ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

Friday, November 4, 2022

HII HAPA HIFADHI YA TAIFA ILIYO KATIKATI YA JIJI LA MWANZA

NA ALBERT G. SENGO/MWANZA Katika kuthibitisha uzalendo wa kweli wa kuthamini na kutambua rasilimali za taifa zitonakazo na sekta ya utalii, watanzania wamehimizwa kujenga utamaduni wa kutembelea hifadhi ya taifa ya kisiwa cha saa nane, ili kuchangia pato la taifa kwa ustawi wa maendeleo. Mkuu wa hifadhi ya taifa ya kisiwa cha saanane Eva Malya, amesema hifadhi hii inavivutio mbalimbali, yakiwemo maeneo ya mapumziko, eneo maalum la usiri la kushuhudia mandhari nzuuri ya ziwa Victoria, jiwe maarufu la kuruka pamoja na ongezelo la ndege na wanyamapori. Ndani ya hifadhi hii kinachostaajabisha watalii wengi, ni jinsi tabia ya ndege dume aina ya tausi inavyojidhihiri akiwa kwenye imaya yake, Hilda Mikongoti ni afisa uhifadhi hifadhi ya taifa ya kisiwa cha saanane. Mkuu wa hifadhi ya taifa ya kisiwa cha saanane Eva Malya, amesema utakapotembelea hifadhi hii hutojutia kupoteza mudauzuri wa hifadhi hii unaelezwa na baadhi ya watalii wa ndani, waliotembelea hifadhi ya saanane.



ALBINO AUAWA NA WAUAJI WAKIONDOKA NA MKONO WAKE.

 NA ALBERT G. SENGO/MWANZA

Yapo mambo ya kijamii ambayo sisi sote tunatakiwa kuungana katika kuyapiga vita na kuyatokomeza kabisa. Mojawapo ya mambo hayo ni mauaji yawatu wenye albinism, ambayo yamekuwa yakiendelea hapa nchini. Hali hii, ambayo sio tu inalitia aibu taifa letu la Tanzania, pia ni ukosewaji mkubwa wa haki za binadamu. Ukichunguza kwa undani kisa kikubwa inasemekana ni imani za kishirikina na kutafuta “utajiri” wa haraka, jambo ambalo ni imani potofu zisizo kuwa na ukweli hata chembe. ....................................................................................................................... HABARI KAMILI SERIKALI imeahidi kufanya jitihada na uchunguzi wa kina kubaini watu waliotekeleza mauaji ya mwanakijiji Joseph Msongoma (49) mkazi wa kijiji na Kata ya Ngula wilayani Kwimba mkoani Mwanza, ambaye ana ulemavu wa ngozi (ualbino) ameuawa kikatili kwa kukatwa na panga huku wauaji wakiondoka na mkono wake wa kulia. Taarifa zinasema tukio hilo lilitokea Jumatano Novemba 2, 2022 saa 4 Usiku baada ya watu hao kufika nyumbani kwa Joseph na kumwita jina lake kisha kumkata mkono wake wa kulia na kutokomea nao kusikojulikana. Mbele ya waandishi wa habari nyumbani kwa marehemu Joseph, Mkuu wa Mkoa wa Mwanza, Adam Malima anatoa tamko kwa Kamati ya Ulinzi na Usalama ya Mkoa wa Mwanza kuhakikisha waliohusika katika tukio hilo wanakamatwa.

Thursday, November 3, 2022

HIZI NDIZO SABABU KWA RAIS SAMIA KUJA NA MJADALA WA KUSAKA NISHATI YA KUPIKIA

  Katika nchi nyingi za kusini mwa janga la Sahara, njia kuu ya kupika ni kwa kutumia mkaa, kuni na mafuta ya taa.


Kwa mujibu wa shirika la Clean cooking aliance Watu milioni 950 wanategemea kuni na mkaa kupikia, idadi inayokadiriwa kukua hadi bilioni 1.67 ifikapo 2050.


Njia hizi za kupikia hutumiwa sana kutokana na kuwa nafuu kwa familia nyingi za kipato cha chini.


Katika meneo ya mjini na vijijini, ni kawaida kukuta majiko ya kupikia yenye mkaa kwenye makazi yao.


Lakini njia hizi za kupikia huwa na madhara ya muda mrefu ya kiafya kwa mujibu wa wataalamu.


Kuna athari za kiafya kwa wazalishaji wa mkaa na watumiaji. Mkaa kimsingi ni kaboni tupu, na mkaa unaochomwa hutoa viwango vya juu vya kaboni dioksidi, kaboni monoksidi, na vichafuzi kama vile masizi, ambavyo vinaweza kuingia ndani kabisa ya mapafu, hasa katika majiko yasiyokua na sehemu za kutolea hewa ya kutosha.


Uzalishaji huu unaweza kuwa na madhara sana, kwa mujibu wa shirika la afya duniani WHO karibu watu milioni 4 kote ulimwenguni hufa kabla ya wakati kila mwaka kutokana na kupikia kwa moto na nishati ngumu kama mkaa.


 Watafiti wanaongeza kuwa huenda athari ikawa kubwa zaidi kutokana na kutokua na takwimu za kutosha katika nchi hizi za kusini mwa janga la Sahara.


Athari za  kiafya

Matumizi ya mkaa na kuni hutoa moshi ambao huleta madhara kwa binadamu


 Kwenye Kuni na mkaa pia hutoa chembembe ndogo ambazo huweza kupenya katika njia ya hewa na kuleta athari kiafya


 Na pia hewa ya Kaboni monoksidi inayotolewa na mkaa na kuni huweza kuingia mwilini na kupenya hadi kwenye damu kisha inaanza kuondoa hewa ya oksijeni kwenye damu, na kusababisha madhara ya muda mrefu na hata kifo kama itaingia kwa wingi.


Kaboni monoksidi, oksidi za nitrojeni, oksidi za sulphate na misombo mingine tete inayotolewa wakati wa usindikaji na uchomaji wa mkaa inaweza pia kusababisha matatizo ya kupumua na hatimaye magonjwa kama vile maambukizi yanjia ya hewa (ARI), ugonjwa sugu wa mapafu (COPD), pumu, saratani ya mapafu au kwa wajawazito kujifungua watoto wenye uzito wa chini.


 ‘’Mkaa na kuni kwa ujumla inaweza kuathiri njia ya hewa na damu lakini mtu akishapata matatizo ya njia ya hewa kutokana na matumizi ya mkaa na kuni, inakua chanzo cha matatizo mengine ya kiafya kama moyo, unakuta mgonjwa moyo umefeli lakini sababu inakua ni matatizo yanatokana na shida ya mapafu ambayo imesbabishwa na matumizi ya mkaa na kuni''. anasema Dkt. Elisha Osati, Daktari bingwa wa magonjwa ya ndani.


