ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

Saturday, January 6, 2018

MBUNGE MGIMWA:WATENDAJI KAMATENI WAZAZI WOTE AMBAO HAWAWAPELEKI WATOTO WAO SHULE

 Mbunge wa jimbo la Mufindi Kaskazini Mahamuod Mgimwa akizungumza na viongozi wa kata ya Kibengu kuhusu maswala mbalimbali ya kimaendeleo sambamba na kutoa maagizo mbalimbali ambayo yatasaidia kuchochea maendeleo ya kata ya hiyo na jimbo hilo kwa ujumla
  Mbunge wa jimbo la Mufindi Kaskazini Mahamuod Mgimwa na viongozi wengine wakisaini kitabu cha wageni katika ofisi ya kata ya Kibengu
  Mbunge wa jimbo la Mufindi Kaskazini Mahamuod Mgimwa akiangalia moja ya mradi wa ujenzi wa vyoo
Diwani wa kata ya Kibengu Zakayo Kilyenyi akiwa na viongozi wa kata ya hiyo mara baada ya kutoka kwenye kikao na mbunge wa jimbo la Mufindi Kaskazini

Na Fredy Mgunda,Mufindi.

 Mbunge wa jimbo la Mufindi Kaskazini amewataka viongozi wa vijiji na kata kuwachukulia hatua za kisheria wazazi wote ambao hawataki kuwapele shule watoto wao wakifaulu mitihani ya shule ya msingi kwenda shule ya sekondari.

Akizungumza na blog hii mbunge Mahamuod Mgimwa alisema kuwa sasa imefika mwisho kwa watoto wa jimbo la Mufindi Kaskazini kuwa soko la wafanyakazi wa kazi za ndani wakati wanauwezo wa kuwa viongozi hapo baadae.

“Nasema tena haiwezekani kila mfanyakazi ukifika daresalaam utasikia katoka Iringa jimbo la Mufindi Kaskazini sasa sitaki kusika swala hilo na wazazi wanaofanya hivyo nitawachulia hatua za kisheria serikali ya awamu ya tano inataka kuwa na wasomi wengi ili kuasaidia maendeleo ya nchi”alisema Mgimwa

Mgimwa alisema kuwa wazazi wa jimbo la Mufindi la Mufinda watafungwa kwa kuwapeleka watoto wao kufanya kazi za ndani pindi wamalizapo shule ya msingi au sekondari kufanya hivyo kunadumaza maendeleo yao.

“Haiwezekani mwanafunzi amefaulu halafu mzazi anampeleka kufanya kazi za ndani siwezi kukubali hata kidogo maana nimegundugua wazazi wengi hawapendi watoto wao waendelee kusoma badala yake wanataka wakafanye kazi za ndani narudia kusema mtoto akifaulu asipopelekwa shule nitamchulia hatua za kisheria huyo mzazi” alisema Mgimwa

Aidha Mgimwa aliwataka wanafunzi wakike kuacha kufanya ngono wakiwa na umri mdogo ili kupunguza mimba za utotoni na kupoteza dira ya maisha wakiwa watoto wadogo na kufanya hivyo kutawapelekea kufungwa jela kwa kuwa sheria itachukua mkondo wake.

“Acheni kufanya tendo la ndoa mkiwa na umri mdogo ili baadae mjenge maisha yetu  viongozi wengine wa wanawake wanavyofanya kazi serikalini na kwenye mashirika mbalimbali ya nje ya nchi na ndani ya nchi”alisema Mgimwa

Mgimwa aliwapongeza walimu wa shule za msingi za jimbo la Mufindi Kaskazini kwa kuendelea kufanya vizuri kwenye mitihani ya kitaifa na kuendelea kuitangaza vizuri jimbo hilo kupitia elimu.

“Kwa kweli nisiwe mnafiki nichukue fursa hii kuwapongeza walimu kwa kufanya vizuri maana kila mwaka elimu inazidi kukua katika jimbo la Mufindi Kaskazi na kuendelea kuitangaza kitaifa” alisema Mgimwa

kwa upande wake mkuu wa shule ya sekondari ya Ilogombe Pastor Haonga alisema kuwa wazazi wengi wa kata ya Kibengu wamekuwa kikwazo cha maendeleo ya wanafunzi kwa kuwakatisha tamaa juu ya umuhimu wa elimu.

“Hapa katika kata hii ya Kibengu wazazi wengi hawapendi watoto wao kwenda kusoma kwa kuwa watakuwa wanapunguza nguvu kazi zao mashambani ndio maana hawawapatii mahitaji muhimu ya kuwasaidia wanafunzi kusoma kwa uhuru” alisema Haonga

Haonga alimuomba mbunge wa jimbo la Mufindi Kaskazini kutafuta wataalam wa saikolojia kuja kuwapa elimu wazazi wa kata ya Kibengu ili kukuza taaluma kwa wanafunzi wa kata hiyo.
“Ukiangalia hali ya ufaulu wa shule hizi ni mzuri lakini kutokana na wazazi kutokujua umuhimu wa elimu wamekuwa hawawapeleki watoto wao sekondari wakifaulu mitihani ya shule ya msingi hivyo inapelekea upungufu wa wanafunzi katika shule ya sekondari ya Ilogombe” alisema Haonga.

