ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

Saturday, January 5, 2013

WACHA PICHA ZIONGEE NA MANENO MACHACHE

Teknolojia ya mtaa huu dhidi ya ndege waharibifu.

Michezo yetu.

Wataalamu wa kesho.

Mkulima safarini.

Supa utelezi...

Shehena.
Barabara za Rock City.
Na mie.

SWALI TOKA KWA MDAU: HIVI TANESCO MKOA WA RUVUMA WALIKOSA NGUZO HADI KUFANYA HIVI ?


Hii ni moja ya nguzo ya umeme ili iliyokatika na kuungiwa mti halisi unaondelea kumea.
 
Tatizo la kutokuwa na umeme wa uhakika litaisha kweli kama umakini wenyewe ndiyo huu? Nahisi uzembe kama huu utakuwepo katika vitengo vingine ndani ya Tanesco.

Friday, January 4, 2013

MWANZA YAMPOTEZA MMOJA KATI YA WANAHABARI WAKE.

Tasnia ya habari jijini Mwanza imempoteza mmoja kati ya wanachama wake ni marehemu Winnifrida H. Kabambo (Hellen) aliyefariki dunia mnamo tarehe 2 mwezi januari 2013,  amezikwa leo kwenye makaburi Lumala yaliyoko wilayani Ilemela jijini Mwanza, marehemu alikuwa mwandishi wa habari wa kituo cha Radio Living Water Fm Mwanza.

Mwili wa marehemu ukiwasili eneo la makaburi ya Lumala.

Mwili wa marehemu Hellen Kabambo ukishushwa kwenye nyumba yake ya milele.

Ni baadhi ya waandishi wa habari Mwanza wakisaini kwenye daftari la rambirambi kutoka kushoto ni Jackline, na Rose Jackob.

Mwenyekiti wa Mwanza Press Club (MPC) Deus Bugahirwa akiweka mchanga kwenye kaburi la marehemu Hellen Kabambo aliyezikwaleo kwenye makaburi Nyasaka yaliyoko wilayani Ilemela Mwanza, marehemu alikuwa mwandishi wa habari wa kituo cha Living Water Fm Mwanza.

Jeneza lenye mwili wa marehemu Hellen Kabambo likiwa kwenye nyumba yake ya milele tayari kwa kufukiwa mavumbini.

Mkurugenzi wa Chuo cha Victoria Institute Of Tourism and Hotel Management Bw. Geleta. (mwenye suti nyeusi katikati)  akishiriki zoezi la kufukiaudongo kwenye kaburi la aliyekuwa mwandishi wa habari wa kituo cha radio Living Water Fm marehemu Hellen Kabambo aliyezikwa leo jioni kwenye makaburi ya Lumala jijini Mwanza.

Mama wa marehemu akiwa ameambatana na watoto wa aliyekuwa mwandishi wa habari wa kituo cha radio Living Water Fm marehemu Hellen Kabambo Hellen Kabambo wakiweka shada la maua kwenye kaburi la marehemu.

Baba wakubwa wakiweka shada la maua kwenye kaburi la marehemu.


Waandishi wa habari wkiwakilisha vyombo mbalimbali vya habari wakiweka shada la maua kwenye kaburi la marehemu Hellen Kabambo wa Living Water Fm, kutoka kushoto ni Jacline (Mwananchi), Rose Jackob na Fabian Fanuel (Living Water Fm & Blogger wa F Plus) 

Ndugu wa marehemu, mama wa marehemu pamoja na watoto wa marehemu walijumuika pamoja kuwasha mishumaa katika tukio la kuhitimisha hatua ya kuupumzisha mwili wa aliyekuwa mwandishi wa habari wa kituo cha radio Living Water Fm marehemu Hellen Kabambo Winnifrida H. Kabambo.

Ndugu jamaa na marafiki wakiwa kwenye hali ya majonzi makaburini kumsindikiza aliyekuwa mwandishi wa habari wa kituo cha radio Living Water Fm marehemu Hellen Kabambo aliyezikwa leo jioni kwenye makaburi ya Lumala. 


