ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

Saturday, March 5, 2016

WANAWAWAKE KUMILIKI ARDHI BADO NI NDOTO MAKETE MKOANI NJOMBE

Hii  ni Ofisi ya afisa Mtendaji Kata ya Iwawa, Kituo cha wakulima

Na Blogs za Mikoa Tanzania
Mila potofu zinazokandamiza wanawake zimeripotiwa kuendelea kushamiri katika baadhi ya mambo baada ya kutembelea katika maeneo tofauti tofauti ya wilaya ya Makete mkoani Njombe na kuzungumza na wakazi wa wilaya hiyo

Katika kijiji cha Iwawa wilaya ya Makete mkoani Njombe mwananchi aliyejitambulisha kwa jina la Jane Sanga amesema wanawake wengi wilayani hapo hawamiliki ardhi kutokana na mila potofu kuwa wamiliki wa ardhi ni wanaume pekee
"Kwa hapa Makete wanawake unaowaona wanamiliki ardhi kwa kiasi kikubwa unakuta ni mjane anaimiliki baada ya kufiwa na mumewe au unakuta mwanamke huyo ana uwezo wa kifedha na ameamua kukunua kipande chake cha ardhi na anakimiliki mwenyewe, hapo hakuna anayemuingilia, na hata wale wajane bado utakuta wanasumbuliwa na ndugu wa marehemu mumewe, kwa hiyo bado hali ni ngumu" amesema Jane
Hiki ni kipande kidogo sana ambacho analima Bi. Jane(Hayupo Pichani)

Mwingine aliyejitambulisha kwa jina la Grace Mbilinyi ambaye amekutwa na mwandishi wetu akiandaa shamba kwa ajili ya kilimo cha mazao ya chakula katika msimu ujao, amesema anamiliki shamba aliloachiwa na marehemu mumewe, licha ya kuendelea kusumbuliwa na ndugu wa marehemu wakidai kuwa mwanamke hataweza kuendeleza ardhi aliyoachiwa na mumewe

"Kwa kweli ni shida lakini Tutafanyaje sasa, mimi ni mama  wa nyumbani ambaye sana sana najishughulisha na ujasiriamali na kilimo kama hivi, kwa sasa ninamiliki hili shamba nililoachiwa na mume wangu kwa ajili ya kilimo, lakini vijimaneno vya ndugu vipo lakini bado sikati tamaa maana uwezo wa kumiliki ninao, na nitaiendeleza kwa kilimo" amesema Bi Grace

James Sigala ni mkazi wa Makete ambaye amekiri kuwepo kwa mila hizo zinazokandamiza wanawake hasa katika umiliki wa ardhi na kusema ingawa elimu inaendelea kutolewa na wanaharakati lakini bado kuna haja ya kuendelea kuitoa ili jamii ibadilike na kuamini kuwa hata wanawake wanaweza kimilikishwa ardhi kama wanaume
Afisa mtendaji kata ya Iwawa Bw. Festo Msigwa akiongea na mwandishi wa Blogs za Mikoa

Blog za Mikoa kupitia Njombe yetu  haikuishia hapo imebisha hodi katika ofisi za kata ya Iwawa iliyoko katika mji mdogo wa Iwawa (Makete Mjini) na kukutana na afisa Mtendaji Bw. Festo Msigwa ambaye amekiri kuwa bado umilikishwaji au umiliki wa ardhi kwa wanawake ni mdogo kutokana na mila potofu 

Amesema katika kata yake zipo kesi za ardhi zinazoletwa katika ofisi yake zikiwemo za wanawake wajane kupokonywa umiliki wa ardhi kutoka kwa ndugu wa mume wake kwa madai kuwa yeye kama mwanamke hawezi kumiliki wala kuiendeleza jambo ambalo limepingwa na kulaaniwa vikali na mtendaji huyo

"Wanawake wanaweza kwanza katika shughuli za shambani wao ndio wachakarikaji kuliko sisi wanaume, fikiria kwa mfano hawa wajane wanaokuja kwenye kesi za ardhi katika baraza la ardhi hapa, unakuta wakati wa uhai wa waume zao wao ndio walikuwa walimaji wazuri na watunzaji wakubwa wa mashamba, sasa kama aliweza toka mwanzoni iweje sasa washindwe" amesema Msigwa

Machi 8 mwaka huu ni kilele cha maadhimisho ya siku ya wanawake duniani ambapo kwa wilaya ya Makete maadhimisho yatafanyika katika kata ya Iwawa katika mji mdogo wa Iwawa

MAGAZETI YA LEO:- KUBENEA AKUTWA NA KESI YA KUJIBU. CUF YATAHADHARISHA SERIKALI ZANZIBAR. CCM WATOA MACHO UMEYA DAR.