Aidha Mfikwa alisema kuwa wamekuwa wakiitisha mikutano ya mara kwa mara lakini bado tatizo kubwa hivyo jitihada zinahitajika kukomesha tabia hiyo kwa kuwa bila hivyo watoto wa kata hiyo wataendelea kuwa wafanyakazi za ndani tu


Zakayo Kilyenyi ni diwani wa kata ya Kibengu  alikiri kuwa wazazi wengi wa kata hiyo hawana elimu juu ya umuhimu wa kujua dhamani ya elimu katika maendeleo ya familia zao na taifa kwa ujumla.

“Kweli kabisa wazazi wa kata ya Kibengu wamekuwa wakiwaambia watoto wasifanye mitihani vizuri ili wasifaulu kwa kuwa wakifaulu watakuwa na gharama kubwa ya kuwasomesha hivyo wakifeli wataenda kuwafanya kazi za ndani na ndio furaha kwa wazazi wa kata ya Kibengu” alisema Kilyenyi

Kilyenyi alisema kuwa uongozi wa kata ya Kibengu utaendelea kutoa elimu kwa wazazi hao ili kurudisha morali ya kuendelea kuwapa mahitaji muhimu yanayohitajika shuleni kwa kwa lengo la kuboresha maisha ya watoto hao.

“Zana potofu zimekuwa kikwazo kikubwa sana katika maendeleo ya wananchi wa kata ya Kibengu hivyo tukiondoa zana hiyo elimu itakuwa kwa wanafunzi wa kijiji hichi” alisema Kilyenyi

Nao watendaji wa vijiji vitano vya kata ya Kibengu ambao ni Dominicus Nyaulingo,Saifod Mwengwa,Haruna Kalenga, Richard Mandili na Demetus Kanyika walisema kuwa wamepokea agizo la mbunge na watalifanyia kazi kwa ukamilifu kwa kufuata sheria ili kuhakikisha watoto wa kata hiyo wanapata elimu kama inavyotakiwa.

Na kata ya Kibengu inajumuisha vijiji vitano ambavyo ni kijiji cha Kibengu,kijiji cha Igereke,kijiji cha Ilogombe,kijiji cha Usokami na kijiji cha Kipanga

KINGUNGE ASEMA YEYE NI CCM NA CHAMA HAKIWEZI KUWA KINYUME CHAKE.


Mzee Kingunge anatibiwa majeraha baada ya kushambuliwa na mbwa. Akiwa katika kitanda cha hospitali amemwambia  Rais Magufuli  kuwa CCM ni chama chake na amekiunda yeye.

“CCM ni chama changu nimetoka tu, tumeachana lakini nimefanya kazi zote, nimekiunda mimi, hakiwezi kuwa kinyume changu,”– Mzee Kingunge 

amesema hayo alipotembelewa na kujuliwa hali na Rais magufuli katika hospitali ya taifa ya muhimbili.

TETESI ZA WACHEZAJI WANAOWINDWA NA VILABU VYA SOKA ULAYA.

Philippe Countinho
Miamba ya soka ya Hispania Barcelona watalazimika kutoa kaisi cha pauni milioni 145, ili kuweza kupata saini ya kiungo Philippe Coutinho kutoka Liverpool.(Daily Mail)
Wakati huo huo Barca wanakaribia kukamilisha usajili wa beki wa kati Yerry Mina kutoka Palmeirasya nchini Brazil.
Riyad Mahrez kutoka Leicester City iwapo Philippe Countinho.
Majogoo wa Anfield Liverpool huenda wakamsajili winga Riyad Mahrez kutoka Leicester City iwapo Philippe Countinho ataenda Barcelon.. (L'Equipe, in French)
Wapinzania wa jiji la Milan, Inter Milan na Ac Milan wote kwa pamoja wanavutiwa na kumsajili kiungo wa Tottenham Mousa Dembele, mwenye miaka 30.(Sky Sports)
Meneja wa Chelsea Antonio Conte anamatumini klabu yake itafanya usajili mwingine baada ya kumsajili Ross Barkley kutoka Everton.(Independent)
Alexis Sanchez.
Manchester City wanataka kumsajili mshambuliaji wa Arsenal Alexis Sanchez kwa dau la pauni milioni 35 katika dirisha dogo la mwezi huu wa Januari.
Newcastle United inavutiwa na kumsajili winga wa Kibrazil Kennedy kutoka Chelsea pia wakihitaji kumsajili Danny Ings anayekipiga na Liverpool na pia kocha wa klabu hiyo Rafa Benitez akihitaji kumpa ofa golikipa wa Man City Joe Hart anayecheza kwa mkopo West Ham. (Telegraph)
Southampton wametenga dau la kiasi cha pauni milioni 17.5 ili kumsajili mshambuliaji wa Monaco Guido Carrilo raia wa Argentina mwenye miaka 26.(Sun)
Tottenham wako tayari kusikiliza ofa ya pauni milioni 30 kuuza kiungo Moussa Sissoko ambae amekaa klabuni hapo kwa miezi kumi na nane baada ya kusajiliwa akitokea Newcastle kwa dau la pauni milioni 30.(Daily Mirror)
Radja Nainggolan,
Kiungo wa Ubelgiji ambaye anafukuziwa na Manchester United sambamba na Chelsea Radja Nainggolan, ameonyesha nia ya kucheza kwenye ligi kuu ya China kunako klabu ya Guangzhou Evergrande. (Gazzetta dello Sport - in Italian)
Meneja wa Arsenal Arsene Wenger ametaja uwezekano wa kumsaini mshambuliaji Pierre-Emerick Aubameyang, 28, kutoka Borussia Dortmund. (Independent)

