ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

Friday, July 22, 2022

SERIKALI YAPIGA STOP SHUGHULI ZA KIBINADAMU KWENYE HIFADHI YA MSITU WA MITI LUNGUZA

 

Mkuu wa wilaya ya Muheza Halima Bulembo  kushoto akipokea wakati msaada wa vifaa vya ujenzi na vifaa tiba kwa baadhi ya taasisi na shule zilizopo jirani na shamba hilo vyenye thamani ya zaidi ya Milioni 10, kutoka kwa Mkuu wa hifadhi wa shamba la miti Lunguza Ellyneema Mwasalanga
Mkuu wa wilaya ya Muheza Halima Bulembo  kushoto akipokea wakati msaada wa vifaa vya ujenzi na vifaa tiba kwa baadhi ya taasisi na shule zilizopo jirani na shamba hilo vyenye thamani ya zaidi ya Milioni 10, kutoka kwa Mkuu wa hifadhi wa shamba la miti Lunguza Ellyneema Mwasalanga
Mkuu wa wilaya ya Muheza Halima Bulembo  kulia akiwa na  Mkuu wa hifadhi wa shamba la miti Lunguza Ellyneema Mwasalanga katikati wakikabidhi msaada huo
MKUU wa wilaya ya Muheza Halima Bulembo katika akiwa na  
Mkuu wa hifadhi wa shamba la miti Lunguza Ellyneema Mwasalanga kulia wakiwa kwenye madawati hayo mara baada ya kukabidhi

Na Oscar Assenga,Muheza

SERIKALI wilayani Muheza Mkoani Tanga imepiga marufuku shughuli za kibinadamu ikiwemo ukataji wa miti katika maeneo ya Hifadhi ya Msitu wa Miti wa Lunguza huku ikieleza haitasita kuwachukulia hatua watakaokaidi.

 

Marufuku hiyo ilitangazwa na Mkuu wa wilaya ya Muheza Halima Bulembo  wakati akipokea msaada wa vifaa vya ujenzi na vifaa tiba kwa baadhi ya taasisi na shule zilizopo jirani na shamba hilo vyenye thamani ya zaidi ya Milioni 10.

 

Akitangaza mkakati huo baada ya kupokea vifaa hivyo alisema kuwa ukataji miti hovyo, uchimbaji wa madini ikiwemo na uchomaji misitu vinasababisha madhara ya kimazingira ikiwemo uhaba wa mvua,hivyo ni muhimu Wananchi wakahifadhi mazingira ya msitu huo .

 

Aliwataka wananchi wanaoishi jirani na msitu huu kushirikiana katika kuhakikisha kunakuwa na usimamizi na matumizi endelevu ya raslimali za misitu ili uweze kuwa endelevu  ikiwemo waweze kunufaika na msitu huu

 

Awali Mkuu wa hifadhi wa shamba la miti Lunguza Ellyneema Mwasalanga  amesema kuwa wametoa msaada huo ikiwa ni sehemu ya kurudisha Kwa jamii katika kusaidia miradi mbalimbali ya maendeleo

 

Alisema kwamba wameweza kutoa msaada wa saruji mifuko 240,viti na meza 40,vifaa tiba 12 vyenye thamani ya sh Mil 2.5 kwa ajili ya zahanati ya kwafungo ambavyo vyote vina thamani ya sh Mil 10.1.

 

Alisema faida nyengine ambazo wanazipata wananchi ni kilimo mseto (taungya) ambapo wananchi huruhusiwa kulima katika maeneo yaliyo andaliwa kwa ajili ya kupandwa au yaliyopandwa yenye miti midogo kwa utaratibu maalumu.

 

Aidha alisema sambamba na hayo wananchi wananufaika na malighafi za kujengea (nguzo,fito) ajira katika maeneo mbalimbali ikiwemo kazi za kuhudumia shamba,uvunaji ,usafirishaji, uchakataji wa malighafi viwandani na kukua kwa biashara mbalimbali katika maeneo ya Muheza.

