ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

Saturday, January 7, 2017

MNAJIMU HASSAN YAHYA HUSSEIN ATABIRI VIFO KWA VIONGOZI WA DINI, SIASA, WASANII, WANAHABARI MWAKA HUU,

Maalim Hassan Yahya Hussein akizungumza katika mkutano na waandishi wa habari, Dar es Salaam leo , kuhusu utabiri wake wa mambo mbalimbali yatakayotokea mwaka huu. PICHA NA RICHARD MWAIKENDA;KAMANDA WA MATUKIO BLOG

Baadhi ya mabo aliyotabiri ni;Kutatokea kashfa kubwa sana ya ngono \au fumanizi itakayowahusu viongozi wa dini, siasa na wasanii maarufu itakayosababisha  viongozi hao kufedheheshwa  na kuanguka kabisa katika tasnia zao.

Mwaka huu pia kutakuwa na vifo vya viongozi wakubwa maarufu wa kisiasa  na kidini, kufa ghafla vifi hivyo vitatokana na msongo wa moyo na shinikizo la damu.


Mioto mingi mikubwa itatokea nchini na duniani.


Viongozi wakubwa wa upinzaniduniani na Tanzania kurejea kwenye vyama walivyovihama.


Vifo vya vya ghafla vya wasanii maarufu dunianiani ikiwemo Tanzania vinaweza vikatokana na fumanizi kuuliwa au kuana wenyewe.


Wimbi kubwa la vifo viliwakumba wanahabari duniani 2016 vitaendelea mwaka huu  Ajali nyingi kuwakuta wanasiasa, watawala na viongozi wa dini katika mwaka huu.

MHANGA WA UKATILI WA KIJINSIA ALISHUKURU SHIRIKA LA KUTETEA HAKI ZA WANAWAKE NA JINSIA (KIVULINI)

Mhanga wa ukatili wa kijinsia Elizabeth Joseph amelishukuru shirika la kutetea haki za wanawake la Kivulini kwa kunusuru ndoa yake baada ya kufukuzwa na ndugu wa mumewe. 

LUFANO NDIYE MWENYEKITI MPYA MZFA UCHAGUZI 2017

UCHAGUZI Mkuu wa Chama cha Mpira wa Miguu Mkoa wa Mwanza (MZFA) uliofanyika juzi jijini Mwanza na kumchagua Vedastus Lufano kwa kura 20 kati ya 34 kuwa Mwenyekiti mpya wa MZFA akimshinda Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya CCM taifa Wilaya ya Ilemela (NEC) Israel Mtambalike aliyeambulia kura 14 tu.

Awali wakati wa mkutano mkuu wa Chama hicho Mwenyekiti aliyemaliza muda wake Jackison Songola aliwashukuru wajumbe 34 na kuomba kuwachagua viongozi wengine wa kuendeleza mpira kwa kuzingati wao ndo wanayo dhamana ya kuchagua viongozi wapya kupitia kura zao hivyo kutegemewa na wadau wa soka kuwapatia watu watakaoendeleza mazuri na kuacha mabaya.

“Viongozi watakaochaguliwa kushika nyadhifa za kuongoza MZFA ni vyema wakashirikiana na wadau mbalimbali pamoja na viongozi tuliomaliza muda wetu kuchukua mazuri tuliyoyaacha ya kuendeleza mpira wa Mkoa wa Mwanza na kuacha yale mabaya ambayo yataonekana kuwa hayana tija katika kuendeleza soka la Mwanza,”alisisitiza Songola.

Naye Mgeni rasmi wa mkutano mkuu huo, Mbunge wa Jimbo la Nyamagana, Stanslaus Mabula (CCM) akifungua mkutano aliwahasa wajumbe wa MZFA kutafakari soka la Mkoa huo ambalo limekuwa likienda mlama kwa kipindi cha miaka 10 iliyopita hivyo kuwa na wajibu wa kuchagua viongozi watakaoguswa na kuendeleza kwa kasi mpira wa miguu.

“Huu si wakati wa porojo, majungu na fitina ni wakati mhimu kwa wajumbe kutumia nafasi yenu ya kuwawakilisha wadau wengine kuchagua viongozi wazuri na wenye nia ya dhati ukizingatia unaungwa mkono na mamia ya wadau mbalimbali hivyo watumie fursa hiyo kutowaangusha wadau wa soka na viongozi mtakaopata nafasi muwendeleze mpira,”alisema.