MKANDARASI WA REA MBEYA NA SONGWE KUCHUKULIWA HATUA

Naibu Waziri wa Nishati, Subira Mgalu akizungumza na wananchi wa Kijiji cha Utengule Usongwe, Mbeya Vijijini (hawapo pichani) alipokuwa kwenye ziara ya kukagua utekelezaji wa Miradi ya Umeme Vijijini Mkoani Mbeya.

Baadhi ya wananchi wa Kijiji cha Utengule Usongwe, Mbeya Vijijini wakimsikiliza Naibu Waziri wa Nishati, Subira Mgalu (hayupo pichani) alipokuwa akizungumza kwenye ziara yake ya kukagua utekelezaji wa Miradi ya Umeme Vijijini Mkoani Mbeya.

Naibu Waziri wa Nishati, Subira Mgalu (kushoto) akimsikiliza Mbunge wa Mbeya Vijijini, Oran Njeza (kulia aliyesimama) wakati wa ziara yake ya kukagua utekelezaji wa Miradi ya Umeme Vijijini Mkoani Mbeya.

Naibu Waziri wa Nishati, Subira Mgalu akizungumza na wananchi wa Kijiji cha Utengule Usongwe, Mbeya Vijijini (hawapo pichani) alipokuwa kwenye ziara ya kukagua utekelezaji wa Miradi ya Umeme Vijijini Mkoani Mbeya.

Mkuu wa Wilaya ya Mbeya, Paul Mtinika (aliyesimama) akizungumza wakati wa ziara ya Naibu Waziri wa Nishati, Subira Mgalu (wa tatu kushoto waliokaa) ya kukagua utekelezaji wa Miradi ya Umeme Vijijini Mkoani Mbeya.

Naibu Waziri wa Nishati, Subira Mgalu (katikati) akiagana na Mbunge wa Mbeya Vijijini, Oran Njeza (kulia) mara baada ya kuzungumza na wananchi wa Kijiji cha Utengule Usongwe, Mbeya Vijijini wakati wa ziara yake ya kukagua utekelezaji wa Miradi ya Umeme Vijijini Mkoani Mbeya. Kushoto ni Meneja wa TANESCO Mkoa wa Mbeya, Mhandisi Benedict Bahati.

MKANDARASI WA REA KUCHUKULIWA HATUA
Shirika la Umeme Tanzania limeagizwa kumchukulia hatua Mkandarasi ambaye ni kampuni ya wazawa ya JV State Grid Electrical & Technical Works Ltd aliyekuwa akitekeleza Mradi wa Umeme Vijijini Awamu ya Pili (REA II) Mikoa ya Mbeya na Songwe kwa kushindwa kukamilisha katika baadhi ya maeneo kwa mujibu wa makubaliano.

Naibu Waziri wa Nishati, Subira Mgalu ametoa agizo hilo Januari 5, 2018 kwenye mkutano na wananchi wa Kijiji cha Utengule Usongwe, Mbeya Vijijini alipokuwa kwenye ziara ya kukagua utekelezaji wa miradi ya Umeme Vijijini.

Mgalu alitoa agizo hilo kufuatia taarifa ya Meneja wa TANESCO Mkoa wa Mbeya, Mhandisi Benedict Bahati ambaye alimueleza kuhusu kampuni hiyo iliyokuwa ikitekeleza Miradi katika Wilaya za Mbarali, Rungwe, Kyela na Ileje kushindwa kukamilisha miradi yake kama ilivyopaswa kulingana na mkataba. 

Alisema Serikali haitowafumbia macho Wakandarasi walioshindwa kukamilisha utekelezaji wa Miradi waliyokabidhiwa kwa mujibu wa makubaliano na aliliagiza Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO) na Wakala wa Nishati Vijijini (REA) kuhakikisha Mkandarasi huyo anapatikana na hatua za kisheria zinachukuliwa dhidi yake kwa mujibu wa makubaliano ya awali.