Mbali na athari za ndani ya mwili, matumizi ya mkaa hususani unaotokana na kuni huweza kuathiri macho kutokana na moshi na chembembe zinatolewa.


''Katika maeneo mengi ya vijijini wanatumia sana kuni kupikia pamoja na mkaa, ule moshi mara nyingi husababisha macho kuathiriwa na mwisho yanakua na rangi nyekunduna wakati mwingine mtu anaweza kushindwa kuona''. anasema dokta Osati.


Kaboni monoxide

Kaboni monoxide (CO), ni gesi isiyo na harufu na isiyo na rangi, na ni gesi yenye sumu ambayo inaweza kukufanya mgonjwa sana ukiipumua.  Inaweza kutengenezwa kwa moto na vifaa vinavyochoma gesi, kuni, mafuta au makaa ya mawe.


 Katika majiko ya kupikia yenye sehemu ndogo za kutolea hewa, mkaa unaweza kutoa viwango vya sumu vya kaboni Monoksidi (CO). Kiasi cha kidogo tu cha mkaa wa kupikia kinaweza kuzalisha viwango vya sumu ya CO.


''Kaboni monoxide ikiingia kwenye damu inaweza kuondoa oksijeni kwenye damu na ikakaa yenyewe na ikiingia kwa wingi huweza kusababisha kifo, na madhara yake ya muda mrefu yapo'' Anaongeza dkt. Osati.


Kwa mujibu wa tafiti mbalimbali watu hufa kila mwaka kutokana na sumu ya kaboni monoksidi wanapochoma mkaa katika maeneo yaliyofungwa kama vile nyumba zao, kwenye kambi au magari ya kubebea watu, au kwenye mahema. Baadhi ya waathiriwa wanakufa kutokana na sumu ya kaboni monoksidi baada ya kuchoma mkaa kwenye hema la chumbani au kambi ili kupata joto.


Nini cha kufanya?

Jamii nyingi barani Afrika hutumia mkaa na kuni kama njia kuu ya kupikia vyakula. Kuacha kabisa matumizi ya mkaa huenda isiwe jambo la uhalisia kwa sasa wakati maeneo mengi hasa ya vijijini hayajafikiwa na teknolojia mbalimbali za majiko ya kisasa.


Hakikisha unapikia na mkaa katika eneo lenye hewa ya kutosha katika nchi nyingi zilizoendelea matumizi ya mkaa kupikia si makubwa, na hufanywa nje maeneo ambayo yana hewa ya kutosha.


Lakini nchi zinazoendelea ni ngumu bado kuepuka matumizi ya mkaa. Kama jiko lako lina dirisha dogo, basi wataalamu wanashauri kupikia nje, eneo la wazi, lenye hewa ya oksijeni ya kutosha.


"Usijaribu kupika na mkaa ndani ya nyumba - haijalishi unafikiri nyumba yako ina hewa ya kutosha kiasi gani," anasema Nicole Rodriguez, RDN, mtaalamu wa lishe na mkufunzi wa kibinafsi anayeishi New York. "Kwa kweli, Tume ya Usalama wa Bidhaa za Wateja inaonya dhidi ya hata kuhifadhi jiko ndani ya nyumba lenye mkaa uliomaliza kutumia"


Kutafuta mbadala wa kuni na mkaa

Teknolojia imeweza kusaidia mapinduzi ya matumizi ya mkaa na kuni katika maeneo mengi duniani, lakini barani Afrika, hususani kusini mwa janga la Sahara bado kuni na mkaa ni njia nafuu kwa familia nyingi


Njia mbadala za mkaa ni pamoja na majiko yanayotumia umeme, gesi ya petroli iliyoyeyuka (LPG), ethanoli, majiko ya gesi yenye ufanisi kwa kutumia biomass (yaani, pellets) na biogas. Aina mbalimbali za teknolojia za kibunifu zinapatikana pia ili kuongeza ufanisi, uwezo wa kumudu, na upatikanaji wa nishati hizi mbadala.


Ingawa mtazamo wa sasa wa biashara ya mkaa na matumizi yake yalyozoeleka si mazuri kwa Afrika hususani Kusini mwa Jangwa la Sahara, bara hili lina uwezo mkubwa wa kutumia nishati safi.


Kwa msaada kutoka kwa serikali, mashirika ya kiraia, na wajasiriamali wa sekta binafsi kupitia kupitishwa kwa kiwango cha nishati ya jua na njia nyingine mbadala za mkaa kunaweza kusababisha mamilioni ya maisha kuboreshwa na maelfu ya jamii safi na zenye afya.

HII HAPA RAMANI YA UWANJA WA NDEGE MSALATO JIJINI DODOMA UTAKAOJENGWA

 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania  Mhe. SAMIA SULUHU HASSAN tarehe 30 Octoba 2022 ameweka jiwe la msingi ujenzi wa uwanja wa Ndege wa kimataifa wa Msalato jijini Dodoma.

Kukamilika kwa ujenzi wa uwanja huu utasaidia kukuza uchumi wa taifa pamoja na kurahisisha usafiri wa anga. Huu ni mwendelezo wa serikali ya awamu ya sita kuhakikisha inaanzisha na kuendeleza miradi ya kimkakati ya kuleta maendeleo nchini.

Wakala wa Barabara Nchini (Tanroads) imesema uwanja cha ndege wa Msalato pindi utakapokamilika utakuwa na uwezo wa kuhudumia abiria milioni 1.5 kwa mwaka.

MWILI WA KICHANGA WAOKOTWA KWENYE DAMPO LA SOKO

 


WAKAZI wa mtaa wa Shibayi kata ya Buhongwa wilayani Nyamagana jijini Mwanza wamekumbwa na taharuki baada ya kuona mwili wa kichanga kinachokadiriwa kuwa na umri wa miezi sita ukiwa umewekwa kwenye boksi na kutupwa katika dampo lililopo kwenye soko la mtaa huo. 

Mwili huo unadaiwa kutupwa leo majira ya mapema asubuhi kwenye dampo ambapo watu waliokuwa wanaokota mabaki ya chakula waliustukia mwili huo wakati wakisakura moja ya mamoksi ambapo hatimaye walinasa mwili huo.