Na mwanga wa milele na umwangazie.

Kutoka kulia ni Liberata Mashimba, Amina Mashimba, Pendo Martin na bibi Elizabeth Masabo.

MPC Team.

MPC Team.

WATEJA WA AIRTEL SASA KUTUMA SMS KWA SHILINGI MOJA.

Meneja Masoko wa Airtel Rahma Mwapachu akiongea na waandishi wa habari wakati wa kuzindua huduma ya SMS kichizi ambapo wateja wa Airtel sasa wanaweza kutuma sma kwa gharama ya shilingi 1 kwa sms masaa 24 kwa siku 7 za wiki, katikati ni Meneja bidhaa na masoko Francis Ndikumwami na kushoto ni Afisa Uhusiano wa Airtel Bi Jane Matinde


Meneja bidhaa na masoko Francis Ndikumwami akionyesha kipeperushi cha huduma ya SMS kichizi  wakati wa uzinduzi wa huduma hiyo itakayowawezesha wateja wa Airtel nchini kutuma ujumbe mfupi wa sms kwa shilingi 1 kwa sms masaa 24 kwa siku 7 za wiki, kulia ni Meneja Masoko wa Airtel Rahma Mwapachu  kushoto ni Afisa Uhusiano wa Airtel Bi Jane Matinde

Meneja bidhaa na masoko Francis Ndikumwami akiongea na waandishi wa habari wakati wa kuzindua huduma ya SMS kichizi ambapo wateja wa Airtel sasa wanaweza kutuma ujumber mfupi (sms) kwa gharama ya shilingi 1 kwa sms masaa 24 kwa siku 7 za wiki, katikati ni na kushoto ni Afisa Uhusiano wa Airtel Bi Jane Matinde na kulia ni Meneja Masoko wa Airtel Rahma Mwapachu

Wateja wa Airtel sasa kutuma SMS kwa Shilingi Moja

·         Ujumbe mfupi utatozwa shilingi 1 badala ya shilingi 54 kwa sms
·         Sms kwenda mtandao wowote nchini

3 January 2013, Airtel Tanzania kampuni ya simu inayoongoza kwa mtandao mpana na huduma bora na bei nafuu leo imetangaza bei mpya yenye  punguzo la gharama za kutuma ujumbe mfupi  ili kuwapati wateja wake urahisi na unafuu wa huduma ya ujumbe mfupi nchini.  Airtel imepunguza gharama za  sms kutoka shilingi 54 hadi shilingi 1 kwa kila sms. 

Akiongea wakati wa uzinduzi wa gharama mpya ya sms Meneja bidhaa na masoko Francis Ndikumwami alisema” Leo tunayofuraha kuzindua SmS Kichizi ofa ya peeke itakayowawezesha wateja wa Airtel kutuma ujumbe mfupi (sms) kwa gharama nafuu. hii ni ya kwanza kutoka Airtel ambapo tumewapatia na kuwawezesha wateja wetu nchi nzima kutuma ujumbe mfupi (sms) kwa gharama nafuu ya shilling 1 kwa kila ujumbe mfupi kwenda kwenye mtandao wowote masaa 27 siku 7 za wiki bila kikomo. sasa wateja wa Airtel watatozwa shilling 125 kwa ujumbe wa kwanza wa sms na zingine zitakazofuata zitatozwa gharama ya shilling moja kwa siku”.

“SMS kichizi huduma ya ujumbe mfupi ni mwendelezo wa kutimiza dhamira yetu ya kutoa huduma bora, kuwapa wateja wetu uzoefu wa pekee katika huduma zetu za wateja na kutoza gharama nafuu. Airtel leo ndio mtandao ulioenea zaidi maeneo mengi nchini na kuwafikia watanzania wengi zaidi kupitia huduma zetu za Airtel money na internet yenye kasi zaidi nchini.” aliongeza Ndikumwami

Gharama hizi mpya za ujumbe mfupi zitatozwa kwenda mitandao ya ndani ya nchini tu na ni  kwa wateja wa Airtel wa malipo ya awali nchini.