“Serikali haijaribiwi, tutachukua hatua kwa Wakandarasi wote walioshindwa kutekeleza Miradi waliyokabidhiwa kwa mujibu wa Sheria; TANESCO na REA, hakikisheni Mkandarasi huyu anapatikana na hatua stahiki za kisheria zinachukuliwa dhidi yake,” alisema Mgalu.

Mgalu aliagiza Mkandarasi huyo apatikane ndani ya Siku Saba ili aeleze sababu za kushindwa kutekeleza mradi huo kwa kiwango kilichokubaliwa na kwa muda wa makubaliano. “Nataka ndani ya Siku Saba tukutane nae aeleze kwanini hajakamilisha mradi kwa mujibu wa mkataba wake,” alisema.

Aliongeza kuwa Serikali imedhamiria kuwainua Wakandarasi wazawa hata hivyo katika utekelezaji wa miradi hiyo ya REA, imedhihirika kwamba walio wengi wameshindwa kutekeleza miradi waliyokabidhiwa kwa mujibu wa makubaliano.

Aidha, Naibu Waziri Mgalu alionya Wakandarasi waliopewa jukumu la kutekeleza Miradi ya Umeme Vijijini Awamu ya Tatu (REA III) kuhakikisha wanatekeleza kwa mujibu wa mkataba na kwamba Serikali haitomvumilia Mkandarasi atakayekwenda kinyume.

“Wakandarasi mnaotekeleza mradi wa REA III; anayeona hawezi kazi atupishe; hatutomvumilia Mkandarasi anayeharibu kazi,” alionya Naibu Waziri Mgalu.

Alisema dhamira ya Serikali ni kuhakikisha Miradi ya Umeme Vijijini inakamilika kwa kiwango kinachokubalika na kwa wakati kama inavyoelekezwa kwenye mikataba waliyoingia na Serikali.

Naibu Waziri Mgalu yupo Mkoani Mbeya kwa ziara ya kukagua na kujiridhisha utekelezaji wa Miradi ya Umeme Vijijini hususan ya REA pamoja na kuzungumza na Wananchi na Wakandarasi kuhusiana na utekelezaji wake.

Friday, January 5, 2018

KWA MARA YA KWANZA TUNDU LISSU AFUNGUKA HAYA MBELE YA WANAHABARI NCHINI KENYA.


Mbunge wa Singida Mashariki, Tundu Lissu amesema kilichotokea kwake kwa maoni yake ilikuwa ni mauaji ya kisiasa moja kwa moja.

Amesema hayo hivi sasa Ijumaa akiwa anatoka hospitali ya Nairobi nchini Kenya.

“Mimi siyo mfanyabiashara awe amemrusha mtu na huwa hapigani baa,” amesema Lissu.

Amesema kuwa risasi 16 zilimpiga mwili wake huku risasi nane zikitolewa Dodoma na risasi saba kutolewa jijini Nairobi huku akibakiwa na moja mwilini mwake.

Ameeleza kuwa sehemu alipopigiwa risasi ni nyumbani kwake alipopangiwa na Bunge kwa kuwa yeye ni Mnadhimu Mkuu wa Kambi ya Upinzani Bungeni hivyo eneo ambalo anakaa ni sehemu palipo salama lakini alimiminiwa risasi 16 na waliofanya hivyo hawajulikani walipo.

Amesema kwa watu waliohesabu risasi zilizopiga gari yale ziko 38 lakini 16 ndizo zilizompata mwilini.

TRA YAENDESHA MNADA MKUBWA WA MAGARI BANDARINI DAR ES SALAAM.Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) imeanza zoezi la kupiga mnada magari yaliyoingizwa kinyamela nchini bila kulipiwa kodi.

Hivi karibuni TRA waliangaza muda wowote kuanzia januari itaanza kupiga mnada magari zaidi ya 300.

Akizungumza Kwaniaba ya TRA,  Scholastika Kavela ambye ni Mkurugenzi Mtendaji wa Wakala wa TRA wa ukusanyaji madeni ya wakwepa kodi na wadaiwa sugu kampuni ya Yono, imekamata Magari hayo na kwamba kwa mujibu wa sheria katika kipindi cha siku 14 wadaiwa wakishindwa kulipa yatapigwa mnada.

Zoezi ambalo tayari limeanza.

NI MOHAMED SALAH TUZO YA MCHEZAJI BORA WA AFRIKA 2017


Mohamed Salah amempiku mchezaji mwenzake wa Liverpool, Sadio Mane na mshambuliaji wa Borussia Dortmund, Pierre-Emerick Aubameyang kutwaa Tuzo ya Mchezaji wa Afrika wa Mwaka 2017.

Mchezaji huyo wa kimataifa wa Misri aliibuka mshindi katika kinyang’anyiro hicho dhidi ya wachezaji wenzake katika mkutano wa Tuzo za Shirikisho la Mpira wa Miguu Afrika mjini Accra.