WAANDISHI WA HABARI KANDA YA ZIWA WANOLEWA KUHUSU MAGONJWA YASIYOAMBUKIZA

 

Mwenyekiti wa vyama vya magonjwa yasiyoambukiza (TANCDA) profesa Andrew Swai akitoa mafunzo kwa waandishi wa habari juu ya magonjwa yasiyoambukizaWaandishi wa habari wakifuatilia mafunzo ya magonjwa yasiyoambukiza



Kuelekea wiki ya Maadhimisho ya magonjwa yasiyoambukiza yatakayofanyika Kitaifa Mkoani Mwanza kuanzia Novemba 5 hadi 12 mwaka huu Waandishi wa habari kutoka Mikoa ya Kanda ya ziwa wamepewa semina juu ya magonjwa hayo.

Semina hiyo iliyoandaliwa na Wizara ya Afya imefanyika leo Jumatano Novemba 2,2022 Jijini Mwanza.

Akizungumza katika semina hiyo Mratibu wa magonjwa yasiyoambukiza kutoka Wizara ya afya Shadrack Buswelu, amesema lengo la kuaandaa mafunzo hayo ni kuwawezesha waandishi wa habari kutoa taarifa ambazo ni sahihi kuhusiana na magonjwa yasiyoambukiza kwenye jamii sanjari na kuwaelimisha ili waweze kuchukua hatua madhubuti za kujikinga dhidi ya magonjwa hayo.

Mwenyekiti wa Shirikisho la vyama vya magonjwa yasiyoambukiza Tanzania (TANCDA) Prof. Andrew Swai, amesema magonjwa yasiyoambukiza yanaenea kwa wingi ikiwemo kisukari, Saratani,magonjwa sugu ya njia ya hewa,kuoza meno, magonjwa ya moyo na mishipa ya damu, na magonjwa ya akili.

MPINA AENDELEA KUCHOKONOA MAKINIKIA.


Dodoma. Mbunge wa Kisesa, Luhwaga Mpina (CCM) kwa mara nyingine ameendeleza moto wake bungeni kuhusu malimbikizo ya kodi zaidi ya Sh360 trilioni zinazotajwa kuwa zinatokana na makinikia.


Jana Jumatano Novemba 2, Mpina amesema ni wakati sasa Watanzania kujua nani alitoa kauli ya kusamehe kodi hiyo kwa nchi masikini kama Tanzania ambayo inahitaji kodi ili iweze kupanga maendeleo.

Katika mchango wake alijikita kwenye taarifa ya Kamati ya Hesabu za Serikali (PAC) akiuliza mambo matatu ambayo ni deni la Taifa ambalo hata hivyo hakulizungumzia zaidi, kodi ya makinikia na uhamishaji wa bidhaa na mauzo.


“Lakini kingine ninajiuliza nani aliruhusu Serikali kulipa kampuni ya Symbion kiasi cha Sh350 bilioni kwa haraka bila kuidhinishwa na Bunge wakati kampuni hiyo inadaiwa mabilioni mengi na Serikali lakini ghafla fedha hizo zililipwa bila kujua zilitoka mfumo upi na kwa ruhusa ya nani,” amehoji Mpina.

Mpina ameitaka Serikali kueleza wazi nani waliosababisha serikali kuingia hasara hiyo kwenye mkataba na kwa nini hawatajwi na hatua gani zichuliwe.

Hoja nyingine ameuliza ni kwa nini Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) inashindwa kukusanya malimbikizo ya kodi ya Sh7.54 trilioni ambazo hazina kesi mahakamani na kati ya hizo Sh3.87 trilioni ni za mwaka mmoja wa 2020/21.

Kuhusu mikopo ya asilimia 10 katika mapato ya halmashauri amesema kumekuwa na kichaka cha kula fedha badala yake mfumo ubadilishwe ili kusudi zianze kukopeshwa kwa njia ya kupitia mabenki ili waweze kuzifuatilia.

MWENYEKITI ALIA MITI YAKE KUKATWA NA TANESCO - YATOA UFAFANUZI.

 

NA ALBERT G. SENGO/MWANZA

OMBI limetolewa na wakazi wa Zenze kata ya Kiseke wilayani Ilemela jijini Mwanza baada ya baadhi ya wananchi kudai kutoshirikishwa katika elimu kuhusu uelewa wa upandaji wa miti ikiwemo oparesheni ya ukataji wa miti jirani ya miundombinu ya shirika hilo. Mwenyekiti wa mtaa wa Zenze Shija Ndungile ni mmoja kati ya wananchi walioathirika na oparesheni ya ukataji wa miti katika makazi yake, amesema kuwa wakati zoezi hili likitekelezwa na Tanesco hapakuwepo na elimu wala taarifa yoyote inayoashiria utekelezaji wa zoezi hilo. Kupata ufafanuzi kuhusu oparesheni hiyo Jembe Fm imebisha hodi katika ofisi za Shirika la Umeme Tanzania Tanesco mkoa wa Mwanza kuzungumza na meneja wa Shirika hilo Mhandisi Said Msemo naye akafunguka. Shirika la umeme Tanzania Tanesco linaendelea na oparesheni ya ukataji wa miti iliyopo jirani na miundombinu ya umeme katika maeneo mbalimbali ya mkoa wa Mwanza ili kulinda usalama wa maisha ya wananchi.

UMETESEKA KWA MENO KIPINDI KIREFU TIBA IPO HAPA, HUTO NG'OA JINO TENA.

 YAFUATAYO NI MAGONJWA YANAYOWEZA KUSHAMBULIA KINYWA NA MENO:-

- Kuoza meno. - Mawe kwenye meno ambayo hupelekea kulegea meno na kung;oka. - Mpangilio mbaya wa meno. - Kutokwa na damu kwenye fizi. - Kuvunjika mifupa ya uso (mandibulura fracture and zygoma na maxilla fractures) - Uvimbe sehemu ya uso hasa kwenye mataya unaozidi siku saba. - Vidonda visivyo pona kwa muda wa zaidi ya wiki mbili kwenye ulimi na sehemu mbalimbali za kinywa. - Harufu mbaya kinywani. Pamoja na kutibu maradhi mengine St. Clare Hospital iliyopo Mkolani Nyahingi wilayani Nyamagana mkoani Mwanza ina idara ya Afya ya Kinywa na Meno ambayo imesheheni wataalamu na vitendea kazi vya kutosha.

Wednesday, November 2, 2022

SERIKALI YAONYA WACHUNGAJI WANAODAI KUWA WANAUWEZO WA KUPONYA UKIMWI


Baraza la Kitaifa la Kudhibiti Ugonjwa wa Kuambikizana nchini Kenya (NSDCC), limewaonya viongozi wa kidini dhidi ya kueneza propaganda kwamba wanaweza kuponya Virusi Vya Ukimwi kupitia nguvu za Mungu. 