Akitangaza matokeo ya uchaguzi huo juzi katika ukumbi wa Chama Kikuu cha Ushirika Nyanza (NCU 1984 Ltd) mwenyekiti wa Kamati ya uchaguzi huo Wakili Anderw Innocent alisema kwamba wajumbe halali wa uchaguzi walikuwa 34 kwa mujibu wa Katiba ya MZFA na walipiga kura kwa mujibu wa taratibu na kanuni na kuwepo wawakilishi wa TFF kufatilia uchaguzi huo.

Innocent aliwataja washindi wa nafasi zote na viongozi wapya wa MZFA na kura zao kwenye mabano nafasi ya Mwenyekiti Vedastus Lufano (20) na Israel Mtambalike (14) hakuna kura iliyoharibika, nafasi ya Makamu Mwenyekiti mgombea mmoja Domity Chisena alishinda kwa kura 22 huku kura za hapana 8 na zilizoharibika 4.

Alimtangaza Katibu wa  MZFA kuwa ni Leonard Charles (18), Gribert John “Dady” (16), Katibu Msaidizi mgombea alikuwa mmoja Khalid  Bitebo alipata kura 14 za hapana 13 na saba ziliharibika hivyo hakushinda nafasi hiyo, nafasi ya Mweka Hazina ni Elastus Mayalla (22), alimshinda Bob Butambala (11) moja iliharibika, Mwakilishi wa Vilabu ni Kevin Patrick (24) na nane za hapana.

Wakili Inoocent aliwataja washindi wengine kuwa ni Mwakilishi wa mkutano taifa wa Shirikisho la Mpira wa Miguu nchini (TFF) aliyeshinda ni Ephraim Majinge (19) Arim Allbah (16) na mchezaji wa zamani wa Yanga African Aron Nyanda akiambulia kura moja tu huku wajumbe wa Kamati tendaji akiwataja ni Juma Mokili(19), Osca Kapinga (24) na Edwin Hansi (11).
Mwenyekiti mpya wa MZFA Vedastus Lufano akitoa shukurani baada ya uchaguzi.
Sehemu ya wajumbe 34 waliokusanyika wakiwa na dhamana ya kuchagua viongozi wapya kupitia kura zao.
Mwenyekiti aliyemaliza muda wake Jackison Songola aliwashukuru wajumbe 34 na kuomba kuwachagua viongozi wengine wa kuendeleza mpira kwa kuzingati wao ndo wanayo dhamana ya kuchagua viongozi wapya kupitia kura zao hivyo kutegemewa na wadau wa soka kuwapatia watu watakaoendeleza mazuri na kuacha mabaya.

MAGOLI YA REAL MADRID ILIPO IGALAGAZA GRANADA HII LEO 7 JAN 2017

Isco Alarcon Goal - Real Madrid vs Granada 1-0 - La Liga 07/01/2017 Karim Benzema Goal - Real Madrid vs Granada 2-0 - La Liga 07/01/2017  Cristiano Ronaldo Header Goal - Real Madrid vs Granada 3-0 - La Liga 07/01/2017 Isco Alarcon Second Goal - Real Madrid vs Granada 4-0 - La Liga 07/01/2017 Casemiro Goal - Real Madrid vs Granada 5-0 - La Liga 07/01/2017

AUSTRIA KUPIGA MARUFUKU WANAWAKE WAISLAMU KUVAA HIJABU.

Waziri wa Mambo ya Nje na Utangamano wa Austria ametoa wito wa kupigwa marufuku vazi la stara la hijabu linalovaliwa na wanawake Waislamu katika maeneo ya umma nchini humo.
Sebastian Kurz, ambaye anatoka katika chama cha kihafidhina cha Christian Conservative People’s Party (OVP), amesema kuwa anaandaa muswada ambao ukipasishwa na kuwa sheria, wanawake wa Kiislamu nchini humo na hususan wafanyakazi wa umma kama vile walimu hawataruhusiwa kufunika vichwa vyao wakiwa kazini.
Amesema sheria hiyo itakuwa kali kushinda ile ya Ufaransa, nchi ambayo ilipiga marufuku vazi la burqa na kutangaza faini kubwa kwa wanaokiuka sheria hiyo.

