ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

Saturday, December 31, 2011

BALOZI OMBENI SEFUE AAPISHWA KUWA KATIBU MKUU KIONGOZI MPYA AKICHUKUWA NAFASI YA LUHANJO.

Rais Jakaya Kikwete akimwapisha rasmi Balozi Yohana Sefue kuwa Katibu Mkuu Kiongozi katika hafla iliyofanyika leo Ikulu jijini Dar es salaam.

Rais Jakaya Kikwete (kushoto) akisisitiza jambo kwa viongozi wakuu, Makamu wa Rais, Dk. Mohamed Gharib Bilal (wa tatu kulia), Waziri Mkuu, Mizengo Pinda (wa pili kulia), Katibu Mkuu Kiongozi mpya, Balozi Ombeni Sefue (wa pili kushoto) na Katibu Mkuu Kiongozi aliyemaliza muda wake, Phillemon Luhanjo muda mfupi baada ya kumwapisha Balozi Ombeni Sefue kuwa Katibu Mkuu mpya, Ikulu, Dar es Salaam. (Picha na Fadhili Akida).

MAADHIMISHO YA MIAKA 10 YA ROBERT CUP NA MAENDELEO YA MPIRA WA KIKAPU MKOA WA MWANZA.

Mgeni rasmi Waziri wa Kazi na Maendeleo ya Vijana mh. Gaudentia Mugosi Kabaka akihutubia katika maadhimisho ya MIAKA 10 ya mashindano ya Robert Cup tokea yalipoanzishwa mwaka 2001 yakiwa na lengo la kumuenzi marehemu Robert Chacha Kabaka aliyekuwa mmoja kati ya waanzilishi wa timu ya mpira wa kikapu ya Butimba Spiders na pia mdau mkubwa wa mpira wa kikapu hapa mkoani.

Mgeni rasmi akiongozwa na Uongozi wa MRBA kukagua timu zilizochuana.

MRBA imekuwa na mpango madhubuti ya kuinua na kuvumbua vipaji kwa kuendesha mashindano ya shule za sekondari kuanzia mwaka 2003 hadi leo.

Chimbuko la mashindano ya Robert Cup lilianzia katika uwanja huu wa chuo cha Ualimu Butimba.

Game likiendelea.

Kaimu Mwenyekiti Sosho Kizito.
"MRBA imetoa Viongozi mbalimbali ngazi za juu kama vile Mama Angelina Mabula mwenyekiti wa hazina Taifa, Mussa K. Mziya Rais wa shirikisho la mpira wa kitapu huku mama Angelina Mabula aliteuliwa tena kuwa mkuu wa Wilaya ya Muleba mwaka 2010"

Waziri wa Kazi na Maendeleo ya Vijana mh. Gaudentia Mugosi Kabaka akimkabidhi Kamishna wa Fiba International, Certificate of Appreciation.

Waziri wa Kazi na Maendeleo ya Vijana mh. Gaudentia Mugosi Kabaka akimkabidhi Mwanahabari wa Star Tv Jackob Markus, Certificate of Appreciation.

Friday, December 30, 2011

LIKIZO TYME NA ROCK CITY....

Jua lileeeeee magharibi.

Hapa kulikuwa na soka la ufukweni.

Kwaheri jua mpaka kesho tena.

Twaarabu la alhamisi at Villa Park Five Stars Morden Taarab walikuwa wakitumbuiza.

Ayo na Mapacha Watatu...

Ayo and G at Rock Bottom

From Left G.Sengo, Sebastian Ndege, Millard Ayo and Brother.

Thursday, December 29, 2011

SUPER D BOXING COACH AJIVUNIA MAFANIKIO 2011

Na Mwandishi Wetu

ALIYEKUWA bondia wa ngumi za kulipwa Rajabu Mhamila 'Super D' ambaye pia ni kocha wa timu ya ngumi ya Ashanti na mkoa wa Ilala kimichezo amesema anajivunia mafanikio makubwa aliyoyapata katika mchezo wa ngumi katika kipindi cha mwaka 2011. Akizungumza na waandishi wa habari Super D ambaye pia ni mpiga picha wa Magazeti ya Busines Time, Majira, Sports Starehe na jarida la Maisha alisema moja ya mafanikio ni kuwaandaa vijana chipukizi wengi na kuwafikisha katika kiwango kizuri cha kuvuna matuna ya mchezo huo.

