Taifa (NHC), wamefanikiwa kujikwamua kiuchumi.

Hii ni historia mpya iliyotengenezwa na vijana hawa ya kutotegemea ajira za Serikali kwa kujiajiri, baada ya kukamilisha ujenzi wa nyumba sita za gharama nafuu, zilizowawezesha kuwapa sifa ya kupata zabuni za ujenzi wa nyumba nyingine bora za kisasa nje na ndani ya nchi.

Akikamilisha ziara ya kukagua miradi hiyo, mkuu wa kitengo cha mawasiliano na huduma kwa jamii wa Shirika la Nyumba la Taifa Susan Omari, amesema wameridhishwa na utekelezaji wa miradi hiyo, na hivyo kuviongezea vikundi hivyo mashine mbili za kufyatulia matofali.

Vikundi hivyo vimewezeshwa, ili kuondokana na kilio cha ukosefu wa ajira, lakini pia kuwaepusha vijana na makundi yanayojihusisha vitendo vya uhalifu ikiwemo suala la matumizi ya dawa za kulevya, wizi na ujambazi.

Mkakati wa Shirika la nyumba la Taifa (NHC) ni kuhakikisha vijana katika maeneo mbalimbali nchini, wanaondokana na tatizo la kilio cha muda mrefu cha ukosefu wa ajira kwa kujiajiri wao wenyewe katika shughuli mbalimba za ujasiriamali.

NA ZEPHANIA MANDIA
GSENGO BLOG.

KITILLYA NA WENZAKE WATAKA UPELELEZI UHARAKISHWE

UPANDE wa utetezi katika kesi inayowakabili Harry Kitillya, aliyekuwa Kamishina Mkuu wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA), Shose Sinare, Mkuu wa Idara ya Ushirikiano na Uwezekezaji katika Benki ya Stanbic na Sioi Solomoni, mwanasheria wa benki hiyo, umeutaka upande wa Jamhuri kuwahisha upelelezi, anaandika Faki Sosi.
Alex Mgongolwa, wakili wa watuhumiwa hao. Mbele ya Hakimu Mkazi Mkuu Respecious Mkeha amedai kuwa upelelezi wa kesi hiyo una muda wa miezi sita bila kukamilika.

Awali, wakili wa serikali Kishenyi Mutalemwa alidai mahakamani hapo kuwa upelelezi wa shauri hilo haujakamilika na kwamba Mkurugenzi wa Mashtaka ameeleza kuwa Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa(TAKUKURU) inaendelea na upelelezi.

Hakimu Mkeha ameitaka Jamhuri kukamilisha Upelelezi wa shauri hilo kwa wakati huku akitangaza kuahirisha kesi hiyo mpaka terehe 4 Novomba, Mwaka huu.

Watuhumiwa hao walipandishwa kizimbani katika mahakama hiyo kwa kosa la kuhujumu uchumi wakidaiwa kughushi nyaraka na kufanikisha uhalifu huo kati Agosti 2012 na Machi 2013 jijini Dar es Salaam.

Kosa la pili, linadaiwa kufanywa na Sinare, tarehe 2 Agosti mwaka 2012 kwa kughushi hati ya mkopo wa Dola za Marekani 550 milioni katika Benki ya Stanbic ya Tanzania na Benki ya Standard ya Uingereza akiiombea fedha Serikali ya Tanzania.

Sinare anatuhumiwa kwa kosa la tatu alilotenda tarehe 13 Agosti 2012, la kupeleka hati ya kughushi kwenye Wizara ya Fedha iliyoonesha kuwa Serikali ya Tanzania itapewa mkopo wa Dola za Marekani 550 milioni kutoka Benki ya Stanbic ya Tanzania na Standard ya Uingereza.

Washitakiwa hao pia wote wanakabiliwa na kosa la kutengeneza mkataba bandia tarehe 5 Novemba, mwaka 2012 jijini Dar es Salaam katika Makao Makuu ya Benki ya Stanbic kupitia Kampuni ya Enterprise Growth Market Advisor (EGM).

Shitaka lingine linalowakabili watuhumiwa wote ni utakatishaji fedha wanalodaiwa kulitenda kati ya mwezi Machi 2013 na Septemba 2015.