Mwanamke wa Kiislamu aliyejistiri kwa mtandio nchini Austria.
Jumuiya inayotambulika ya Kiislamu nchini Austria ya IGGIO imekosoa muswada huo na kusisitiza kuwa, kuwabagua wafanyakazi wa umma kwa misingi ya dini yao ni kinyume cha sheria za nchi na ni hatua inayokanyaga moja kwa moja uhuru wa kuabudu. 
Vazi la burqa, lililopigwa marufuku katika nchi kadhaa za Ulaya
Haya yanajiri mwezi mmoja baada ya Angela Merkel, Kansela wa Ujerumani kutoa wito wa kupigwa marufuku vazi la niqab nchini humo.
Oktoba mwaka jana, Bulgaria ilijiunga na baadhi ya nchi za Magharibi kama Canada, Ubelgiji na Ufaransa, zilizopiga marufuku vazi la staha la burqa, linalovaliwa na wanawake Waislamu.


MOTO WATEKETEZA NYUMBA 1 MOROGORO.

Simu Tv :Watu 11  wa familia moja wanusurika kifo baada ya jengo kuteketea kwa moto mkoani Morogoro.

KILIO CHA WAKULIMA IRINGA.

Baadhi ya wananchi mkoani Iringa waiomba serikali kuwapelekea mbegu za muda mfupi katika kukabiliana na tatizo la uhaba wa mvua.

UPELELEZI WAKWAMISHA KESI YAKITILYA.

KESI ya uhujumu uchumi inayomkabili aliyekuwa Kamishna wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA), Harry Kitilya na wenzake, imeahirishwa hadi Januari 20 mwaka huu kutokana na upelelezi kutokamilika.
Wakili Mwandamizi wa Serikali, Mutalemwa Kishenyi alidai jana katika Hakimu Mkazi wa Mahakama ya Kisutu, Wilbard Mashauri kuwa kesi imekuja kwa ajili ya kutajwa na kwamba hakimu anayesikiliza kesi hiyo, Cyprian Mkeha, hayupo.

Kishenyi alidai kuwa upelelezi wa kesi hiyo haujakamilika, hivyo aliomba tarehe nyingine kwa ajili ya kutajwa. Hakimu Mashauri alikubaliana na ombi hilo na kuahirisha kesi hiyo hadi Januari 20 mwaka huu. Katika shauri lililopita, Hakimu Mfawidhi, Mkeha aliutaka upande wa mashitaka kueleza upelelezi wa kesi hiyo umefikia hatua gani.

Wakili Esterzia Martin alidai kuwa jalada la kesi hiyo lipo Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (Takukuru), kwa ajili ya kuendelea kuchunguza nyaraka.

Hivyo, aliomba apangiwe tarehe nyingine kwa ajili ya kueleza upelelezi umefikia wapi. Mbali na Kitilya, wengine ni mshindi wa Mashindano ya Urembo (Miss Tanzania) mwaka 1996, Shose Sinare na Mwanasheria wa Benki ya Stanbic, Sioi Solomon. Kwa pamoja, washtakiwa hao wanakabiliwa na mashtaka manane, likiwemo kutakatisha fedha, dola za Marekani milioni sita.

Wanadaiwa kutenda makosa hayo katika tarehe tofauti kati ya Machi 2013 na Septemba 2015 wakati wa mchakato wa mkopo wa Dola za Marekani milioni 550 wa Serikali ya Tanzania kutoka Benki ya Standard ya Uingereza.

Friday, January 6, 2017

VIDEO JINSI BARCELONA ILIVYOKUNG'UTWA NA ATHLETIC BILBAO USIKU WA KUAMKIA LEO.

Athletic Bilbao vs Barcelona 2-1 - All Goals & Extended Highlights - Copa del Rey 05/01/2017 HD

HUYU NDIYE MCHEZAJI BORA WA AFRIKA MWAKA 2016

Shirikisho la soka barani Afrika Caf, January 5 2017 Abuja Nigeria ilifanyika hafla ya utolewaji wa tuzo za soka za mwaka 2016 na tuzo hizo utolewa kwa wachezaji waliyofanya vizuri kwa mwaka husika kwa kupigiwa kura.
Mchezaji wa timu ya taifa ya Algeria na timu ya Leicester City ya England Riyad Mahrez alitangazwa mshindi wa tuzo ya mchezaji bora Afrika.
 Mahrez ambaye alipata kura 361, huku Pierre-Emerick Aubameyang akishika nafasi ya pili kwa kupata kura 313 wakati Sadio Mane wa Liverpool amemaliza nafasi ya tatu kwa kupata kura 186.






Mahrez mwenye miaka 25, aliisaidia tumu yake Leicester kushinda taji la ligi kuu soka England msimu uliopita, tiyari ameshinda tuzo ya mcehzaji bora wa England sambamba na mchezaji bora wa BBC Afrika.

MANDELA NI NEMBO YA MAPAMBANO DHIDI YA UBAGUZI WA RANGI ASEMA MWAKILISHI WA IRAN UN.