Kubenea akutwa na kesi ya kujibu.CUF yahadharisha serikali Zanzibar. CCM watoana macho umeya Dar. Wingu latanda DART.

Maalim Seif kurejea nchini na msimamo kabambe. Wafanyabiashara za dawa za kulevya kufilisiwa. Sita wafa maji ziwa Victoria.

Friday, March 4, 2016

JIPU SEKTA YA ELIMU:- MKUU WA MKOA WA MWANZA AMEAMURU KUKAMATWA KWA WALIMU 8 WA SHULE YA SEKONDARI MIHAMA KWA KOSA LA KUJIHUSISHA NA MAPENZI NA WASICHANA WA KIKE SHULENI HAPO.

Walimu 8 akiwemo mwalimu mkuu wa shule ya sekondari Mihama katika Manispaa ya Ilemela mkoani Mwanza wanashikiliwa na Jeshi la Polisi kwa kosa la kujihusisha kimapenzi na wanafunzi shuleni hapo.

Moja ya athari zinazotajwa kujitokeza na hata kuathiri dira ya elimu kwa waafunzi shuleni hapo ni tukio la mmoja wa wanafunzi wa kike shuleni hapo aliyelazimika kuhama mkondo wa Sayansi na kwenda Art kufuatia manyanyaso aliyokuwa akifanyiwa na mmoja wa walimu hao aliyekuwa akimtaka kimapenzi
Hatua hiyo inakuja kufuatia agizo la Mkuu wa mkoa wa Mwanza Magesa Mulongo kuwataka wakamatwe kutokana na uchunguzi wa awali uliofanywa na hatimaye kubainika kuhusishwa na tuhuma hizo. BOFYA PLAY KUSIKILIZA.

Licha ya kutaja majina ya wahusika, Hamis Maulid ambaye ni Afisa Elimu mkoa wa Mwanza aliongeza kwa kusema kuwa wamefikia hatua hiyo baada ya tume iliyoundwa kuchunguza tuhuma hizo kubaini kuwa walimu hao walitenda kosa hilo. BOFYA PLAY KUSIKILIZA.


Mmoja wa watuhumiwa Joseph D. Malifedha ambaye ni Mkuu wa Shule hiyo ya Sekondari.
Baadhi ya maafisa wa idara mbalimbali zilizo husishwa kwenye uchunguzi huo kwa umakini wakinukuu baadhi ya vipengele muhimu wakati wa usomaji wa taarifa.
Sehemu ya kusanyiko hili imejumuisha waalimu wa shule hiyo waandishi wa habari pamoja na watumishi wa idara za elimu serikalini ndani ya mkoa wa Mwanza.
Maafisa toka idara ya Elimu, Takukuru, Majeshi, Dawati la Jinsia, Chama cha Walimu na wafanyakazi ni sehemu ya kamati.
Mkuu wa mkoa wa Mwanza Magesa Mulongo (kushoto aliyesimama meza kuu) akitoa maelekezo ya nini kifanyike kwa walimu hao kama hatua ya kwanza mara baada ya kukumbwa na tuhuma hiyo.
Jeshi la polisi liliwakamata mara moja watuhumiwa hao kwaajili ya hatua nyingine za kisheria.
Ufafanuzi toka TUKTA.
Baadhi ya wanafunzi wamehamishwa shuleni hapo mara baada ya kukubwa na kadhia hiyo, lakini jeh ni nini hatma ya wanafunzi walio kumbana na udhalimu huo na hata kuaathirika kisaikolojia? Mkuu wa mkoa wa Mwanza Magesa Mulongo ANAFUNGUKA ZAIDI.


Watuhumiwa mikononi mwa polisi.