AMREF WAENDESHA MAFUNZO KWA WAKUFUNZI WA MRADI WA WAWE MKOANI IRINGA

  

Mmoja ya wakufunzi kutoka Shirika la Amref Health Africa akiendelea kutoa elimu ya usimamizi na uratibu kwa wakufunzi wa vikundi vya kijamii na vya wajasiriamali kutoka vijiji 67 vya mradi wa WAWE katika kata za mradi
Mmoja ya wakufunzi kutoka Benk ya NMB akiendelea kutoa elimu ya usimamizi na uratibu kwa wakufunzi wa vikundi vya kijamii na vya wajasiriamali kutoka vijiji 67 vya mradi wa WAWE katika kata za mradi
Mmoja ya wa washiriki wa mafunzo ya usimamizi wa fedha akiendelea kupata elimu ya usimamizi na uratibu wa vikundi vya kijamii na vya wajasiriamali kutoka vijiji 67 vya mradi wa WAWE katika kata za mradi
Mmoja ya wa washiriki wa mafunzo ya usimamizi wa fedha akiendelea kupata elimu ya usimamizi na uratibu wa vikundi vya kijamii na vya wajasiriamali kutoka vijiji 67 vya mradi wa WAWE katika kata za mradi
Baadhi ya wa washiriki wa mafunzo ya usimamizi wa fedha wakiendelea kupata elimu ya usimamizi na uratibu wa vikundi vya kijamii na vya wajasiriamali kutoka vijiji 67 vya mradi wa WAWE katika kata za mradi
Mmoja ya wakufunzi kutoka Shirika la Amref Health Africa akiendelea kutoa elimu ya usimamizi na uratibu kwa wakufunzi wa vikundi vya kijamii na vya wajasiriamali kutoka vijiji 67 vya mradi wa WAWE katika kata za mradi
Baadhi ya wa washiriki wa mafunzo ya usimamizi wa fedha wakiendelea kupata elimu ya usimamizi na uratibu wa vikundi vya kijamii na vya wajasiriamali kutoka vijiji 67 vya mradi wa WAWE katika kata za mradi

Na Fredy Mgunda,Iringa.

 
Shirika la Amref Health Africa linaendelea na utekelezaji wa miradi yake miwili, iliyopo Iringa ambako ni pamoja na Mradi wa usafi wa mazingira na uwezeshaji wanawake na mradi wa Maji na Maendeleo.

 Mradi kwa kushirikiana na vyombo vingine vya usimamizi na uratibu vinashiriki katika ufunguzi na uendeshaji wa semina ya siku tatu kwa wakufunzi wa vikundi vya kijamii na vya wajasiriamali kutoka vijiji 67 vya mradi wa WAWE katika kata za mradi. 

Semina hii inalenga kufundisha elimu ya usimamizi wa fedha na uongozi kwenye vikundi, uundaji wa umoja wa usimamizi wa vikundi kwenye vijiji vya mradi pamoja na kuandaa mpango kazi wa usimamizi wa vikundi na utoaji taarifa kwa kila mwezi.

Mradi wa usafi wa mazingira na uwezeshaji wanawake. (WAWE- Wash and Women Empowerment)- unaotekelezwa katika jamiii zinazolima chai na kahawa katika Halmashauri ya wilaya ya Mufindi na Kilolo. Mradi huu wa mwaka mmoja unafadhiliwa na Starbucks Foundation na kutekelezwa na shirika la Amref Health Africa. 

Mradi huo unalenga kuboresha afya na ustawi wa kiuchumi wa wanawake na vijana 87,500 katika jamii zinazolima kahawa na chai katika wilaya za Kilolo na Mufindi. Utekelezaji wa mradi huu utaondoa vikwazo vya elimu, afya bora, lishe endelevu na usafi wa vyoo na maji salama

WASIOENDELEZA MASHAMBA YA MKONGE KUNYANG'ANYWA

 

Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Bodi ya Mkonge Tanzania (TSB), Saddy Kambona


*****************

Muheza, Tanga
Serikali imesema watu waliopewa mashamba katika Shamba la Mkonge la Kibaranga (Kibaranga Sisal Estate) lililoko Muheza mkoani Tanga na hawajayaendeleza au wameyaendeleza kwa mazao mengine watanyang’anywa.

Shamba hilo lenye Hekta 5,600 ambalo linamilikiwa na Bodi ya Mkonge na kusimamiwa na Amcos ya Kibaranga baada ya serikali kulirudisha kutoka Halmashauri ya Wilaya ya Muheza ambao walionyesha kusua sua katika uendelezaji wa shamba hilo. 

Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Bodi ya Mkonge Tanzania (TSB), Saddy Kambona amesema hayo jana katika kikao na viongozi wa Chama cha Ushirika wa Mazao na Masoko (Amcos) cha Kibaranga na wa kijiji ambapo pamoja na mambo mengine wananchi walitaka kujua utaratibu wa kuendeleza maeneo hayo kwa ujenzi wa nyumba.