Salah, ambaye ataikosa mechi ya Kombe la FA raundi ya tatu dhidi ya Everton, Ijumaa usiku, amefurahia mwaka wa mafanikio kwa klabu na kwa taifa lake pia.

Baada ya kufunga mara 10 akiwa Roma kati ya Januari na Mei, mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 25 aijiunga na Liverpool kwa uhamisho wa rekodi kwa klabu hiyo na kwa haraka ameshafanikiwa kuweka kimiani magoli 24 katika michuano yote.

Akiongea kuelekea hafla hiyo, Salah aliwaambia waandishi: “Nadhani tuna timu bora ya taifa na tumefanya vizuri kwenye Kombe la Afrika na kufuzu Kombe la Dunia.”

Salah pia alizifumania nyavu mara mbili katika ushindi wa Misri wa 2-1 dhidi ya Congo kufuzu Kombe la Dunia Oktoba kuhakikisha timu yake ya taifa inapata tiketi ya kushiriki Kombe la Dunia kwa mara ya kwanza baada ya miaka 28.

HUYU NDIYE DJ Scratch AKIONESHA MA-UFUNDI YAKE NA KUZUNGUMZIA MAISHA YA SANAA YAKE.DJ maarufu sana nchini Marekani ambaye kwa sasa ana kula mialiko yenye mkwanja mikubwa balaa, amekuwa kivutio cha wengi kuingia kwenye tasnia hiyo.

Alianzia wapi na vipi na ni nani aliye mvutia akatumbuakia huku?
Amefunguka. 

MPINA ATOZA FAINI MILIONI 180 VIWANDA VYA KUCHAKATA MINOFU YA SAMAKI, WENGINE WASIMAMISHWA.WAZIRI WA MIFUGO NA UVUVI, MHE LUHAGA MPINA AMEWAAMURU WAMILIKI WA VIWANDA VITANO VYA KUCHAKATA MINOFU YA SAMAKI VILIVYOKO JIJINI MWANZA KULIPA FAINI YA SHILINGI MILIONI 180 NDANI YA SAA 24 BAADA YA KUBAINIKA KUCHAKATA SAMAKI WASIORUHUSIWA

AKIWA KWENYE ZIARA MKOANI MWANZA WAZIRI MPINA AMESEMA VIWANDA HIVYO VIMEKIUKA SHERIA YA UVUVI NAMBA 22 YA MWAKA 2003 NA KANUNI ZAKE ZA MWAKA 2009  SAMBAMBA NA SHERIA YA USIMAMIZI WA MAZINGIRA NAMBA 20 YA MWAKA 2004.

WAZIRI MPINA ATOZA FAINI YA MILIONI 180 VIWANDA VYA KUCHAKATA MINOFU YA SAMAKI, AWASIMAMISHA KAZI VIGOGO WATATU KITENGO CHA UDHIBITI WA USALAMA NA UBORA WA MAZAO YA UVUVI KITENGO CHA MWANZA

Meneja uchakataji wa Kiwanda cha kuchakata samaki Victoria cha jijini Mwanza, Endwin Okwong’o (aliyeshika kofia) akimuelezea Waziri wa Mifugo na Uvuvi, Mhe. Luhaga Mpina (mwenye miwani), namna ambavyo wanapokea samaki kutoka kwa mawakala na kuwachambua kabla ya hatua ya kuchakata kiwandani hapo kulia ni Katibu Mkuu wa Wizara ya Uvuvi, Dkt.Yohana Budeba
 Waziri wa Mifugo na Uvuvi, Mhe. Luhaga Mpina(mwenye kofia), akimpima urefu samaki aina ya Sangara kwenye rula maalum ili kubaini kama ana urefu unaotakiwa kisheria kwenye kiwanda cha Nile Perch Limited jijini Mwanza, kushoto Dkt. Yohana Budeba Katibu Mkuu Uvuvi na kulia ni Bwana Gabriel Mageni Afisa Mvuvi Mkuu. Samaki chini ya sentimita 50 na mwenye zaidi ya sentimita 85 hawaruhusiwi kisheria
kuvuliwa.
 
 Waziri wa Mifugo na Uvuvi, Mhe. Luhaga Mpina akimbeba samaki aina ya sangara aliyevuliwa kinyume na taratibu alipokuwa katika ukaguzi wa mazao ya uvuvi katika Kiwanda cha Nature Fisheries Limited Jijini Mwanza, kushoto ni Katibu Mkuu wa Wizara hiyo Dkt Yohana Budeba na kulia ni Afisa Uvuvi Mkuu Bw. Boniface
Shatila.
Samaki mzazi aina ya Sangara aliyevuliwa kinyume na taratibu(alikuwa na urefu wa sentimita 120), samaki ambaye akiachwa ziwani kwa muda  wa miezi mitatu ana uwezo wa kuzaa samaki milioni tatu, na kuongeza idadi kubwa ya jamii hiyo ya samaki katika ziwa Victoria.
WAZIRI wa Mifugo na Uvuvi, Luhaga Mpina amewaamuru wamiliki wa viwanda vitano vya kuchakata minofu ya samaki vilivyoko jijini Mwanza kulipa faini ya shilingi milioni 180 ndani ya saa 24 baada ya kubainika kupokea na kuchakata samaki asioruhusiwa kwa kukiuka Sheria ya Uvuvi namba 22 ya mwaka 2003 na kanuni zake za mwaka 2009  sambamba na Sheria ya usimamizi wa Mazingira namba 20 ya mwaka 2004