Katika taarifa Jumapili, Oktoba 29, NSDCC ilionya umma kuhusu ya madai ya wachungaji kwamba mgonjwa wa VVU aliponywa kupitia maombi. 

NSDCC lilishikilia kuwa dawa ya kutibu ugonjwa huo bado haijapatikana na kuwa kuwapotosha wafuasi wao kutasababisha maafa nchini. "Japo tunakubali kwamba maombi ni muhimu kwa ustawi wa kiroho, kisaikolojia kwa waumini wengi, madai ambayo hayajathibitishwa ya uponyaji wa VVU kwa imani hapo awali yamesababisha kupotezwa kwa."

 "Hadi sasa, hatuna tiba iliyothibitishwa ambayo inaweza kusimamiwa katika kituo cha afya cha umma," taarifa hiyo ilisoma kwa sehemu. 

Baraza hilo lilizua wasiwasi kuwa madai hayo potovu yanaweza kuathiri utumizi wa dawa za kurefusha maisha kwa wagonjwa na hivyo kuhujumu hatua zilizopigwa a serikali katika kudhibiti ugonjwa huo. 

"Kutatizika kwa matibabu ya VVU kuna matokeo mabaya ikiwa ni pamoja na uharibifu wa viungo vya mwili ambao hauwezi kurekebishwa," NSDCC ilieleza. 

NSDCC lilitoa wito kwa viongozi wa kidini kuongoza kondoo wao kwa kushughulikia matatizo ya kijamii na kitamaduni ambayo watu walioambukizwa wanakabiliwa nayo ili kupiga jeki vita dhidi ya ugonjwa huo hatari. 

"Tunawaomba jamii ya kidini kufanya kazi kwa karibu na waumini na washirika wengine ili kutokomeza unyanyapaa unaohusiana na ubaguzi ambao unaendelea kupuuza mafanikio yaliyopatikana katika vita vya VVU," shirika lilisema. 

Taarifa ya NSDCC inajiri siku chache baada ya kusambaa kwa habari za mwanamume mmoja ambaye alikuwa na VVU alipimwa na kuthibitishwa kwamba amepona virusi hivyo baada ya maombi. 

 Mnamo Agosti, Wizara ya Afya ilitangaza kwamba maambukizi ya VVU nchini yalikuwa yamepungua. Hata hivyo, ilizua wasiwasi kufuatia kuongezeka kwa maambukizo mapya miongoni mwa vijana. 

Ripoti ya WHO mnamo Julai 2022, ilionyesha kote duniani kulikuwa na maambukizi mapya 4000 ya Ukimwi kila siku mwaka wa 2021 miongoni mwa vijana hususan wanaotumia dawa za kulevya, wafanyabiashara wa ngono, wanaume wanaofanya ngono na wanaume, wafungwa na watu waliobadili jinsia. 

Vile vile kulikuwa na jumla ya maambukizi 1.5 milioni mwaka 2021 sawa na 2020. 

MWANAUME APIGWA RISASI NA KUUAWA NA WAHUNI WAKIFIKIRI BEGI LAKE LIMEJAA PESA.

 


Mwanamume Donholm amefariki dunia baada ya majambazi kumpiga risasi mara nne, na kumpokonya begi waliofikiri lina pesa, ila kupata limejaa vikombe vya karatasi. 

Nicodemus Munyasya alipigwa risasi na kuuawa na majambazi waliodhania alikuwa na begi la pesa.  

 Nicodemus Munyasya mwenye umri wa miaka 38, alikuwa ametoka kwenye benki kupeleka hundi, wakati wanaume wawili waliojihami walimfuata kwa kutumia boda boda na kumpiga risasi. 

Kwa mujibu wa ripoti kwenye jarida la the Daily Nation, polisi wanashuku kwamba majambazi hao walikuwa wanamjua mwendazake, wakati alipomshambulia eneo la Savannah na kumnyang'anya begi hilo. 

"Alikuwa amebeba begi la mizigo lililokuwa na vikombe vya karatasi, wakati majambazi hao walipodhania zilikuwa ni pesa,” taarifa ya polisi ilisema.

Munyaswa alipigwa risasi mara tatu mguuni na mara moja kwenye kifua. 

Mwili wake umepelekwa kuhifadhiwa katika chumba cha maiti kwenye Hospitali ya Mama Lucy.

Kituo cha Sayansi Tanga (STEM PARK TANGA) kuzindua mradi wa kufikia wanafunzi waliopo mbali na kituo.

 





Na Oscar Asaenga, TANGA

KITUO cha Sayansi cha Jijini Tanga ( STEMARK TANGA) watazindua mradi wa kuangalia namna ya kuweza kuwafikia wanafunzi waliopo umbali wa kilomita tano ili kuhakikisha nao wananufaika na mafunzo ya sayansi kwa vitendo. 

 Hayo yalisemwa leo na Meneja wa Kituo cha Sayansi kilichopo eneo Kisosora Jijini Tanga Max George wakati akizungumza na Nipashe kuhusu namna walivyojipanga kuwafikia wanafunzi waliopo pembezoni kilomita 5 kutoka kwenye kituo hicho na Jiji laTanga. 

 Alisema kwamba wao watakuwa wakiwafuata shuleni ambapo mpango huo utaanza Novemba 5,2022 watatembelea shule zote na kuwafikia wanafunzi 800 kwa kipindi cha wiki nne na watakuwa wakienda kila Jumamosi. 

 Alisema kwamba kupitia mpango huo wanaamini utawasaidia wanafunzi wengi wenye ndoto za kusoma masomo ya sayansi kwa vitendo na hivyo kuongeza wataalamu kupitia fani hiyo siku zinazo. " 

Lengo letu hili ni kuhakikisha wanafunzi wanaokaa umbali wa Kilomita 5 kutoka eneo la Kituo nao tuweze kuwafikia lakini pia namna ya kuzifikia na shule za binafsi na tumetembelea shule 20 mpaka sasa"Alisema. 

 Aidha alisema kwamba katika kituo hicho wamekuwa wakihakikisha wanafunzi wanasoma masomo ya sayansi kwa vitendo ambapo wanafanya kazi moja kwa moja walimu na maafisa kwa kuangalia namna ambao unarahisisha ufundishaji walimu kwa kutoa namna mbalimbali ufundishaji wa masomo hayo unakuwa rahisi.

 "Watawasaidia walimu na wanafunzi namna mtaala unavyohitaji kwa kuanzisha mfumo ambao walimu na wataalamu wa kituo cha sayansi tunamuandalia mazoezi kwa vitendo ili kumrahisishia anapomaliza inakuwa ni rahisi watoto kuelewa wanachofundishwa na inakwenda ngazi ya msingi mpaka sekondari"Alisema.