Ghulam Ali Khosro.
Mwakilishi wa Kudumu wa Iran katika Umoja wa Mataifa amemtaja hayati mzee Nelson Mandela kuwa nembo ya mapambano dhidi ya ukandamizaji na ubaguzi wa rangi.

Mwakilishi huyo wa kudumu wa Iran katika Umoja wa Mataifa ameyasema hayo baada ya kutembelea maonyesho ya picha za Nelson Mandela yaliyotayarishwa katika makao makuu ya Umoja wa Mataifa na mwanasanaa wa Kiirani kwa jina la Maitham Shah Babai. 

 Mwanasanaa huyo wa Kiirani ambaye ni mpiga picha, mtengeneza filamu na mwandishi kijana anafanya maonyesho ya picha ya hayati mzee Nelson Mandela kiongozi wa mapambano dhidi ya ubaguzi wa rangi nchini Afrika Kusini tangu tarehe 3 hadi 6 mwezi huu wa Januari. 

Maonyesho hayo yamefanyika katika moja ya kumbi za kijamii katika makao makuu ya Umoja wa Mataifa mjini New York Marekani.

Ghulam Ali Khosro  Mwakilishi wa Kudumu wa Iran katika Umoja wa Mataifa jana alipongeza jitihada za msanii huyo kijana wa Iran katika siku ya pili ya kufanyika maonyesho hayo huko New York. 
Mzee Nelson Mandela (kushoto), enzi za uhai wake

Khosro baadaye aliandika katika kitabu cha kumbukumbu baada ya kutembelea maonyesho hayo ya picha za mzee Nelson Mandela kuwa, " Nelson Mandela shujaa wa mapambano dhidi ya ubaguzi wa rangi, mapambano ya mshikamamo wa kitaifa na kukabiliana na ukandamizaji".


 Nelson Mandela kiongozi aliyeongoza mapambano dhidi ya ubaguzi wa rangi nchini Afrika Kusini (Apartheid) na rais wa zamani wa nchi hiyo aliaga dunia tarehe 5 Disemba mwaka 2013 akiwa na umri wa miaka 95.

Thursday, January 5, 2017

WATU WATANO WANASHIKILIWA NA JESHI LA POLISI KWA KOSA LA KUJIHUSISHA NA KILIMO CHA BHANGI WILAYANI SENGEREMA.

Pichani watuhumiwa watatu kati ya watano waliokamatwa wakilihudumia shamba la bangi wilayani Sengerema.

TAARIFA YA JESHI LA POLISI MKOA WA MWANZA KWA VYOMBO
VYA HABARI LEO TAREHE 5.1.2017


KWAMBA TAREHE 4 /1/ 2017 MAJIRA YA SAA SITA USIKU (00:00) KATIKA MAENEO YA KIJIJI CHA NYABUTANGA KATA YA BUKOKWA TARAFA YA BUCHOSA WILAYA YA SENGEREMA MKOA WA MWANZA, ASKARI WALIFANIKIWA KUWAKAMATA WATU WATANO AMBAO NI 1. JULIUS NDALO MIAKA 80, 2. GEORGE JULIUS MIAKA 22, 3. JOSEPH JULIUS MIAKA 28, 4. MABULA JULIUS MIAKA 17, NA 5. TABU DAWA MIAKA 34 WOTE WAKAZI WA KIJIJI CHA NYABUTANGA, KWA KOSA LA KUJIHUSISHA NA KILIMO CHA BHANGI KITENDO AMBACHO NI KINYUME NA SHERIA, AMBAPO JUMLA YA MICHE YA BHANGI 17, 794 ILIWEZA KUPATIKANA KATIKA MASHAMBA YAO.

AWALI ASKARI WALIPATA TAARIFA KUTOKA KWA RAIA WEMA JUU YA UWEPO WA WATU WANAOJIHUSISHA NA KILIMO CHA BHANGI KATIKA KIJIJI CHA NYABUTANGA, NDIPO MAJIRA TAJWA HAPO JUU ASKARI WALIKWENDA MAENEO YA MASHAMBA YALIYOPO KIJIJINI HAPO  NA KUKUTA MASHAMBA MAWILI YENYE UKUBWA WA EKARI TATU YAKIWA YAMEPANDWA BHANGI PAMOJA NA MAHINDI. ASKARI WALIFANYA OPERESHENI USIKU HUO YA KUNG’OA MICHE YOTE YA BHANGI KATIKA MASHAMBA HAYO, AMBAPO KIASI CHA MICHE 17,794 YA BHANGI ILIPATIKANA NA KUFANIKIWA KUWAKAMATA WATU WATANO TAJWA HAPO JUU AMBAO WANADAIWA KUMILIKI  MASHAMBA HAYO.

