Bunduki 34 za kivita na za kiraia zilizokuwa zikimilikiwa na wanavijiji wa Tarafa ya Sale Wilayani Ngorongoro Mkoani Arusha ,zimesalimishwa ikiwa ni hatua ya kutii agizo la kamati ya ulinzi na Usalama Mkoani humo, iliyotoa siku saba kwa wananchi wote wanaomiliki silaha kuzisalimisha .
Agizo hilo linafuatia kutokana na mfululizo Wa matukio ya mauaji ya watu katika eneo hilo ambao February 21,2016 pekee watu watatu wa Jamii ya wasonjo waliuwawa kwa kupigwa risasi na watu wanaosaidikiwa kuwa wafugaji Wa kimasai huko katika kitongoji cha Meje Kijiji cha Kisangiro Wilayani Ngorongoro,Kamanda Wa Polisi Mkoani Arusha Liberatus Sabas amesema baadhi ya silaha zilisalimishwa na wamiliki na nyingine zilitelekezwa porini.
Tupe maoni yako
0 comments:
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.