Pia Waziri Mpina amechukizwa na kitendo cha viwanda hivyo kufadhili uvuvi haramu na kueleza kuwa ni bora kutokuwa na kiwanda hata kimoja cha samaki kuliko kuendelea kuwa na viwanda vinavyofadhili uvuvi haramu na kutishia kuvifunga viwanda vyote sambamba na kutaifisha samaki, magari na boti zinazobeba samaki wasioruhusiwa.

Waziri Mpina amesema hayo leo kwa nyakati tofauti wakati alipofanya ziara kutembelea viwanda vinavyochakata samaki jijini Mwanza ambapo pia amemuagiza Katibu Mkuu Wizara ya Mifugo na Uvuvi, Dk.  Yohana Budeba kuwasimamisha kazi maofisa watatu wa Kitengo cha Udhibiti wa Usalama na Ubora wa Mazao ya Uvuvi Kituo cha Mwanza kutoka Wizara ya Mifugo na Uvuvi kwa kushindwa kutekeleza majukumu yao kwa mujibu wa sheria na kulisababishia Taifa hasara kubwa.

Maofisa hao ambao Waziri Mpina ameagiza wasimamishwe kazi na kuchukuliwa hatua kali za kinidhamu ni pamoja na Philemon Mugabo,Dorina Mlenge na John Bosco Rubajuna

Waziri Mpina ametaja viwanda vilivyokutwa vikichakata samaki wasioruhusiwawakiwemo samaki wazazi na samaki wachanga  na idadi ya kilo zilizokamatwa kwenye mabano kuwa ni pamoja na Nile Perch Fish (920), Victoria Fish (131), Nature Fish (150), Omega Fish (580), Tanzania Fish Processing (842) huku magari 41, boti 15, Nyavu haramu 294 wakiwa na samaki wachanga na wazazi ambapo sheria inakataza kuvuliwa samaki chini sentimita  50 na juu ya sentimita 85 .

Majina ya viwanda hivyo na faini zao walizotozwa Nile Perch sh milioni 25, Tanzania Fish Processing sh. milioni 50, Victoria Perch Milioni 30, Nature Fish milioni 25, Omega Fish Ltd milioni 50 ambapo amesisitiza kuwa adhabu hiyo ni ya kwanza na ya mwisho na kwamba ikithibika tena wenye viwanda waendelea kufadhili uvuvi haramu hatua za kuvifunga viwanda na kutaifisha mali ikiwemo mitumbwi, boti na magari yatakayokuwa yanabeba samaki hao itafuata.

Waziri Mpina amesema ukanda wa Ziwa Victoria ulikuwa na Viwanda 13 vya kuchakata samaki vilivyokuwa na uwezo wa kuchakata tani 1,065 kwa siku lakini kutokana na kushamiri kwa uvuvi usiongatia sheria kumesababisha viwanda 5 kufa kutokana na kukosekana malighafi na kwamba viwanda 8 vilivyobaki sasa vinachakata tani 171 tu kwa siku huku ajira zikiwa zimeporomoka kutoka ajira 4, 088 na kufikia 2,179 tu.

Mpina amesema tayari Rais Dk John Magufuli ameshatoa maagizo kwa wavuvi kuachana na uvuvi haramu sambamba na wenye viwanda kutofadhili uvuvi huo huku pia Makamu wa Rais, Samia Suluhu Hassan naye akisisitiza jambo hilo na Wizara ya Mifugo na Uvuvi ikikemea vikali huku Sheria za nchi nazo zikikataza  jambo hilo lakini wenye viwanda kwa makusudi wameamua kudharau maagizo ya viongozi wakuu wa nchi jambo ambalo Wizara ya Mifugo na Uvuvi chini ya uongozi wake Waziri Mpina haliwezi kukubalika kamwe.

Katibu Mkuu Wizara ya Mifugo na Uvuvi (Uvuvi) Dk. Yohana Budeba amesema kama watumishi wa wizara yake wangesimamia majukumu yao kikamilifu mambo hayo aliyobaini Waziri Mpina yasingejitokeza huku akikiri kupokea maagizo yake yote na atayasimamia kwa haraka kuona anatekelezwa.