Alisema pamoja na hilo pia ameweza kushirikiana vema na wadau wa ngumi pamoja na mapromota mbalimbali wanaoandaa mapambano makubwa kwa kutoa mchango wake wa vifaa vya ngumi ili kufanikisha mapambano mbalimbali yaliyofanyika katika kipindi cha mwaka huu.

Katika hatua nyingine Super D amekua akitoa mafunzo ya mchezo wa ngumi pamoja na kutambua sheria mbalimbali kwa njia ya DVD zikisambazwa na kocha wa mchezo huo mkoa wa kimichezo wa Ilala 'Super D' kwa ajili ya kuwapa mambondia mbalimbali mbinu za mchezo na mashabiki kujua sheria za masumbwi.

Ndani yake wakiwemo mabondia Floyd Mywether, Manny Paquaio, Amiri Khanny, Mohamedi Ali, Mike Tayson David Haye na wengine ambapo kutakuwa na matukio ya mazoezi yao katika mataifa yao ikumbukwe kuwa ni mabingwa wa dunia. na kutakuwa na mapambano makubwa matano ya utangulizi.

Alisema mipango yake kwa mwaka 2012 ni kuhakikisha anaendelea kuwainua mabondia wengine chipkizi akiwemo bondia Shomari Mirundi na Ibrahimu Class ambao amewataja ni mabondia wazuri wanaohitaji kuendelezwa vipaji vyao.

Alisema bondia Ubwa Salum ambaye alimtwanga Mustapha Doto,kwa pointi 60-57 alishinda ambapo pambano hilo lilikuwa moja ya mapambano ya utangulizi ya pambano kubwa la Rashidi Matumla na Maneno Osward lililofanyika DEsemba 25 mwaka huu.

Wednesday, December 28, 2011

CHUKUWA KUKU WA SIKUKUU....!!!!


ZAWADI hii ya kuku ni maalumu kwako katika kuukaribisha mwaka MPYA 2012.

Chakufanya chagua mojawapo ya kuku hawa aliye juu ama iliyeko chini kamata usherehekee mwaka MPYA Mwanawane.
Aksante!!!!

STONE CLUB NA SHANGWE ZA SIKUKUU

'The New Stone club' Hadhi ya burudani imerejea Mwanza...

AMPLIFAYA INAKULA GOOD TIME ROCK CITY HADI 'NYUIYA'

Mkali wa kunyetisha 'Taarifa Kumi kali za kila siku' kupitia Clouds Fm kipindi chaitwa 'Aplifaya' Millard Ayo hivi sasa yuko ardhi ya miamba 88.1 kwa nia ya kujumuika na marafiki kushea good time za kuikaribisha 2012. Wazee wa Stone club Mupooooo!!!!?

Millard yu shabiki sana wa magari sampuli za kizamani.

"I need to buy this car"

'Rolls Royce' Moja kati ya Expensive car duniani.

Tuesday, December 27, 2011

CHINA WAFANYA MAJARIBIO YA TRENI IENDAYO KWA KASI 500km/h SUPER HIGH-SPEED TRAIN

BEIJING (Reuters) - Mwishoni mwa juma Wachina wametambulisha rasmi treni iendayo kwa kasi (super-rapid train) ambayo imehakikiwa kwa kufanyiwa majaribio na ufanisi mkubwa kupatikana, taarifa zizidi kusema kuwa mzigo unauwezo wa kusafiri kwa mwendo kasi wa kilometa 500 kwa saa (mfano Mwanza to Arusha), as the country moves ahead with its railway ambitions despite serious problems on its high-speed network. The train, made by a subsidiary of CSR Corp Ltd, China's largest train maker, is designed to resemble an ancient Chinese sword, the official Xinhua news agency reported.

It "will provide useful reference for current high-speed railway operations," it quoted train expert Shen Zhiyun as saying.

But future Chinese trains will not necessarily run at such high speeds, CSR chairman Zhao Xiaogang told the Beijing Morning News.

"We aims to ensure the safety of trains operation," he said.

China's railway industry has had a tough year, highlighted by a collision between two high-speed trains in July which killed at least 40 people. Construction of new high-speed trains in China has since been a near halt.

In February, the railways minister, Liu Zhijun, a key figure behind the boom in the sector, was dismissed over corruption charges that have not yet been tried in court.