WATUHUMIWA WAPO KATIKA MAHOJIANO NA JESHI LA POLISI, PINDI UCHUNGUZI UKIKAMILIKA HAPO BAADAE WATAFIKISHWA MAHAKAMANI, UPELELEZI NA MISAKO YA KUTAFUTA WATU WENGINE AMBAO WANAJIHUSISHA NA KILIMO HARAMU CHA BHANGI BADO UNAENDELEA.

KAMANDA WA POLISI MKOA WA MWANZA NAIBU KAMISHINA WA POLISI AHMED MSANGI ANATOA WITO KWA WAKAZI WA JIJI NA MKOA WA MWANZA AKIWATAKA KUACHA TABIA YA KUJIHUSISHA NA SHUGHULI ZISIZO HALALI AMBAZO ZINAKWENDA KINYUME NA SHERIA NA TARATIBU ZA NCHI, BALI WAFANYE KAZI HALALI, LAKINI PIA ANAENDELEA KUWAOMBA WANANCHI KUTOA USHIRIKIANO KWA JESHI LA POLISI ILI LIWEZA KUDHIBITI UHALIFU KATIKA MKOA WETU WA MWANZA.

IMETOLEWA NA:
DCP: AHMED MSANGI

KAMANDA WA POLISI (M) MWANZA

MAANDALIZI YA AIRTEL RISING STARS CLINIC YAKAMILIKA.

Afisa Uhusiano Airtel Tanzania Jane Matinde akizungumza na waandishi wa habari juu ya kuanza kwa kliniki ya mpira wa miguu ya Airtel Rising Stars inayoshirikisha wachezaji nyota 65 waliochaguliwa kutoka katika msimu wa  sita wa michuano hiyo, cliniki ya mafunzo inategemea kuanza wiki ijayo jijini Dar es Salaam. Kulia ni Mwenyekiti wa maendeleo wa soka la vijana Ayoub Nyenzi.
Kocha wa timu chini ya miaka 17 Oscar Milambo akizungumza na waandishi wa habari wakati wa kutangaza kuanza kwa kliniki ya soka ya Airtel Rising Stars inayoshirikisha wachezaji nyota 65 waliochaguliwa kutoka katika msimu wa sita wa michuano hiyo. Kulia ni Mwenyekiti wa maendeleo wa soka la vijana Ayoub Nyenzi, na wa pili kulia ni Mkurugenzi wa Ufundi TFF Salum Madadi na kushoto Afisa Uhusiano Airtel Tanzania Jane Matinde.
Mkurugenzi wa Ufundi TFF Salum Madadi akiongea na waandishi wa habari wakati wa kutangaza kuanza kwa kliniki ya Airtel Rising Stars wiki ijayo jijini Dar es Salaam, kliniki hiyo itashirikisha wachezaji nyota 65 waliochaguliwa kutoka katika msimu wa  sita wa michuano hiyo. Kulia ni kocha wa timu ya taifa ya vijana Oscar Milambo, wa pili kulia mwenyekiti wa maendeleo wa soka la vijana Ayoub Nyenzi na Afisa Uhusiano Airtel Tanzania Jane Matinde.

Maandalizi ya Airtel Rising Stars clinic yakamilika

Dar es Salaam, Jumatano 4 Januari 2017,Kliniki ya soka ya Airtel Rising Stars iyokuwa ikisubiriwa kwa hamu kubwa inatarajiwa kuanza Jumatatu, Januari 16 kwenye uwanja wa Karume huku wavulana 40 na wasichana 25 waliofanya vyema kwenye michuano ya vijana chini ya umri wa miaka 17 ya Airtel Rising Stars 2016 wakishiriki. Kufanyika kwa kliniki hiyo kutakuwa ni hitimisho ya michuano ya Airtel Rising Stars msimu wa sita.

Kliniki hiyo itakuwa ya siku sita na itaendeshwa na makocha wa timu ya soka ya taifa Oscar Milambo akisaidiwa na Kim Paulsen kwa wavulana huku wasichana wakifundishwa na kocha mkuu wa Kili Queens Sebastian Nkoma.