Afisa Mazingira kutoka Baraza la Taifa la Hifadhi na Usimamizi wa Mazingira(NEMC), Mhandisi Boniphace Guni amesema wenye viwanda hivyo wamekutwa na makosa ya kupatikana na samaki waliochini wa ukubwa, kukutwa na samaki wachanga kinyume cha Sheria ya Usimamizi Mazingira namba 20 ya mwaka 2004 pamoja na Sheria ya Uvuvi namba 22 ya mwaka 2003 ambapo wamekiuka kifungu namba 58(I)(a)  hivyo wamestahili adhabu hiyo ya kulipa faini ya milioni 180 ndani ya saa 24 

Thursday, January 4, 2018

BAADA YA BENKI KUU KUZIFUNGA BAADHI YA BENKI NCHINI WANANCHI WENYE FEDHA ZAO WALIOKUWA WAKIHITAJI KULIPA ADA ZA WATOTO WAO WAHAHA

NJOMBE
Baadhi ya wananchi na wateja wa benk ya wananchi Njombe NJOCOBA wameanza kukutana na ugumu wanapohitaji kuzipata huduma za kibenk mara baada ya benk hiyo kutangazwa kufungwa na benk kuu ya Taifa.

Na.amiri kilagalila
Wakizungumza hii leo mara baada ya kufika katika ofisi za benk hiyo ili kupata huduma na kukuta imefungwa,wamesema kuwa hali kwa sasa itakuwa ngumu kwao kutokana na maandalizi ya watoto kwenda shule huku fedha yao ikiwa imehifadhiwa katika benk hiyo.
Insert…………………………….wananchi
Mara baada ya kuzungumza na wateja nje ya benki hiyo nimehitaji kupata ufafanuzi kwa wahusika juu ya swala hilo ambalo limeanza kuonekana ni changamoto kwa baadhi ya wateja ambapo nimekutana na askari wa jeshi la polisi pamoja na mmoja wa watumishi katika benki hiyo na kusema kuwa kwa sasa swala hilo lipo mikononi mwa benki ya Taifa.
Insert…………………………………….polisi na mtumishi
Aidha mwenyekiti wa halmashauri ya mji wa Njombe ERDWIN MWANZINGA ambapo ndipo inapatikana benk alikuwa karibu na mazingira ya benki hiyo hii leo na kusema kuwa huenda benk kuu imefikia uamuzi wa kuifunga benk ya NJOCOBA kutokana na kushindwa kutoa huduma na kuwaomba wananchi kuwa watulivu kutokana na fedha walizozihifadhi.
Insert…………………..mwanzinga
Hata hivyo kwa kipindi kifupi kilichopita Benki ya Wananchi Njocoba imekuwa ikilalamikiwa kwa kushindwa kutoa huduma za kifedha kwa wakati hali iliyowalazimu wateja kuwa na shaka kufilisika kwake mapaka hii leo kuwa miongoni mwa benk zilizofungiwa, aidha benki nyingine zilizofungiwa na kufutiwa leseni zao na benki ya taifa hii leo ni pamoja na COVEANAT Bank, Efata Bank Limited, Kagera Farmers Cooperative Bank Limited na Meru Community Bank Limited.

BOT YAZIFUTIA LESENI BENKI 5


 Benki Kuu ya Tanzania(BoT) imezifutia  leseni ya kufanya biashara benki tano na kuziweka chini ya ufilisi.

Taarifa iliyotolewa leo Alhamisi na BoT imezitaja benki hizo kuwa ni Covenant Bank For Women (Tanzania) Limited, Efatha Bank Limited, Njombe Community Bank Limited, Kagera Farmers' Cooperative Bank Limited, na

Meru Community Bank Limited.

BoT imeeleza kuwa imefanya hivyo kwa mamlaka iliyopewa chini ya kifungu cha 56(1)(g), 56(2) (a), (b) na (d), 58(2)(i), 11(3)(c) na (j), 61(1) na 41(a) cha Sheria ya Mabenki na Taasisi za Fedha ya mwaka 2006, Benki Kuu ya Tanzania imeamua kuzifunga; kusitisha shughuli zake zote za kibenki; kufuta leseni zake za biashara ya kibenki; na kuziweka chini ya ufilisi.

“Kwa mamlaka iliyopewa chini ya kifungu Na. 41(a) cha Sheria ya Mabenki na Taasisi za Fedha ya mwaka 2006; Benki Kuu ya Tanzania imeiteua Bodi ya Bima ya Amana (The DEPOSIT INSURANCE BOARD) kuwa mfiiisi kuanzia tarehe 04 Januari 2018,” imeeleza taarifa hiyo.”

“Uamuzi huu umechukuliwa baada ya Benki Kuu ya Tanzania kujiridhisha kuwa benki hizi zina upungufu mkubwa wa mtaji kinyume na matakwa ya Sheria ya Mabenki na Taasisi za Fedha ya mwaka 2006 na kanuni zake. Upungufu huo wa mtaji unahatarisha usalama wa sekta ya fedha na kwamba kuendelea kutoa huduma za kibenki kwa benki hizo kunahatarisha usalama wa amana za wateja wake.”

