ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

Saturday, December 3, 2016

HATIMAYE LEO MACHINGA WAONDOSHWA KATIKATI YA JIJI LA MWANZA

Zoezi la kuwaondoa wafanyabiashara ndogo ndogo kutoka katika maeneo yasiyoruhusiwa katikati ya jiji la Mwanza imefanyika kwa ufanisi kufuatia jeshi  la polisi kwa kushirikiana na mgambo kufanya operesheni  bomobomoa katika eneo la makoroboi na Tanganyika usiku wa kuamkia leo la kuimarisha ulinzi katika maeneo mbalimbali ya jiji.

wakizungumza na vyombo vya habari jijini Mwanza Wakuu wa wilaya za Nyamagana na Ilemela wamesema zoezi la kuwapanga wafanyabiashara ndogo ndogo maarufu kama machinga katika maeneo mapya Nyegezi, Kiloleli na Buzuruga linaendelea.

Hii ni moja ya operesheni zilizofanywa na Mgambo wa Halmashauri ya Jiji la Mwanza na kukamilika kwa ufanisi mkubwa katika kuwaondoa wafanyabiashara ndogo ndogo maarufu kama machinga kutoka katika maeneo yasiyoruhusiwa katikati ya jiji.

Operesheni hii ya kuwaondoa watu wanaofanyabiashara katika maeneo yasiyoruhusiwa ilianza usiku kwa kuwakamata wanawake wanaofanya biashara ya ngono na wazururaji, na baadaye kufanya bomoa bomoa katika eneo la makoroboi na Tanganyika na mtaa wa soko kuu, maeneo ambayo ni shughuli nyingi jijini.

                                     Zephania Mandia wa gsengoblog.

MAJALIWA :TUMIENI BIDHAA ZINAZOZALISHWA NA VIWANDA VYA NDANI

 Mwenyekiti wa Kampuni ya Lodhia Group  Bw. Arun Lodhia akimpokea Waziri Mkuu wa Jamhuri wa Muungano wa Tanzania  Mhe. Majaliwa Kassim Majaliwa ili kuzindua kiwanda cha Lodhia Plastic kinachotengeneza Mabomba ya Maji ,kilichopo Njiro jijini Arusha Leo, 3 Disemba 2016.
Mwenyekiti wa Kampuni ya Lodhia Group Bw. Arun Lodhia akitoa maelezo kwa Waziri Mkuu wa Jamhuri wa Muungano wa Tanzania  Mhe. Majaliwa Kassim Majaliwa wakati alipofika kuzindua kiwanda cha Lodhia Plastic kinachotengeneza Mabomba ya Maji ,kilichopo Njiro jijini Arusha Leo, 3 Disemba 2016.
 Mwenyekiti wa Kampuni ya Lodhia Group  Bw. Arun Lodhia (wa kwanza kushoto waliokaa) akiteta jambo na Waziri Mkuu wa Jamhuri wa Muungano wa Tanzania  Mhe. Majaliwa Kassim Majaliwa akifuatiwa na Mkuu wa Mkoa wa Arusha Mhe. Mrisho Gambo na Naibu waziri wa kilimo ,Mifugo na Uvuvi Mhe. William Ole Nasha wakati walipofika kuzindua kiwanda cha Lodhia Plastic kinachotengeneza Mabomba ya Maji ,kilichopo Njiro jijini Arusha Leo, 3 Disemba 2016.
Waziri Mkuu wa Jamhuri wa Muungano wa Tanzania  Mhe. Majaliwa Kassim Majaliwa akikata utepe tayari kwa uzinduzi wa  kiwanda cha Lodhia Plastic kinachotengeneza Mabomba ya Maji ,kilichopo Njiro jijini Arusha Leo, 3 Disemba 2016.
 Kutoka Kushoto (mwenye suti bluu) ni Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Lodhia Group  Bw. Sailesh Pandit,  Mwenyekiti wa kampuni ya Lodhia Group Bw. Arun Lodhia wakiongozana na  Waziri Mkuu wa Jamhuri wa Muungano wa Tanzania  Mhe. Majaliwa Kassim Majaliwa ndani ya kiwanda cha Lodhia Plastic kinachotengeneza Mabomba ya Maji ,kilichopo Njiro jijini Arusha Leo, 3 Disemba 2016.
Waziri Mkuu wa Jamhuri wa Muungano wa Tanzania  Mhe. Majaliwa Kassim Majaliwa akisaini kitabu cha wageni mara baada ya kuzindua kiwanda cha Lodhia Plastic kinachotengeneza Mabomba ya Maji ,kilichopo Njiro jijini Arusha Leo, 3 Disemba 2016.
 Mwenyekiti wa Kampuni ya Lodhia Group  Bw. Arun Lodhia akimkaribisha Waziri Mkuu wa Jamhuri wa Muungano wa Tanzania  Mhe. Majaliwa Kassim Majaliwa ili kuongea na hadhara iliyopo kwenye kiwanda hicho mara baada ya kuzindua kiwanda kinachotengeneza Mabomba ya Maji ,kilichopo Njiro jijini Arusha Leo, 3 Disemba 2016.
Waziri Mkuu wa Jamhuri wa Muungano wa Tanzania  Mhe. Majaliwa Kassim Majaliwa akiongea machache mara baada ya kuzindua kiwanda cha Lodhia Plastic kinachotengeneza Mabomba ya Maji ,kilichopo Njiro jijini Arusha Leo, 3 Disemba 2016.
 Waziri Mkuu wa Jamhuri wa Muungano wa Tanzania  Mhe. Majaliwa Kassim Majaliwa akizindua jiwe la msingi katika kiwanda cha Lodhia Plastic kinachotengeneza Mabomba ya Maji ,kilichopo Njiro jijini Arusha Leo, 3 Disemba 2016.
Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Lodhia Group  Bw. Sailesh Pandit akiagana na  Waziri Mkuu wa Jamhuri wa Muungano wa Tanzania  Mhe. Majaliwa Kassim Majaliwa mara baada ya kuzindua kiwanda cha Lodhia Plastic kinachotengeneza Mabomba ya Maji ,kilichopo Njiro jijini Arusha Leo, 3 Disemba 2016.
Mwenyekiti wa kampuni ya Lodhia Group Bw. Arun Lodhia akiagana na  Waziri Mkuu wa Jamhuri wa Muungano wa Tanzania  Mhe. Majaliwa Kassim Majaliwa mara baada ya kuzindua kiwanda cha Lodhia Plastic kinachotengeneza Mabomba ya Maji ,kilichopo Njiro jijini Arusha Leo, 3 Disemba 2016.


Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Lodhia Group  Bw. Sailesh Pandit akisoma risala mbele ya Mgeni rasmi ambaye niWaziri Mkuu wa Jamhuri wa Muungano wa Tanzania  Mhe. Majaliwa Kassim Majaliwa ndani ya kiwanda cha Lodhia Plastic kinachotengeneza Mabomba ya Maji ,kilichopo Njiro jijini Arusha Leo, 3 Disemba 2016. Picha zote Gadiola Emanuel

habari na  Woinde Shizza , Arusha.

 Halmashauri za majiji, manispaa na miji wametakiwa kutumia mabomba ya maji yanayozalishwa nchini badala ya kuagiza bidhaa hiyo toka nje ili kuweza kuvinufaisha  viwanda vya ndani.

               

Hayo yamebainishwa na waziri mkuu wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Kassim Majaliwa wakati akizindua kiwanda cha   kutengeneza mabomba ya Plastic ya maji yenye  ukubwa wa aina mbalimbali  (Lodhia Plastics ) kilichopo njiro jijini hapa.

Alisema kuwa haiana haja ya halmashauri  au majiji kuagiza bidhaa mbalimbali nje ya nchi  wakati  nchi yetu inaviwanda vya kutosha vya kutengeneza bidhaa hizo.“Sioni sababu ya wahandisi wa Halmashauri na washauri elekezi halmashauri kushinikiza wakandarasi wa hapa Arusha kwenda kununua mabomba ya maji nje ya mkoa wakati hapa kuna kiwanda kama Lodhia ambacho kinatengeneza hizo bidhaa kwakweli hii labda iwe   ni chuki tu”alisema Majaliwa ambaye ameanza ziara ya siku nane mkoani Arusha.Alisema ni muhimu kwa halmashauri kununua mabomba hayo kwa matumizi ya miradi ya maji na kuunga mkono juhudi zinazofanywa na wawekezaji wa ndani.“Washauri wa miradi mbalimbali acheni chuki …waache wakandarasi wanunue bidhaa bora zilizothibitishwa na Shirika la Viwango la Taifa (TBS) na Shirika la Viwango la Kimataifa (ISO),” alisema.

Aidha alitoa mfano, kwa upande wa Mkoa wa Arusha kuna mpango wa kujenga mradi mkubwa wa maji utakaogharimu dola za Marekani milioni 200, na katika utekelezaji wake ni lazima watoe kipaumbele cha kutumia mabomba yanayozalishwa na kiwanda hicho.

Mradi huo ukikamilika unatarajiwa kumaliza kero ya maji kwa wakazi wa jijini hapa.