Watuhumiwa mikononi mwa polisi.
Kikao cha maamuzi kilifanyika hapa.

FURAHIA WIKIENDI YAKO NA PROMOSHENI YA AIRTEL INTERNATIONAL OFA.

Furahia wikiendi yako na promosheni ya airtel international ofa
Airtel inakupa punguzo kila wikiendi kupiga simu za kimataifa kwenda  USA, CANADA, INDIA , CHINA, KENYA, SA, UGANDA, na nyingine nyingi tu kwa bei nafuuu sana.
Twanga kokote ufurahie maongezi na uwapendao

Airtel mtandao bomba kwa smartphone yako

BUNDUKI 34 ZA KIVITA NA ZA KIRAIA ZILIZOKUWA ZIKIMILIKIWA NA WANANCHI ZASALIMISHWA KWA JESHI LA POLISI JIJINI ARUSHA

 Kamanda Wa Polisi Mkoani Arusha Liberatus Sabas akionesha moja ya baadhi ya silaha zilizosalimishwa na wamiliki na  nyingine zilizotelekezwa porini.

Bunduki 34 za kivita na za kiraia zilizokuwa zikimilikiwa na wanavijiji wa Tarafa ya Sale Wilayani Ngorongoro Mkoani Arusha ,zimesalimishwa ikiwa ni hatua ya kutii agizo la kamati ya ulinzi na Usalama Mkoani humo, iliyotoa siku saba kwa wananchi wote wanaomiliki silaha kuzisalimisha .

Agizo hilo linafuatia kutokana na mfululizo Wa matukio ya mauaji ya watu katika eneo hilo ambao February 21,2016 pekee watu watatu wa Jamii ya wasonjo waliuwawa kwa kupigwa risasi na watu wanaosaidikiwa kuwa wafugaji Wa kimasai huko katika kitongoji cha Meje Kijiji cha Kisangiro Wilayani Ngorongoro,Kamanda Wa Polisi Mkoani Arusha Liberatus Sabas amesema baadhi ya silaha zilisalimishwa na wamiliki na  nyingine zilitelekezwa porini.

POMBE NA UKATILI WA KIJINSIA

Fahamu mambo megi kutoka kwa wadau wa TAMWA, wakikufahamisha kuhusu masuala ya pombe na ukatili wa kijinsia.

SERIKALI YAMPONGEZA BONDIA CHEKA

.
bondia cheka na NapeWaziri wa Habari, Mh. Nape Nnauye (kulia) akiangalia kwa makini mkanda wa ubingwa wa bondia Francis Cheka. Wengine wanaoshuhudia ni Bondia mwenye Francis Cheka, Rais wa Oganaizesheni ya ngumi za kulipwa nchini T.P.B.O Yassin Abdalla 'Ostadhi' na Promota wa Francis Cheka, Juma Ndambile

Serikali kupitia Waziri wa Habari, Utamaduni, Wasanii na Michezo, wamepongeza juhudi za wanamichezo wa Tanzania wanavyoiwakilisha vyema Tanzania hasa katika mambo mbalimbali ikiwemo Michezo kama alivyofanya Bondia Francis Cheka.

Akitoa pongezi hizo mapema leo, Waziri wa Habari, Mh. Nape Nnauye aliyetembelewa ofisini kwake na bondia huyo pamoja na viongozi wa soka akiwemo Rais wa chama cha Ngumi pamoja na Promota wa bondia huyo, Waziri Nape ameelezea kuwa kadri wanamichezo wanavyofanya vizuri ndiyo wanavyoendelea kuipa sifa kemkem nchi hivyo wataendelea kushirikiana nao.

Mbali na kumpongeza bondia, Francis Cheka, Waziri Nape pia alimpongeza mdogo wa bondia huyo Francis Cheka, Cosmas Cheka ambaye naye aliambatana na msafara huo ambapo katika pambano lake naye alishinda mkanda wa WBF, kwa pointi dhidi ya mpinzani wake.

Aidha, Waziri Nape alimkabidhi cheti cha shukrani bondia, Cheka kama ishara ya kutambua mchango wake huo na kuiletea heshima Taifa kwa ushindi wake.
Bondia, Francis Cheka katika pambano lake hilo, alipigana na Raia wa Serbi anayeishi Marekani, Bondia, Geard Ajetovic ambapo katika pambano lao hilo, lililofanyika jijini Dar es Salaam, Cheka alishinda kwa pointi.

