Baada ya tetesi kuvuma zilizo jaa ukweli kuhusiana na Mama wanamitindo
maarufu hapa Tanzania, Asya Idarous Khamsin kustaafu kuandaa jukwaa la ‘Lady In
Red, sasa leo 6/Feb/2018 Asya
amedhibitisha tetesi hizo kama
ifuatavyo.
Akizungumza na
wandishi wa habari katika ukumbi wa King Solomon Asya amesema kuwa Jukwaa la
Lady in Red mpaka sasa limedumu kwa muda wa miaka 15 likiwa chini yake. Pia alifafanua dhamira ya jukwaa la Lady in Red ambapo
alisema jukwaa hilo lilianzishwa kwa lengo la kukuza vipaji vipya kwenye Tasnia
ya Mitindo hapa Tanzania, ndio maana jukwaa asilimia kubwa huwa linapandisha
upcoming Designers maana ndio jukwaa lao la kujidaia.
Aidha aliongeza kuwa kustaafu kuandaa jukwaa la Lady in Red
haimaanishi kwamba ataachana na mambo ya ubunifu, “siwezi kuacha maana ndio
kazi inayo niweka mjini” alisisitiza Asya.
“Kilicho kikubwa nimeamua kutoa fursa kwa wanamitindo ambao wamekulia
kwenye jukwaa hilo”.
Kumbuka Lady in Red 2018 itafanyika 9/Feb/2018 katika ukumbi
wa King Solomon uliopo Dar es salaam- Namanga. Siku hiyo ndipo Asya atakapo
jivua kuandaa na kukabidhi Designers wengine jukwaa hilo usikose. Kwako mdau wa
mitindo endelea kuisambaza kwa walimwengu wote asante.
Tupe maoni yako
0 comments:
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.