Friday, May 1, 2026
DKT. MWIGULU ASHIRIKI MAADHIMISHO YA SIKU YA WAFANYAKAZI DUNIANI NJOMBE
WAZIRI MKUU, Dkt. Mwigulu Nchemba, leo Mei 1, 2026, ameshiriki Maadhimisho ya Siku ya Wafanyakazi Duniani (Mei Mosi) yaliyofanyika mkoani Njombe.
Mgeni Rasmi katika maadhimisho hayo alikuwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Dkt. Samia Suluhu Hassan.
Akizungumza katika maadhimisho hayo, Waziri Mkuu Dkt. Mwigulu ametoa wito kwa wafanyakazi wote nchini kuwa wavumilivu na kuto kata tamaa katika majukumu yao ya kazi ili kufikia mafanikio ya pamoja.
Kaulimbiu ya maadhimisho hayo ilikuwa: “Kazi zenye Staha ni Nguzo Imara kwa Maendeleo Endelevu katika Utekelezaji wa Dira ya Taifa 2050.”
Thursday, April 30, 2026
Tanzia : MWANDISHI WA HABARI EDITHA KARLO AFARIKI DUNIA
.jpg)
Mwandishi wa habari wa mkoa wa Kigoma, Editha Karlo, amefariki dunia baada ya kuugua kwa muda mfupi.
Taarifa za kifo chake zimethibitishwa na Kaimu Mwenyekiti wa Chama cha Waandishi wa Habari mkoa wa Kigoma, Jacob Ruvilo, aliyesema kuwa marehemu alifariki Jumatano mchana Aprili 28,2026 akiwa nyumbani kwao wilayani Kasulu.
Kwa mujibu wa taarifa hiyo, kabla ya umauti wake marehemu alikuwa akipatiwa matibabu katika Hospitali ya Rufaa ya Muhimbili jijini Dar es Salaam.
Kifo cha Editha Karlo ni pigo kwa familia, ndugu, marafiki na tasnia ya habari mkoani Kigoma na nchini kwa ujumla.
Wednesday, April 29, 2026
NI YANGA DHIDI YA SIMBA KOMBE LA MUUNGANO 2026
Michuano ya Muungano Cup 2026 inafikia tamati leo kwa mchezo wa Fainali kupigwa katika dimba la New Amaan.
Ni Yanga SC dhidi ya Simba SC.
Mechi hii itachezwa kuanzia saa 2:15 usiku na kuruka mbashara AzamSports1HD.
Je, Yanga SC ambae ni bingwa mtetezi atalitetea Kombe ama kuvuliwa Ubingwa na Mnyama?
#MuunganoCup
Monday, April 27, 2026
SIKU YA UHURU WA AFRIKA KUSINI.
Kwa niaba ya Serikali na wananchi wa Jamhuri ya Afrika Kusini, napenda kutoa salamu za dhati kwa Mheshimiwa Rais Samia Suluhu Hassan, Serikali na wananchi wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, raia wa Afrika Kusini wanaoishi Tanzania, makampuni ya Afrika Kusini, pamoja na washirika na marafiki wetu wa Kitanzania tunapoadhimisha Siku ya Uhuru wa Afrika Kusini tarehe 27 Aprili 2026.
Mwaka huu inatimia miaka 32 tangu Waafrika Kusini walipotumia haki yao ya kidemokrasia kupiga kura kwa uhuru kwa mara ya kwanza mwaka 1994, hatua iliyofungua enzi mpya iliyojengwa juu ya utu, usawa, kutokuwepo kwa ubaguzi wa rangi, kutokuwepo kwa ubaguzi wa kijinsia, na utawala wa sheria. Siku ya Uhuru inaendelea kuwa kumbukumbu muhimu ya kujitoa mhanga kwa wale waliopigania ukombozi na haki, na kwa ajili ya Afrika Kusini ya kidemokrasia inayowahusu wote wanaoishi ndani yake.
Mwaka huu pia inatimia miaka 30 tangu Mahakama ya Katiba ilipoidhinisha Katiba tarehe 4 Desemba 1996, mafanikio makubwa yaliyoweka msingi wa dola ya kidemokrasia inayozingatia utu wa binadamu, usawa na uhuru. Katiba inaendelea kuwa sheria kuu ya Jamhuri yetu na nguzo muhimu katika kukuza utawala unaowajibika, kulinda haki za msingi, na kuimarisha taasisi za kidemokrasia.
Tunapoadhimisha tukio hili muhimu hapa Tanzania, tunafanya hivyo kwa kuthamini kwa kina uhusiano wa kihistoria na wa kudumu kati ya mataifa yetu mawili. Tanzania ilichangia kwa kiasi kikubwa katika mapambano ya ukombozi ya Afrika Kusini kwa kuunga mkono harakati za ukombozi na kuonesha mshikamano wakati wa nyakati ngumu. Historia hiyo ya pamoja inaendelea kuunda uhusiano unaojengwa juu ya heshima ya pande zote, Uafrika (Pan-Africanism), na dhamira ya pamoja ya amani, maendeleo na ustawi.
