ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

Saturday, July 16, 2011

MWANAUCHUMI....

Mafuta ya kibaba ....

CHEREKO CHEREKO YUSUPH KIKWETE APATA JIKO.

Maharusi katika picha ya pamoja na Mh. Rais Kikwete na mama Salma.

Bwana harusi Yusuph kikwete akifungishwa ndoa na Sheikh.

Eee Swahibaaaa upoooo!!! Rais JK akisalimiana na Mh. Mudhihir Mudhihir walipokutana katika sherehe hizo.

Mama Salma na wamama wa viongozi wengine shereheni.

Sheik akitoa mawaidha.

Rais Jakaya Kikwete na Makamu wake Dkt. Mohamed Gharib Bilal wakiongozana ktk uwanja wa ikulu ndogo bagamoyo wakati walipofika kuhudhuria sherehe ya ndoa ya mdogo wake rais Kikwete yusuph kikwete iliyofanyika katika uwanja huo na kuhudhuriwa na wageni mbalimbali na viongozi.

Picha zote na Muhidin Sufiani.

KIKAO CHA MKUU WA MKOA UONGOZI WA JIJI PAMOJA NA WAFANYABIASHARA WAKUBWA NA WAMACHINGA -16/07/2011

Kikao cha mkuu wa mkoa, uongozi wa jiji pamoja na wafanyabiashara wakubwa na wadogo kimefanyika leo katika ukumbi wa ofisi za jiji mkoani Mwanza.

Suala kubwa lililojadiliwa ndani ya kikao hicho ni vurugu za wamachinga zilizotokea hivi karibuni na kusababisha watu kadhaa kujeruhiwa, upotevu wa mali na hasara ya mapato kwa serikali kwani kwa siku nzima hakuna biashara iliyofunguliwa, hivyo kikao hicho kilikaa kujadili nini chanzo na ufumbuzi.

Huku akitolea mfano moja ya taarifa iliyotoka katika gazeti la Mzawa ikieleza kiini cha vurugu hizo na kuwataja Mh. Wenje (mbunge) na Mh. Manyerere (Meya wa jiji) kuwa ndiyo waliochochea vurugu hizo baada ya kutajwa na mwenyekiti wa kamati ya mipango miji na Mazingira ya Halmashauri ya jiji la Mwanza Bw. Henry Matata (Diwani CHADEMA), Mfanyabiashara Mohamed Msukuma amesikitishwa sana na kitendo cha wanasiasa kuendekeza propaganda kwa maslahi yao na kutaka uchunguzi ufanyike na watakaobainika hatua kali za kisheria zichukuliwe juu yao.

Kwa mujibu wa gazeti hilo, katika mahojiano maalum Bw. Matata amenukuliwa akiwaonya baadhi ya wanasiasa waliochochea vurugu hizo kwa maslahi yao binafsi nakutaka wakamatwe na kufikishwa mbele ya vyombo vya sheria ili kukomesha vurugu za mara kwa mara zinaziofanywa na wafanyabiashara wadogo wadogo jijini hapa. Pia kiongozi huyo ameshangazwa na namna ya vyombo vya dola vinavoshindwa kuwachukulia hatua baadhi ya wanasiasa ambao wamekuwa chanzo cha uvunjifu wa amani kila kukicha. Amewalaumu viongozi hao kwa kuiyumbisha Halmashauri ya jiji kwa wao kugeuka kuwa watoa idhini na vibali bila kuzingatia kanuni, taratibu na sheria zilizowekwa.

Ndani ya kikao hicho Bw. Matata alithibitisha kauli yake kwa kusema kuwa "Dawa ya ugonjwa ni kujua tatizo nami nipo hapa kwaajili ya Wananchi na siyo marafiki toka chama changu, ni ukweli ulio wazi Meya wa jiji na Mbunge wanapaswa kuheshimu maamuzi sahihi yanayoafikiwa vikaoni kwa ajili ya maslahi ya jiji la Mwanza badala ya kusaka umaarufu, Meya na Mbunge wanapaswa kuacha kuingilia mambo kwa kujifanya wao kuwa watendaji wakati sheria zipo"

Akijibu hoja na shutuma dhidi ya jiji kwa upande wake mkurugenzi wa jiji Bw. Wilson Kabwe amesema kuwa siyo kwamba wamachinga hawajapewa sehemu kwaajili ya kufanya biashara bali kuna maeneo rasmi yaliyoruhusiwa kwa wao kufanya biashara tena kwa muda ulioafikiwa na si eneo hilo la msikiti lililoleta vurugu kwa wachache kulivamia, ambalo kimsingi linahitajika kuwa wazi kwaajili ya wanaotoka na kuingia ibadani.