Ubingwa huo alioshinda Bondia Francis Cheka, ni Ubingwa wa Mabara unaotambuliwa na Shirikisho la Ngumi Duniani (WBF).

Tazama MO tv, kuona habari hiyo hapa:
Imeandaliwa na Andrew Chale,Modewjiblog/MO tv
bondia chekaBondia Francis Cheka akizungumza na wanahabari mapema leo (hawapo pichani) wakati walipomtembelea Waziri wa Habari, Mh. Nape Nnauye ofisini kwake jijini Dar es Salaam. kushoto kwake ni Rais wa Oganaizesheni ya ngumi za kulipwa nchini T.P.B.O Yassin Abdalla 'Ostadhi'
bondiaWaziri wa Habari, Utamaduni, Wasanii na Michezo, Mh. Nape Nnauye (kulia) akisikiliza kwa makini wakati wa kupokea shukrani kutoka kwa bondia Francis Cheka (katikati) aliyekuwa akizungumza na wanahabari (hawapo pichani) mapema leo. kushoto ni Rais wa Oganaizesheni ya ngumi za kulipwa nchini T.P.B.O Yassin Abdalla 'Ostadhi'
bondia napeWaziri wa Habari, Nape akijaribisha kuvaa mkanda wa ubingwa wa Bondia Francis Cheka kama ishara ya kumfikishia na kuuvaa kwa niaba ya watanzania wote..
bondia cheka 1Waziri Nape (katikati) akimpa mkono wa pongezi bondia Cosmas Cheka ambaye ni mdogo wa bondia Francis Cheka ambaye naye alishinda katika pambano lake la WBF.
bondi cheka.."Hongera kwa ubingwa Francis Cheka".. Waziri Nape akimpa mkono wa hongera bondia Francis Cheka wakati wa pongezi hizo mapema leo Machi 4.2016
bondia Cheka4Waziri Nape akimkabidhi cheti cha shukrani bondia Francis Cheka kama ishara ya kupokea mchango wake hadi kuitangza na kuiletea heshima kubwa nchi ya Tanzania. (Picha zote na Andrew Chale, Modewjiblog).
Mwisho. Waziri Nape apiga ‘stop’ tiketi za TFF, ataka malipo ya kielekroniki uwanja wa Taifa
Waziri wa Habari, Utamaduni, Wasanii na Michezo, Mh. Nape Nnauye ametoa agizo rasmi juu ya matumizi ya tiketi za Kielekroniki michezoni kwa kulitaka Shirikisho la Soka la Tanzania (TFF) kuakikisha linatumia tiketi hizo kuanzia Machi 9.2016 na kuachana na tiketi za kawaida huku akibainisha kuwa wataendelea kulifuatilia suala hilo kwa ukaribu na hatua zaidi ilikuziba mianya ya udanganyifu.
Nape amebainishahayo muda huu wakati anazungumza na vyombo vya habari kuelezea suala la Michezo hapa nchini ikiwemo suala hilo la mfumo wa malipo kwa njia ya Kielekroniki ambapo awali Waziri Mkuu Kassim Majaliwa alitoa agizo la matumizi ya mfumo huo.
Akielezea suala hilo, amesema litaondoa ‘figisufigsu’ za mara kwa mara ambazo watu wamekuwa wakilalamikia mapato ikiwemo hayo ya Uwanja wa Taifa.
“Baada ya Machi 8 mwaka huu. Mechi zote zitakazochezwa uwanja wa Taifa, tiketi zote zitatumika ni zile za kieletroniki. Hii ni mara baada ya michezo yote mitatu iliyobaki ambayo TFF wanamalizia tiketi zao ambazo wamebazibakisha na zinaisha Machi 8. Safari hii tutafuatilia na kukagua wenyewe. Hatutakubali kuendelea kuvumilia hujuma katika hili.” Ameeleza Nape katika mkutano huo.
Tazama MO tv hapa kushuhudia habari hiyo:
Na Andrew Chale,modewjiblog
NapeWaziri wa Habari, Utamaduni, Wasanii na Michezo, Mh. Nape Nnauye (Kulia) akizungumza na mwanahabari (Hawapo pichani) wakati akitoa tamko hilo muda huu juu ya kuitaka TFF, kuakikisha inatumia mfumo wa malipo ya Kielekroniki kuanzia Machi 9 na kuendelea kwa michezo yote ndani ya Uwanja wa Taifa huku akielezea kuwa wataendelea kufuatilia ilikubaini udanganyifu zaidi katika suala la mapato la milangoni katika michezo yote. (Picha na Andrew Chale, Modewjiblog).