Akiongea kuhusu muda wa huduma hii Francis Ndikumwami alieleza, Airtel tunawajali wateja wetu hivyo huduma hii ya SMS Kichizi sio promosheni ni huduma ya kudumu.

Airtel bado inaendelea na promosheni yake ya msimu wa sikukuu ya Amka millionea ambapo wateja wengi nchini nzima wameendelea kujishindia pesa taslimu ambapo wateja zaidi ya 300 wameshajishindia jumla ya pesa taslimu zaidi ya shilling million 120 hadi sasa.

AJIRUSHA GHOROFANI BUGANDO NA KUFA.

Jengo la Hospitali ya Rufaa ya Bugando lililopo katika vilima vya Bugando jijini Mwanza kama linavyoonekana hii leo tarehe 04/januari/2013, lina urefu wa ghorofa tisa.
Mkazi mmoja wa mtaa wa Kigongo Ferry katika wilaya ya Misungwi mkoani Mwanza, Bi Tekila Daudi mwenye umri wa miaka 28 amefariki dunia baada ya kujirusha kutoka ghorofa ya nne katika Hospitali ya Rufaa ya Bugando (BMC) jijini hapa.

Kwa mujibu wa Afisa Muuguzi msaidizi wa Hospital hiyo Bi. Adera Buberwa alisema kuwa tukio hilo lilitokea Decemba 30, majira ya saa sita mchana.

Bi Buberwa alisema kuwa marehemu alikuwa amelazwa katika hospitali hiyo tangu disemba 19, mwaka 2012, kwa ajili ya kupatiwa matibabu ya ugonjwa wa uvimbe tumboni pamoja na tatizo la moyo.

"Marehemu alikuwa amelazwa wodi namba 4 ambapo tayari alikuwa ameshapatiwa matibabu ya upasuaji ya uvimbe tumboni" aliongeza Afisa huyo muuguzi.

Bi. Buberwa sanjari na hayo alisema kuwa marehemu alifikishwa katika hospitali hiyo baada ya kupatiwa rufaa kutoka katika hospitali ya mkoa wa Mwanza, Sekou Toure.

Jeshi la Polisi Mkoa wa Mwanza limethibitisha kutokea kwa kifo hicho.

Thursday, January 3, 2013

BARAZA LA MADIWANI MANISPAA YA ILEMELA LAENDELEA KUKUMBWA NA MTAFARUKU KWA MADIWANI WA CHADEMA KULISUSIA, KIKAO CHAENDELEA, MEYA ASISITIZA MSIMAMO WAKE WA KUTOWATAMBUA MADIWANI WA3 ALOWATIMUA.

Meya wa Manispaa ya Ilemela ambaye pia ni diwani wa kata ya Kitangili, Bw. Henry Matata akitoa ufafanuzi ndani ya kikao cha baraza la madiwani kilicho fanyika leo jijini Mwanza na kuhusisha pia na wataalamu wa vitengo mbalimbali na idara zake wa wilaya hiyo .

Na. ALBERT G. SENGO: MWANZA
BARAZA la Madiwani wa Manispaa ya Ilemela limendelea kukumbwa na mtafaruku kwa Madiwani wa Chama cha CHADEMA Wilayani humo kuendelea na msimamo wao wa kutomtambua Meya  Bw. Henry Matata (CHADEMA) ambaye ni Diwani wa Kata ya Kitangiri na kususia kikao cha Baraza hilo kilichofanyika leo katika ukumbi wa ofisi za Mkuu wa Wilaya hiyo eneo la Busweru jijini Mwanza.

Mkurugenzi wa Manispaa hiyo Bw. Zubery Mbihna mara tu alipomaliza kuwasilisha ajenda saba za kikao hicho Diwani wa Nyakato Bw.Josephat Manyerere (CHADEMA) alinyanyuka na kutaka ajenda ya Maswali na Majibu iwe ya kwanza kujadiliwa na Chama Chake  kiwe cha kwanza kuwasilisha maswali yake iliyokuwa imeyaandaa hali iliyoleta mabishano makali na kelele za malumbano hali iliyopelekea  Madiwani wote wa CHADEMA kutoka nje ya ukumbi.