Amani hailindwi bali amani hujengwa na kutunzwa, matokeo ya wamachinga ni Indiketa tu za mabaya yanayokuja hivyo tusipojipanga basi tumekwisha! Tutakuja kuteketea wote!

Watu wa daladala, wamachinga, pikipiki na wengine wote, wako mjini kwa haki tatizo ni kutozingatia sheria nao watumishi wa serikali na wananchi wametetereka katika kuzisimamia sheria, hilo limebainika ndani ya kikao hicho hii leo.

Viongozi wa jiji washirikiane na viongozi wa wamachinga kwa taarifa, nchi ya China imeweza kukabiliana na suala kama hili mara baada ya kuwashirikisha wadau husika kwa taratibu na kanuni.

Kwa kujifunza mapungufu yaliyotokea kwa utaratibu na ujenzi wa MACHINGA COMPLEX DAR, tayari halmashauri ya jiji la Mwanza imepanga kujenga soko maalum katikati ya jiji kwa ajili ya wamachinga na wafanyabiashara wengine yaani 'ONE TRADE CENTRE' litakalojumuisha biashara aina zote.

Sambamba na wamachinga hao kuamriwa kutoka maeneo wasiyo ruhusiwa, pia imegundulika kuwa machafuko hayo ya mara kwa mara yamesababishwa na migogoro ya kiuongozi baina ya viongozi waliopo ndani ya Shirika la wamachinga Mwanza waliojitenga ambao nao wana uongozi wao uliotoa maamuzi ya kugawa maeneo ya biashara bila kuzingatia kanuni zilizowekwa ikiwa ni pamoja na ugawaji wa eneo hilo lililoleta vurugu.

Mkuu wa mkoa amewaagiza viongozi hao kuitisha mkutano haraka iwezekanavyo utakao husisha pande zote wakubaliane kuja na maamuzi ya pamoja yatakayowasilishwa kwenye ofisi ya mkuu wa mkoa.

Friday, July 15, 2011

HOT ISSUE KANDA YA ZIWA HII HAPA!!...!!!

TUKIO KUFANYIKA NDANI YA MV UMOJA
hUU nDIyO mPAngO mzIMA!!...

MAADHIMISHO YA MIAKA 50 YA UHURU WA TANGANYIKA MJINI MAGU

Bi Winfrida Chaukole akimuonesha Mkuu wa Mkoa wa Mwanza Abbas Kandoro, vifaa vya asili ambavyo vilikuwa vikitumiwa tangu enzi na wazazi wa wazee waasisi wa taifa letu kulia kwake ni Mwenyekiti wa CCM mkoa wa MwanzaBw. Clement Mabina.

Muziki enzi za Mwalimu.

Kazi nyingine za mikono kwenye mabanda mbalimbali maonyesho ya miaka 50 ya Uhuru wa Tanganyika.



Wakuu wakitoka eneo la mabanda ya maonyesho.

Baadhi ya wananchi walio hudhuria sherehe ya maadhimisho ya miaka 50 ya uhuru wa Tanganyika viwanja vya wazi wilayani Magu mkoani |Mwanza.

Ngoma za watu wa kabila la Sukuma kwenye maonyesho.

Mbina'

Ili kuboresha Elimu, jumla ya maabara 250 kujengwa kwenye kata mbalimbali mkoani Mwanza.

KISHA..
Baadae wakati maonyesho yakiendelea kongamano lafanyika wilayani humo, kwa upande wake mkuu wa mkoa wa Mwanza Abbas Kandoro ametoa wito kwa wenyeviti wa vijiji kusimamia vyema mali na miundo mbinu ya taifa kama vile mkongo wa mawasiliano ambapo kuna baadhi ya watu wameanza kuifukua na kuiba rasilimali zilizowekwa, vyuma vya madaraja ambapo baadhi ya watu wamekuwa waking'oa na kwenda kuuza kama vyuma chakavu pia alisisitiza suala la amani kama mhimili wa Taifa.

Kongamano hilo lililojumuisha wadau mbalimbali kama vile Wazee waliozaliwa siku ya Uhuru, Wataalam wa mashirika taasisi binafsi na za mashirika ya umma la kujadili, kutathmini na kuainisha maendeleo yaliyopatikana ndani ya miaka 50 tangu Uhuru wa Tanganyika .

Thursday, July 14, 2011

CHEREKO YA BINTI WA JACKOB ZUMA ILIVYOKUWA

Bi harusi (binti wa Zuma) na safari kuelekea kanisani kufungishwa ndoa.