 Hata hivyo alisema mfumo huo waliouanzisha unawezesha watoto kuanza kupenda masomo ya sayansi kabla hata ya kuanza kutumia maabara na hivyo kuweza kujifunza kwa tija na mafanikio makubwa.

DC MOYO AWAPONGEZA CWT MANISPAA YA IRINGA KWA KUTOA ELIMU BORA KWA WANAFUNZI.

 

Mkuu wa wilaya ya Iringa Mohamed Hassan Moyo akiongea na walimu viongozi wakati wa mkutano wa wa chama cha walimu Manispaa ya Iringa (CWT) na kuwapongeza kwa kazi nzuri ya kufaulisha wanafunzi kwa asilimia kubwa
Mwenyekiti wa chama cha walimu Manispaa ya Iringa (CWT) Frank Lupeke akiongea na waalimu viongozi wakati wa mkutano mkuu wa chama hicho Manispaa ya Iringa
Baadhi ya walimu viongozi wakiwa kwenye mkutano mkuu wa Chama cha walimu Manispaa ya Iringa
Katibu wa chama cha walimu Manispaa ya Iringa akiongea na walimu viongozi wakati wa mkutano mkuu wa chama hicho.


Na Fredy Mgunda, Iringa.


Mkuu wa wilaya ya Iringa Mohamed Hassan Moyo amewapongeza walimu wa Manispaa ya Iringa kwa kuendelea kutoa elimu bora kwa wanafunzi wanaosoma katika shule hizo.
Akizungumza kwenye mkutano wa kikatiba wa chama cha walima Manispaa ya Iringa,Moyo alisema kuwa walimu wanaofundisha shule mbalimbali zilizopo Manispaa ya Iringa wamekuwa wakifaulisha wanafunzi kwa wastani unaotakiwa kitaifa.

Moyo alisema kuwa bila walimu kujituma na kujitoa kwa moyo wa dhati wanafunzi hawawezi kupata elimu bora wala hawawezi kufaulu kwa alama kubwa za kitaifa.

Alisema kuwa anatambua kunachangamoto nyingi za walimu na kuwaomba kuwa na subira wakati serikali ikiendelea kuzitafutia ufumbuzi changamoto hizo kwa awamu kama ambavyo wameanza kwenye ujenzi wa madarasa,kupandisha madaraja na mishahara.

Moyo alisema kuwa suala la kikokoto amelichukua na atalifikisha sehemu husika kwa sababu lipo kitaifa zaidi hivyo aliwatoa hofu kuwa serikali inatambua changamoto ya kikokotoo.

Moyo alimazia kwa kuwataka walimu kuwa na nidhamu ya kazi kwa kuacha kunywa pombe wawapo kazini,mapenzi na wanafunzi pamoja na utolo muda wa kazi kwa baadhi ya walimu.

Kwa upande wake mwenyekiti wa chama cha walimu Manispaa ya Iringa, mwalimu Frank Lupeke alisema kuwa walimu wa Manispaa ya Iringa licha ya kufaulisha kwa asilimia kubwa lakini wanakumbana na changamoto ya ubovu na uchakavu wa miundombini ya madarasa na baadhi ya nyumba za walimu ambazo zipo.

Mwalimu Lupeke alisema kuwa asilimia kubwa ya walimu wanakaa mbali na eneo la kazi kutokana kukosekana kwa nyumba za kuishi walimu na kusababisha kupunguza ufanisi wa kazi kwa walimu hao.

Alisema kuwa serikali ikifanikiwa kutatua changamoto hiyo ya miundombini madarasa na nyumba za walimu hata ufaulu na ufanisi wa kazi kwa walimu utaongezeka kwa asilimia kubwa.

Mwalimu Lupeke alimuomba mkuu wa wilaya ya Iringa Mohamed Hassan Moyo kupeleka kilio cha walimu cha kutaka kurejeshewa posho za kufundishia kama ilivyokuwa awali kwani kufanya hivyo kutarudiaha na kuongeza morali ya walimu kufundisha.

Lakini mwalimu Frank Lupeke alisema kuwa anampongeza Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan kwa kuwapunguzia adha wananchi ya ujenzi wa madarasa kwa kuamua kujenga vyumba vya madarasa na ofisi za walimu katika kila shule sekondari nchi nzima.

Mwalimu Lupeke alimazia kwa kuwataka walimu wa Manispaa ya Iringa kuwa na nidhamu ya kazi ili kuilinda taaluma hiyo ya ualimu ambayo imekuwa ikiheshimika hata nchini na nje ya nchi.

TAKUKURU TANGA YABAINI USAJILI WA WAGONJWA HEWA WA VVU KWENYE MIFUMO YA USAJILI WA WAGONJWA VITUO VYA AFYA

 

Mkuu wa Takukuru Mkoa wa Tanga Zainabu Bakari akizungumza na Waandishi wa Habari wakati akitoa taarifa kwa kipindi cha Julai hadi Septemba 2022.


NA OSCAR ASSENGA,MUHEZA..


TAASISI ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa mkoa wa Tanga(Takukuru) imefanikiwa kudhibiti wagonjwa hewa 313 wa VVU kwenye mfumo wa usajili wa wagonjwa hao wilayani Muheza.

Hayo yalibainishwa leo na Mkuu wa Takukuru Mkoa wa Tanga Zainabu Bakari  akizungumza na Waandishi wa Habari wakati akitoa taarifa kwa kipindi cha Julai hadi Septemba 2022.

Ambapo alisema Takukuru kupitia vyanzo vya siri ilibaini kuwa watoa huduma za afya wanaohusika na kusajiliwa watu wanaoishi na Virusi vya Ukimwi,wamekuwa wakifanya udanganyifu kwa kuwaingiza majina hewa ili kuonesha takwimu za wanaoishi na VVU kuonekana zipo juu kwa maslahi yao binafsi.

Mkuu huyo wa Takukuru Mkoa wa Tanga alisema alisema katika ufuatiliaji wa Takukuru Mkoa ulibaini kuwa wahudumu wa afya wanaohusika na zoezi la kuwasajili na kuwafuatilia wagonjwa wanaoishi na VVU wamekuwa wakilipwa posho ya gharama ya usafiri ka mawasiliano kiasi cha sh 20,000 kwa siku kila wanapotoka kwenda kukutembelea wagonjwa hao.