Akizungumzia maandalizi ya kliniki hiyo, Mwenyekiti wa Maendeleo ya soka la vijana kutoka Shirikisho la Mpira wa miguu Tanzania (TFF), Nyenzi Ayoub alisema “kliniki hiyo itatoa fursa kwa vijana kujifunza mbinu mpya za mpira, na kupata mafunzo kutoka kwa makocha wazoefu ili  kuongezewa vipaji vyao. ‘Sisi TFF tumefanya maandalizi yote ya kliniki na tumeichukua kwa uzito wa hali ya juu kwa kuwa ndio njia sahihi ya kupata wachezaji wa timu zetu za taifa, Serengeti Boys na Taifa Queens’, alisema Ayoub.

Tunaamini ya kwamba kliniki haitakuwa na mafanikio kwa wachezaji tu bali na timu zetu kupata wachezaji walio bora. Tumekuwa tukishuhudia wachezaji wazuri wenye vipaji kwenye kila msimu wa Airtel Rising Stars. Nachukua nafasi hii kuzishauri klabu zetu za mpira wa miguu kujitokeza kuangalia wachezaji wakati wa siku sita za kliniki hii ya Airtel Rising Stars, aliongeza Ayoub.

Kwa upande wake, kocha mkuu wa timu ya Taifa ya vijana chini wa umri wa miaka 17 Oscar Milambo alisema, ‘Wachezaji watafundishwa nidhamu ya mpira, ndani na nje ya uwanja, jinsi kumiliki mpira mbele ya mchezaji wa timu pinzani, kutoa pasi za uhakika pamoja na mafunzo ya nadharia. Sambamba na hayo wachezaji pia watakuwa na fursa ya kukutana na wenzao na hii itakuwa na hamasa kwao kwani wengi wao itakuwa mara ya kwanza kupata mafunzo kutoka kwa makocha. Milambo aliongeza kuwa vijana hao watafundishwa jinsi mchezaji anavyotakiwa kujitunza kwa manufaa ya kuendelea kutunza kipaji chake.

Akizungumza juu ya kliniki hiyo,  Afisa Uhusiano Airtel Tanzania Jane Matinde alisema michuano ya Airtel Rising Stars 2016 imekuwa na mafanikio makubwa na kuwa kufanyika kwa kliniki kutahitimisha Airtel Rising Stars msimu wa sita na kufungua pazia kwa maandalizi ya Airtel Rising Stars msimu wa saba. Michuano ya Airtel Rising Stars mwaka 2016 tuliunganisha na promosheni ya kampuni ya Airtel ya ‘Airtel Fursa’ ambayo ni maalum kwa kuwawezesha vijana kufanikisha malengo yao.

Matinde aliongeza kuwa Airtel inajivunia kuwa sehemu ya mradi huu wa kukuza vipaji vya soka kwani imesaidia kubadilisha soka la Tanzania. Airtel Rising Stars inalenga kutafuta vipaji chipukuzi kuanzia ngazi ya chini mpaka ngazi ya Taifa, kampeni yetu ya Airtel Fursa inalenga kuwainua vijana na kuwawezesha kufikia ndoto zao inaenda sambamba na program hii ya Airtel Rising Stars na tunajisikia furaha kuendelea kuwafikia vijana katika Nyanja mbalimbali aliongeza Matinde.

Wachezaji zaidi ya 1000 wavulana na wasichana walishiriki kwenye michuano ya Airtel Rising Stars 2016 kutoka mikoa ya Mwanza, Morogoro, Mbeya, Arusha, Kinondoni, Ilala, Temeke,Lindi na Zanzibar.

Wednesday, January 4, 2017

TANZIA: ANNA SENKORO, MWANAMKE WA KWANZA KUGOMBEA URAIS TANZANIA (2005), AFARIKI DUNIA.


Aliyekuwa mgombea urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania mwanamke wa kwanza hapa nchini (Uchaguzi 2005) kupitia chama cha APPT-Maendeleo, Dr. Anna Claudia Senkoro ameaga dunia.

Inadaiwa aliugua ghafla usiku wa kuamkia leo na amefariki baada ya kukimbizwa hospitali asubuhi ya leo.

Msiba upo nyumbani kwake, Tabata Segerea jijini Dar.

Taarifa zaidi zitafuatia...

====
Matokeo ya Urais 2005)

Jakaya Kikwete (CCM)
9,123,952
80.28%

Ibrahim Lipumba (CUF)
1,327,125
11.68%

Freeman Mbowe (CHADEMA)
668,756
5.88%

Augustine Mrema (TLP)
84,901
0.75%

Sengondo Mvungi (NCCR-Mageuzi)
55,819
0.49%

Christopher Mtikila (DP)
31,083
0.27%

Emmanuel Makaidi (NLD)
21,574
0.19%
Dr_Anna_Claudia_Senkoro.jpg

Anna Senkoro (PPT-Maendeleo)
18,783
0.17%

Leonard Shayo (MAKINI)
17,070
0.15%

Paul Kyara (SAU)
16,414
0.14% 


Bwana Ametoa Bwana ametwa

MWENYEKITI TUME YA UCHAGUZI NCHINI GAMBIA AMEKIMBIA NCHI AKIHOFIA USALAMA WAKE.


