ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

Saturday, February 16, 2019

BAADHI YA WAKRISTU HUSALI JUMUIYA ILI WAZIKWE VIZURI?



 Jumuiya zinaboresha sana maisha ya kiroho ya waamini iwe ni mjini au kijijini. Kwanza waamini wana ushirika wa kuhimizana kufanya mema. Mtu anajisikia asiwaangushe wenzake kwa maisha mabaya. Mtu ana jina lake kama Mkristu analoona lazima kulinda hadhi yake.

Anajiona mwenza wa wengine, anaingia nyumba zao nao wanaingia ya kwake hata kama ni maskini. Jumuiya ni kama SACCOS ya maadili mazuri na wema. Jumuiya inampa mtu heshima na hadhi.

Jumuiya inamtoa mtu katika upweke. Anapata watu ambao anaweza kuongea nao mambo mbali mbali yakiwemo yale yanayompa shida. Kiurahisi atapa mtu wa kuweza kumpa ushauri katika maisha yake. 

Pamakuwepo na mshikamano katika raha na shida, matukio kama ndoa au kifo na mengine ya maisha, lakini wengi baadhi yao wanaogopa kutoshiriki Jumuiya wakihofia kutengwa siku wakiwa na shida hasa misiba, Jeh hili liko vipi? 

Tupe maoni yako

0 comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.