Awali wakati wa mkutano mkuu wa Chama hicho Mwenyekiti aliyemaliza muda wake Jackison Songola aliwashukuru wajumbe 34 na kuomba kuwachagua viongozi wengine wa kuendeleza mpira kwa kuzingati wao ndo wanayo dhamana ya kuchagua viongozi wapya kupitia kura zao hivyo kutegemewa na wadau wa soka kuwapatia watu watakaoendeleza mazuri na kuacha mabaya.
“Viongozi watakaochaguliwa kushika nyadhifa za kuongoza MZFA ni vyema wakashirikiana na wadau mbalimbali pamoja na viongozi tuliomaliza muda wetu kuchukua mazuri tuliyoyaacha ya kuendeleza mpira wa Mkoa wa Mwanza na kuacha yale mabaya ambayo yataonekana kuwa hayana tija katika kuendeleza soka la Mwanza,”alisisitiza Songola.
Naye Mgeni rasmi wa mkutano mkuu huo, Mbunge wa Jimbo la Nyamagana, Stanslaus Mabula (CCM) akifungua mkutano aliwahasa wajumbe wa MZFA kutafakari soka la Mkoa huo ambalo limekuwa likienda mlama kwa kipindi cha miaka 10 iliyopita hivyo kuwa na wajibu wa kuchagua viongozi watakaoguswa na kuendeleza kwa kasi mpira wa miguu.
“Huu si wakati wa porojo, majungu na fitina ni wakati mhimu kwa wajumbe kutumia nafasi yenu ya kuwawakilisha wadau wengine kuchagua viongozi wazuri na wenye nia ya dhati ukizingatia unaungwa mkono na mamia ya wadau mbalimbali hivyo watumie fursa hiyo kutowaangusha wadau wa soka na viongozi mtakaopata nafasi muwendeleze mpira,”alisema.
Akitangaza matokeo ya uchaguzi huo juzi katika ukumbi wa Chama Kikuu cha Ushirika Nyanza (NCU 1984 Ltd) mwenyekiti wa Kamati ya uchaguzi huo Wakili Anderw Innocent alisema kwamba wajumbe halali wa uchaguzi walikuwa 34 kwa mujibu wa Katiba ya MZFA na walipiga kura kwa mujibu wa taratibu na kanuni na kuwepo wawakilishi wa TFF kufatilia uchaguzi huo.
Innocent aliwataja washindi wa nafasi zote na viongozi wapya wa MZFA na kura zao kwenye mabano nafasi ya Mwenyekiti Vedastus Lufano (20) na Israel Mtambalike (14) hakuna kura iliyoharibika, nafasi ya Makamu Mwenyekiti mgombea mmoja Domity Chisena alishinda kwa kura 22 huku kura za hapana 8 na zilizoharibika 4.
Alimtangaza Katibu wa MZFA kuwa ni Leonard Charles (18), Gribert John “Dady” (16), Katibu Msaidizi mgombea alikuwa mmoja Khalid Bitebo alipata kura 14 za hapana 13 na saba ziliharibika hivyo hakushinda nafasi hiyo, nafasi ya Mweka Hazina ni Elastus Mayalla (22), alimshinda Bob Butambala (11) moja iliharibika, Mwakilishi wa Vilabu ni Kevin Patrick (24) na nane za hapana.
Wakili Inoocent aliwataja washindi wengine kuwa ni Mwakilishi wa mkutano taifa wa Shirikisho la Mpira wa Miguu nchini (TFF) aliyeshinda ni Ephraim Majinge (19) Arim Allbah (16) na mchezaji wa zamani wa Yanga African Aron Nyanda akiambulia kura moja tu huku wajumbe wa Kamati tendaji akiwataja ni Juma Mokili(19), Osca Kapinga (24) na Edwin Hansi (11).
Mwenyekiti mpya wa MZFA Vedastus Lufano akitoa shukurani baada ya uchaguzi. |
Sehemu ya wajumbe 34 waliokusanyika wakiwa na dhamana ya kuchagua viongozi wapya kupitia kura zao. |
Tupe maoni yako
0 comments:
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.