TMC YATAMBULISHA VIPAJI VYA MASAUTI. SASA KUVITAMBULISHA KATIKATI YA TUKIO LA KUSAKA VIPAJI LA MISS TANZANIA JUMAMOSI HII 22 OCT 2016 JEMBE BEACH.

💯...... Wayaaaaaa siku moja kabla ya usiku wa kusaka vipaji katika #misstztalent ya Miss Tanzania 2016, TMC imetambulisha vipaji leo ndani ya #KAZINANGOMA ya JEMBE FM hawa mabinti wawili toka Team maua classic wanaimba hao.... Hapa wakiwa katika picha ya pamoja na Rais wao @bobwhite_pamba (C) Usije laumu kuwa sikukwambia ni tarehe 22/October yaani Jumamosi hii #JembeBeachResort kiingilio buku 5 tu. #VyumaVimekaza #DebeNAjembe

TMC YATAMBULISHA VIPAJI VYA MASAUTI. SASA KUVITAMBULISHA KATIKATI YA TUKIO LA KUSAKA VIPAJI LA MISS TANZANIA JUMAMOSI HII 22 OCT 2016 JEMBE BEACH.

💯...... Wayaaaaaa siku moja kabla ya usiku wa kusaka vipaji katika #misstztalent ya Miss Tanzania 2016, TMC imetambulisha vipaji leo ndani ya #KAZINANGOMA ya JEMBE FM hawa mabinti wawili toka Team maua classic wanaimba hao.... Hapa wakiwa katika picha ya pamoja na Rais wao @bobwhite_pamba (C) Usije laumu kuwa sikukwambia ni tarehe 22/October yaani Jumamosi hii #JembeBeachResort kiingilio buku 5 tu. #VyumaVimekaza #DebeNAjembe

WAKENYA KWA MR. NICE HAWAAMBIWI KITU SABABU NI HII.....


Mwanamuziki, Lucas Mkenda ‘Mr Nice’ amesema ukongwe wake kwenye muziki ndiyo kitu ambao kinampatia mashavu zaidi nchini Kenya.
Akiongea na Bongo5 Alhamisi hii, Mr Nice amesema Kenya ni sehemu pekee ambazo anaweza kufanya show nyingi bila mashabiki kumchoka.
“Najivunia kuwa rafiki namba moja wa Wakenya,” alisema Mr Nice. “Hiyo ni silaa yangu kubwa katika muziki wangu, kwa hiyo labda ni kwa sababu tayari tumeshatengeneza chemistry nao toka naanza kufanya muziki,”
Muimbaji huyo ambaye anafanya vizuri na albamu yake ya Kioo, hivi karibuni alijaza umati wa mkubwa katika show yake iliyofanyika katika club moja huko nchini Kenya.
Muimbaji huyo ijumaa hii atakuwa mjini Kisumu na Jumamosi atakuwa katika jiji la Nairobi maeneo ya Embakassy katika muendelezo wa show zake.

BOMOA BOMOA YAKUMBA NYUMBA 150 DAR, VITA KUKABILI NJAA YATANGAZWA, SERIKALI YAREJESHA SH 8,500 KWA WANAFUNZI VYUO VIKUU.


Bomoa bomoa yakumba nyumba 150 Dar, Vita kukabili njaa yatangazwa, Serikali yarejesha sh 8,500 kwa wanafunzi vyuo vikuu. Pata undani wa dondoo hizi za magazeti ya leo hapa.


Serikali yatangaza ukame na njaa, majambazi hatari wauawa bunduki 7 zakamatwa, Makada 10 wavuliwa uanachama wa CCM. Habarika na dondoo hizi za magazeti ya leo hapa. 

Mkurugenzi ampigisha deki mwalimu, Madeni ya Mbowe yaitesa CHADEMA, Bunge laigomea serikali kisa posho. Pata dondoo za magazeti ya leo hapa.

Thursday, October 20, 2016

WANAFUNZI PAMBA SEC WARIPOTI VIPIGO.


Wanafunzi wa shule ya sekondari ya pamba jijini mwanza wameiomba serikali kukomesha vitendo vya ukatili wanavyotendewa na walimu wao ikiwemo  vipigo kupita kiasi pamoja na baadhi yao kuvuliwa nguo wakati wa kuchapwa viboko.