Alisema kwamba fedha hizo kulipwa na Shirika la Afya la Amref kwa kazi ya kufuatilia kila mgonjwa kwa lengo la kuhakikisha hali yake kiafya inaimarika kwa maana ya kutumia dawa kwa wakati na huduma nyengine zinazostahili.

Aidha alisema fedha hizo kulipwa moja kwa moja kwa mhudumu husika kupitia namba yake ya simu ya mkononi na ndiyo sababu inavyopelekea watumishi wasio waadilifu kuweka takwimu hewa kwa lengo la kujiongezea posho.

Alieleza katika ufuatiliaji uliofanywa na Takukuru kwa baadhi ya Zahanati ilibainika kuwa ni kweli kuna wagonjwa ambao hiyo halisi kwa maana ya upatikanaji wake na hivyo kufanya udhibiti kwa kuchukua hatua.

Alisema kwamba hatua walizoanza kuchukua ni kufikisha kikao cha pamoja kati yao na ofisi ya Mganga Mkuu wa wilaya na watendaji wake wote wanaohusika na kuwahudumia watu wanaoishi na VVU  pamoja na Amref.

" Katika kikao Takukuru iliwasilisha yaliyobainika katika ukaguzi wa kutembelea Jumla ya zahanatini 7 kati ya 16 zilizopo katika wilaya ya Muheza na kubaini tatizo hilo"Alisema.

Hata hivyo alisema kwamba katika kikao kazi hicho taasisi hiyo mkoani hapa ilimuagiza Mganga Mkuu wa wilaya ya Muheza kufanya uhakiki wa takwimu za wagonjwa wote wanaoishi na VVU na kutoa taarifa ya uhakiki.

Alisema baada ya agizo hilo ilibainika kuwepo kwa Jumla ya wagonjwa hewa 313 ambapo idadi hiyo iliondolewa kwenye mfumo.

Pia alisema wahusika katika usajili wa wagonjwa hao hewa wamepewa barua za kujitoleza kwa kitendo cha usajili wagonjwa hewa huku Wizara ya Afua ikitoa maelekezo ya kufanyika uhakiki kwa wateja wanaotumia dawa ambao sio halisi.

Hata hivyo Taasisi hiyo inaendelea kuwasihi watumishi wote wa Umma kufanya kazi kwa mujibu wa kanuni,taratibu,sheria na kiongozi iliyopo katika utekelezaji wa majukumu yao.

Tuesday, November 1, 2022

DAVIDO APOTEZA MTOTO KWA KIFO CHA UTATA.


 Ni siku ya huzuni kwa mwanamuziki Davido na mchumba wake, Chioma Rowland, baada ya kumpoteza mtoto wao wa kiume, Ifeanyi Adeleke. 

Mwanawe Davido anasemekana kuzama kwenye bwawa la kuogelea bomani kwao katika kisiwa chao cha Banana, Lagos, Nigeria, Oktoba 31. 

Kwa mujibu wa ripoti za vyombo vya habari, mtoto huyo wa miaka mitatu alipatikana akiwa amepoteza fahamu kwenye bwawa la kuogelea na kukimbizwa katika hospitali ya Lagos, ambapo alitangazwa kuwa amekata roho. 

 Davido na Chioma walikuwa mbali katika Jimbo la Ibadan kwa mkutano wa familia msiba ulipotokea. 

Habari za kusikitisha zilienea kwenye mitandao ya kijamii, na Kamanda wa Polisi wa Jimbo la Lagos, Benjamin Hundeyin, alithibitisha kifo cha mtoto huyo wa miaka mitatu. Kulingana na ripoti ya BBC Pidgin, mmoja wa wafanyakazi wa nyumbani wa Davido alipiga ripoti kuhusu tukio hilo lililotokea Jumatatu usiku katika kituo cha polisi cha eneo hilo. 

Kufikia sasa, wafanyikazi wanane wa mwimbaji huyo wamehojiwa na polisi. 

AY Comedian alisema: "Kifo cha mtoto si cha kawaida, si cha haki na ni cha kusikitisha. Hii imeniuma sana." Naviomusic alisema: "Pole kwako, kaka yangu @davido. Mtoto Ifeanyi Apumzike Kwa Amani." 

Steflon Don alisema: "Nawaombeeni dua Chioma na Davido ❤️." 


Nyota huyo wa muziki alisherehekea siku ya kuzaliwa ya mwanawe wa pekee wa kiume mnamo Oktoba 20, 2022, kwa ujumbe mtamu. "Nakuombea kwa moyo wangu wote Mungu akupe afya njema na furaha tele kwa muda wote uwezavyo kibinadamu. 

Utakuwa na mafanikio makubwa kuliko yangu Happy birthday, son @davidifeanyiadeleke !!! #BIG3 ," alichapisha ujumbe huo akisindikiza na picha murwa za bingwa huyo mdogo. 

Akisherehekea tunda la kwanza la tumbo lake la uzazi, Chioma aliandika ujumbe mtamu kwake Ifeanyi, na akasema: “Happy birthday mpenzi wa maisha yangu. Mama anakupenda sana, Mungu akujalie mema siku zote. 

Mungu amekuwa mwaminifu sana kwetu na nashukuru sana kuitwa mama yako. Nakutakia mafanikio makubwa zaidi ya wazazi wako. katika jina la Yesu, amina. Nakupenda pacha wangu." 

NIGERIA: WAHUNI WAVAMIA IBADA YA KANISANI, WAMTANDIKA PASTA NA KUHARIBU MALI YA MAMILIONI JUMANNE


Kile ambacho kilipaswa kuwa ibada nzuri ya Jumapili mbele za Mungu kiligeuzwa kuwa fujo na uharibifu wa mali ya kanisa yenye thamani ya mamilioni ya shilingi. Mchungaji Emmanuel Samweli alipigwa akiwa kanisani mwake. 

 Kundi la washambuliaji likiongozwa na Kamishna wa Polisi Henry Njoku aliyekuwa na bunduki pia walimfanyia vurugu kasisi Emmanuel Samuel Bares, mwangalizi mkuu wa Kanisa la Higherlife. 

Katika mahojiano na Legit TV, Emmanuel alifichua kuwa tukio hilo lilianza saa moja asubuhi wakati akielekea kanisani na familia yake huku akipigiwa simu kuwa kulikuwa na tingatinga kwenye kiwanja hicho. 

 Kupitia mazungumzo ya simu, mtumihi huyo wa Mungu alionyesha kwamba lengo la kuvamiwa lilikuwa ni kuangusha hekalu wakati walianza kubomoa jengo hilo kabla hajafika. Mchungaji alipofika kanisani, yeye pia alivamiwa na vijana hao waliokuwa na hamaki. 