Hoja hiyo ilitolewa na Mwenyekiti wa Kibaranga Amcos, Paulo Haule ambaye alisema amepata maombi ya wananchi wananchi katika eneo hilo wakitaka kujenga makazi ndani na pembezoni mwa shamba hilo.

Akijibu hoja hiyo, Kambona alisema shamba hilo liligawiwa eka tatu kwa kila mkulima ili walime na kuendeleza zao la mkonge lakini wengine wamefanya kilimo cha mazao mengine kinyume na makubaliano.

“Labda niwakumbushe tu hili shamba linaitwa Kibaranga Sisal Estate, ni shamba la mkonge si shamba la michungwa. Lakini pia niwaambie wakazi wa Muheza popote walipo wajue kuwa hawajapewa hizi ardhi ili wajenge nyumba, walipewa zile eka tatu tatu ekari moja ulime mkonge halafu ndiyo upande mazao yako mengine.

“Tunafahamu Mheshimiwa Waziri Mkuu amefika hapa mara tatu na mara zote amesisitiza suala la uongezaji wa uzalishaji na ndiyo sababu ya shamba hili kurudishwa Bodi ya Mkonge baada ya kuonekana kuwa tangu imekaa halmashauri hakuna uendelezaji wa kilimo cha mkonge uliofanyika kuanzia shamba lenyewe na mashine ambayo inatakiwa ifufuliwe ili ianze kuchakata mkonge.  

“Kwa hiyo serikali imesema shamba lirudi Bodi ya Mkonge na bodi iratibu shughuli za uendelezaji wa hili shamba,” alisema Kambona.

Alisema Bodi ya Mkonge ikishirikiana na Amcos ya Kibaranga ambayo ni moja ya Amcos changa lakini zinakuja vizuri kwa sababu ya umadhubuti wa uongozi ambapo wanashirikiana nao vizuri wakisaidia ugawaji kwa maana ya kuleta hali ya utulivu kwenye shamba hilo na kuhakikisha wanaratibu masoko ya mkonge kwa wale waliofikia hatua ya kuvuna.

“Sasa niwaambie tu wananchi wa Kibaranga, Mheshimiwa Mkuu wa Wilaya ya Muheza, Halima Bulembo wakati amekuja tu mwaka jana alifanya kikao hapa na akarejea maagizo ya Waziri Mkuu kwamba waliopewa mashamba hapa walime mkonge, hili ni shamba la mkonge kwa hiyo walime mkonge.

“Kama umepewa shamba na hujaliendeleza, shamba hilo utanyang’anywa na kupewa mtu mwingine ambaye yuko tayari kulima mkonge. Kwa hiyo isikupe sifa kwamba mimi ninayo hati halafu una miaka sita tangu upewe hilo shamba hujaendeleza kwa kilimo cha mkonge,” alisema.

Aidha, Kambona alisema Bodi itatoa tarehe ambayo ikivuka hiyo tarehe mashamba hayo yote yataanza kugawiwa upya kwani hawataki kuona mapori wanataka kuona mkonge ukiwa umeshamiri.

Alisema shamba hilo ni kubwa ambapo likipandwa mkonge tayari linakuwa limeshafikia lengo la serikali kwa asilimia kubwa kwani litakuwa limeongeza uzalishaji kuelekea tani 120,000 ifikapo mwaka 2025.

“Kwa hiyo wananchi watambue hivyo na serikali iko makini sana ni kweli wale ambao hawataendeleza mashamba yao kwa kilimo cha mkonge tutawanyang’anya, umepanda machungwa ndani ya shamba la Kibaranga tutakunyang’anya hilo eneo tumpe mtu mwingine,” alisema.

Pamoja na mambo mengine, Kambona alisema Wilaya ya Muheza ina ardhi nzuri kwa kilimo cha machungwa nje ya shamba la Kibaranga na Shamba la Kibaranga limetengwa kwa ajili ya kilimo cha mkonge tu na mazao mengine ambayo ni ya muda mfupi kama mahindi au alizeti ni sawa kulima ndani ya mkonge.

Alisema Bodi ya Mkonge ndiyo itaratibu ni namna gani ya kuendeleza shamba hilo na eneo na watu wote watazingatia masharti ambayo yatatolewa na Bodi kwenye namna ya uendelezaji wa shamba hilo.

