Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. SAMIA SULUHU HASSAN tarehe 30 Octoba 2022 ameweka jiwe la msingi ujenzi wa uwanja wa Ndege wa kimataifa wa Msalato jijini Dodoma.
Kukamilika kwa ujenzi wa uwanja huu utasaidia kukuza uchumi wa taifa pamoja na kurahisisha usafiri wa anga. Huu ni mwendelezo wa serikali ya awamu ya sita kuhakikisha inaanzisha na kuendeleza miradi ya kimkakati ya kuleta maendeleo nchini.
Wakala wa Barabara Nchini (Tanroads) imesema uwanja cha ndege wa Msalato pindi utakapokamilika utakuwa na uwezo wa kuhudumia abiria milioni 1.5 kwa mwaka.
Tupe maoni yako
0 comments:
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.