Wakizungumza wakati wa mdahalo wa kujadili ukatili wa kijinsia, baadhi ya wanafunzi wa shule hiyo wamesema kuwa ukatili wanaotendewa na walimu wao umekuwa ukichangia mahudhurio hafifu shuleni na hivyo kusababisha wengi wao kushuka kitaaluma.

Wanafunzi wa shule ya sekondari ya pamba iliyoko jijini mwanza wakijadili vitendo vya ukatili wanavyotendewa na jamii,wazazi pamoja na walimu wao.

Baadhi ya wanafunzi hao wametumia fursa hiyo kulalamikia ukatili wa vipigo kutoka kwa walimu wao.

Wakizungumzia malalamiko hayo,baadhi ya walimu wa  sekondari ya pamba wakawa na neno.

Mdahalo huo uliandaliwa na shirika la kutetea haki za wanawake na watoto la KIVULINI ambapo mkurugenzi wa shirika hilo YASINI ALLY  amewashauri walimu wa shule hiyo kuimarisha mahusiano  yao na wanafunzi.

Wanafunzi wa shule ya sekondari ya pamba pia wameeleza kutendeana ukatili wao kwa wao.

BARAZA LA TAIFA LA USALAMA BARABARANI LAKUTANA KUJADILI MAENDELEO YA MKAKATI WA KUPUNGUZA AJALI.

Mwenyekiti wa Baraza la Taifa la Usalama Barabarani  ambaye pia ni Naibu Waziri wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni, akizungumza na wajumbe wa baraza hilo wakati wa kikao cha kujadili maendeleo ya Mkakati wa Kupunguza Ajali za Barabarani. Kulia ni Katibu Mtendaji wa baraza ambaye pia ni Kamanda wa Kikosi cha Usalama Barabarani, Mohamed Mpinga.Kikao hicho kimefanyika katika ukumbi wa wizara hiyo, Dar es Salaam. (Picha na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi)
Katibu Mtendaji wa Baraza la Taifa la Usalama Barabarani nchini  ambaye pia ni Kamanda wa Kikosi cha Usalama Barabarani, Mohamed Mpinga, akifungua kikao cha kujadili maendeleo ya Mkakati wa Kupunguza Ajali za Barabarani.Kushoto ni  Mwenyekiti wa Baraza la Taifa la Usalama Barabarani  ambaye pia ni Naibu Waziri wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni. Kikao hicho kimefanyika katika ukumbi wa wizara hiyo, Dar es Salaam. (Picha na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi)
Mwenyekiti wa Baraza la Taifa la Usalama Barabarani  ambaye pia ni Naibu Waziri wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni, akiongoza kikao cha kujadili maendeleo ya Mkakati wa Kupunguza Ajali za Barabarani. Kushoto  ni Katibu Mtendaji wa baraza ambaye pia ni Kamanda wa Kikosi cha Usalama Barabarani nchini, Mohamed Mpinga.Kikao hicho kimefanyika katika ukumbi wa wizara hiyo, Dar es Salaam.(Picha na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi)
Mjumbe wa Baraza la Taifa la Usalama Barabarani kutoka Kikosi cha Usalama Barabarani, Mrakibu Msaidizi wa Jeshi la Polisi, Mossi Ndozero, akiwasilisha taarifa ya maendeleo ya Mkakati wa Kupunguza Ajali za Barabarani kwa Mwenyekiti wa Baraza la Taifa la Usalama Barabarani  ambaye pia ni Naibu Waziri wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni(hayupo pichani), wakati wa kikao cha kujadili maendeleo ya mkakati huo, kilichofanyika katika ukumbi wa wizara, Dar es Salaam. (Picha na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi)
Mjumbe wa Baraza la Taifa la Usalama Barabarani, Hamza Kasongo(kulia), akichangia mada wakati wa kujadili  taarifa ya maendeleo ya Mkakati wa Kupunguza Ajali za Barabarani wakati wa kikao cha kujadili maendeleo ya mkakati huo.Kushoto ni mjumbe wa baraza hilo Henry Bantu. Kikao hicho  kilifanyika katika ukumbi wa wizara, Dar es Salaam.(Picha na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi)

IMEANDALIWA NA KITENGO CHA MAWASILIANO SERIKALINI, WIZARA YA MAMBO YA NDANI YA NCHI.

AWAUWA KWA KUCHOMWA NA KITU CHENYA NCHA KALI MWANZA.

NA ANNASTAZIA MAGINGA, 
GSENGO BLOG,
Mwanza.

