ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

Saturday, September 5, 2015

UZINDUZI WA KAVASHA CLUB NA KITABU CHA JIFUNZE LINGALA MTUNZI TCHIMANGA ASSOSSA


Uzinduzi wa Dar Kavasha Club pamoja na uzinduzi wa kitabu cha kujifunza Kilingala utafanyika leo tarehe 05-Sep-2015 kuanzia saa 12 jioni katika ukumbi wa MRC Mikocheni, ukumbi ulio nyuma ya Shopperz Plaza.

Uzinduzi huo utasindikizwa na burudani  kutoka kwa wana Bana Marquis bendi inayoongozwa na mwanamuziki Tshimanga Kalala Assosa, ambaye pamoja na kuwa ni kati ya wanamuziki waliokuweko katika enzi ya uanzishwaji na ukuaji wa mtindo wa Kavasha, akiwa mwanamuziki wa bendi kama Negro Success, Lipualipua, Orchestra kamale, na Orchestra Fuka fuka.
Uzinduzi huu ulikuwa ufanyike mwezi wa 5 lakini ukaahirishwa kutokana na mvua kubwa iliyonyesha siku ambapo uzinduzi huo ulipangwa kufanyika.

Kiingilio cha onyesho hili ni BURE. Na hakika tukio hili ni la aina yake katika tasnia ya muziki wa dansi

MANSOOR SHANIF HIRANI AIMARISHA KIKOSI CHAKE KUELEKEA


Uzinduzi wa kampeni za Chama cha Mapinduzi CCM jimbo la Kwimba umefanyika leo na hapa mgombea wa nafasi ya Ubunge kupitia chama hicho Mansoor Shanif Hiran akizungumza na Wajumbe, mabalozi, wenyeviti wa mitaa mbalimbali, makatibu pamoja na wagombea nafasi ya udiwani kujiweka sawa.
Mjumbe wa NEC jimbo la Kwimba Mhe. Mahewa Lameck akimwaga darasa kwa wajumbe wa mkutano.
Wajumbe wa mkutano.
Mipango mikakati...Nini kifanyike...Uzinduzi wa kampeni za Chama cha Mapinduzi CCM jimbo la Kwimba umefanyika leo na hapa mgombea wa nafasi ya Ubunge kupitia chama hicho Mansoor Shanif Hiran akizungumza na Wajumbe, mabalozi, wenyeviti wa mitaa mbalimbali, makatibu pamoja na wagombea nafasi ya udiwani kujiweka sawa.
Wajumbe wa mkutano, kusanyikoni na kulia ni Dogo Mansoor.
Mipango mikakati.
Ushindi hapa lazima.
Familia ya mgombea wa kiti cha ubunge jimbola Kwimba Mansoor Shanif Hiran katika muonekano wa kutoa sapoti kuelekea ukumbi wa mkutano.
Wajumbe mkutanoni.
Hapa kazi tu....!!
Umakini.
Ni lazima kujipanga.
PICHA NA ZEPHANIA MANDIA.

MASHEIKH 6 RAIA WA TANZANIA WALIOKUWA WAKISHIKILIWA NCHINI CONGO WAREJEA NCHINI.

Masheikh 6 raia wa Tanzania waliokuwa wakishikiliwa nchini Congo wawasili nchini huku wakieleza kilicho wasibu.

LOWASSA ALIPOTINGA MKOANI KIGOMA.

