ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

Saturday, February 16, 2019

NAIBU WAZIRI JUMA AWESO AMETOA WIKI TATU KWA MKANDARASI KUKAMILISHA MRADI WA MAJI WA SAWALA

Naibu waziri wa maji Juma Aweso ametoa wiki tatu kwa kampuni ya mavonoa’s kuhakikisha wanakamilisha ujenzi wa mradi wa maji wa Sawala uliopo jimbo la Mufindi kusini katika wilaya ya Mufindi mkoani Iringa
NAIBU waziri wa maji Juma Aweso akimbana mkandarasi wa kampuni ya mavonoa’s kwa kushindwa kukamilisha ujenzi wa mradi wa maji wa Sawala uliopo jimbo la Mufindi kusini katika wilaya ya Mufindi mkoani Iringa

NA FREDY MGUNDA,IRINGA.



NAIBU waziri wa maji Juma Aweso ametoa wiki tatu kwa kampuni ya mavonoa’s kuhakikisha wanakamilisha ujenzi wa mradi wa maji wa Sawala uliopo jimbo la Mufindi kusini katika wilaya ya Mufindi mkoani Iringa.
Akizungumza mbele ya wananchi,wabunge na wafanyakazi wa halmashuri hiyo,waziri Aweso alisema kuwa amekuwa akipokea malalamiko mengi ya mkandasi huyo ambaye amekuwa hana mahusiano mazuri na viongozi wa halmashauri hiyo.
“Mimi niseme ukweli nakupa wiki tatu kuhakikisha unamalizia ujenzi wa mradi wa maji wa Sawala la sivyo utaniona mbaya na mimi ni mkali kweli kwa wakandasi wamepewa kazi na serikali na wanashindwa kutekeleza mradi kama ambavyo mkabata ulisema hivyo nakupa wiki tatu kuhakikisha wananchi wanapata maji” alisema Aweso
Aweso alisema serikalia ya awamu ya tano haita kubari kumuanda mkandarasi yeyote Yule aliyepewa kazi na serikali anashindwa kukamilisha mradi wakati fedha amepewa,mkandarasi huyo atachukuliwa hatua za kisheria haraka sana kwa kuwa saizi hakuna mtu kutumia vibaya pesa za serikali kama ilivyokuwa huko nyuma.
“Walizoea kuzichezea pesa za serikali miaka ya huko nyuma kwa sasa hakuna mkandarasi tayeweza kuichezea serikali ya awamu hii kwa kuwa sisi wateule wa Rais wetu Dr John Pombe Magufuli hakuna anayekubari kutumbuliwa kisa wakandarasi kufanya vibaya kwenye miradi waliyopewa” alisema Aweso
Aidha naibu waziri Aweso aliwatoa hofu viongozi wa halmashuri ya wilaya ya Mufindi kuhusu mkandarasi huyo kuwa akishindwa kutekeleza mradi huo ndani ya wiki tatu hizo basi sheria itachukua mkoando wake.
“Mkuu wa wilaya,mbunge,mkurugenzi na mwenyekiti wa halmashauri niwahakikishieni kuwa nitatakuja tena tarehe mbili mwezi wa tatu hapa kuja kuangalia kuwa huu mradi umefikiwa wapi na makubariano yetu ameyatekeleza mkandarasi huyu” alisema Aweso
Awali mkuu wa wilaya ya Mufundi Jamhuri William alimueleza naibu waziri kuwa mkandarasi huyoamekuwa anaidharau serikali kwa kuwa mara kwa mara ameandikiwa barua na serikali ya wilaya lakini hajawahi kujibu hata mara moja kitendo kinachoashiria dharau.
“Huyo mkandarasi amekuwa anatusumbua sana maana tunamuita mara kwa mara hataki kuitika wito wetu hivyo hizo ndio dharau kubwa kiasi kwamba anashindwa hata kuendelea kutekeleza mradi huu ambao wananchi wanategemea kuwa mkombozi wao” alisema Jamhuri William
Mkuu wa wilaya alisema kuwa atamkamata na kuwa ndani mkandarasi huyo kwa kuwa anachelewesha kuteleza mradi huo wa maji na kusababisha wananchi kuichukia serikali kwa kusema kuwa wametoa ahdi hewa kitua ambacho sio kweli.
“Mheshimiwa naibu waziri hapa Sawala tunashindwa hata kufanya mikutano ya hadhara kwa ajili ya huu mradi wa maji ambao mwazoni wananchi walijenga imani kubwa wakati wa kusainiana mkataba wa kutekeleza mradi huu” alisema Jamhuri William
Akitoa malalamiko hayo mwenyekiti wa halmashauri ya wilaya ya Mufindi Festo Mgina alimwambia naibu waziri wa maji Juma Aweso kuwa hamhitaji tena huyo mkandarasi kwa kuwa amekuwa kikwazo cha kuleta maendeleo ya wananchi kwa kushindwa kutekeleza mradi huo wa maji.
“Huyu kwetu ni kero kubwa mno mheshimiwa naibu waziri wa maji,sisi kama halmashauri hatupo tayari kufanya kazitena na huyu mkandari kwa ujeuri wake na kushindwa kuiheshimu sekali ya wilaya kwa kushindwa kumtua ndo mwanamke” alisema
Nao baadhi ya wananchi walijitokeza hapo walimwambia naibu waziri kuwa mkandarasi huyo hafanyi kazi ipasavyo kwa kuwa amesikia waziri unakuja ndio na yeye ameanza kazi jana tu ya kukarabati tenki hili la maji ili ukifika uone kama yupo anafanya kazi wakati sio kweli.
Hata hivyo naibu waziri Juma Aweso alimalizia kwa kusema kuwa ifikapo tarehe mbili mwezi wa tatu mradi huo uwe umekamilika na wananchi waweze kupata maji na kufanikisha adhima ya Rais ya kumtua ndoo mwanamke.