MTU  mmoja alieyefahamika kwa jina la Dema Charles (20) Mkazi wa kata ya Ibungulo Wilayani Magu ameuwawa na wengine wawili kujeruhiwa na watu wasio julikana kwa kuchomwa na kitu chenye ncha kali katika miili yao.

Tukio hilo limetokea tarehe 18 saa 5 ambapo marehemu aliuwawa kwa kuchomwa na kitu chenye ncha kali Shingoni huku Mariamu Lukas (26) alijeruhiwa kwenye mkono na Kipele Makubi (90) ambaye ni baba wa nyumba hiyo alijeruhiwa mgongoni  na kichwani na kwamba wako hospitalini kwa matibabu zaidi.

Akizungumza na waandishi wa habari leo kamanda wa polisi Amed Msangi amesema watu hao ambao hawakufahamika kwa wakati walifika kwenye nyumba hiyo usiku na kuanza kufanya maujai hayo na kwamba upelelezi bado unaendelea.

Kwa mujibu wa kamanda amesema kufuatia upelelezi wa awali imesadikika kuwa ni kisasi ndicho kinalipizwa na watu hao kwani imekuwa ni jaribio la nne wakiwa wanamatafuta mama mwenye nyumba hiyo ambaye hakufahamika jina lake na kwamba siku ya tukio hakuwepo.

MAJAMBAZI 8 WASHIKILIWA NA POLISI MWANZA.

Kamanda Ahmed Msangi.
NA. ANNASTAZIA MAGINGA, Mwanza

JESHI la polisi Mkoani Mwanza linawashikilia watu nane wanaosadikika kuwa ni majambazi katika matukio mawili tofauti waliofanya uhalifu wa unyang’anyi wa mali pamoja na wizi wa gari.

Akizungumza na waandishi wa habari Kamanda wa polisi Mkoani hapa Ahmed Msangi leo, amesema kuwa kwenye tukio la kwanza wamefanikiwa kukamata watu sita  wakiwa na silaha mbili  za kienyeji zikiwa na risasi 23 ambazo zilikuwa zikifyatuliwa juu na kufanya unyang’anyi.

Tukio hilo limetokea Oktoba 18 saa 7 mchana huko maeneo ya buswelu Wilaya ya Ilemela Mkoani hapa  ambapo walipora fedha 35,000 na mali ambazo hazijajulikana.

“Watu tuliowakamata ni Jeremiah Marigia(Mkumbo)(25) mkazi wa Singida ambapo alitoka kwenye Mkoa huo kwa ajili ya kufanya uhalifu Mwanza na tulipomuhoji alikiri kufanya vitendo hivyo na kuwataja wenzake watano kuwa wanazo silaha na wanazitunzia kwa mganga wa kienyeji na tulipoenda kweli tuliwakuta na kuwakamata lakini kwenye tukio hilo hakuuwawa mtu yeyote”amesema Msangi.

Siku hiyo hiyo  saa 8 mchana Watu wawili Rahim Feka (28) na Ally Kahalale(32) wote wakazi wa jiji la Dar-es-salaam wamekamatwa na jeshi hilo wakiwa na gari la wizi T 778AZB aina ya Land cruiser liloibwa Manispaa ya Ilala Mkoani humo  kwa ajili ya kuliuza jijini hapa.

Kamanda amesema kuwa gari hilo limepatikana Buzuruga baada ya jeshi hilo kufanya upelelezi kufuatia taarifa walizozipokea kutoka Dar-es-salaam kuwa kuna wizi wa gari hilo na huenda limeletwa Mkoani Mwanza.

“Hawa watu bado tunaendelea kuhojiana nao yawezekana wana mtandao unaofanya kazi za kuiba magari kutoka huku Mwanza na kuyauza Dar au kuiba Dar na kuyuza mikoa mingine kwa hiyo wananchi tuwe makini na vitu vya wizi kwa sababu gari haliuzwi kama bakuli mnadani na baada ya mahojiano tutawapeleka Dar ili hatua za kisheria ziweze kuchukuliw dhidi yao”amasema Msangi. 

MAPATO YA MINADA WILAYANI SERENGETI YAONGEZEKA.

Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Serengeti Mhe. Juma Porini Keya(katikati) akitoa risiti ya malipo kwa kutumia kifaa cha kieletroni (POS)
Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Serengeti Mhe. Juma Porini Keya (kushoto) akipokea maelezo toka kwa mkusanyaji wa mapato Charles Ghati katika mnada wa kijiji cha Rung'abure, Katikati ni Kaimu Mtunza Fedha Bw. Terry Hurson.
Wafanya Biashara wakifanya malipo katika mnada wa kijiji cha Rung'abure Kata ya Rungaabure Wilayani Serengeti.

“Halmashauri ya Wilaya ya Serengeti imefanikiwa kuongeza mapato yatokanayo na minada mbali mbali inayofanyika ndani ya Wilaya”

Hayo yamesemwa na Terry Hurson ambae ni Kaimu Mtunza Fedha wa Halmashauri ya Wilaya ya Serengeti alipokuwa anazungumza na Waheshimiwa Madiwani wanaounda Kamati ya Fedha, Uongozi na Mipango waliofanya ziara katika Mnada wa Kijiji cha Rung’abure kilichopo Kata ya Rung’abure. 

Ziara hiyo ya ukaguzi ni mwendelezo wa taratibu zilizowekwa na Serikali kwa kuwahusisha Waheshimiwa Madiwani wanaounda Kamati ya Fedha, Uongozi na Mipango kutembelea miradi kila baada ya miezi mitatu (Robo Mwaka wa Serikali)

Kamati ya Fedha Uongozi na Mipango inayoongozwa na Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Serengeti, Juma Porini Keya pamoja na Katibu wa Kamati hiyo ambaye ni Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Serengeti Juma Hamsini pamoja na wajumbe wa Kamati walijionea jinsi ukusanyaji wa mapato unavyofanyika kwa kutumia vifaa vya kieletroniki (POS) vinavyotumika pia kutoa risiti za malipo. “Mapato ya Minada yameongezeka kutokana na kuzuia mianya ya ukwepaji wa kodi na matumiz ya POS” alisema Terry Hurson. 

Ukusanyaji wa mapato unafanywa na watumishi wa Serikali, hii ni baada ya Serikali ya awamu ya tano ikiongozwa na Rais Dkt. John Pombe Magufuli kuzitaka Halmashauri zote nchini kukusanya mapato na kuacha kutumia wazabuni katika kukusanya mapato kwenye masoko na minada.

GNRC WAHITIMISHA SIKU YA KIMATAIFA YA KUTOKOMEZA UMASKINI KIPEKEE.

Wanafunzi wa shule ya Msingi  Oysterbay wakiwa kwenye picha ya pamoja na Baraka Chedego kutoka GNRC -Tanzania kabla ya kuanza kwa mechi ya mpira wa miguu
Wanafunzi wakiwa katika mdahalo.
Vainess Mbaga  (Education Officer) akitoa elimu kwa watoto.
Washiriki wa Mdahalo wakisalimiana na Mama Joyce Mdachi kutoka GNRC na viongozi wengine wa shule.
Mtanange dimbani.
Maufundi zaidi na vyenga.....
Kipyenga kimelia.
Huduma ya kwanza.
Elimu ya Futboli.
Ushirika na ushirikiano.
Mduariko.
Marafiki.
Skul baraza.
Mfano wa vyeti walivyotunukiwa wanafunzi kutoka na ushiriki mzuri wa siku hii ya kipekee.
Kila tarehe 15 Oktoba, Dunia nzima huadhimisha Siku ya Kimataifa ya Kutokomeza Umasikini, ambapo mwaka huu  kauli mbiu ya  siku hiyo ilikuwa ni
‘’KUTOKA UDHALILISHAJI NA UTENGWAJI MPAKA USHIRIKISHWAJI ‘’.

Mtandao wa Dini mbalimbali kwaajili ya watoto ulimwenguni  uitwao Global Network of Religion for Children (GNRC-Tanzania) wamefanikiwa kuhitimisha siku hii kwa namna ya pekee kabisa ambapo tangu tarehe 15 Oktoba wamekuwa wakiandaa matukio mbalimbali yaliyolenga kuwajengea uwezo watoto haswa wa Shule za msingi kwa kuandaa mashindano tofautitofauti kama Midahalo na Michezo ikiwa na lengo la  kuwajengea watoto uwezo (capacity building)  na kuwapa elimu ambayo itaweza kuwakomboa katika janga la umasikini .