Katibu wa wilaya wa chama cha mapinduzi (CCM) wilaya ya Mufindi mkoani
Iringa Elirehema Nassar akiwa kwenye ziara ya kusherekea miaka 41 ya chama hicho kwa kufanya shughuli mbalimbali za kijamii
Na Fredy Mgunda,Mufindi.
CHAMA cha mapinduzi wilaya ya Mufindi mkoani
Iringa kimewataka viongozi wa halmashauri ya mji wa mafinga kufanyakazi kwa
weledi unaotakiwa kuwatumikia wananchi katika kutatua changamoto zinazozuia
kuleta maendeleo.
Hayo yamesemwa na katibu wa wilaya wa chama hicho
Elirehema Nassar wakati wa kusikiliza kero za wananchi walipokuwa wanasherekea
miaka 41 ya chama cha mapinduzi katika wilaya hiyo.
Nassar alisema kuwa mmezisikia kero za wananchi
lakini hapa mnajibu kisiasa na sio kitaalamu,sasa naomba nipatiwe majibu ya
kutosha na yenye ukweli na sio uongo mnaotudanya hapa.
“Hapa mnaleta siasa kwenye kero za wananchi
sitaki kusikia siasa kwenu watendaji mnaulizwa maswali ya msingi ambayo ni kero
za wananchi harafu mnajibu majibu mepesi hivyo haiwezekani” alisema Nassar
Nassar aliwataka viongozi wa serikali ya
halmashauri ya mji wa Mafinga kuacha kukaa maofisini na badala yake wanatakiwa
kwenda kutatua kero za wananchi waliokiweka madarakani chama cha mapinduzi
hivyo achene kufanya kazi kimazoea
“Wiki nzima unamkuta mfanyakazi wa serikali yeye
ni kupiga soga tu ofisi huku wananchi wanateseka na kero mbalimbali ambazo muda
mwingine hazina tija hivyo nikibaini hili nitalala mbele na huyo mtumishi”
alisema Nassar
Aidha Nassar amewataka wafanyakazi kubuni viradi
iliyofanyiwa utafiti na iwe inatija kwa wananchi kwa ajili ya kuleta maendeleo
ambayo yatadumu kwa miaka mingi.
“Mnaanzisha miradi ambayo haina tija mfano hapa
mmeanzia mradi wa soko la kuchoma nyama lakini hakuna mwananchi au
mfanyabiashara anajua jinsi gani ya kufanya biashara hiyo hivyo ni marufuku
kufanya miradi ambayo sio shirikishi kwa wananchi” alisema Nassar.
Pia Katibu huyo aliwataka watumishi hao wa
serikali kuhakikisha wanaenda kuwaelimisha wananchi kuhusu kodi wanazozita
zilipwe kuliko kumwambia mwananchi alipe kodi ambayo hajui inatokana na nini na
kwa nini analipa,lakini kukuwa na elimu ya kutosha hakutakuwa na migongano.
Sambamba na kuwaasa watumishi wa serikali Katibu
Nassar aliwaambia wananchi na mafinga na wanachama wa CCM wa Wilaya ya Mufindi
kuacha kujenga nyumba bila ya vibali vya serikali na mwisho wa siku mwananchi
anakuja kupata hasara pale anapoambia abomoe kwani ikon je ya mipango miji.
Nao wananchi na Wanaccm wa Wilaya walitoa kero
zao mbalimbli kwa watendaji wa Halmashauri ya Mji wa Mafinga,ambapo walizitaka
kero hizo kama uchafu wa Mazingira kwa baadhi ya maeneo,huduma mbovu katika
Hospitali ya Wilaya baadhi ya mitaa na kata moja kutokuwa na watendaji wa
kabisa.
Nyingine ni baadhi ya shule za mshingi kukosa
miundo mbinu kama matundu vyoo sanjali na upungufu wa vyumba vya madarasa, na
tatizo la upatikanaji wa mbolea za kilimo sambamba na dawa ya kuulia wadudu
waharibifu wanaokula mazao, na kuwataka watendaji hao kushugulikia kero
hizo haraka.