Taarifa hiyo imeeleza kuwa BoT inapenda kuuhakikishia umma kuwa itaendelea kulinda maslahi ya wenye amana katika mabenki kwa lengo la kuleta uhimilivu katika sekta ya fedha.

ARSENAL, CHELSEA NI BONGE LA MECHI, MWISHO IMEKUWA MABAO 2-2Arsenal na Chelsea zimemaliza mechi yao kwa sare ya mabao 2-2 kwenye Uwanja wa Emirates, London/
Mechi hiyo ya Ligi Kuu England ilikuwa na mvuto mkubwa baada ya mabao yote manne kufungwa katika kipindi cha pili.

Arsenal walianza kufunga kupitia Jack Wilshere lakini Chelsea wakasawazisha kupitia mkwaju wa penalti wa Eden Hazard.

Chelsea walifanikiwa kuongeza kupitia Marco Alonso dakika zikiwa zinayoyoma, beki wa kulia wa Arsenal, Hector Bellerin akasawazisha katika dakika za nyongeza.

CCM WILAYA YA GEITA WALAANI JESHI LA ZIMA MOTO KUWATOZA FEDHA KUBWA WACHIMBAJI BILA YA KUWAPATIA RISITI

Baadhi ya wachimbaji wa kijiji na kata ya Rwamgasa wakiendelea na kazi ya uchanjuaji wa madini ya dhahabu.

Moja kati ya wamiliki wa mialo ya uchenjuaji wa madini ya dhahabu akionesha risti ambayo sio ya EFD ambayo wamekuwa wakipatiwa baada ya kununua kifaa cha kuzimia moto.

Katibu mwenezi wa chama cha mapinduzi(CCM)Wilayani Geita Jonathan Masele akizungumza na wachimbaji baada ya kufika kwenye maeneo yao ya kazi na kukutwa baadhi ya makarasha yamefungwa na Jeshi la Zima moto na uokoaji.

Eneo la kuchenjulia dhahabu likiwa limefungwa na jeshi la zima moto na uokoaji.


Mwenyekiti wa chama cha mapinduzi Wilayani Geita,Barnabas Mapande akikagua moja kati ya mtungi wa kuzimia moto wakati alipofika kuzungumza na kusikiliza changamoto za wachimbaji.

Kifaa cha kuzimia moto kikiwa kwenye eneo la kuchenjulia dhahabu.
Na,Joel Maduka,Geita.
Chama cha mapinduzi Wilayani Geita kimelaani kitendo cha jeshi la zima moto na uokoaji kuwatoza gharama kubwa  bila ya kuwapa stakabadhi za serikali  baadhi ya wachimbaji wadogo wa dhahabu kwenye kijiji cha Lwamgasa huku  wakifungiwa shughuli  za uchenjuaji madini hayo kutokana na baadhi yao kugoma kununua kifaa cha kuzimia moto.

Akizungumza baada ya kufika kwenye machimbo hayo na kujionea namna ambavyo wachimbaji hao wamefungiwa shughuli zao Katibu Mwenezi wa CCM Wilayani Humo Bw Jonatham Masele,amesema CCM imesikitishwa na jeshi la zima moto kuwatoza  Sh Lakini moja na elfu ishirini.

“Kiukweli sisi kama chama tumesikitishwa sanaa na kitendo cha jeshi la zima moto kuuza kwa bei kubwa bila ya kutoa risti mitungi hii ya gesi ya kuzimia moto na jambo jingine kuwafungia watu shughuli zao bila ya kuwapa elimu jambo hili sio nzuri tunaomba wajitahidi kuwaelimisha kwanza awa watu nasio kujichukulia hatua ya kuwafungia”Alisema Masele.

Bw Lehamu Lugiko , Mzee Mathew Kajoro  na Mwananyanzara Hamis wameelezea sababu kubwa ambayo imeendelea kuwapa mashaka wachimbaji kuwa ni kuuziwa mitungi ya kuzimia moto bila ya kupewa Elimu ambayo itawasaidia kupambana na majanga ya moto huku wakisikitishwa na kitendo cha kufungiwa kwa shughuli zao.

Mkuu wa Jeshi la zimamoto na uokoaji  Mkoani Geita Bw Elisa Mgisha amesema wao sio wasambazaji kwani kuna watu ambao ni mawakala na kwamba suala la risti za EFD inatokana na wafanyabiashara wenyewe na kuhusu kuuziwa kwa bei kubwa ni kwamba wao wanapotoa kibari cha mawakala yeye ndiye mwenye jukumu la kupanga bei ya kuuza mtungi vile ambavyo anaonelea.


Mwenyekiti wa CCM wilaya ya Geita Bw Barnabas Mapande amemtaka mkuu wa jeshi la zima moto kushughulikia tatizo hilo na kuacha kuendelea kuwakandamiza wananchi na wafanyabiashara pindi wanapokuwa kwenye shughuli zao za kujitafutia kipato.