TANESCO SONGWE WAPEWA SIKU TATU KUJIELEZEA.

 Mkuu wa Mkoa wa Songwe Brig. Jen. (Mst) Nicodemus E Mwangela akisaini kitabu cha wageni ofisi ya TANESCO Songwe wakati alipoenda kufahamu mpango wa kumaliza matatizo ya umeme mkoani hapa, Kushoto kwake ni Kaimu Meneja TANESCO Mkoa wa Songwe, Aristidia Clemence
Kaimu Meneja TANESCO Mkoa wa Songwe Aristidia Clemence akimuonyesha Mkuu wa Mkoa wa Songwe Brig. Jen. (Mst) Nicodemus E Mwangela picha ya nguzo zilizochanika kutokana na radi na vikombe vilivyopasuka katika nguzo.
Shirika la Umeme Nchini TANESCO Mkoa wa Songwe limepewa siku tatu kuandaa mkakati utakaoeleza namna ya kumaliza matatizo ya umeme ikiwemo katizo la mara kwa mara la umeme na tatizo la kiwango kidogo cha umeme.
Mkuu wa Mkoa wa Songwe Brig. Jen. (Mst) Nicodemus E Mwangela  ametoa agizo hilo mapema leo asubuhi alipofika ofisi za TANESCO Songwe kufuatia kukatika mara kwa mara kwa umeme na pia kila siku ya Jumamosi ambapo alimtaka Meneja wa shirika hilo kueleza mkakati wa kumaliza tatizo hilo.
“Nimekuja hapa kwakuwa naona sasa tunageuka makubaliano ya kukata umeme kila jumamosi tu, sasa katikati ya wiki umeme unakatika sana, lakini hata hayo makubaliano ya jumamosi naona muda unaenda tu hatujui lini mtakamilisha matengenezo mnayoyafanya kila Jumamosi”, Brig. Jen. (Mst) Mwangela.
Ameongeza kuwa Mkoa unapata athari kubwa kufuatiwa kutokuwepo umeme wa uhakika kwakuwa shughuli za uzalishaji viwandani, shughuli za majumbani zinazohitaji umeme na hata baadhi ya huduma za kijamii zinazohitaji uwepo wa umeme wa uhakika zinaathiriwa huku akielezea kuwa wananchi hawapewi taarifa.
“Nawaelekeza kuanzia sasa mkizima umeme au hata ikitokea hitilafu taarifa na sababu zitolewe ili ifahamike umeme umekatika kwa sababu zipi, tatizo la umeme kwetu limeshakuwa kero kubwa kwani  hakuna maendeleo hususani ya viwanda bila umeme”, amesisitiza Brig. Jen. (Mst) Mwangela.
Brig. Jen. (Mst)  Mwangela. amewataka TANESCO Songwe waongeze ujuzi na maarifa kutoka kwa maeneo mengine ambao wameweza kutatua matatizo kama hayo pia wafahamu mahitaji ya vifaa vinavyotakiwa kwa ajili ya matengenezo wanayoyafanya.
Naye Kaimu Meneja TANESCO Mkoa wa Songwe Aristidia Clemence amesema kuwa kukatika umeme mara kwa mara kunatokana na Mvua zonazoendelea kunyesha kwani husababisha nguzo kuanguka na pia radi hupasua vikombe katika nguzo.