“Sasa watakaochukua hatua za kufanya makubaliano au mauziano huko nje bila kufuata utaratibu ambao utawekwa na Bodi ya Mkonge wasishangae kuona watapoteza hizo ardhi kwa sababu Bodi itawanyang’anya na hatutambui hayo mauziano tutawapa watu ambao wamefuata utaratibu wa kumilikishwa haya mashamba,” alisema.

Alisema bodi inataka watu wajue kilimo cha mkonge ni kilimo makini na kilimo ukikizingatia kitabadilisha hali ya maisha kwa haraka sana.

Kwa upande wake Mkurugenzi wa Maendeleo ya Mazao na Masoko wa Bodi ya Mkonge, Olivo Mtung’e, alisema kwa sasa suala la kujenga makazi ndani ya shamba hilo haliwezekani kwani litaleta mgogoro kutokana na ukweli kwamba baadhi ya watu watauza maeneo yao na baada ya muda mfupi patakuwa makazi ya kudumu.

“Tukisema tujenge huu mgogoro hautakuwa mdogo kwa sababu sisi Waafrika familia zetu huwa zinaongezeka tu ukijenga wewe leo kesho mtoto wako pia atataka kujenga kwa ajili ya makazi, kwa hiyo maana ya kuwa shamba la mkonge itaondoka, kwa hiyo suala la kujenga makazi ya kudumu kwa sasa hapana,”alisema.

Wednesday, July 20, 2022

SERENGETI BALLOON SAFARIS WILDLIFE.

 A short introduction to the wonderful Serengeti Balloon Safaris. Where you can see amazing views and wildlife from a hot-air balloon, soaring over the incredibly beautiful Serengeti national park.

Tuesday, July 19, 2022

MBUNGE ROSE TWEVE AWAOMBA UVCCM KUMSEMA VIZURI NA KUMUUNGA MKONO RAIS SAMIA

 

 
Mbunge wa Viti maalum Mkoani Iringa kupitia chama cha mapinduzi (CCM) Rose Tweve akiongea na vijana wa UVCCM  kwenye moja ya baraza alilohudhuria 
Mbunge wa Viti maalum Mkoani Iringa kupitia chama cha mapinduzi (CCM) Rose Tweve akiwa na furaha na vijana wa UVCCM mkoa wa Iringa alipokuwa mgeni rasmi kwenye moja ya mabaraza ya vijana hao.
Mbunge wa Viti maalum Mkoani Iringa kupitia chama cha mapinduzi (CCM) Rose Tweve akiwa na mwenyekiti wa UVCCM wilaya ya Iringa Vijijini.


Na Fredy Mgunda,Iringa.

Mbunge wa Viti maalum Mkoani Iringa kupitia chama cha mapinduzi (CCM) Rose Tweve ameipongeza jumuiya ya Umoja Wa Vijana wa Chama Cha Mapinduzi (UVCCM) mkoa wa Iringa kwa kazi kubwa wanayoifanya ya kukijenga chama.


Mbunge Rose Tweve alisema kuwa vijana wamekuwa wanafanya kazi kubwa wakati wa uchaguzi na kwenye kampeni mbalimbali za serikali kama ambavyo hivi Sasa wanavyofanya kwenye SENSA.

Alisema kuwa ni muhimu Kwa Kila mwananchi kuhesabiwa katika zoezi Hilo la sensa Ili kuiwezesha Serikali kupanga bajeti Kwa usahihi Ili kufikisha maendeleo Kwa Kila mwananchi kulingana uhitaji na idadi kamili ya watu.

Katika hatua nyingine mbunge Rose Tweve alisema kuwa bajeti ya mwaka 2021/2022 imesheheni miradi mingi ya kimaendeleo kama vile barabara,elimu,afya,Kilimo na ni bajeti ambayo itasaidia kutatua changamoto za wananchi wote.

Tweve aliwaomba vijana kuendelea kumuunga mkono Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan kwa kazi kubwa anayoifanya ya kuleta maendeleo katika kila sekta hapa nchini jambo ambalo linawafanya wananchi kukuza uchumi wao na taifa kwa ujumla.

Alimazia kwa kusema kuwa hiki ni kipindi cha uchaguzi hivyo vijana wanapaswa kugombea nafasi mbalimbali na kushiriki katika jumuiya mbalimbali ambazo zinaendelea kufanya uchaguzi ili kupata viongozi walio bora kukiongoza chama cha mapinduzi (CCM).