Mwenyekiti wa Tume ya Uchaguzi nchini Gambia amekimbia nchi akihofiwa usalama wake.
Familia na watu wa karibu na Alieu Momar Njai, wamesema Mwenyekiti wa Tume ya Uchaguzi Gambia amekimbia nchi baada ya kutishiwa maisha kwa kumtangaza Adama Barrow mshindi wa uchaguzi wa Disemba Mosi mwaka uliomalizika 2016. 
Hata hivyo wamesema Momar Njai hakutoa maelezo zaidi kuhusu ni nani aliyemtishia maisha na ni wapi amekimbilia

MSAKO WA WEZI WA UMEME SASA WAHAMIA JIJINI MWANZA. MMOJA ANASWA.


Shirika la umeme nchini(TANESCO) mkoa wa Mwanza limetakiwa kuimarisha ukaguzi wa mita ambazo hazilipiwi umeme ili kubaini watu wanaojihusha na wizi wa nishati ya umeme kwa lengo la kudhibiti vitendo hivyo ambavyo vimeshamiri jijini  mwanza.

Msako dhidi ya wezi wa nishati ya umeme ukiwa umebisha hodi katika nyumba moja ya makazi na biashara iliyoko mtaa wa rufiji jijini mwanza.

Msako umefanyika kwenye nyumba moja mkoani hapa baada ya mmiliki wake Greshen Magana kutoa taarifa kwa maafisa wa shirika la umeme nchini (TANESCO) juu ya kuwepo kwa wizi wa umeme unaofanywa na mtu aliyemkabidhi kuwa msimamizi wa  nyumba yake iliyo na makazi pamoja na biashara iliyoko eneo la rufiji jijini Mwanza.

Lakini Magana amewezaje kubaini wizi huo ilhali haishi kwenye nyumba hiyo?na vipi juu ya Matokeo ya ukaguzi ulioongozwa na Afisa usalama wa TANESCO mkoa Mwanza John Chilale...! BOFYA PLAY KUSIKILIZA TAARIFA HII. 

Wizi wa umeme kwenye nyumba hiyo ya makazi na biashara iliyoko eneo la rufiji jijini mwanza unakadiriwa kulisababishia shirika la Umeme TANESCO makadirio ya hasara ya zaidi ya shilingi milllioni tatu tangu februari mwaka jana.

VIJANA MKOANI DODOMA WANUFAIKA NA MRADI WA AIRTEL FURSA.

Meneja mauzo Airtel mkoa wa Dodoma, Hendrick Bruno (kushoto) akiongea na Fikiri Chinji (kulia) anayejishughulisha na ufundi seremala  juu ya maendeleo na changamoto za biashara baada ya kuwezeshwa na Airtel kupitia mpango wake wa Airtel FURSA “Tunakuwezesha”, wakati Airtel ilipotembelea kwenye karakana yake katika Mtaa wa Ng’ong’ona manispa ya Dodoma ili kujionea maendeleo yake pamoja kupanga jinsi ya
kuboresha zaidi biashara yake.