Baba na Mwana katika dance la Harusi.


Hakika ni siku ya Furaha kwa kila mtu mwana familia kwani mambo yalipangwa yakapangika, bi harusi aliwasili kanisani kwa kutumia usafiri wa asili huku akisindikizwa na babaye mh.Rais Zuma.








Kisha mzee mzima akagonga snape ya tabasamu la ukweli akiwa na bintiye mara tu baada ya kufika eneo husika.



















Bwana na Bi harusi katika spesho' dance.

Pete za maharusi.

Drafti la meza kuu.

Si manjo-njo hayo na mikogo toka kwa kaka wa bi harusi na mkewe


Poz la karibu kaka wa bi harusi na mkewe.

PARTY YA LADY JAY DEE & MABINGWA WA KAGAME CASTLE CUP AT NYUMBANI LOUNGE.....!!!

Lapa linawakilisha Mwananchi wa kawaida, Mzalendo, Mlala hoi

Ilikuwa ni bonge la paty lililoandaliwa na Mwanamuziki wa kimataifa kutoka nchini Tanzania, Mwanadada Lady Jay Dee katika kuwapongeza Young Africans kunyakuwa kombe la Kagame na kulibakiza nchini.

Insu kamili tembelea www.ladyjaydee.blogspot.com

WAREMBO 15 WA MISS LAKE ZONE HAWAHAPA!!


Tracy Sospeter (20) Shinyanga

Lydia Mlimi (21) Mara

Glory Samwel (19) Shinyanga

Violeth Paschal (18) Mara

Sylvia Anatory (19) Kagera

Jaanath Abdul (21) Kagera

Irene Karugaba (21) Mwanza


Jackline Dismas (20) Shinyanga

Nani kati ya hawa kutawazwa Miss Lake Zone 2011? Shughuli kufanyika ndani ya meli ya Mv Umoja jumamosi ya tarehe 23 july 2011 jijini Mwanza.

Wednesday, July 13, 2011

KOFIA YA JESHI LA JWTZ YAFUNGA BARABARA

Leo jioni kwa mara nyingine, Jijini Mwanza kumetokea vurugu iliyopelekea wananchi kufunga barabara kuu ya Mwanza - Musoma kwa kutumia magogo, matawi na kuchoma matairi.

Kizuizi kikimaliziwa kuondoshwa barabarani.
Sekeseke limekuja tu mara baada ya askari wa Jeshi la Polisi waliokuwa katika Operesheni maalum inayoendeshwa ya kukamata pikipiki zenye makosa ya usalama wa barabarani, kumshambulia kwa kipigo askari wa Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ).

Askari huyo wa JWTZ (pichani aliyekifua wazi), ambaye jina lake halikuweza kufahamika mara moja, alikumbwa na mkasa huo, baada ya askari polisi kukamata pikipiki yake kwa lengo la kukagua uhalali wa kuendeshwa barabarani.

Hata hivyo, wakati askari polisi wakimhoji huku pikipiki nyingine takribani kumi na tano zikiwa zimekamatwa, askari huyo wa JWTZ alimgeukia mmoja wao na kumuamuru kuvua kofia aliyokuwa amevaa kwa madai kwamba, ni mali ya JWTZ.

Amri ya askari huyo wa JWTZ ilipingwa na askari polisi, ambao walifura kwa hasira nakuanza kumpa kipigo.

Kitendo hicho kiliwaudhi wananchi waliokuwa wakifuatilia tukio hilo wakidai kuonewa mara kwa mara na askari hao, ambao waliingilia kati na kuanza kuwashambulia askari hao kwa mawe.

Askari hao walipoona wamezidiwa, walikimbilia katika kituo cha polisi cha Market na wananchi hao waliendelea kuwashambulia kwa mawe.

Vurugu hizo zilizotokea katika eneo la Nyakato, zilisababisha Barabara ya Musoma kufungwa kwa muda hali iliyo sababisha hata msafara wa mkuu wa mkoa wa Mwanza Abbas Kandoro ulio kuwa ukitokea wilayani Magu kwenye maonyesho ya Saba saba nao pia kujisitiri kituoni hapo kuhofia usalama.

Kutokana na vurugu hizo, askari polisi wa Kikosi cha Kutuliza Ghasia (FFU) walifika na kuanza kuwatawanya wananchi hao kwa mabomu ya machozi huku wakikamata baadhi ya watuhumiwa walioonekana kuhusika na sakata hilo.

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mwanza, Simon Sirro, alithibitisha kuwapo operesheni ya kukamata pikipiki na kusisitiza kuwa zoezi litaendelea.