Alisisiza haoni umuhimu wa halmashauri na wakandarasi kununua mabomba kutoka nje ya Arusha au nje ya nchi wakati kuna mabomba yanayozalishwa na wawekezaji wazawa na yanakidhi viwango.

“Serikali  yetu itaendelea kuwaenzi na kuwalinda wawekezaji wote wa ndani ambao wamekuwa msaada mkubwa wa kutoa ajira ambayo ni janga kwa taifa na dunia kwa ujumla”alisema Majaliwa.

Awali Mwenyekiti wa Bodi ya Lodhia Group, Arun Lodhia, alisema serikali ichukue nafasi ya kuzungumza na wenye viwanda mara kwa mara ili kujua matatizo yao na kuyatafutia ufumbuzi.

Alisema viwanda chini ya kampuni hiyo, vinazalisha bidhaa nyingi zenye ubora lakini makampuni yanashindwa kununua na kupenda zaidi kununua bidhaa za nje.

Kwa upande wake, Mkurugenzi Mtendaji wa kiwanda hicho, Sailesh Pandit, alisema  kwamba wanashindwa kuuza mabomba ya maji na malighafi nyingine katika miradi mikubwa ya maji iliyopo mkoani Arusha.

Alisema wanashindwa kufanya hivyo licha ya bidhaa zao kuwa na TBS na ISO kutokana na hujuma wanazofanyiwa na baadhi ya wahandisi na washauri elekezi wa miradi.

“Imeshatokea mara kadhaa kwa wakandarasi wanaotekeleza miradi kuzuiwa kununua mabomba ya maji kutoka Lodhia Plastics na badala yake hulazimishwa kununua mabomba kutoka nje ya mkoa hivyo kuwasababishia gharama za ziada,” alisema.

Kuhusu ajira, alisema kiwanda hicho kimetoajiri  Watanzania kati ya 1, 200 hadi 1, 300 lakini pia Watanzania zaidi ya 500 wananufaika kutokana na kushiriki katika utoaji wa huduma mbalimbali kiwandani hapo.

Alisema mtandao wa viwanda vinne vinavyomilikiwa na kampuni ya Lodhia Group wanalipa kodi wastani wa Sh. bilioni 20 kwa mwaka.

Kwa upande wao, baadhi ya makandarasi, Samuel Lugemalila wa Kampuni ya Vest Tanzania Ltd na Kastuli Mandange kutoka Fraju Group Ltd  na Maxmilian Iranghay  wa kampuni Wining Spirit Construction Ltd, walitoa ushuhuda kuhusu namna washauri waelekezi na watumishi wengine wanavyowakataza kununua bidhaa za Lodhia Plastics na kuwataka wanunue zinazotengenezwa nje ya mkoa.

Walisema kitendo hicho kinawashababisha kushindwa  kukamilisha miradi yao kwa wakati na kuwaongezea gharama kubwa.
Aidha waliiomba serikali kuondoa urasimu kwa wahasibu kulipa malipo kwa wakati licha ya miradi kukaguliwa na kupata cheti cha uhakiki wa kazi.

MREMBO ANNA NITWA AFANIKISHA UKARABATI WA CHOO CHA WODI YA KINAMAMA WANAJIFUNGUA WATOTO NJITI

 Mlimbwende anayeshikilia Taji la Urembo la Mkoa wa Dodoma (Miss Dodoma 2016/17), Anna Nitwa (wa pili kulia) akiwa na Mbunge wa Jimbo la Dodoma Mjini ambaye pia ni Naibu Waziri, Ofisi ya Waziri Mkuu, Kazi, Vijana na Ajira, Anthony Mavunde (wa pili kushoto) pamoja na madaktari wakati wakielekea kwenye Wodi ya Wazazi wanaojifungua Watoto kabla ya wakati (Njiti), katika Hospitali ya Mkoa wa Dodoma, Desemba 1, 2016.

Mrembo huyo ambaye aliguswa na hali aliyoikuta hapo awali wakati alipotembelea Wodi ya Wazazi wanaojifungua Watoto kabla ya wakati (Njiti) hasa pale alipoona mazingira ya choo cha kina Mama hao kuwa si ya kuridhisha kwa afya ya mama na Mtoto na ikizingatiwa kuwa watoto hao wanahitaji uangalizi wa hali ya juu, alijitolea kukikarabati Choo hicho na Desemba 1, 2016 alikikabidhi kwa uongozi wa Hospitali hiyo ya Mkoa wa Dodoma.