 
Kampuni na Taasisi mbalimbali hapa nchini zimeaswa  kuiga mfano wa Kampuni ya simu za mkononi ya  Airtel Tanzania kwa kuwawezesha vijana mbalimbali  kujiajiri wenyewe kupitia   mradi wa Airtel Fursa,ili kupunguza tatizo la Ajira hapa nchini.
Hayo yamebainishwa na mmoja kati ya waliofaidika na mradi wa Airtel Fursa kijana mjasiriamali anayejihusisha na  fani ya ufundi seremala  Fikiri Chinji aishie katika kijiji cha Ng”ong”ona manispaa ya Dodoma wakati alipotembelewa na Airtel ili kutadhimini maendeleo yake.
Fikiri alisema wapo vijana wengi ambao wapo mtaani wakitafuta ajira na wengine wakikumbwa na changamoto za mitaji ili kuendesha biashara zao, program kama hii ya Airtel Fursa ni vyema ikafanywa na makampuni mengi ili kuinua uchumi wa vijana  jamii nan chi kwa ujumla
Mpaka sasa nawashukuru sana Airtel kwa kuniwezesha mtaji ambao umeweza kuinua biashara yangu, kupitia program hii nimeweza kutanua biashara yangu ya ufundi selemala na kuanzisha biashara ya welding. Sambamba na kutanua biashara pia nimeweza kuajiri vijana  saba na kuongeza vifaa vingine zaidi, nawashukuru Airtel kwa kunishika mkono.”
Meneja mauzo Airtel mkoa wa Dodoma, Hendrick Bruno (kulia) akishuhudia matumizi ya moja ya vifaa alivyowezeshwa kijana Fikiri Chinji anayejishughulisha na ufundi seremala kwa kupitia mpango wa Airtel FURSA “Tunakuwezesha” miezi tisa iliyopita, wakati Airtel ilipotembelea kwenye karakana yake katika Mtaa wa Ng’ong’ona manispaa ya Dodoma ili kujionea maendeleo yake pamoja kupanga jinsi ya kuboresha zaidi biashara yake.
 Akizungumza katika eneo hilo Afisa Airtel kanda ya kati, Hendrick  Werner amesema kijana Fikiri Chinji ameweza kupiga hatua kwa kuongeza vifaa vingine toka alipowezeshwa na Airtel Fursa, kukuza biashara pamoja na kutengeneza ajira kwa vijana wengine na  kuwataka vijana wengine kuiga mfano wa fikiri kwa  kuanzisha vikundi mbalimbali na kuwatafuta wadau  watakao wawezesha kupita program mbalimbali ikiwemo hii ya Airtel Fursa.
Airtel Fursa ni mradi wa kijamii wenye dhumuni la kuhamasisha vijana, kuwapa nafasi ya kujiendeleza kibiashara na ujuzi utakoawawezesha kuimarisha biashara zao. Pambana group ni kikundi kingine kilichonufaika na mradi wa Airtel Fursa Dodoma ambacho kina vijana zaidi ya 15.

TRUMP AMUONYA OBAMA DHIDI YA KUWAHAMISHA WAFUNGWA WA GUANTANAMO..

Rais mteule wa Marekani Donald Trump amemuonya rais anayeondoka wa nchi hiyo Barack Obama juu ya kuwahamisha wafungwa wa jela ya Guantanamo iliyoko nchini Cuba.
Trump ameandika katika ukurasa wake wa mtandao wa kijamii wa Twitter  kuwa:  "Hakuna kuwahamisha wafungwa zaidi wa Gitmo, hawa ni watu hatari ambao hawafai kuachwa warejee katika uwanja wa mapambano."  

Mwezi uliopita, Josh Earnest, msemaji wa Ikulu ya White House ya Marekani alisema kuwa, serikali itafanya uhamisho wa mwisho wa wafungwa Guantanamo kabla ya kuondoka madarakani Rais Obama Januari 20. Iliarifiwa kuwa wafungwa hao watakabidhiwa serikali za Italia, Oman, Saudi Arabia na Imarati.
Jela ya Guantanamo iliyoko Cuba.
Mwezi Agosti mwaka uliopita, Wizara ya Ulinzi ya Marekani (Pentagon) iliwahamisha wafungwa 15 wa jela ya kutisha ya Guantanamo na kuwapeleka katika Umoja wa Falme za Kiarabu (UAE), ukiwa ni uhamisho mkubwa zaidi wa wafungwa hao kufanywa na utawala wa Rais Barack Obama wa Marekani.

Mara kwa mara shirika la kutetea haki za binadamu la Amnesty International limekuwa likikosoa vikali mienendo mibaya ya Marekani dhidi ya wafungwa wa jela hiyo na kusisitiza kuwa,  kuwanyima huduma za lazima kama matibabu wafungwa wa Gitmo, kunadhihirisha ni kwa kiasi gani serikali ya Washington isivyoheshimu mikataba ya kimataifa. Aidha Kamati ya Umoja wa Mataifa ya Kupiga Vita Utesaji huko nyuma iliilaani Marekani kwa kukataa kuchunguza vitendo vya utesaji na unyanyasaji unaofanyiwa washukiwa wa ugaidi katika jela ya Jeshi la Marekani ya Guantanamo Bay.
Donald Trump (kulia) na Barack Obama.
Rais Barack Obama wa Marekani Januari mwaka 2009 aliahidi baada ya kushinda uchaguzi kuwa katika muda wa mwaka mmoja angeifunga jela ya Guantanamo, ahadi ambayo ameshindwa kuitekeleza hadi sasa ambapo anaondoka madarakani.