“Niliingia ndani ya kanisa kusali na kumshukuru Mungu, wakanishikilia pale, wakanichana nguo zangu na kuanza kunipiga, wakaniburuza chini jinsi ilivyonekana kwenye video,” aliendelea na kuongeza kuwa alipokea kichapo kikali ndani ya kanisa. Mchungaji alionyesha kusikitishwa na ukweli kwamba kanisa halikupewa karatasi zozote za korti au notisi ya kuondoka, walionekana tu kuvamiwa na hekalu kubomolewa. 

Kasisi huyo alidokeza kuwa hema lililoharibiwa pekee lilikuwa la thamani ya mamilioni, bila kusahau vifaa vilivyomgharimu zaidi ya N15 milioni (KSh 4.1m), pamoja na ala za muziki na viti. 

Prince Ken Joseph, mtoto wa Chifu Patrick alithibitisha taarifa za Mchungaji Emmanuel, akisema shamba ni lao na lilikodishwa kwa kanisa. "Baba yangu alilikodisha kwa Mchungaji Emmanuel Samuel. Kanisa limekuwa hapa kwa muda na sasa Pedro ambaye ametokea katika hali ya kutatanisha amedai ardhi hiyo ni yake," alisema.

 Alifichua kuwa Pedro alishtakiwa lakini alikataa kufika mahakamani, akimshutumu kamishna wa polisi kwa kuchukua sheria mkononi mwake. 

Prince alimshutumu Njoku kwa kujisifu kuwa yeye ni mkubwa kuliko mahakama na akaelekeza kuwa pasta aondoke mahali hapo au angewatuma vijana wake kwenda kuliharibu kanisa lake. 

UVCCM IRINGA VIJIJINI: IRINGA SIO SOKO LA WAFANYAKAZI WA NDANI

 

Mwenyekiti wa UVCCM wilaya ya Iringa Elia Kidavile akitoa vyeti kwa wahitimu wa shule ya msingi Mlolo wakati wa mahafali ya 59 toka kuanzishwa kwa shule hiyo.
Mwenyekiti wa UVCCM wilaya ya Iringa Elia Kidavile akitoa kiasi cha shilingi laki mbili kwaajili ya kukarabati sakafu za shule ya msingi Mlolo wakati wa mahafali ya 59 toka kuanzishwa kwa shule hiyo

 Na Fredy Mgunda, Iringa.


MWENYEKITI wa jumuiya ya vijana wa chama cha mapinduzi wilaya ya Iringa vijijini (UVCCM) Elia kidavile amewataka wanafunzi wanaohitimu darasa na saba kukata kwenda kufanya kazi za ndani pindi wanapohitimu elimu ya msingi.


Akizungumza kwenye mahafali ya darasa la saba katika shule ya msingi Mlolo,Elia kidavile alisema kuwa kumekuwa na wimbi kubwa la madalali kuwarubuni wanafunzi kwenda kufanya kazi za ndani pindi tu wanapomaliza elimu msingi jambo ambalo limekuwa likikatisha ndoto za watoto wengi.

Kidavile aliwataka wazazi kukataa kabisa jambo hilo ambalo halina afya kwa maendeleo ya wananchi wa wilaya ya Iringa vijijini pamoja na Taifa kwa ujumla.

Alisema kuwa serikali ya awamu ya sita inayoongozwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan inatoa elimu bure kuanzia shule ya msingi hadi sekondari hivyo hakuna haja ya wazazi kuwapeleka watoto wao kwenda kufanya kazi za ndani pindi wanapohitimu elimu ya msingi.

Kidavile alisema kuwa mzazi yoyote yule anakayekutwa amempeleka mtoto wake kufanya kazi za ndani basi sheria zitachukua mkondo wake na UVCCM wilaya ya Iringa vijijini haikubaliani kabisa na wazazi wanaowapeleka watoto kufanya kazi za ndani,hivyo wazazi wanatakiwa kuwapeleka sekondari mara baada ya matokeo kutoka.

Alisisitiza kwa jamii ya wananchi wa Kijiji cha Mlolo kutoa taarifa kwa viongozi wa Kijiji,kata,tarafa na wilaya iwapo kuna mzazi amempeleka mtoto wake kufanya kazi za ndani au mtoto ametoroka kwenda kufanya kazi za ndani ili sheria ichukue mkondo wake.

Aidha mwenyekiti wa UVCCM wilaya ya Iringa vijijini Elia kidavile alichangia kiasi cha shilingi laki mbili kwa ajili ya kukarabati sakafu za shule ya msingi Mlolo ambao imeharibika ili kuwawezesha walimu kutoa elimu bora bila kuwa na hofu ya miundombini ya darasa.

Awali akizungumza mbele ya mgeni rasmi,mwalimu mkuu wa shule ya msingi Mlolo Salum Mtewa  alisema kuwa shule hiyo inakabiriwa na changamoto za ukosefu wa kompyuta,photokopi mashine, upungufu wa madawati, upungufu wa walimu na upungufu wa vifaa vya michezo kwa wanafunzi.

Mwalimu Mtewa alisema kuwa anashukuru mchango alioutoa mwenyekiti wa UVCCM wilaya ya Iringa vijijini Mheshimiwa Elia kidavile katika shule hiyo ya msingi Mlolo.

Alisema kuwa anaungana na mgeni rasmi kukemea kitendo cha wanafunzi kwenda kufanya kazi za ndani pindi wanapohitimu elimu ya msingi kuwa kunawapotezea ndoto za maisha yao.

MENO YA TEMBO YENYE UZITO WA KILO 34 YAKAMATWA IRINGA

 

Kamanda wa jeshi la polisi mkoa wa Iringa ACP Allan Bukumbi akionyesha vipande viwili vya meno ya Tembo pamoja silaha haramu ambazo jeshi la polisi wamezikamata na nyingine zimerudishwa kwa hiyari na wananchi wa mkoa wa Iringa akiwa pamoja na Kamanda uhifadhi nyanda za juu kusin Joas makwati
Kamanda wa jeshi la polisi mkoa wa Iringa ACP Allan Bukumbi akionyesha vipande viwili vya meno ya Tembo pamoja silaha haramu ambazo jeshi la polisi wamezikamata na nyingine zimerudishwa kwa hiyari na wananchi wa mkoa wa Iringa akiwa pamoja na Kamanda uhifadhi nyanda za juu kusin Joas makwati
Kamanda wa jeshi la polisi mkoa wa Iringa ACP Allan Bukumbi akionyesha vipande viwili vya meno ya Tembo pamoja silaha haramu ambazo jeshi la polisi wamezikamata na nyingine zimerudishwa kwa hiyari na wananchi wa mkoa wa Iringa akiwa pamoja na Kamanda uhifadhi nyanda za juu kusin Joas makwati.