Akizungumza mbele ya wanahabari pamoja na uongozi wa Hospitali hiyo, Mrembo Anna Nitwa alisema "Siku ya Novemba 4, 2016 nilitembelea Wodi ya Watoto Njiti wakati wa kujiandaa na siku ya maadhimisho ya watoto wazaliwao kabla ya wakati ambayo ilikua Novemba 17, Niliona mazingira ya choo kilichokua kinatumiwa na Wazazi wa Watoto Njiti pamoja na wauguzi wao, hakikua katika hali nzuri. Hivyo niliahidi kushirikiana na washikadau mbalimbali ili kuweza kukarabati.

Aliendelea kusema kuwa "Wazazi wangu pamoja na watu wachache walioguswa waliweza kushirikiana nami kuchangia fedha za kukarabati choo hicho, na kazi ya ukarabati imekamilika na sasa nimekikabidhi.

Kwa Upande wa Mbunge wa Jimbo la Dodoma Mjini ambaye pia ni Naibu Waziri, Ofisi ya Waziri Mkuu, Kazi, Vijana na Ajira, Anthony Mavunde aliyeambatana na Mrembo huyo Hospitalini hapo, alimpongeza kwa kazi nzuri aliyoifanya na kumuahidi kuijenga korido ambayo itaunganisha Wodi hiyo na choo ili kuwasaidia wakina mama hao kuwa katika mazingira ya ulinzi hasa nyakati za usiku, kwani kwasasa choo hicho kipo kwa nje ya wodi hiyo, hivyo korido ikijengwa itawasaidia sana. 

Kwa upange wake Mganga Mkuu wa Hospitali ya Dodoma,Dkt. James Charles alitoa shukrani kwa Mrombo huyo kwa jitihada zake za kufanikisha ukarabati huo, na hasa kwa moyo wake wa kujitolea, na kuwaomba Watanzania wengine kujitolea kufanikisha mahitaji mengine Hospitalini hapo.
Mlimbwende anayeshikilia Taji la Urembo la Mkoa wa Dodoma (Miss Dodoma 2016/17), Anna Nitwa (kushoto) na Mbunge wa Jimbo la Dodoma Mjini ambaye pia ni Naibu Waziri, Ofisi ya Waziri Mkuu, Kazi, Vijana na Ajira, Anthony Mavunde (katikati) wakiwa katika Wodi ya Wazazi wanaojifungua Watoto kabla ya wakati (Njiti), katika Hospitali ya Mkoa wa Dodoma, Desemba 1, 2016.
Mbunge wa Jimbo la Dodoma Mjini ambaye pia ni Naibu Waziri, Ofisi ya Waziri Mkuu, Kazi, Vijana na Ajira, Anthony Mavunde akiangalia namna Choo hicho kilivyokarabatiwa kwa jitihada za Miss Dodoma 2016/17, Anna Nitwa.
Kinavyoonekana kwa ndani.
Mlimbwende anayeshikilia Taji la Urembo la Mkoa wa Dodoma (Miss Dodoma 2016/17), Anna Nitwa akiwa amewabeba watoto Mapacha, wakati alipotembelea Wodi ya Wazazi wanaojifungua Watoto kabla ya wakati (Njiti), katika Hospitali ya Mkoa wa Dodoma, Desemba 1, 2016.

POLISI MWANZA YANASA MAJAMBAZI WANNE, WAWILI WAUAWA.

 Majambazi waliokuwa wakitikisa kwa siku kadhaa jijini mwanza kwa maeneo ya Bukanga na Kishiri usiku wa kuamkia leo yamekamatwa kupitia msako maalum uliofanywa na jeshi la polisi Mwanza likiongozwa na Kamanda Ahmed Msangi .

Katika msako huo majambazi wanne wamenaswa huku wengine wawili wakiuawa.
Jeshi la Polisi, Kanda ya Ziwa linawashikilia watoto 11 wenye umri wa kuanzia miaka sita hadi 14 waliokutwa kwenye nyumba moja wilayani Nyamagana ambako askari waliivamia kwa lengo la kukamata watu waliowahisi kuwa ni majambazi.

Mmoja wa watu watatu waliokutwa kwenye nyumba hiyo, alitoroka baada ya kurusha bomu la mkono, kabla ya polisi kudhibiti waliosalia kwa kushirikiana na wanakijiji.

Tukio hilo ni mwendelezo wa matukio ya watoto kukutwa kwenye mazingira tata yanayodhaniwa kuwa na uhusiano na mafunzo ya ugaidi au uhalifu. Pia limetokea wakati idadi ya watoto wanaotangazwa kupotea ikizidi kukua.