MKUU WA MAJESHI AONGOZA KUWAAGA MAOFISA MAJENERALI 16 WA JWTZ WALIOSTAAFU

Mnadhimu Mkuu mstaafu wa Jeshi la Wananchi Tanzania (JWTZ), Luteni Jenerali Samuel Ndomba (kwenye gari kushoto) na Mkuu wa Vikosi vya Kulinda Amani Umoja wa Mataifa, Luteni Jenerali mstaafu, Paul Ignas Meela wakitoa heshima katika hafla ya kuagwa iliyofanyika Viwanja vya Twalipo Mgulani Dar es Salaam leo mchana. Maofisa Majenerali 16 waliostaafu Utumishi Jeshini waliagwa.
Brigedia Jenerali mstaafu, Msangi (kulia mbele), akikagua gwaride maalumu waliloandaliwa maofisa hao wastafu wakati wakiagwa rasmi baada ya kumaliza utumishi wao jeshini.
Mkuu wa Jeshi la Kujenga Taifa (JKT), mstaafu Meja Jenerali, Raphael Muhuga, akikagua gwaride hilo.
Wanafamilia wa wastaafu hao wakiwa kwenye hafla hiyo ya kuagwa jamaa zao.
Ukaguaji gwaride rasmi ukiendelea.
Maofisa hao wastaafu wakiwa jukwaa kuu.
Hapa maofisa hao wakiwa wamesimama wakati gwaride likipita jukwaa kuu na kutoa heshima.
Mkuu wa Majeshi, Jenerali, Davis Mwamunyange (kushoto), akisalimiana na kumpongeza Mkuu wa Vikosi vya Kulinda Amani Umoja wa Mataifa, Luteni Jenerali mstaafu, Paul Ignas Meela katika hafla hiyo.
Askari wa JWTZ wakifuatia matukio mbalimbali kwenye 
hafla hiyo.
Mnadhimu Mkuu mstaafu wa Jeshi la Wananchi Tanzania (JWTZ), Luteni Jenerali Samuel Ndomba, akikagua gwaride hilo maalumu kwa ajili ya kuagwa.
Gwaride likipita mbele ya jukwaa kuu kutoa heshima.

Gwaride likipita mbele ya jukwaa kuu kutoa heshima.
Mkuu wa Majeshi, Jenerali, Davis Mwamunyange (kushoto), akisalimiana na Mnadhimu Mkuu wa Jeshi hilo mstaafu, Luteni Jenerali, Samuel Ndomba.
Wapiga picha wa magazeti wakiwa kazini kuchukua matukio mbalimbali.
Taswira ya jukwaa kuu katika hafla hiyo.
Wastaafu hao wakiwa katika picha ya pamoja na mkuu wa majeshi.
Mkuu wa majeshi, Davis Mwamunyange (katikati), akiwa katika picha ya pamoja na wakuu wa majeshi wastaafu. Kushoto Robert Mboma na George Waitara (kulia).
Mkuu wa majeshi akiwa katika picha ya pamoja na familia ya Mnadhimu Mkuu wa JWTZ, Luteni Jenerali, Samuel Ndomba.
Hapa ni furaha tupu kwa kustaafu utumishi ndani ya jeshi.
Askari wa JWTZ wakiwa imara wakati wa kuwaaga maofisa hao.
Mnadhimu Mkuu mstaafu wa Jeshi la Wananchi Tanzania (JWTZ), Luteni Jenerali Samuel Ndomba (kwenye gari kushoto) na Mkuu wa Vikosi vya Kulinda Amani Umoja wa Mataifa, Luteni Jenerali mstaafu, Paul Ignas Meela wakitoa heshima katika hafla ya kuagwa iliyofanyika Viwanja vya Twalipo Mgulani Dar es Salaam.
Hapa ni saluti wakati wakiwaaga wapiganaji wenzao.