Na Fredy Mgunda, Iringa.

JESHI la polisi mkoa wa Iringa kwa kushirikiana na askari wa hifadhi ya taifa ya Ruaha wamefanikiwa kukamata vipande viwili vya meno ya tembo vyenye uzito wa kilo 34 katika kijiji cha makongomi kata ya isalavanu Wilaya ya Mufindi Mkoani Iringa.

Akizungumza na waandishi wa habari kamanda wa polisi mkoa wa Iringa ACP Allan Bukumbi alisema kuwa tarehe 27.10.2022 majira ya saa 07:00 mchana huko katika kijiji cha makongomi kata ya isalavanu Wilaya ya Mufindi jeshi la Polisi Iringa kwa kushirikiana na askari wa hifadhi ya taifa ya Ruaha walifanikiwa kumkamata Crispin Muyinga miaka 35, mkulima wa makongomi akiwa na vipande viwili vya meno ya Tembo alivyokuwa amevificha kwenye msitu kwe mfuko wa salphet rangi nyeupe.

ACP Bukumbi alisema kuwa jeshi la polisi lilifanikiwa kumkamata Niko Kisinga mwenye umri wa miaka 40, mkazi wa Ilwazutwa na John Antony mwenye umri wa miaka 53, mkazi wa Mwanyenga wakiwa na nyamapori inayodhaniwa kuwa ya mnyama pofu iliyobanikwa na watuhumiwa hao walikutwa na vipande 60 vya nondo na baruti chupa mbili ambazo zote wanazitumia kwenye shughuli za uwindaji haramu.

Aidha ACP Bukumbi alisema kuwa jumla ya silaha kumi na tatu ambazo mbili ni aina ya Shortgun na kumi na moja ni aina ya Gobore ambazo zilisalimishwa katika vituo vya Polisi, ofisi za watendaji na maeneo mengine kwasababu mbalimbali zikiwemo wamiliki kuwa na umri mkubwa, na pia kutokuwa na uhalali wa umiliki baada ya kurithi silaha hizo kutoka kwa wazazi.


Alisema kuwa Jeshi la Polisi Mkoa wa Iringa linatoa wito kwa wananchi wa Mkoa wa Iringa kutoa ushirikiano kwa kuendelea kutoa taarifa mbalimbali za watu wanaomiliki silaha kinyume cha sheria ili hatua kali zichukuliwe dhidi yao baada ya muda wa kusalimisha kwa hiari kufika ukomo

ACP Bukumbi alimazia kwa kuyataja maeneo ambayo bado wamiliki wa silaha kinyume na sheria ambapo alisema  "kutoka vyanzo vyetu vya taarifa bado kuna wananchi ambao wanamiliki silaha haramu maeneo yote ya hifadhi pamoja na mengine kama udekwa, Ruaha mbuyuni (Kilo lo), Wasa, Nyang'oro (Iringa) na Igoweko (Mufindi)".

Monday, October 31, 2022

MARAIS WATATA AFRIKA WALIODINDA KUACHIA UONGOZI, TATIZO NI NINI?

 

Picha za baadhi ya marais wa Afrika ambao wamekuwa uongozini kwa muda mrefu na wangali uongozini. 

Bara la Afrika lina viongozi ambao baadhi wametawala tangu mataifa yao kupata uhuru. Baadhi ya viongozi hawa wakitawala kwa takriban miaka 40. 

Marais hawa hudai kuwa ni msukumo wa raia wao kuwa waendelee kuwahudumia licha ya vilio vya wengi wa wapinzani ambao hulalamikia kunyanyaswa na kura zao kuibwa. 

Katika miaka ya hivi karibuni, baadhi ya marais hawa wameondolewa mamlakani lakini wengine wachache wamesalia. 

Hii ni orodha ya rais watano ambao wametawala kwa muda mrefu barani Afrika: 


1. Teodoro Obiang Nguema – miaka 42 Rais wa Guinea ya Ikweta Teodoro Obiang Nguema ndiye rais aliyeoongoza kwa miaka mingi zaidi duniani nab ado angali mamlakani. 

Amekuwa uongozini kwa miaka 42. Alichukua mamlaka mwaka 1979 baada ya kumpindua mjomba wake. Teodoro Obiang Nguema ambaye amekuwa rais wa Guinea ya Ikweta kwa miaka 42 sasa. 

 2. Paul Biya – miaka 39 Rais huyu wa miaka 89 ameiongoza Cameroon tangu mwaka 1982. Mwaka 2018, alichaguliwa kwa muhula mwingine wa miaka saba. Paul Biya amekuwa rais wa Cameroon tangu mwaka 1982. 


3. Denis Sassou Nguesso – miaka 37 Huyu ni rais wa Congo-Brazzaville. Rais Sassou Nguesso amekuwa ofisini kwa miaka 37 sasa. 

Kwanza alihudumu kuanzia 1979 hadi 1992 na kurejea 1997 baada ya kukamilika kwa vita nchini humo. Alichaguliwa tena mwa muhula mwingine wa miaka mitano katika uchaguzi wa 2021. Rais Denis Sassou Nguesso ameiongoza Congo Brazzaville kwa miaka 37 sasa. 



 4. Yoweri Museveni – miaka 35 Rais wa Uganda Yoweri Museveni amekuwa uongozini tangu mwaka wa 1986 aliposhinda vita vilivyomwondoa mamlakani Amin Dada na utawala wake wa kiimla. 

Alichaguliwa kwa muhula wake wa sita katika uchaguzi wa Januari 2021. 

Rais wa Uganda Yoweri Museveni. Amekuwa mamlakani tangu mwaka wa 1986. 

6. Isaias Afwerki – miaka 29 Rais pekee ambaye a,efahamika na raia wa Eritrea tangu taifa hilo kupata uhuru ni Isaias Afwerki. Amekuwa mamlakani tangu Aprili 1993 ambapo ameongoza kwa miaka 29 sasa. 

Sunday, October 30, 2022

VIINGILIO SHIRIKISHO YANGA.

Kuelekea mchezo wa Yanga ya Tanzania dhidi ya Club Africain ya Tunisia, Hatua ya mtoano Shirikisho utakaochezwa siku ya Jumatano ya tarehe 02.November.2022 katika dimba la Mkapa jijini Dar es salaam tayari viingilio kwa mchezo huo vimeshatajwa.

VIINGILIO

Yanga wasema Watanzania wajiandae kutetema.