Mwaka jana watoto 18 kutoka mikoa tofauti walikutwa kwenye nyumba moja mkoani Kilimanjaro ambako walikuwa wanafundishwa dini na ushonaji, na wiki moja baadaye watoto kumi na moja walikutwa kwenye nyumba moja, tukio ambalo liliumiza vichwa polisi.

Mwezi uliopita, polisi wa Kanda Maalumu ya Dar es Salaam waliwakamata wanawake wanne na watoto wanne waliokuwa wamefichwa kwenye kambi iliyopo Kilongoni, Vikindu mkoani Pwani wakidaiwa kufundishwa jinsi ya kutumia mambo ya dini na harakati za ugaidi.

Katika matukio mawili ya Mwanza na jingine la mkoani Shinyanga yaliyotokea usiku wa kuamkia jana, polisi wameua watu watatu na kukamata wengine kumi na moja.

Pia jeshi hilo limekamata bunduki mbili aina ya SMG na AK 47zikiwa na magazine saba na bastola moja zote zikiwa na risasi 183 katika matukio hayo.
Friday, December 2, 2016

MBUNGE WA ARUSHA MJINI SASA NI MPAKA MWAKANI

Familia ya Mbunge wa Arusha Mhe.Godbless Lema (mke wake na watoto) wakimuaga baba yao baada ya kukosa dhamana tena leo na kurudishwa mahabusu.

Kesi yake itatajwa tena February 02, mwaka 2017.

Hii ni kusema kuwa msimu huu wa sikukuu Lema hatosherehekea pamoja na familia familia yake. Atakuwa peke yake gerezani, na familia itakua na upweke wa kumkosa baba. What a painful situation.

Baadhi ya wanachama wa chama anachotoka Mbunge huyo (CHADEMA) Wamesikika wakisema kuwa hawaja kata tamaa juu ya hatua hiyo "Safari ya demokrasia si rahisi, Mungu ipe uvumilivu familia hii, na umjalie Lema afya njema gerezani" alisikika mmoja wao.

SHEHENA ZA SAMAKI ZAKAMATWA JIJINI MWANZA.


 Msako unaoendeshwa na maafisa wa uvuvi mkoani Mwanza, wa kuwakamata watu wanaojihusisha na uvuvi haramu ziwa Victoria, umefanikiwa kakamata shehena ya samaki aina ya Sangara tani tano zenye thamani ya Sh. Milioni 26.

Msako huo unakuja baada ya hivi karibuni, Waziri wa Kilimo, Mifungo na Uvuvi, Dk. Charles Tizeba, kuwatupia lawama maofisa wa uvuvi kanda ya ziwa kushindwa kudhibiti vitendo vya uvuvi haramu.

Oparesheni hiyo inayoendeshwa katika ziwa Victoria, imekamata sangara ambao hawapaswi kuvuliwa chini ya sheria ya 22 ya mwaka 2003 inayozuia Sangara wachanga centimita 50 na centimita 85 ambao ni wazazi.

Akizungumza na Gsengo BLOG mara baada ya kukamata samaki hao, Afisa Mfawidhi wa usimamizi na uvuvi kanda ya Mwanza, Lameck Mongo, alisema samaki hao, walikamatwa katika eneo la sabasaba Kata ya Pasiansi mjini hapa.

Mongo alisema kuwa samaki hao, kilo 520 sawa na tani tani, wametaifishwa katika kiwanda kinachomilikiwa na mfanyabishara, Oswald Hakimu, anaefanya biashara ya kuchakata, kuuza na kuhifadhi samaki.
Alisema samaki centimita 50 ni samaki wachanga ambao bado wanatakiwa kukuwa ili waweze kuzaa huku wale wa centimita 85 ni samaki wakubwa wasioruhusiwa kuvuliwa wanapaswa kuendelea kuzaa.

"Tumekamata samaki wachanga kilo 4,809 na wakubwa ni kilo 410, ambao hawapaswi kuvuliwa kwa mjibu wa sheria ya 22 ya mwaka 2003 na hatutakubali kuona watu wakiendelea kuvua samaki wasioruhusiwa, "alisema Mongo.

Mongo alisema kuwa baada ya kuzitaifisha samaki hizo, watazigawa kwa taasisi za umma, ikiwemo gerezani na vituo vya watu wasiojiweza na watoto yatima baada ya kupata kibari kutoka mahakamani.

Hata hivyo, alisema pamoja na kukamata samaki hao, watamchukulia hatua za kisheria mmiliki wa kiwanda hicho, ambae hata hivyo, alikimbia baada ya kuwaona maofisa hao wa uvuvi kiwandani kwake.

NA ZEPHANIA MANDIA WA GSENGOBLOG.