Na Dotto Mwaibale

JESHI la Wananchi Tanzania (JWTZ), limewaaga Mameja generali, Luteni na Brigedia Generali 16, akiwemo, aliyekuwa Msaidizi wa Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi na Usalama, Luteni Generali Samwel Ndomba.

Tukio la kuwaaga majenerali hao ambao wamestaafu  utumisho wao jeshini limefanyika jijini Dar es Salaam leo katika viwanja Twalipo Mgulani saa tatu hadi saa tatu asubuhi ambapo liliambatana na gwaride maalumu la vikosi mbalimbali vya Anga, nchini kavu, majini pamoja na Jeshi la Kujenga Taifa (JKT).

Hafla hiyo ya kuwaaga Magenerali hao iliongozwa na Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi na Usalama (CDF), Davis Mwamunyange ambapo waaga hao ni wa vyeo mbalimbali vya Brigedia Generali waliokuwa nane, Meja Jenerali sita na Luteni wawili na kuhudhuliwa na viongozi mbalimbali na wastaafu wa jeshi hilo.

Majenerali hao kila mmoja alipata fursa ya kukagua gwaride kila alipowasili viwanjani hapo ambapo kati yao ni Luteni Generali walipata heshima ya pekee na kufanyiwa gwaride lililokuwa tofauti na wengine.

Majenerali hao ni Mnadhim Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi na Usalama JWTZ, Luteni Jenerali Samwel Ndomba ambaye pia aliwahi kuwa Mkuu wa Wilaya ya Ngara, Mkuu wa Utumishi katika jeshi hilo na Mkuu wa Mkoa wa Arusha.

Wengine ni Mkuu wa Tawi la Usalama na Utambuzi jeshini, Luteni Jeneral Paul Ignas ambaye pia aliwahi kuwa ni Mkuu wa Mjeshi ya kulinda amani Darfur nchini Sudani.

Kwa upande wa Mameja Jenerali ambao walipewa heshima na kukagua vikosi hivyo ni Mkuu wa Jeshi la Nchi kavu, Meja Jenerali Salum Kijuu, Mkuu wa Utumishi Jeshini, Meja Jenerali Vicent Mlitaba, Mkuu wa Jeshi la Anga, Meja Jenerali Joseph Kapwani, Mkuu wa Chuo cha Ukamanda na Unadhimu kilichopo Duruti mkoani Arusha Meja Jenerali Ezekiel Kiunga.

Wengine ni Mkuu wa Shirika la Mzinga mkoani Morogoro, Meja Jenerali Chalres Mzanila, Mkuu wa Jeshi la Kujenga Taifa (JKT), Meja Jenerali Raphael Mhunga.

Na wengine ambao ni Mabrigedia ni Mkuu wa Chuo cha Kijeshi cha Sayansi ya Tiba Lugalo, Brigedia Jenerali Dk.Luhindi Msangi , Mkuu Tawi la Ukaguzi jeshini ambaye pia aliwahi kuwa mkaguzi wa majeshi ya SADC, Brigedia Jenerali Emanuel Maganga.

Wengine ni Mkuu wa Tawi la Akiba, Brigedia Jenerali Agustino Gailanga ambaye pia aliwahi kuwa mpambe wa Rais mstaafu, Benjamin Mkapa, Mratibu wa Miradi ya Maendeleo Jeshini, Brigedia Jenerali Mrisho Abdallah , Mkuu wa Kikosi cha Ndege cha usafirishaji, Brigedia  Jenerali Ezra Ndimugwango.

Na wengine ni Kamanda wa Brigedi ya Tembo mkoani Songea, Brigedia Jenerali John Chacha, Mkurugenzi wa Mahusiano ya Kimataifa jeshini, Brigedia Jenerali Martini Mwankanye na Mkuu wa Shule ya 'Eflantria' mkoani Arusha, Brigedia Harodi Mzirai.

Akizungumza mara baada ya hafla hiyo Luteni Jenerali mstaafu Ndumba alifurahia hatua hiyoa na kubainisha kuwa kwa sasa wanaenda kuanza maisha mapya.