SALAMU KWA WADAU TOKA RADIO FRANCE

"Kwa marafiki na wasikilizaji wetu barani Afrika na duniani kote kwa ujumla, Wafanyakazi wote wa Idhaa ya Kiswahili ya Radio France Internationale iliyoko Dar Es Salaam – Tanzania, wanakutakia Heri ya Kris masi na Mwaka Mpya wa 2012 wenye fanaka."

Monday, December 26, 2011

GOSPEL FESTIVAL 2011 YATIKISA MWANZA

Mgeni rasmi aliyemwakilisha mkuu wa mkoa wa Mwanza Diwani wa Mkolani Stanslaus Mabula akimkabidhi Mtumishi wa Mungu Dr. Moses Kulola Cheti kutambua mchango wake katika muziki wa Injili.

Hakika ilikuwa ni siku ya kipekee kwani eneo lilipata mibaraka kwa kusheheni watumishi wa Mungu kila kona, pichani ni Mtumishi wa Mungu Bishop Malisa akisikiliza kwa umakini yaliyokuwa yakijiri viwanjani hapo naye alitunukiwa cheti cha kutambua mchango wake katika Muziki wa Injili.

Kwaya

Marafiki waalikwa, hapa ilikuwa mwanzo kabisa katika Tamasha hilo kubwa la aina yake lililofanyika leo jioni Uwanja wa CCM Kirumba jijini Mwanza .

Mwimbaji wa Muziki wa Injili nchini Tumsifu Rufutu akiwa katika vazi la Musa akiinyoosha fimbo yake kuigiza tendo la kuitenganisha watu mithili ya bahari.

Tumsifu Rufutu aka Musa akiwaongoza wahudhuriaji aka wana wa Israel..

Mara safari ya kuelekea Kaanani kupitia wimbo wake maarufu mwambie Farao ikawadia..

Wageni wetu walio hudhuria tamasha hilo la kwanza lijulikanalo kwa jina la Gospel Festival 2011.

Wageni ni kuimba na kusifu.

Mgeni rasmi aliyemwakilisha mkuu wa mkoa wa Mwanza Diwani wa kata ya Mkolani Stanslaus Mabula akimkabidhi cheti Mtumishi wa Mungu Bishop Charles Sekelwa kwa mchango wake wa kuendeleza muziki wa Injili.

Mtumishi wa mungu Bishop Zenobius Isaya akionyesha cheti alichotunukiwa na Kampuni ya F Plas Intertainment kuthamini mchango wake katika kukuza muziki wa injili.

Mapambano Kwaya kutoka Geita...

Vijana Anglican Nyamanoro Choir wakipata flash ya pamoja.

Wakongwe Aic Makongoro Kwaya nao wakipata flash ambapo hii ni moja kati ya kwaya zilizo tunukiwa cheti maalum kwenye tamasha la Gospel Festival 2011.

Ni fursa ya Moja kati ya Wadhamini Winning Shoping Centre akitangaza huduma zao kwa umati uliohudhuria tamasha hilo pembeni yake amesimama Meneja mipango wa F. Plus Intertainment Albert G. Sengo

Mwimbaji Daniel Safari (R) na (L) wakiwa na mkurugenzi wa F Plus Intertainment Fabian Fanuel (C)

VIONGOZI ACHENI TAMAA - MAASKOFU

MAASKOFU nchini wametumia ibada za mkesha na Sikukuu ya Krismasi jana, kuwataka viongozi wa umma nchini kuacha ubinafsi, tamaa na kujilimbikizia mali kwa sababu tabia hizo zinaweza kuliingiza taifa katika machafuko. Askofu wa Dayosisi ya Mashariki na Pwani ambaye pia ni Mkuu wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT), Dk. Alex Malasusa akisalimia watoto nje ya lango kuu la Kanisa la Azania Front baada ya kumalizika kwa Ibada ya Krismasi jijini Dar es Salaam. (Picha na Mohamed Mambo)

Askofu Mkuu wa Kanisa Katoliki Jimbo Kuu la Tabora, Mhashamu Paul Ruzoka, amesema tabia hizo zimekuwa ikiwafanya wananchi wakate tamaa, kwa sababu inawasababisha viongozi wenye tamaa kushindwa kufuata maadili ya utumishi wa umma na hivyo kugeuka kama maadui wao kwani wanashindwa kutenda haki.