Mbunge huyo alifanikiwa kutembelea mabaraza yote ya umoja wa vijana wa chama cha mapinduzi (UVCCM) mkoa wa Iringa ambayo ni Baraza la UVCCM Iringa vijijini, Manispaa ya Iringa, Mufindi na kilolo.

MWAUWASA YASAINI MKATABA WA EURO MILIONI 2

Mkurugenzi Mtendaji wa MWAUWASA, Mhandisi Leonard Msenyele (kulia) akisaini mkataba. Kushoto ni Mkuu wa Kitengo cha Ununuzi MWAUWASA, Poas Kilangi.
Mkurugenzi wa Kampuni ya NETWAS, Griphin Symphorian (kulia) akisaini mkataba. Kushoto ni Mhandisi Mshauri wa Kampuni ya SEURECA Afrika Mashariki, Christophe Lacarin.
Mkurugenzi Mtendaji wa MWAUWASA, Mhandisi Leonard Msenyele (wa pili kushoto) akibadilishana mkataba na Mhandisi Mshauri wa Kampuni ya SEURECA Afrika Mashariki, Christophe Lacarin mara baada ya kusaini.
Mkurugenzi Mtendaji wa MWAUWASA, Mhandisi Leonard Msenyele (wa pili kushoto) na Mhandisi Mshauri wa Kampuni ya SEURECA Afrika Mashariki, Christophe Lacarin mara baada ya kusaini mkataba.
Mkurugenzi Mtendaji wa MWAUWASA, Mhandisi Leonard Msenyele (katikati) akizungumza wakati wa hafla ya utiaji saini mkataba wa kufanya upembuzi yakinifu, usanifu na usimamizi wa ujenzi wa mradi wa miundombinu ya kupeleka maji maeneo ya kusini mwa Jiji la Mwanza.

 

Na Mohamed Saif

Serikali kupitia Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira Mwanza (MWAUWASA) imesaini mkataba wa Euro Milioni Mbili na Kampuni ya SEURECA Consulting Engineering ya Ufaransa itakayoshirikiana na Kampuni ya NETWAS ya Tanzania kufanya upembuzi yakinifu, usanifu na usimamizi wa ujenzi wa mradi wa miundombinu ya kupeleka maji maeneo ya Kusini mwa Jiji la Mwanza.

Akizungumza wakati wa kusaini mkataba Jijini Mwanza hivi karibuni, Mkurugenzi Mtendaji wa MWAUWASA, Mhandisi Leonard Msenyele alisema mkataba huo ni hatua za awali za utekelezaji wa mradi wa kufikisha huduma ya maji kwenye maeneo ya Wilaya za Nyamagana, Misungwi na Magu.  

Kwa upande wa Wilaya ya Nyamagana Mhandisi Msenyele alitaja maeneo yatakayonufaika kuwa ni Buhongwa, Nyamazobe, Sahwa, Lwanhima, Fumagila, na Kishiri wakati kwa upande wa Wilaya ya Misungwi maeneo ya Usagara, Nyashishi, Nyang’homango, Kigogo Ferry, Bujingwa na Fella yatanufaika na kwa upande wa Wilaya ya Magu ni Kisesa, Bujora, Isangijo, Kanyama, Igekemaja na Ihayabuyaga.

Aidha, alifafanua kwamba mkataba huo umegawanyika katika sehemu mbili ya kwanza ikiwa ni kufanya upembuzi yakinifu, tathmini ya athari za mazingira na kijamii na usanifu na sehemu ya pili ni kumsimamia mkandarasi atakayetekeleza mradi huo.

Mhandisi Msenyele amebainisha kuwa uhitaji wa huduma ya maji kwenye maeneo hayo ni mkubwa na kwamba wananchi wa maeneo hayo wanayo matarajio makubwa na mradi huo hasa ikizingatiwa kuwa baadhi ya maeneo hadi hivi sasa hayana mtandao wa majisafi.

“Kuna uhitaji mkubwa wa huduma ya maji kwenye maeneo haya; ni matumaini yangu kwamba kutokana na uzoefu wenu mtafanya kazi kwa mujibu wa mkataba, wananchi wanahitaji maji, hawataki kutusikia tukizungumzia habari za michakato,” alisisitiza Mhandisi Msenyele.

Amezihakikishia kuzipa ushirikiano wa karibu kampuni hizo na alizielekeza kuanza shughuli zake mara moja ili mapema mwaka 2023 shughuli za ujenzi wa mradi zianze ambazo alisema zitahusisha ujenzi wa vituo vinne vya kusukuma maji, ujenzi wa matenki manne ya ujazo tofauti ya kuhifadhia maji, uchimbaji wa mitaro na ulazaji wa bomba za kusambazia maji zenye urefu wa takriban kilomita 400.  