Amesema matatizo ya Umeme Mkoa wa Songwe yataisha pale ambapo Mradi wa Umeme wa Gridi ya Taifa kutoka Iringa mpaka Nkangamo Momba, wa Kilovoti 400 utakapokamilika kwani kwa sasa umeme unaopatikana ni mdogo na unapatikana kwenye laini moja yenye Zaidi ya Kilometa 1200 tofauti na mikoa mingine yenye line kumi na umeme wa kutosha.
“Hata sisi tunaumia umeme unapokatika kwani tunatambua umuhimu wa umeme na ndio maana tunafanya kazi usiku na Mchana, Mkoa huu ulikuwa na matatizo ya nguzo chakavu pia baadhi ya vikombe vimeharibika ndio maana kila jumamosi tunazima umeme ili kubadilisha nguzo na vikombe hivyo”, ameeleza Clemence.
Clemence ameongeza kuwa kwa sasa kuna ujenzi wa switching station ambao unatarajiwa kukamilika hivi karibuni na kusaidia endapo kuna hitilafu imetokea sehemu moja umeme usikatike mkoa mzima tofauti na sasa ambapo hitilafu ikitoa wilaya moja mkoa mzima unakosa umeme.
“Pia tatizo lililopo sasa ni hitilafu ikitokea mkwajuni Songwe umeme ukikatika ni Mkoa Mzima ila ujenzi huu wa Switching Station utasaidia kuondoa tatizo hilo, pia mradi ule wa Iringa wa Gridi ukikamilika matatizo ya umeme yatakwisha hivyo nawasihi wenye viwanda na wenye nia ya kuwekeza kwenye viwanda wasikate tamaa”, amefafanua Clemence.
Kwa upande wao wananchi Mkoani Songwe wameiomba serikali iwasaidie uwepo wa umeme wa uhakika ili waweze kuzalisha na kufanikisha uchumi wa viwanda, aidha wamesema kukatika kwa umeme mara kwa mara kunaathiri upatikanaji  wa huduma za kijamii kama vile baadhi ya huduma za afya hospitalini.

BAADHI YA WAKRISTU HUSALI JUMUIYA ILI WAZIKWE VIZURI?



 Jumuiya zinaboresha sana maisha ya kiroho ya waamini iwe ni mjini au kijijini. Kwanza waamini wana ushirika wa kuhimizana kufanya mema. Mtu anajisikia asiwaangushe wenzake kwa maisha mabaya. Mtu ana jina lake kama Mkristu analoona lazima kulinda hadhi yake.

Anajiona mwenza wa wengine, anaingia nyumba zao nao wanaingia ya kwake hata kama ni maskini. Jumuiya ni kama SACCOS ya maadili mazuri na wema. Jumuiya inampa mtu heshima na hadhi.

Jumuiya inamtoa mtu katika upweke. Anapata watu ambao anaweza kuongea nao mambo mbali mbali yakiwemo yale yanayompa shida. Kiurahisi atapa mtu wa kuweza kumpa ushauri katika maisha yake. 

Pamakuwepo na mshikamano katika raha na shida, matukio kama ndoa au kifo na mengine ya maisha, lakini wengi baadhi yao wanaogopa kutoshiriki Jumuiya wakihofia kutengwa siku wakiwa na shida hasa misiba, Jeh hili liko vipi?