Hata hivyo Meya Bw. Matata kwa kuzingatia taratibu, kanuni na sheria zilizopo za Halmashauri hiyo aliwatuliza wajumbe waliosalia wakiwemo wataalaamu kisha akatangaza kuendelea na ajenda kama zilivyo wasilishwa na Mkurugenzi wa Manispaa hiyo ambaye pia ni Katibu wa Baraza la Madiwani.

Kufuatia mtafaruku huo uliopelekea Madiwani wa CHADEMA kutoka na kususia kwa mara nyingine kikao cha baraza, Meya wa Halmashauri ya Manispaa ya Ilemela ananini cha kusema juu ya hali hiyo na hali hii ya kutokukubalika na madiwani wenzake wa CHADEMA anaichukuliaje… BOFYA PLAY MSIKILIZE


Licha ya kusaini kitabu cha mahudhurio na kususia kikao hicho, madiwani hao wa CHADEMA baadaye walionekana wakiingia kwenye chumba cha mhasibu wa Manispaa ya Ilemela na kuchukuwa posho zao za kuhudhuria kikao hicho cha kujadili masuala ya maendeleo.
Naibu meya wa Manispaa ya Ilemela Bw. Dede Swila (CCM) akichangia hoja kwenye kikao hicho ambacho kilianza na zengwe pamoja na makeke mengi lakini kiliisha kwa salama.

Taswira ya kikao toka juu.

Wataalamu na wafanyakazi wa idara mbalimbali wakifuatilia yanayojiri ndani ya kikao hicho.

Diwani wa kata ya Buswelu Thobias Mpemba akichangia hoja kati ya ajenda zilizo wasilishwa.

Afisa habari wa Ofisi ya Halmashauri ya Wilaya ya Ilemela Bi. Viola (kushoto) akiwa na ameketi meza moja na wataalamu na wafanyakazi wa idara mbalimbali wakifuatilia yanayojiri ndani ya kikao hicho.

Mtaalamu wa moja kati ya vitengo wilaya ya Ilemela akitoa ufafanuzi kwamoja ya hoja zilizowasilishwa. 

Mtaalamu.

Mkuu wa wilaya ya Ilemela.

Meya wa Manispaa ya Ilemela ambaye pia ni diwani wa kata ya Kitangili, Bw. Henry Matata mara baada ya yaliyojadiliwa kufikia tamati katika uwasilishwaji na kutolewa ufafanuzi aliahirisha kikao hicho kilichohudhuriwa na madiwani na kuhusisha wataalamu wa vitengo mbalimbali na idara zake toka wilayani humo.

Jengo la Ofisi za Halmashauri ya Manispaa ya Ilemela.

AIRTEL YAZAWADIA WASHINDI WA MWEZI WA "AMKA MILLIONEA" PROMOSHENI SHILLINGI MILLIONI 30

Afisa Uhusiano wa Airtel bi Jane Matinde akiongea na waandishi wa habari wakati wa kuendesha droo ya mwenzi  wa washindi wa Amka Millionea, Ambapo moja kati ya washindi ni  bw Rickson Richard kutoka Arusha aliyejishindia shillingi million 15. pichani  Katikati ni Meneja Bidhaa Francis Ndikumwami akifatiwa na Mwakilishi wa Bodi ya Bahati nasibu ya taifa bw Sadiki Elimsu


Meneja Bidhaa Francis Ndikumwami na Mwakilishi wa Bodi ya Bahati nasibu ya taifa bw Sadiki Elimsu wakitafuta washindi wa mwenzi wa promosheni ya Amka Millionea ambapo Ambapo moja kati ya washindi ni bw Rickson Richard kutoka Arusha ambaye amejishinid kitita cha shillingi million 15.  wakishuhudia ni waandishi wa habari , kulia ni Afisa Uhusiano wa Airtel bi Jane Matinde