Akihubiri katika Ibada ya Krismasi Kitaifa jana katika Kanisa la Mtakatifu Theresia Mtoto wa Yesu mjini Tabora, Askofu Ruzoka, pia aliwataka viongozi kuhakikisha kuwa utekelezwaji wa sera ya Kilimo Kwanza nchini, haiathiri wananchi na kuwaacha bila ya kuwa na ardhi.

Akizungumzia athari za kutokuwepo kwa Azimio la Arusha, alisema ni pamoja na kuwepo kwa mbio za utajiri baina ya viongozi, kutofuatwa kwa maadili ya uongozi, kutokuwa na miiko, kuongezeka kwa posho katika vikao vingi na kuibuka kwa mrabaha katika kazi mbalimbali za kiserikali na kukithiri kwa tamaa.

Naye Mchungaji Mwaipopo wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT) Usharika wa Kanisa Kuu, Dodoma Mjini, amewataka wabunge kuacha ubinafsi wa kujilimbikizia posho kwani hali ngumu ipo kwa kila Mtanzania.

Alisema anashukuru viongozi kutambua maisha ya Dodoma yako juu kiasi kwamba hawawezi kuishi kwa posho ya Sh 70,000 kwa siku.

Alisema maisha ni magumu Dodoma kwa kila mtu si kwa wabunge tu, iweje kundi hilo dogo lisikilizwe je wananchi wakimbilie wapi?

“Kuna kukata tamaa kila kona, kuna majanga ya kutisha, mafuriko, ajali sasa hivi kifo kimetawala duniani kote.” Alisema Mchungaji Mwaipopo.

Naye Askofu wa Dayosisi ya Central Tanganyika, Godfrey Mhogole wa Kanisa la Anglikana, amemlalamikia Ofisa Elimu wa Mkoa wa Dodoma kwa kufuta matokeo ya watoto waliofaulu darasa la saba mwaka huu.

Alisema iwapo ofisa huyo hataondolewa, yuko tayari kumshitaki kwa kiongozi wa nchi. Alisema kuna haja kwa Ofisa Elimu Mkoa kuangalia kwa kina suala hili kwani halileti picha nzuri katika sura ya elimu nchini.

Alisema katika Shule ya Msingi ya Bishop Stuart DCT iliyopo Msalato mwaka huu walifaulu wanafunzi wanne tu, hali iliyoleta mshtuko kwao.

Alisema kwa miaka mingi shule hiyo imekuwa ikifaulisha sana wanafunzi, lakini anashangaa mwaka huu wanafunzi waliofaulu wamefutiwa matokeo.

Aidha, Askofu Telesphor Mkude wa Jimbo Katoliki la Morogoro, amemwomba Rais Jakaya Kikwete kuwawajibisha watendaji wa Serikali ‘wachakachuaji’ wanaohusika kwa namna moja ama nyingine kuruhusu wananchi kujenga makazi mabondeni na waliosababisha udanganyifu katika mtihani wa Darasa la Saba.

“Yaliyotokea kwa wenzetu walioathiriwa na mafuriko baadhi ya maeneo ya Jiji la Dar es Salaam, ni janga kubwa sana na wanahitaji kusaidiwa na Watanzania wote, lakini ninaunga mkono kauli ya Rais Kikwete aliyowaambia waliojenga mabondeni wahame,” alisema Askofu Mkude.

Askofu Mkuu wa Kanisa Katoliki Jimbo Kuu la Dar es Salaam, Mwadhama Polycarp Kardinali Pengo ameonya kile alichosema ni baadhi ya watu kuwageuzia na kuwatungia maneno watu wanaojitokeza kupinga dawa za kulevya.

Amesisitiza kuwa dawa za kulevya ni janga la taifa ambalo mapambano dhidi yake hayapaswi kubezwa na mtu yeyote kutokana na namna zinavyoathiri vijana na pia watu wazima.

chanzo: Gazeti la Habari leo

Sunday, December 25, 2011

PICHA ZA UKUTANI NA X MASS

Cuthbert G.(R) na Cedrick G. (L).

Cedrick G. akiview ziwa Victoria.

Chuma hichoo tha way to Saa nane island.

Ze familia

Kasa

Toleka nyuuzi bin nyuz'

Ze view.

Elephant.

Mie.

Ze friends kona.