Mgombea Urais wa Jamhuri ya Muungani wa Tanzania katika mwamvuli wa UKAWA kupitia Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Mh. Edward Lowassa, akitembelea kuelekea kwenye Helkopta anayoitumia kwa ziara za Kampeni, iliyokuwepo kwenye Uwanja wa Ndege wa Mpanda, alipokuwa akielekea Mkoani Kigoma kuendelea na ziara zake ya Kampeni, leo Septemba 4, 2015.
Mgombea Urais wa Jamhuri ya Muungani wa Tanzania katika mwamvuli wa UKAWA kupitia Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Mh. Edward Lowassa, akipokea saluti kutoka kwa Askari Polisi, wakati alipowasili kwa Helkopta, kwenye Uwanja wa Nguruka Kati, Uvinza, Mkoani Kigoma  kulikofanyika Mkutano wa Kampeni za Mgombea huyo, leo Septemba 4, 2015.PICHA ZOTE NA OTHMAN MICHUZI, KIGOMA
Mgombea Urais wa Jamhuri ya Muungani wa Tanzania katika mwamvuli wa UKAWA kupitia Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Mh. Edward Lowassa, akikaribishwa na Mwenyeji wake, Mgombea Ubunge wa Jimbo la Kigoma Kusini katika mwamvuli wa Ukawa kupitia Chama cha NCCR-Mageuzi, David Kafulila, mara baada ya kuwasili kwenye Uwanja wa Nguruka Kati, Uvinza, Mkoani Kigoma, kulikofanyika Mkutano wa Kampeni za Mgombea huyo, leo Septemba 4, 2015.Katikati ni Mwenyekiti wa CHADEMA, Mh. Freeman Mbowe.
Mgombea Urais wa Jamhuri ya Muungani wa Tanzania katika mwamvuli wa UKAWA kupitia Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Mh. Edward Lowassa, akiwasalimia wananchi wa Kigoma Kusini, waliokuwa wamefurika kwenye Uwanja wa Nguruka Kati, Uvinza, Mkoani Kigoma  wakati wa Mkutano wa Kampeni, uliofanyika leo Septemba 4, 2015.
Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Mh. Freeman Mbowe, akiwahutubia wananchi wa Uvinza, leo Septemba 4, 2015.
Mgombea Urais wa Jamhuri ya Muungani wa Tanzania katika mwamvuli wa UKAWA kupitia Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Mh. Edward Lowassa, akiwahutubia wananchi wa Mji wa Uvinza, Jimbo la Kigoma Kusini, leo Septemba 4, 2015.
Mgombea Urais wa Jamhuri ya Muungani wa Tanzania katika mwamvuli wa UKAWA kupitia Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Mh. Edward Lowassa, akimnadi kwa wananchi, Mgombea Ubunge wa Jimbo la Kigoma Kusini katika mwamvuli wa Ukawa kupitia Chama cha NCCR-Mageuzi, David Kafulila, katika Mkutano wa hadhara wa Kampeni, uliofanyika kwenye Uwanja wa Nguruka Kati, leo Septemba 4, 2015.
Mgombea Urais wa Jamhuri ya Muungani wa Tanzania katika mwamvuli wa UKAWA kupitia Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Mh. Edward Lowassa, akiptia ujumbe maalum ulioandaliwa na Wananfunzi wa Shule ya Msingi Nguruka, Mkoani Kigoma, leo Septemba 4, 2015.
Mgombea Ubunge wa Jimbo la Kigoma Kusini katika mwamvuli wa Ukawa kupitia Chama cha NCCR-Mageuzi, David Kafulila, akiwahutubia wananchi wa Jimbo lake, wakati wa Mkutano wa Kampeni za Mgombea Urais wa Jamhuri ya Muungani wa Tanzania katika mwamvuli wa UKAWA kupitia Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Mh. Edward Lowassa, uliofayika kwenye  Uwanja wa Nguruka Kati, Uvinza, Mkoani Kigoma, leo Septemba 4, 2015.
Baadhi ya wananchi wa Mji wa Kigoma Kusini, wakionyesha furaha yako kwa Mgombea Urais wa Jamhuri ya Muungani wa Tanzania katika mwamvuli wa UKAWA kupitia Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Mh. Edward Lowassa,wakati wa Mkutano wa hadhara wa Kampeni, uliofanyika kwenye Uwanja wa Nguruka Kati, Uvinza, Mkoani Kigoma
Baadhi wa wasanii wa wakighani mashairi yao kwa umahiri mkubwa.


Usikivu kwa wananchi wa Uvinza.