Afisa Uhusiano wa Airtel bi Jane Matinde akiongea na Mshindi wa Amka Millionea bw Rickson Richard (19) kutoka Arusha  mara baada ya kuibuka kuw mshindi wa shillingi million 15 wa promosheni ya Amka millionea, Katikati ni Meneja Bidhaa Francis Ndikumwami akifatiwa na Mwakilishi wa Bodi ya Bahati nasibu ya taifa bw Sadiki Elimsu

TAARIFA ZAIDI.
Airtel yawazawadia washindi wa mwenzi wa “Amka Millionea” promosheni shilingi million 30
·         Washindi wawili wapatikan, Kila mmoja aondoka na kitita cha shilling million 15
2 January 2013  Kampuni ya simu za mkononi ya Airtel inayotoa huduma nafuu na yenye wigo mpana zaidi wa mawasiliano, leo iwatangaza washindi  wa mwenzi wa promosheni “Amka Millionea” wa pesa taslimu  million 30 mara baada ya kuibuka washindi kupitia droo iliyofanyika leo asubuhi ambapo kila moja ameibuka na  kitita cha shilingi milioni 15 pesa taslimu.

Akitangaza washindi hao mara baada ya droo iliyofanyika katika makao makuu ya Airtel Afisa uhusiano wa Airtel Jane Matinde alisema” Airtel inawapa nafasi nyingine watanzania  kushiriki na Kushinda fedha taslimu kwa kupiti promosheni yetu hii kabambe ya “Amka Millionea” iliyozinduliwa mwanzoni mwa mwenzi December, mpaka sasa wateja zaidi ya 300 wamejishindia zawadi za pesa taslimu zenye thamani  zaidi ya shilingi million 120.  Promosheni ya Amka millionea inawazawadia wateja wa Airtel  Kila siku , kila wiki na leo tunashuhudia wateja wawili wa mwisho wa mwenzi wakiibuka kuwa washindi wa shilingi million kumi na tano kila mmoja.

Tunaendelea kuwajali na kuwazawadia wateja wetu nchi nzima kuhakikisha washindi wengi wanapatikana, tunaendelea kuimarisha dhamira yetu ya kutoa huduma bora zenye viwango vya juu na kudhihirisha kauli mbiu yetu ya jisikie huru, aliongeza Matinde.

LOWASSA ALIVYOUKARIBISHA MWAKA WILAYANI KWAKE.

Waziri Mkuu Mstaafu na Mbunge wa Jimbo la Monduli,Mh. Edward Lowassa na Mkewe Mama Regina Lowassa wakiwapungua mikono wageni waalikwa wakati wa hafla ya Chakula cha Mchana aliyoiandaa kwa ajili ya kusherehekea Mwaka Mpya wa 2013,iliyofanyika nyumbani kwake Monduli.

Mbunge wa Jimbo la Kilindi,Mh. Beatrice Shelukindo (wa pili kulia) akiambatana na Mbunge wa Jimbo la Bariadi,Mh. Andrew Chenge wakati wakiwasili kwenye hafla ya Chakula cha Mchana iliyokuwa imeandaliwa na Waziri Mkuu Mstaafu na Mbunge wa Jimbo la Monduli,Mh. Edward Lowassa kwa ajili ya kuukaribisha Mwaka Mpya wa 2013.

Wafanyabiashara maarufu jijini Arusha,Papa King na Mdau Mathias (MNEC) wakiwasili kwenye hafla hiyo.

Waziri Mkuu Mstaafu na Mbunge wa Jimbo la Monduli,Mh. Edward Lowassa akihutubia wageni mbali mbali waliohudhulia hafla ya Chakula cha Mchana aliyoiandaa kwa ajili ya kuukaribisha Mwaka Mpya wa 2013,iliyofanyika nyumbani kwake,Monduli.

waalikwa wakipata Chakula nyumbani kwa Mh. Lowassa.