Kwa upande wake Mhandisi Mshauri wa SEURECA Afrika Mashariki, Christophe Lacarin ameihakikishia Serikali kuwa watakamilisha shughuli za mradi kwa wakati na kwa ubora mkubwa kulingana na uzoefu wa muda mrefu walionao kwenye shughuli za usanifu na usimamizi wa miradi.

“Tunauhitaji huu mradi, tunaimani kwa ubora wa kazi zetu mradi huu utatuletea miradi mingine mingi na tumetekeleza miradi mingi maeneo mbalimbali duniani ambayo inaendelea kututengenezea mazingira ya kupata kazi,” alisema Lacarin.

Naye Mkuu wa Kitengo cha Ununuzi MWAUWASA, Poas Kilangi alisema mkataba huo ni wa miezi 44 na utekelezaji wake unapaswa kuanza ndani ya siku 28 kutoka siku ya utiaji saini.

WAZIRI MCHENGERWA AMWAGA VIFAA VYA MICHEZO SHULE ZOTE WILAYA YA RUFIJI,AANZISHA LIGI YA SENSA

 Na John Mapepele

Waziri wa Utamaduni, Sanaa na Michezo na Mbunge wa Jimbo la Rufiji.  Mhe, Mohamed Omary Mchengerwa ametoa vifaa vya michezo kwa shule zote za msingi na Sekondari na wanafunzi wanamichezo wote  wanaoshiriki kwenye mashindano ya michezo kwa shule za Msingi (UMITASHUMTA) na Mashindano  ya Shule za Sekondari (UMISSETA) kwa mwaka 2022 Wilaya ya Rufiji.

Mhe. Mchengerwa amekabidhi  vifaa hivyo kwa Mkuu wa Wilaya ya Rufiji Julai 17, 2022 kwenye  shule ya Sekondari ya Ikwiriri   Wilaya ya Rufiji ambapo amesema ameamua  kufadhili vifaa hivyo katika Wilaya ya Rufiji ili kuiendeleza michezo kwa kuwa michezo ni biashara  na ajira kubwa  kwa vijana.


“Nimeamua kusaidia vifaa hivi kwakuwa natambua  kwa sasa michezo ni miongoni mwa chanzo cha ajira na biashara kubwa duniani hivyo ni vema kufanya michezo kwa umakini mkubwa ili kujipatia ajira” amefafanua

Amewataka wachezaji hao kuwa na nidhamu na kujituma kwa kufanya mazoezi ili waweze kushinda kwenye  mashindano mbalimbali.

“Nendeni mkajitume, michezo ni ajira na  furaha wasikilizeni walimu wenu,  hata shuleni  mtafanya  vizuri”amesisitiza Mhe. Mchengerwa.

Aidha amesema dhamila ya Serikali kwa sasa  ni kuendeleza michezo ambapo amemshukuru Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Mhe, Samia Suluhu Hassan kwa jitihada kubwa anazofanya kwenye michezo  katika kipindi kifupi cha utawala wake ambazo zimeleta  mapinduzi makubwa kwenye sekta  hiyo.

Vifaa hivyo vimegharimu zaidi ya milioni 23 ambazo zimenunua zaidi ya jezi seti 200, trakisuti pea 100, kofia 200 na mipira 100.

Pia amefadhili Ligi ya mpira wa miguu ya   sensa katika Wilaya ya Rufiji ambapo ametoa seti 6 za jezi kwa timu sita na  mipira  12 kwa ajili ya mashindano  hayo.


Amesema lengo la mashindano hayo ni kuhamasisha  wananchi  kushiriki kuhesabiwa  kwenye sensa ya kitaifa  yam waka huu  kwa manufaa mapana ya wananchi wa Rufiji na Taifa kwa ujumla.


Aidha, amewahimiza wananchi wa Wilaya ya Rufiji na watanzania wote kujitokeza kwa wingi Agosti 23, mwaka huu kuhesabiwa kwenye zoezi la sensa kitaifa.

Mwenyekiti wa Halimashauri ya Wilaya ya Rufiji amemshukuru Mhe. Mchengerwa  kwa jitihada  zake  na mchango wake kwenye sekta ya michezo ambapo amemhakikishia kuwa michango anayotoa itatumika vizuri ili  kupata matokeo chanya.