Leo, Afrika Kusini na Tanzania zinafurahia ushirikiano imara katika nyanja za kisiasa, kiuchumi, kiutamaduni, pamoja na mahusiano ya watu kwa watu, unaoonesha maono ya pamoja ya umoja wa Afrika, ushirikiano wa kikanda, na ukuaji jumuishi. Afrika Kusini inaendelea kujitolea kufanya kazi kwa karibu na Tanzania ili kuimarisha zaidi uhusiano wa pande mbili na kuchangia kwa maana katika Ajenda 2063 ya Umoja wa Afrika pamoja na ajenda ya maendeleo ya kimataifa.
Ninatoa shukrani zangu za dhati kwa wenyeji wetu, washirika wetu, na jamii ya Waafrika Kusini nchini Tanzania kwa kuungana nasi katika maadhimisho haya muhimu.
Heri ya Siku ya Uhuru.
Mheshimiwa Noluthando Mayende-Malepe
Balozi wa Jamhuri ya Afrika Kusini hapa nchini Tanzania
UWANJA WA BENJAMIN MKAPA KUKAMILIKA MIEZI SITA IJAYO.

Kupitia ukurasa wake wa Instagram, Msigwa amesema maboresho hayo yanahusisha sehemu ya kuchezea (pitch), ambayo inatarajiwa kufikia viwango vya kisasa ndani ya kipindi cha miezi sita.
Ameeleza kuwa lengo ni kuwa na uwanja wenye viwango vya kimataifa, sambamba na kuboresha maeneo mengine ikiwemo sehemu za wageni maalum (lounges), vyumba vya kubadilishia nguo, ubao wa matokeo pamoja na mwonekano wa jumla wa uwanja.
Aidha, ameomba radhi kwa mashabiki wa soka kwa kutoweza kuutumia uwanja huo katika dabi ya Kariakoo iliyopangwa kufanyika Mei 3, 2026.
Hata hivyo, amesisitiza kuwa baada ya maboresho kukamilika, uwanja huo utakuwa katika hali bora zaidi na utadumu kwa matumizi ya muda mrefu.



NI SIMBA NA YANGA FAINALI YA MUUNGANO 2026
Timu ya Simba SC imefanikiwa kwenda Fainali ya Kombe la Muungano baada ya ushindi wa mabao 3-0 dhidi ya wenyeji, Mlandege FC usiku wa jumapili ya tarehe 26 Uwanja wa New Amaan Complex, Zanzibar.
Mabao ya Simba SC yamefungwa na mshambuliaji mzawa, Suleiman Abdallah Mwalimu ‘Gomez’ dakika ya 61, winga Muivory Coast, Alain Anicet Oura dakika ya 76 na kiungo wa Kimataifa wa Afrika Kusini, Neo Gift Maema dakika ya 89.
Simba SC itakutana na mtani wake, Simba SC katika Fainali ya Kombe la Muungano 2026 Jumatano, Aprili 29 kuanzia Saa 2:15 usiku hapo hapo New Amaan Complex.
Ikumbukwe juzi mabingwa hao, watetezi, Yanga SC walifanikiwa kwenda Fainali ya Kombe la Muungano baada ya ushindi wa mabao 2-1 dhidi ya Azam FC hapo hapo Amaan Complex.
Hii ni maana yake miamba hiyo ya soka nchini italutana mara mbili ndani ya wiki moja, kwani Mei 3 watamenyana katika mechi ya marudiano ya Ligi Kuu ya NBC Tanzania Bara kuanzia Saa 12:00 jioni Uwanja wa Meje Jenerali Isamuhyo, Mbweni, Dar es Salaam.
Sunday, April 26, 2026
YANGA WATINGA FAINALI, MACHO SASA KWA DABI NZITO INAYOFUATA?
'LEO WANAUME WA MWANZA MMEFIKIWA' KARIBU KIKAONI
NA ALBERT G.SENGO/MWANZA
Jumapili hii, yaani LEO - tarehe 26 Aprili 2026, jiji la Mwanza linakuwa kitovu cha mjadala muhimu unaomhusu mwanaume wa kizazi cha sasa. Ndani ya Ukumbi wa Benki Kuu ya Tanzania (BOT – Capri Point), tukio maalum la Mwanza Wanaume Summit 2026 linafanyika, likiwaleta pamoja wanaume kutoka pande mbalimbali za Kanda ya Ziwa na kwingineko. Kuanzia saa 8 mchana hadi saa 12 jioni, washiriki watapata fursa ya kipekee ya kujifunza, kuhamasishana na kujenga mtazamo mpya unaoendana na changamoto na fursa za maisha ya leo kuanzia majukumu ya kifamilia hadi mchango wao katika jamii na taifa. Katika mazungumzo haya yenye uzito, Maxwell Stanslaus Shing’oma, Rais wa Taasisi ya Wanaume Tanzania (Men At Work Global), anafungua pazia kwa kueleza kwa kina dhamira ya kongamano hili na kwa nini ni muhimu kwa maendeleo ya mwanaume wa kizazi hiki.......
.jpeg)
.jpeg)
.jpeg)
.jpeg)
.jpeg)
.jpeg)
.jpg)


